ad

ad

AMOS MAKALLA AFIWA NA BABAYAKE MZAZI


Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla.
Naibu Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla anasikitika kutangaza kifo cha babake mzazi, Gabriel Makalla kilichotokea usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa waziri Palm Residence Ocean Road namba 18E Dar es Salaam, Mwili utaagwa Jumapili katika Kanisa la Azania Front saa 6 mchana.
Marehemu Gabriel Makalla
Baada ya hapo mwili utasafirishwa kwenda Mvomero kwa mazishi yatakayofanyika Jumatatu saa 7 mchana. Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi,  amina.

No comments

Powered by Blogger.