MASOGANGE ATANGAZIWA NDOA SAUZI
Modo Agnes Masogange.
Modo Agnes Masogange ameonekana
kumdatisha mwanaume aliyefahamika kwa jina la Louis Donald wa nchini
Afrika Kusini baada ya jamaa huyo kuposti mtandaoni picha tofauti akiwa
amepozi kimahaba na Agnes na kueleza kuwa, huyo ndiye mke wake wa kufa
na kuzikana.
Jamaa huyo amekuwa akieneza habari kuwa, Masogange ni ‘mtu’ wake
kitendo kilicholifanya Ijumaa ambalo awali lilikuwa na taarifa kuwa,
Agnes amechumbiwa na msanii aitwaye Evance Komu limtafute mrembo huyo
ili afafanue na alipopatikana alisema:
“Hiyo ishu ipotezee bwana, maswali gani hayo unaniuliza?” alihoji
Masogange aliyeonekana kutotaka kuweka wazi ishu zake za kimapenzi.

Post a Comment