ad

ad

Kumbe Vikiungwa Vitamu - 03






 ILIPOISHIA
“Manka karibu.”
“Asante bosi, kazi iliyokuwa na haraka nayo tayari.”
“Ooh, vizuri sana sikutegemea ungeifanya kwa muda mfupi hivi.”
“Najitahidi japo nilikuwa na muda mrefu sijagusa computer,” nilimjibu huku nikimkabidhi kalatasi, nami nikiachia tabasamu pana ambayo huogopa kuitoa kwa wanaume ili kuepusha ungongano wa mawazo.
Ilikuwa ugonjwa wa wanaume kila ninapotabasamu mashavu huweka visima ‘dimples’  wanaume wengi ulikuwa uchawi mkubwa kwao. Kila mwanaume niliyekutana naye alipenda kunifurahisha ili aone madhari mantashau ya mashavu yangu.

Lakini pamoja na yote sikuwa na sifa ya kumteka mwanaume kimapenzi zaidi ya kunionja na kuniacha. Wasiwasi wangu huenda mwili wangu hauna asali itakayo mfanya mwanaume yoyote atakaye nionja anirudie mara mbili. Basi baada ya kupokea aligeuka na kuondoka kurudi ofisini kwangu.

Nilipofika mlangoni nilikumbuka kitu nilitaka kumuuliza bosi,  niligeuka ili nimuulize kitu. Niligeuka ghafla na kukutanisha macho na bosi ambaye kumbe nyuma yangu alikuwa akinifuatia. Maskini kaka wa watu alishtuka mpaka akadondoka chini, nilijikuta namuonea huruma.

Nilirudi hadi chini alipokuwa amekaa bila kuonesha kujinyanyua, mwili wake haukuwa mkubwa sana nilimshika mkono ili kumnyanyua.

“Hapana Manka nitanyanyuka mwenyewe.”

“Hapana bosi naomba unipe mkono,” nilimwambia kwa sauti ya huruma yenye kubembeleza. Alinipa mkono na kumnyanyua, baada ya kunyanyuka nilitoa kitambaa changu na kumfuta sehemu yenye vumbi.

“Tosha Manka sehemu zingine nitafuta mimi.”

“Hapana bosi ni wajibu wangu kufanya hili.”

Aliniacha nimfute kisha nilimtengenezea kiti na kumuomba akae.

“Unaweza kukaa.”

Bila kuongeza neno alikaa kwenye kiti chake huku uso wake ukionesha aibu imemtawala.

“Pole bosi,” nilimwambia kwa sauti ya chini.

“Asante.”

“Hukuumia?”

“Nipo sawa.”

“Pole sana.”

“Asante Manka, nipo sawa kaendelee na kazi.”

Niligeuka na kuondoka hata nilichotaka kumuuliza nilikiacha na kupanga kumuuliza kupitia simu yangu ya mezani. Nilitoka hadi ofisini kwangu kuendelea na kazi, kabla ya kuanza kazi nilijikuta nikijiuliza kilichomdondosha bosi wangu ni nini.

Wasiwasi ulikuwa uleule bosi kapagawa na mimi, kitu ambacho sikutaka kinitokee kwa muda ule kwani ilikuwa mapema sana. Niliamini kabisa bosi kwa mtazamo wa nje alikuwa amepata bonge la mwanamke, lakini ndani sikuwa na sifa zile za kukaa na mwanaume kwa muda mrefu.

Niliyapuuza na kuendelea na kazi, nilikumbuka kuna kazi nilitaka kupata maelekezo kwa bosi. Nilimnyanyua simu kumpigia baada ya kuita kwa muda ilipokelewa.

“Haloo bosi.”

“Ooh..Aah...Nani Manka,” maskini bosi wangu alionesha kiwewe bado hakijamtoka.

“Bosi mbona hivyo?”

“Aah, kawaida tu, unasemaje?”

“Ok, bosi nilikuwa nauliza hii kazi ya malipo kuna maandishi ya mkono nayo niyaandike?”

“Hakuna tatizo, yaandike kama ilivyoandikwa.”

Nilikata simu na kuendelea ka kazi yangu kama kawaida, baada ya muda nikiwa bize simu ya mezani iliita, nilinyanyua na kupokea.

“Haloo bosi.”

“Ndiyo Manka jiandae tukapate lunch.”

“Nashukuru bosi.”

Baada ya kukata simu, niliangalia saa kubwa ya ukutani  iliyokuwa mbele yangu, ilionesha ni saa saba kasoro kumi mchana. Nilimalizia kazi yangu ili nipate muda wa kwenda kula, nikiwa bado nimeinama nikirekebisha tatizo la kisarufi nilishtuliwa na sauti ya bosi.

“Manka tunaweza kwenda.”

“Hakuna tatizo bosi, namalizia kurekebisha sarufi.”

“Utamalizia tukirudi.”

