ad

ad

SASA UHAKIKA, NANI ANARUDI KWAO URENO, ROJO ANATUA MAN UNITED


Sasa uhakika Luis Nani anarudi kwao Ureno kuichezea Sporting Lisbon ambayo ilimkuza kisoka.

Manchester United imefikia makubaliano dili la pauni milioni 16 na Wareno hao kumnasa beki Marcos Rojo raia wa Argentina
Rojo, alishasema ni ndoto yake kujiunga na United na sasa anajiunga nayo. Ila United itaendelea kulipa mshahara wa Nani hadi mwisho wa mkataba.
Rojo mwenye miaka 24 anakuwa kati ya wachezaji walioingia kwenye listi ya United baada ya kuanza Ligi Kuu England kwa kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Swansea.

No comments

Powered by Blogger.