DALLAS: WOLPER ‘PLIZ’ TURUDIANE TU!
Sexy lady wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe.
Yule zilipendwa wa sexy lady wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper
Massawe aitwaye Ramadhan Abdallah Mtoro ‘Dallas’ anadaiwa kukumbuka
shuka kukiwa kumeshakucha ikielezwa kwamba eti anabembeleza kurudiana na
staa huyo waliyetengana takriban mwaka mmoja uliopita ili wakamilishe
taratibu za kufunga pingu za masha.
Akizungumza na Amani hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Lango la Jiji uliopo Magomeni, Dar, Dallas alisema kuwa anamshangaa Wolper kumkatalia ombi lake la kurudisha uhusiano wao wa kimapenzi huku akijua fika kuwa bado anampenda. “Nampenda sana Wolper. Pliz namuomba turudiane tu.
Ningejua kipindi kile nilivyorudi kutoka nje ningefunga naye ndoa kwani sasa hivi angekuwa ni mke wangu niliyechaguliwa na Mungu lakini ndiyo hataki,” alisema Dallas. Kwa upande wa Wolper alisema kuwa Dallas kwa sasa ni mshikaji wake tu na atabaki kuwa hivyo lakini kuhusiana na mapenzi, hakuna kitu kama hicho.

Post a Comment