Nilisave kisha nilizima computer na kunyanyuka, nilijitengeneza vizuri nguo niliyovaa. Kwa chati nilimuona bosi wangu koo likimcheza kama mtu mwenye kiu kikali. Baada ya kuhakikisha nipo sawa tulitoka hadi kwenye gari lake kisha tulikwenda kwenye moja ya hoteli ya kifahari ambayo ilinikumbusha mbali enzi nipo kwenye ndoa yangu.

Tulipofika Mateja alionesha kutojiamini sana kwangu kitu ambacho sikuamini mwanaume kama yeye kuwa katika hali ile. Sikuwa na sifa kubwa zaidi ya mwanamke aliyepoteza matumaini ya kupata hadhi mbele ya mwanaume. Niliamini kaniona kwa nje hanijui  ndani nilivyo ndio maana ananipapatikia.

Nilijua akikipata anachokitafuta kwangu pengine ndiyo siku ya kunifukuza kazi, lakini sikuwa na jinsi kila mwanaume mwenye pesa aliamini mwanamke sahihi wa kukaa naye ni mimi. Baada ya kuketi kwenye viti vyetu muhudumu alifika na kutaka oda zetu.

“Manka agiza chochote ukitakacho kwa bei yoyote.”

“Asante, nataka kula unachokipenda wewe,” utanishangaa kwa nini nimesema vile, nilifanya vile ili kumtoa wasiwasi na kumfanya awe huru kwangu japo si katika suala la mapenzi.

“Hapana Manka nataka wewe leo ndio uchague chakula tutakacho kula.”

“Sawa,” nilichagua chakula ambacho wote tulikuwa.

Baada ya chakula wakati wa kunywa vinywaji Shaka aliniuliza.

“Samahani.”

“Bila samahani.”

“Manka, umeolewa?”

“Sijaolewa.”

“Una mchumba sina?”

“Sina.”

“Rafiki wa kiume?”

“Sina.”

“Manka mbona unanidanganya.”

“Kweli bosi.”

“Hivi Manka kwa umbile alilokujali muumba usiwe na mwanaume?”

“Si kwamba sijawahi mwanaume ila kwa sasa sina.”

“Kweli?”

“Kweli kwa nini nikufiche ili iwe nini?”

“Mara nyingi watu wamekuwa si wakweli.”

“Huo ndio ukweli wangu.”

“Kwa nini mrembo kama wewe huna rafiki wa kiume?”

“Sina bahati nimeamua kuishi peke yangu.”

“Ina maana hata ombi langu litagonga ukuta?”

“Ombi gani?”

“Kwa vile huna mtu nilifikili unafaa kuwa mke wangu.”

“Aaah, bosi,” kauli ile ilinishtua sikupenda kuisikia masikioni mwangu.

Sikuwa na jibu la moja kwa moja,  moyo mapigo ya moyo walinienda mbio na machozi yalinitoka. Mateja alishtuka kuniona nikitoka machozi badala kumpa jibu lake.

“Manka vipi?”

“Hataa,” nilitikisa kichwa.

“Mbona machozi yanakutoka.”

“Kauli yako imenishtua.”

“Kivipi?”

“Sikutegemea kuniambia neno hilo mapema kiasi hiki.”

“Manka, penzi limuingiapo mtu huwa kama kichaa aliyekatikiwa na mishipa ya fahamu. Niyasemayo si mimi ni moyo wangu naomba unihurumie.”

“Ni kweli, lakini sina bahati kila siku mapenzi limekuwa likinitesa.”

“Kivipi?”

“Mpaka leo sijajua sababu ya kuachwa na wanaume.”

“Ni wazi wote waliopita walikuwa na tamaa ya kukujua ulivyo na si mapenzi ya dhati. Lakini nakuamini mimi ndiye mwanaume sahihi kwako.”

“Hiyo kauli kwangu nimeizoea, lakini mwisho wa siku mambo huwa kinyume.”

“Niamini Manka, nitakuwa mume mwema.”

“Mmh nitashukuru, lakini usinitende utaniumiza.”

“Siwezi.”

Baada ya chakula tulirudi ofisini, hatukufanya sana kazi Mateja alikuwa na uchu wa fisi. Aliniomba tufunge ofisi twende tukastarehe, sikuwa na pingamizi nilifunga kazi na kuongozana naye kwenye gari lake. Mateja alinipeleka kwenye hoteli ya kifahari ya nyota tano.

Kwa vile shida yake niliijua sikushtuka kumsikia akiuliza chumba cha VIP, baada ya kulipia tulikwenda kwenye chumba kilichokuwa ghorofa la pili. Chumba kilichokuwa cha kifahari, ambacho kilikuwa kipo katika hadhi ya juu. Katika maisha yangu sikuwahi kuingia kwenye chumba kizuri kama kile.

Chumba nilikiona kilikuwa kinapendeza lakini wasiwasi wangu bosi wangu atakipata alichokifikilia kukipata mwilini mwangu. Sikutaka nami kijiweka nyuma kwani nilikumbuka kauli za Bi Shuu mama mlezi wangu shangingi mstaafu, kuwa niwapo mbele ya mwanaume nijionesha nipo tayari kumpa kile anachokitaka.

