VITILIVYOGO (PAPA NA MUHOGO) - 02
“Mchumba baadaye,” mdada alimuaga Shaka.
“Po..po..a,” Shaka alijibu huku akiwa hajiamini.
Mdada aliingia kwenye gari na kuondoka na kumwacha Shaka akiwa amesimama walipomuacha na kulitazama gari mpaka lilipopotea machoni mwake.
“Shaka vipi?” Beka alimshtua alipokuwa amesimama.
Lakini Shaka alionekana yupo mbali mpaka alipomfuata na kumshtua.
“Oya, mwana vipi?”
“Poa.”
“Mbona umesimama kama nguzo?”
“Wee acha tu, yule demu amejua kunidhalilisha.”
“Kivipi?”
“Ataniitaje mbele ya bwana’ake?”
“Sasa tatizo nini kwani Betty nani yako?”
“Hata kama siyo mtu wangu, lakini anajua nampenda kwa nini anifanye vile?”
”Shaka acha ujinga yaani umekasirika, yule demu anakupenda kama mdogo wake kutokana na kukufahamu. Huna hadhi ya kuwa mpenzi wake, shukuru umepewa fedha, hebu ona kama fedha ya shule umepewa elfu hamsini na mchizi wake, yeye Betty anayempa raha anapewa shilingi ngapi?”
“Lakini mapenzi siyo fedha,” Shaka alijitetea.
“Hata kama siyo fedha, Betty matawi wewe acha kuchekesha wenye mapengo.”
“Poa, lakini lazima nimweleze ukweli kuliko kuteseka moyoni.”
“Mmh! Kazi kwako.”
MIAKA SITA ILIYOPITA
Shaka akiwa darasa la sita, siku moja alikuwa anatoka shule. Alipokaribia kwao, mara lilisimama gari aina ya BMW X6 na kuteremka dada mmoja ambaye kwake alikuwa mgeni. Japokuwa alikuwa kijana mdogo alipomuona yule mdada moyo ulimpasuka.
Yule mdada mrembo alikuwa amevaa gauni jepesi fupi kidogo lililoishia juu ya magoti. Baada ya kuteremka kwenye gari aliagana na dereva kwa kuchezesha vidole huku akisema kwa sauti ya madaha.
“Bai baby.”
“Poa baadaye,” sauti ilitoka kwenye gari na lile gari liliondoka na kumfanya yule dada aanze kutembea. Alitembea kwa mwendo wa madaha kama anaiogopa ardhi. Mkononi akiwa na mfuko kuonesha anatoka kufanya shopping super market kutokana na nembo ya mfuko.
Kwa vile Shaka hakuwa mbali alikaza mwendo ili aweze kumsogelea yule mdada kwa karibu ili macho yake yaweze kuufaidi utundu wa muumba. Alipofika karibu alipunguza mwendo na kuendelea kufaidi kwa raha zake huku akijisemea: “Kweli wenye hela wanafaidi.”
Umbile la nyuma la yule mdada lilikuwa na mvuto huku makalio yakipishana kama yanasikia baridi au abiria wa Mbagala wakigombea langoni wa daladala majira ya jioni.
Japokuwa alikuwa ameshaanza mapenzi ya baba na mama, lakini siku ile alikuwa kwenye hali mbaya, mnofu ulinyanyuka kama umebanikwa.
Alijikuta akitamani angalau yule dada ampe nafasi ya kuugusa mwili wake hata sekunde moja ili asikie joto lake.
Hakuongeza mwendo, alitembea kuhakikisha anaendelea kubaki nyuma, baada ya mwendo mfupi, mfuko uliokuwa umebeba matunda ulipasuka na kufanya matunda kudondoka chini. Bila kuangalia nguo aliyovaa aliinama kuokota na kufanya nguo ipande juu na kuweka mambo yote hadharani mpaka kufuli jekundu alilovaa lilionekana baada ya upepo kulinyanyua gauni.
Shaka alizidi kuchanganyikiwa kuona mambo ya ndani ya mdada mrembo aliyekuwa mbele yake. Bila kujielewa alijikuta akiingia kwenye kazi ya kumsaidia kuokota matunda. Aliifanya kazi ile kwa muda mfupi na kumkusanyia matunda yake yote.
“Ooh! Asante mdogo wangu,” yule mdada alimshukuru Shaka.
“Hakuna tatizo da mzuri.”
“Jamani kwani mi mzuri?”
“Tena sana.”
“Asante mdogo wangu, basi kaniletee mfuko pale dukani,” yule mdada alitoa noti ya elfu tano na kumpa Shaka.
Shaka alikimbilia dukani kununua mfuko na kurudi haraka, alipofika alimpa mfuko na chenji yake.
“Asante mdogo wangu, chenji chukua.”
Shaka alitaka kukataa kuchukua lakini yule dada alimbembeleza achukue, kwa vile hakutaka kumudhi alichukua. Shaka aliishia njiani na yule dada aliendelea mbele. Hakutaka kuingia kwao haraka, alijificha sehemu na kuendelea kuangalia utundu wa muumba alioufanya kwa yule mdada. Baada ya kupotea machoni kwake ndipo alipoelekea kwao.
***
Siku ya pili ilikuwa Jumamosi ambayo Shaka hakwenda shule, alijikuta akienda kukaa chini ya mti kumsubiri yule mdada ili amuone moyo wake utulie. Alijikuta akikaa muda mrefu bila kumuona, alipotaka kuondoka alimuona akipita kutoka mjini akiwa na mfuko wa plastiki kuonesha anatoka tena shopping.
