MADAWA YA KULEVYA DIAMOND KIMENUKA
Stori: Shakoor Jongo na Makongoro Oging’
NIkweli kimenuka! Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ yupo
kikaangoni, habari zinadai kwamba kila anaponyanyua miguu, kikosi cha
kupambana na kuzuia madawa ya kulevya nchini chini ya kamishna wake,
Godfrey Nzowa nao wananyanyua miguu yao kumfuatilia, Amani limesheheni.
Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipozi.
Habari za kiintelijensia zilidai kwamba, kisa cha kikosi hicho
kufanya hivyo kinadaiwa kuwa, serikali inamhofia kujihusisha na biashara
hiyo haramu ya kusafirisha madawa ya kulevya ‘unga’ nje ya nchi kwa
kutumia kivuli cha kwenda kufanya shoo.
Akizungumza na wanahabari wetu jijini Dar, Jumatatu iliyopita, afisa
mmoja wa ngazi ya juu wa kitengo hicho ambaye hakupenda kuchorwa jina
gazetini, alisema Diamond amepewa maelekezo yote muhimu.
MAELEKEZO ALIYOPEWA
“Tumempa maelekezo Diamond,
atuletee mikataba ya shoo zote anazokwenda kuzifanya nje ya nchi ili
tujiridhishe kama kweli ni halali au anakwenda kwa ajili ya biashara
nyingine.
“Hiyo yote inatokana na uchunguzi wetu kwake kuhusu akaunti zake za
benki kuonesha kwamba ana fedha nyingi sana zinazotia shaka kama
amezipata kihalali,” alisema afisa huyo.
‘Diamond Platnumz’ akiwa kazini.
KUNUNUA NYUMBA
Afisa huyo aliendelea kusema
kwamba, uchunguzi wao pia umebaini kwamba, msanii huyo wa Bongo amekuwa
akinunua nyumba kila anaporejea kutoka kwenye shoo zake nje ya nchi,
jambo ambalo taasisi haiamini kama kweli analipwa pesa nyingi kwa shoo
moja, kiasi cha kumwezesha kununua nyumba jijini Dar.
“Tumebaini kwamba Diamond kila akirudi nchini kutoka kwenye shoo zake
hununua nyumba. Analipwa kiasi gani cha fedha kule kwenye shoo? Hapa
ndipo tunaposimamia sisi,” alisema afisa huyo huku akigongea msumari
kuwa Diamond mwenyewe amekatazwa kuzungumza kwenye vyombo vya habari
kuhusu kutakiwa kuwasilisha mikataba ya shoo zake za nje.
KUNA UKWELI?
Amani lilifuatilia na kubaini kwamba, Diamond aliporejea kutoka kwenye
safari yake ya Marekani hivi karibuni, alinunua nyumba kwa Sh. milioni
80 iliyopo maeneo ya Mwananyamala-Magengeni, Dar.
Siku za nyuma,
msanii huyo aliwahi kuripotiwa kununua nyumba zaidi ya mbili maeneo ya
Kijitonyama, Dar, kiasi cha kuandikwa na vyombo vya habari kwamba
amenunua mtaa.
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa.
KUHUSU AKAUNTI YA BENKI
Diamond mwenyewe aliwahi
kuhojiwa katika Kipindi cha Take-One kinachorushwa hewani na CloudsTV
ambapo alipoulizwa akaunti yake inasomaje, alijibu kuwa ina zaidi ya
bilioni moja hivi.
DONDOO ZA UWEZO WA DIAMOND
1. Ana utajiri unaozidi shilingi bilioni 1.
2. Yupo kwenye mazungumzo na promota wa Rwanda kufanya shoo moja ya
uwanjani ambayo anaweza kulipwa dola 120,000 (zaidi ya Sh. milioni 190).
3. Malipo ambayo hupokea kwa shoo zake nyingi za nje ya nchi hayashuki chini ya dola 25,000 (zaidi ya Sh. milioni 40).
4. Tangu mwaka 2011 mwishoni akaunti yake haijawahi kushuka chini ya Sh. milioni 100.
5. Anamiliki nyumba kadhaa jijini Dar ambazo amepangisha watu.
6. Ili kuvunja mkataba na aliyekuwa meneja wake, Papa Misifa ilibidi amlipe Sh. milioni 18.
NZOWA AZUNGUMZA NA AMANI
Gazeti hili lilimtafuta
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya
Tanzania, Nzowa ambapo alipopatikana na kuulizwa, alisema:
Sehemu ya madawa ya kulevya yaliyowahi kukamatwa.
“Ni kweli! Sisi kila mtu mwenye kipato cha kutia shaka lazima
tumchunguze. Diamond kama ana mali zote kwa nini tusimchunguze.
Ikithibitika anajihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya ama zake
ama zetu huo ndiyo utaratibu wetu.”
DIAMOND SASA
Amani lilimsaka Diamond na kumuuliza kama analijua kasheshe hilo ambapo alisema:
“Najua, ila nimegundua kuna watu wamepanga kunishusha chini kisanii ndiyo wanaoeneza taarifa kwamba mimi nasafirisha unga.”
Amani: Sasa unadhani kwa nini hao watu unaosema wamependa kukushusha
kisanii wasitumie njia nyingine, hasa ya sanaa wakatumia hiyo ambayo
unasema si kweli?
Diamond: We elewe hivyo kaka (akakata simu).
SAFARI ZA NJE
Kwa kipindi kirefu sasa Diamond
ambaye ni mpenzi wa Wema Isaac Sepetu, amekuwa akisafiri nchi mbalimbali
kwa shoo na mambo binafsi ambapo mbali na nchi kibao za Bara la Afrika,
ameshasafiri nchi nyingi zikiwemo Marekani, Uingereza, China, Norway,
Ujerumani, Dubai na nyinginezo.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS

Post a Comment