Usajili wa Kisiga Simba waweka rekodi Msimbazi
NDAPO
Simba itampa mkataba kiungo wao wa zamani, Shaban Kisiga basi atakuwa
ni mchezaji maarufu na mzoefu aliyeweka rekodi ya kusajiliwa kwa bei
chee zaidi Msimbazi katika usajili wa msimu ujao.
Achana na wachezaji wadogo waliopandishwa kwenye timu ya vijana ya Simba ambao wamepewa dau la kishkaji kwavile ndio wanakua.
Friends of Simba ambao wako karibu sana na kamati ya usajili wameamua kwa pamoja kwamba Kisiga ada yake isizidi Sh4 milioni na mshahara akiambulia Sh800,000 kwa mwezi. Wameamua huo mzigo ndio unamtosha na asiongezewe.
Huo huenda ukawa usajili utakaotia fora kwani atakuwa ni mchezaji wa kwanza mzoefu kwenye ligi kusajiliwa kwa ada ndogo katika usajili wa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
“Ni mmoja wa wachezaji waliopendekezwa kusajiliwa lakini bado hakubaliki na wengi kutokana na kiwango chake, hata kama atasajiliwa basi kiwango chake cha kumpa ni hakitazidi Sh 4 milioni ama chini ya hapo ambacho ni kama ada yake ya usajili,” alisema kigogo huyo mwenye ushawishi mkubwa kwenye usajili wa Simba.

Hata hivyo bado mazungumzo ya kumalizana naye
yanaendelea kwa mchezaji huyo ambaye msimu uliopita aliichezea Mtibwa
Sugar lakini waliamua kuachana naye baada ya kushuka kwa kiwango chake.
Wajumbe wa Kamati ya Usajili iliyo chini ya
Mwenyekiti Zacharia Hanspoppe na Makamu wake, Kassim Dewji bado
hawajafikia mwafaka juu ya mchezaji huyo mzoefu. Habari kutoka kwa mmoja
wa viongozi wa Simba zilieleza kwamba bado kuna utata juu ya mchezaji
huyo kwani baadhi ya
wajumbe wanamkubali huku wengine wakipinga usajili wa kiungo huyo.

Post a Comment