Alipokaribia alipokuwa amekaa Shaka alitaka kujikwaa na kusababisha baadhi ya matunda kwenye mfuko kudondoka. Shaka alijikuta akitoka mbio na kuwahi kuokota na kumpa yule mdada kabla hajainama kuokota. Yule dada alipokea na kushukuru, alipomuangalia aliyemuokotea alishtuka.
“Ha! Ni wewe?”
“Ndiyo.”
“Jamani, yaani nina bahati na wewe!”
“Mmh! Kawaida tu,” Shaka alijibu huku akiondoka.
“Hebu rudi mdogo wangu,” mdada alimwita Shaka ambaye alirudi na kuonesha aibu ambayo ilimshtua sana yule dada.
“Mmh! Mdogo wangu mbona hivyo?” alimuuliza huku akimshika kichwani.
“Mm..mmh!” Shaka mdomo ulikuwa mzito.
“Una nini mdogo wangu?”
“Nipo sawa.”
“Jamani mbona una aibu kiasi hicho?”
“Mm..mmh,” Shaka alijibu akiwa ameangalia chini kwa aibu.
“Unaitwa nani?”
“Shaka.”
“Unakaa wapi?” Shaka hakujibu alionesha kwa kidole.
“Mbona una aibu, unanipenda?”
Shaka aliitikia kwa kichwa na kumfanya mdada acheke.
“Basi mchumba wahi nyumbani,” mdada alisema huku akitoa noti ya elfu mbili na kumpa Shaka.
Shaka alipokea na kuondoka kurudi nyumbani, lakini hakufika mbali aligeuka kumtazama mdada ambaye kwake alikuwa mkubwa sana. Alijikuta akijisahau na kuendelea kumtazama mpaka alipopotea kwenye macho yake. Baada ya kupotea alitikisa kichwa na kuelekea nyumbani kwao roho yake ikiwa kwatu japokuwa alikuwa hajala toka asubuhi.
***
Shaka alijikuta akiingia kwenye mateso ya kujitakia, kila alipokosa kumuona yule mdada mrembo alikuwa kama mgonjwa. Kila alipotoka shule hakwenda kucheza, alikaa kwenye mti mpaka alipopita na kumsalimia kisha aliondoka.
Hali ile ilimfanya na yule mdada kumzoea Shaka kila alipokosa kumuona alipita hadi kwao kumuulizia.
Wote walijua ni utani Shaka kuwa na mpenzi kama yule dada kutokana na umri na hadhi. Siku zilikatika huku Shaka akizidi kumzoea yule mdada aliyefurahi mapenzi aliyomuonesha. Ilifikia hatua akawa anaenda nyumbani kwa yule mdada aliyekuwa akikaa kwao na kuzungumza naye kisha alirudi kwao.
Moyoni alijiapiza ipo siku atamweleza ukweli ili ijulikane moja, lakini kila alipotaka kumweleza alisita kwa kujiona bado hakuwa na kigezo cha kuweza kupewa penzi hata la kuonjeshwa.
Miaka ilikatika huku Shaka akiwa karibu na yule mdada mrembo, alipofika kidato cha nne aliamini ule ulikuwa muda muafaka kwake kumweleza anachokitaka kwake. Tayari alikuwa ameshaanza kugawa dozi ya uhakika kwa wapenzi wake Uswahilini. Shuleni Shaka hakupata demu kutokana na kuonekana hana kitu, hata mavazi yake yalikuwa ya kawaida tofauti na wanafunzi wenzake waliokuwa masharobaro waliokuwa waking’oa watoto wa kishua, mademu wengi wazuri shuleni alikula kwa macho.
Hali ya maisha ya kwao ilimbana na kumfanya afikirie masomo sana. Hakuwa na uwezo wa kuwashawishi wanafunzi wenzake, kwa vile hakwenda na wakati wengi walimuona bado yupo anolojia wakati wenzake wapo dijitali. Hali ile ilimfanya Shaka kucheza sana na mademu wa uswazi.
Baada ya kuvumilia mateso, siku moja alijiapia liwalo na liwe, lazima alitoe la moyoni. Wakati huo alikuwa ameshalifahamu jina lake, mdada mrembo alikuwa akiitwa Betty.
Kama kawaida alimsubiri muda wa kupita kutoka mjini, ila siku ile alimweleza Shaka kuwa atachelewa kwa kuwa atakuwa na mishemishe mingi. Majira ya saa moja usiku alirejea na kumkuta Shaka yupo kwao. Kwa vile alikuwa amemzoea alimpokea mfuko na kwenda naye hadi kwao.
Baada ya mazungumzo na kula chakula cha usiku, Shaka aliaga ili arudi nyumbani kwao. Betty alimsindikiza hadi nje ya nyumba yao akiwa amejifunga upande wa khanga na nguo ya ndani tu. Hakutaka kufika mbali kutokana na alivyokuwa amevaa kwani alikuwa anajiandaa kwenda kuoga.
“Shaka kesho basi.”
Shaka alijikuta akijikaza kiume kumweleza kilicho moyoni mwake muda mrefu.
“Samahani mchumba.”
“Bila samahani.”
“Kuna jambo moja linanisumbua muda mrefu.”
“Muda mrefu! Linazidi mwaka?”
“Si mwaka, miaka.”
“Miaka mingapi?”
“Sita.”
“Sita! Jambo gani hilo mchumba?”
“Betty nakupenda sana,” Shaka alijitoa muhanga.
“Jamani kumbe ni hilo, mbona hata mimi nakupenda mchumba.”
“Nataka zaidi ya hilo unalofikiria.”
“Unamaanisha nini?”
“Yaani tuwe wapenzi.”
ITAENDELEA SIKU YA KESHO COMMENT HAPA CHINI
MTUNZI: DK. AMBE
Endelea kulike ==>www.facebook.com/2jiachie

Post a Comment