VITILIVYOGO (PAPA NA MUHOGO) - 01
“Kweli wakubwa wanafaidi,” maneno yalimtoka
Shaka baada ya kumtazama mdada mmoja aliyekuwa akipita na kutikisa
kichwa kuonesha ameteswa vya kutosha na mdada yule aliyepita akielekea dukani katika vazi la khanga moja akionesha ametoka kuoga na kukimbilia dukani mara moja.
Rafiki yake Beka alimuuliza kulikoni kusema vile baada ya kumuangalia yule dada ambaye alikuwa mkubwa kwake kiumri?
“Shaka vipi mwana?”
“Yule sister ananiua sana.”
“Shaka unachekesha, anakuua kivipi?”
“Nampenda ile mbaya.”
“Hata ukimpenda utafanya nini?”
“Yaani kuna kipindi huwa natamani kumwambia anavyoutesa moyo wangu, lakini naogopa tunaheshimiana sana, kibaya amenizoea sana.”
“Lakini Shaka yule demu mbona kakuzidi vitu vingi, kwanza mkubwa kwako pili anaonekana mtu wa matawi, wewe mwanafunzi hata akikubali japo najua ni sawa na jua kuwaka mchana, utampa nini?”
“Hilo najua, lakini sina jinsi nitaendelea kula kwa macho, ipo siku nitamwambia ukweli, liwalo na liwe.”
“Mmh! Makubwa, unafikiri atafanyaje?”
Wakiwa katikati ya mazungumzo, gari moja aina ya BMW X6 lilitokea na kwenda kusimama sehemu na kuwafanya wote wang’ae macho. Baada ya gari kusimama waliacha kuzungumza na kutaka kujua limefuata nini maeneo yale. Mara honi ilipigwa.
Alitoka yule mdada anayemtesa Shaka akiwa amependeza kwa kuvaa gauni fupi lililoweza kuyaweka mambo yote nje kama akiinama, kwa vile nyuma mwenyezi Mungu alimjalia kigauni kilining’inia juujuu.
Mdada alitembea taratibu kuelekea kwenye gari, kabla ya kulifikia gari aligeuka na kumuona Shaka, alishtuka na kushika kifuani na kusema:
“Ha! Mchumba, njoo mchumba wangu,” mdada alisema huku akinyoosha mkono kuonesha anamwita Shaka.
Shaka alisogea mpaka alipokuwa amesimama yule mdada ambaye alikuwa akiutesa moyo wake. Mdada alimsogelea, akamkumbatia na kumchumu kisha alimwita mtu aliyekuwa kwenye gari.
“Jimmy my baby.”
“Unasemaje baby?” sauti iliuliza toka ndani ya gari.
“Njoo mara moja.”
Mara ulifunguliwa mlango kwenye gari na kuteremka jamaa mmoja aliyeonekana amekwiva umatemate.
“Waoo mpenzi.”
Mdada alimkumbatia jamaa aliyeshuka kwenye gari na kubusiana pande tatu kisha alimshika begani mdada na kumsamilia Shaka.
“Mambo dogo?”
“Poa bro.”
“Heloo baby unasemaje?” jamaa alimuuliza mdada huku akichezea kidevu.
Kitendo kile kilikuwa kama kumdhalilisha Shaka kutokana na jinsi aliyompenda yule mdada na walivyokuwa wakiheshimiana.
“Unamuona huyu?” mdada alimuliza mwanaume wake huku akiwa amemshika mkono Shaka.
“Ndiyo.”
“Basi baby kijana huyu ananipenda sana.”
Kauli ile ilimshtua sana Shaka na kujiuliza yule mdada amemwita kumdhalilisha?
“Kwa hiyo?” jamaa alimuuliza akiwa amemkazia macho Shaka aliyekuwa katika vazi la tisheti na kaptula ya shule na chini alikuwa amevaa ndala.
“Siyo kwa hiyo, kijana huyu ameanza kunipenda toka yupo darasa la nne mpaka leo hii. Bahati mbaya bado mdogo lakini angekuwa mkaka mkubwa ningeshampa, ananipenda sana nina imani mpenzi wake akimpenda kama mimi atafaidi.”
“Mpe tu. Kwani sasa hivi huyu hachukui mademu?” jamaa alichomekea.
“Jimmii, huyu mtoto mdogo nitampeleka wapi?”
“Sasa mapenzi yake yatayeyukia wapi?”
“Kwani hana mpenzi, si unamuona kachangamka.”
“Kwa hiyo ndicho ulichoniitia?”
“Hapana, naomba elfu kumi nimpe mchumba wangu akatese kesho shule.”
Jamaa bila kusema kitu aliingiza mkono mfukoni na kutoa pochi kisha alihesabu wekundu watano na kumpa Shaka.
“Dogo zinatosha?” jamaa alimuuliza baada ya Shaka kuzipokea.
“Zi..zi..natosha brother,” Shaka alijikuta akitetemeka kupokea fedha.
“Jamani mchumba unaniangusha, elfu hamsini unatetemeka hivyo, ungepewa milioni ingekuwaje?” Mdada alimtania Shaka.
“Poa dogo baadaye,” Jimmy alisema huku akimshika mdada kiunoni na kuelekea naye kwenye gari.
“Mchumba baadaye,” mdada alimuaga Shaka.
“Po..po..a,” Shaka alijibu huku akiwa hajiamini.
Mdada aliingia kwenye gari na kuondoka na kumwacha Shaka akiwa amesimama walipomuacha na kulitazama gari mpaka lilipopotea machoni mwake.
“Shaka vipi?” Beka alimshtua alipokuwa amesimama.
Lakini Shaka alionekana yupo mbali mpaka alipomfuata na kumshtua.
“Oya, mwana vipi?”
“Poa.”
“Mbona umesimama kama nguzo?”
“Wee acha tu, yule demu amejua kunidhalilisha.”
“Kivipi?”TUKUTANE SIKU YA KESHO
MTUNZI: DK. AMBE
Endelea kulike ==>www.facebook.com/2jiachie

Post a Comment