Siku zote aliniambia nijiamini ili kumfanya mwanaume naye ajiliuze mara mbili mbili ataniingiaje. Sikupoteza wakati baada ya kuingia tu chumbani nilivua nguo zote na kubakia kama kuku aliyenyonyolewa. Sikuchelewa kumsaula na yeye tukawa sale sale maua.

 Nilitembea kama miss kuelekea kwenye kabati kuchukua taulo kwa makusudi nimuoneshe umbile langu ambalo mwanzo huwa utata kwa wanaume.

Lakini wakiisha nipata nakuwa kama Big G iliyotafunwa na kuisha utamu mwisho wake hutemwa. Kwa kweli sikupenda kutongozwa siku moja na siku hiyo hiyo kumvulia mwanaume nguo ya ndani.

 Niliamini kabisa kujilahisi vile lazima thamani yangu ingepungua lakini kama ningemzungusha, kidogo thamani yangu kwake ingepanda. Nilijua lazima ataniona maharage ya Msanga maji nusu kijiko. Lakini sikuwa na jinsi kutokana na njia aliyotumia kwa kweli nilijikuta siwezi kuuruka mtego wake mwepesi. Sikuwa ndege mjanja lakini nilinaswa kijinga sana, japo sikujua tatizo langu lakini nilipokuwa natembea na kumuachia umbile la nyuma lililokuwa linawatesa wanaume wengi. Niliinama makusudi kama najikuna mguu ili tu nizidi kumpagawisha.

Kitu kilichofanya Mateja azidi kuwa katika wakati mgumu, wakati nafungua kabati nitoe taulo Mateja alikuwa tayari yupo nyuma yangu na kunikumbatia kwa nyuma. Nilijua uzalendo ulikuwa umemshinda, mambo yalianzia pale.

Tulianza kubadilishana mate palepale kwenye kabati, baada ya muda aliona anachelewa, mwanaume alinibeba juujuu mpaka kitandani. Kwa vile mchicha ulikuwa umeishakolea nazi tuliumwaga juu ya ubwabwa na kuanza kujimegea tataribu. Mateja alionekana ana pupa kama mamba mwenye njaa, hakuchelewa kukifikisha chombo ukingoni mwa bahari.

Baada ya mapumziko mafupi tulirudi ndani ya ngarawa kuendelea na safari, katika vitu ambavyo katika maisha yangu nilikuwa sivipendi ni usumbufu ndani safari. Ooh geuka hivi, lala hivi, inama hivi, nyanyuka hivi, kwa upande wangu niliona usumbufu lakini nilivumilia kwa vile ndiyo ilikuwa siku yetu ya kwanza kukutana.

Kama ningekuwa nimemzoea ningempasha, kwani hakuna starehe ya mapenzi mpaka kusumbuana kumgeuza mwenzako kituko,ile kwangu sikuona mapenzi zaidi ya adhabu. Siku zote niliamini baada ya safari ndefu mtu humwaga mzigo na kutelemka. Siku ile tulikaa kaa mpaka saa tatu usiku baada ya kuoga na kula alinirudisha nyumbani.

Kabla ya kuondoka Mateja aliniahidi vitu vingi ikiwemo kunijengea nyumba kuninunulia gari na kuyabadili maisha yangu kwa ujumla. Siku ile moja tu alinipatia laki tano taslimu, sikuamini niliona miujiza kupata raha na kiasi kikubwa cha pesa kama kile.

Nilipofika nyumbani nilimkuta Bi Shuu yupo chumbani kwake, Nilifungua mlango wa chumba changu na kuingia ndani. Nilipowasha taa nilishtuka kumuona Bi Shuu kanisimamia nyuma, akuzungumza chochote ila alinikata jicho kali.

“Shikamoo Bi Shuu”

“Hainisaidii kitu”

“Mbona hivyo mama yangu”

“Kazi gani ya kutoka saa moja asubuhi kurudi saa tano za usiku?”

Mmh, makubwa nimekuwa mtoto mdogo wa kuwa chini yake kwa kila kitu. Nilijua uchawi wa Bi Shuu ni nini, niliinama na kuchukua mkoba wangu na kufungua. Nilihesa nyekundu tano na kumpa.

“Za nini?”

“Katumie tu”

“Za kodi?”

“Walaa, nimekutunuku tu mama yangu.”

“Kweli!?”

“Kweli unafili uliyonifikiza madogo”

Bi Shuu alifurahi na kunikumbatia na kusahau aliyobwatuka muda mfupi, baada ya kunipandisha na kunishusha alisema.

“Weee mwana kulikoni”

“Kaa chini nikupashe kazi imekuwa kaziiiii”

“Usiniambie”
 ITAENDELEA SIKU YA KESHOOOOOOOOO

No comments

Powered by Blogger.