MH! MISSED CALL YA SHEMEJI - 07
“Shemeji ingia chini ya kitanda,” shemeji mtu alimwambia Beka huku
akifunua godoro, akabinyua chaga za upande mmoja. Beka alizama ndani
yake, ile anamalizikia tu, Aisha akagonga mlango…
“Dada,” aliita kwa sauti iliyojaa utulivu.
Dada yake alirudisha chaga polepole kisha akafunika godoro vizuri na kurudishia shuka kama awali…
“Dada.”
“Ee.” “Samahani, nina shida.”
TAMBAA NAYO…ada mtu huyo alifungua mlango na kusimama katikati akijifanya hajui shida ya mdogo wake…
“Beka simwoni humu ndani dada.”
“Ndani wapi?”
“Chumbani. Nimekuja sebuleni hayupo, nimekwenda bafuni, chooni kote hayupo.”
“Kwa hiyo yuko kwangu siyo?”
“Sina maana hiyo dada. Kwani we huoni kuwa ni tatizo? Nimekwambia ili tusaidiane kujua alipo.”
“Ohoo! Nilidhani unamaanisha yuko kwangu. Maana umesema sehemu nyingi umemwangalia hayupo. Nikasema makubwa! Kwani ametokaje?”
“Nadhani mimi nilikuwa sijaamka.”
“Simaanishi hivyo, namaanisha alipotoka amevaa nini?”
“Naamini ametoka na bukta tu, maana haipo na ndiyo huwa anaivaa anapokuwa amelala. Mimi nahisi hajatoka nje ya nyumba hii.”
“Unarudi palepale. Unaposema hivyo atakuwa wapi kama si kwangu sasa?”
“Dada tuyaache hayo, tumtafute.”
“Simu yake?”
“Simu kaizima, ipo chumbani.”
***
Kule chini ya kitanda, Beka alianza kupata maumivu kwani alijipinda sana kutokana na ufupi wa kitanda kiasi kwamba hakuweza kulala kwa kunyooka.”
“Da! Ukisikia mateso ya kujitakia ndiyo haya. Sasa hapa kisa nini? Lakini kwa namna nyingine kisa ni yeye mke wangu na ugumu wake wa kunipa haki yangu.”
***
Dada mtu alichukua kanga nyingine kutoka kwenye msumari nyuma ya mlango, akajifunika juu na kutoka. Lakini alipotoka tu, Aisha alinyoosha mkono akachukua funguo kwa ndani na kuufunga mlango huo kwa nje…
“Sasa tunaanzia wapi?” aliuliza dada mtu akiwa ameshafika sebuleni sasa.
“Humuhumu ndani dada.”
“Uani ulikwenda?”
“Sijaenda.”
“Sasa kwa nini usiende. Kule si ndiyo anaweza kuwepo maana ya Mungu mengi.”
Aisha alikuwa kama hamuelewielewi dada yake kwa kauli zake. Mara aseme ‘kwa hiyo yupo humu kwangu?’ mara ‘ya Mungu mengi.’
“Dada unaposema ya Mungu mengi una maana gani?”
“Nina maana labda yuko uani.”
“Sasa atakwenda kwa njia gani wakati mlango umefungwa? Kama alitoka uani nani alifunga mlango kwa ndani baada ya yeye kutoka na humu ndani niko mimi, wewe na yeye tu?”
“Kwa hiyo bado una maana ni mimi nilifunga mlango baada ya yeye kutoka si ndiyo?”
“Ha! Dada bwana! Sina maana hiyo mimi.”
“Sasa maana yako ni nini we Aisha?”
“Mbona una hasira dada?”
“Hata ungekuwa wewe ungepata hasira.”
***
Kule chumbani, Beka alijua kwamba shemejiye na mkewe wametoka kwenda kumtafuta, akasukuma chaga kisha akatoka, akazirudisha vilevile. Alisimama chumbani humo na kuangaza huku na kule. Alijua akitoka atakutana nao. “Huyu mwanamke hajui kama niliwahi kupitia mafunzo ya kijeshi, sasa tangu lini askari anaweza kufumaniwa kirahisirahisi, mimi ndiyo Beka bwana nimezaliwa mjini na kukulia mjini!” Beka alizungumza moyoni kisha akapanda kwenye dari.
Alipozama, akarudishia mfuniko, akatambaa kwa upole akikumbuka kwamba, kuna mfuniko mwingine kwenye bafu chumbani kwake. Alifanikiwa kushukia huko bafuni ambapo alisimama kwa muda akihema kwa sana. Alivua bukta na kujimwagia maji.
Mlio wa maji bafuni ulimshtua Aisha, akaenda mbio chumbani na kumkuta mumewe anaoga…
“Beka,” aliita Aisha kisha akatoka mbio kwenda chumbani kwa dada yake akijiuliza ataukuta mlango ukiwaje? Alishangaa kuukuta umefungwa kwa funguo nje lakini pia bado alijua kama mumewe angekuwa humo, asingeweza kutoka mpaka afunguliwe kwa nje na ndiyo maana yeye alifunga.
Alirudi tena hadi chumbani. Wakati huo dada yake alikuwa sebuleni akimshangaa. Alipokwenda chumbani kwake, dada mtu huyo alishangaa kukuta mlango umefungwa kwa nje na funguo ikining’inia. Akazama ndani na kuinua godoro hakumwona Beka!
“Mh! Huyu vipi? Yaani ametoka akaamua kuufunga mlango kwa nje? Mbona balaa, mkewe atajua,” alisema moyoni.
Hakujua kama mlango huo ulifungwa na mdogo wake.
***
“
Ulikuwa wapi Beka?” aliuliza Aisha kwa sauti iliyopandwa na midadi…
“Chooni.”
“Una uhakika?”
“Ningekuwa sina uhakika ningekwambia sijui nilikokuwa.”
“Mimi nimeita sana hukuitika. Bafuni nimekuja sijakuona.”
“Ulitaka niitike nikiwa chooni?”
Aisha alikosa jibu la moja kwa moja. Alitoka mpaka sebuleni na kumjulisha dada yake, alipomkosa akaenda chumbani na kumwambia kwamba, mumewe kumbe alikuwa chooni na sasa ametoka yupo bafuni anaoga.
“Kwa hiyo hakupotea kama ulivyokuwa unaamini?” aliuliza dada mtu huyo.
“Inawezekana.”
***
Kulikucha, dada mtu huyo akawa na dukuduku la kutaka kujua shemeji yake alitokaje ndani ya chumba hicho mpaka mkewe akaamini? Akawa anamtafuta aongee naye kabla hajaenda kazini.
ITAENDELEA JIONI YA LEO HAPA

Post a Comment