BATULI, MTUNISI SI WAPENZI TENA!
WAMEMALIZANA! YOBNESH Yusuph ‘Batuli’ anayekimbiza
kunako soko la Bongo Movies, amefunguka kuwa hataki kusikia habari za
aliyekuwa mpenzi wake aliye pia msanii mwenzake, Mtunisi kwani mapenzi
yalishaisha.
Staa anayekimbiza kunako soko la Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli akipozi.
Akistorisha na paparazi wetu, Batuli alisema hataki kumsikia wala
kujua habari za Mtunisi kwani mapenzi yalikuwa zamani lakini kwa sasa
kila mtu ana maisha yake yaani yeye Mtunisi ana mke na yeye ana mpenzi
wake.
“Mimi kwa sasa nina maisha yangu na Mtunisi ana maisha yake
nawashangaa wanaoniandama kwa maneno kwamba bado niko naye, jamani
Mtunisi ana mke na mimi nina mpenzi hivyo sitaki kusikia habari hizo
kabisa,” alisema Batuli.
Post a Comment