TRAFIKI MWINGINE FEKI ANASWA DAR! VIDEO NA PICHA ZIKO HAPA
KWA mara nyingine tena
makachero wa polisi wamefanikiwa kumnasa trafiki feki ambaye anadaiwa
kutikisa Jiji la Dar es Salaam kwa ukamataji wa magari na kuwatoa fedha
madereva, Uwazi lina mchapo kamili.
Trafiki feki aliyenaswa na Polisi anadaiwa kutikisa Jiji la Dar es Salaam
Chanzo chetu ndani ya jeshi la polisi, kinaeleza kwamba trafiki huyo
feki anayejulikana kwa jina la Robinson Seif (30) anayejifanya kuwa na
cheo cha staf sajenti alikamatwa juzi Jumamosi akiwa ‘kazini kwake’.
Kamishna Kova (katikati) akionesha kidole kwa polisi feki aliyekamatwa.
Chamazi - Temeke jijini Dar es Salaam baada ya
kupatikana kwa taarifa zake.Chanzo hicho kilidai kwamba askari huyo
aliwahi kuwa polisi wa usalama barabarani Kibaha mkoani Pwani lakini
alifukuzwa kwa kukosa sifa ya kuendelea na kazi hiyo.
Akipelekwa kituo cha Polisi.
Inadaiwa kuwa, baada ya kuonekana na makosa
mbalimbali jeshi la polisi lilimfikisha katika mahakama yao na akapewa
adhabu ya kuachishwa kazi.“Madereva wameshangilia sana, ni kama sherehe
tu kwao, maana jamaa amewapiga mabao sana akijifanya ni trafiki,”
kilipasha chanzo hicho.
Sura ya ‘karibu’ ya askari huyo feki aliyekamatwa, Robson Seif Mwakyusa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, ACP Kihenya Kihenya
amekiri kukamatwa kwa askari huyo na kwamba alikutwa yupo katika kazi
zake hizo akijidai kuwa askari wa usalama barabarani.
...akijitetea.
“Huyu Seif amekuwa akiwadanganya wananchi kuwa yeye ni trafiki na
kuwachukulia fedha, sare alizokutwa amevaa ni zetu lakini bado
tunachunguza alipozitoa, pia tunafuatilia mambo mengine, nitatoa taarifa
kamili baadaye,” alisema Kamanda Kihenya.
Kova akionyesha baadhi ya sare za jeshi la polisi alizokamatwa nazo polisi huyo feki.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Ulrich Matei, alipoulizwa kwa
njia ya simu alikiri Seif kuwahi kufanya kazi mkoani Pwani huku
akifafanua kuwa ni kati ya askari nane waliofukuzwa kazi Januari mwaka
huu kwa makosa mbalimbali.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
Post a Comment