ad

ad

TOROJO BAMIA (Winga teleza) - 10

“Lily wewe tu, tulia ule raha.”
“Yaani yule mchovu anikome tena anikome.”
“Wewe mwenyewe kuamua kuishi Masaki au Tandale kwa Mtogole.”
“Baby sihami Masaki hapa nimefika sihami tena.”
Lily alinyanyuka na kwenda kutoa nguo mwililini ili aweze kujitawala zaidi. Alipofika kwenye kabati  alitoa nguo zote na kubakia na bikini iliyoupendezesha mwili wake na kuelekea alipokuwa amekaa Shuku ambaye macho yalikuwa yamemtoka kama mjusi kabanwa na mlango asiamini na yeye kwa mara ya kwanza anakula mtoto wa viwango.
Shuku alijikuta akijisemea kwa sauti ya chini:
“Kweli fedha mwana haramu, leo Shuku nakula mtoto wa kiwango.”
“Baby vipi mbona unanishangaa?”
“Sikushangai bali penati nilitopiga lilikuwa bonge la penati kama la Pirlo.”
“Baby kumbe na wewe unacheza mpira?”
“Siyo penati ya uwanjani.”
“Sasa penati gani tena hiyo?”
“Si kukuchagua wewe.”
“Jamani baby kumbe hivyo?”
“Lily wewe bonge la demu.”
“Asante mpenzi.”
Wakati huo Lily alikuwa amefika kwa Shuku na kuanza kumpembua kimoja baada ya kingine kisha alimshika mkono hadi bafuni. Lily alikuwa mzoefu kuingia sehemu kama zile japo hakuwahi kuingia hoteli yenye hadhi ya juu kama ile.
Kama ingekuwa amemuachia kila kitu afanye Shuku angeumbuka, alizoea vigesti vya vichochoroni vya buku mbili au kumbambia changudoa kichochoroni na kumalizana juu kwa juu, lakini anga kama zile hakuota kuingia na kama ingekuwa fedha yake basi angempeleka demu kwenye hoteli isiyo kuwa na gharama kama ile.
Baada ya kuingia bafuni waliingia kwenye jakuzi na kujimwagia maji huku Lily akionesha utundu wake asionekane hayupo nyuma  kila kitu alikifanya yeye ili Shuku ajue na yeye mambo kama yale si mageni kwake. Kufanya ile kulimpa nafasi Shuku ambaye pia alikuwa mgeni wa vitu vile kujifunza kupitia kwa Lily  kwa haraka ili siku ya pili asiwe mgeni tena. Baada ya utundu wa Lily aliomfanya Shuku apasue yai mdomoni huku akigugumia kama dume la njiwa.
Kwa mara ya kwanza alijikuta akipata raha mwanzo mwisho alizokuwa akiziona kwenye kioo. Naye aliapa kuonesha yeye nani ndani pichi. Baada ya kumaliza kuoga walirudi kitandani huku Lily akionekana kupandwa na mahanjamu kila jicho lake lilipotua kwenye muhogo wa Shuku mwili ulimsisimka.
“Baby muhogo unanisisimua nipe niugegede mwenzio mate yananidondoka.”
Shuku alikuna nazi na kuchemsha maji baada ya tui kuchemka alitia mchele na kumfanya mtoto wa kike kutatalika kama makalio yanaumwa na siafu kwa kukipandisha juu kiuno na kuiacha nyonga ukate mawimbi huku Shuku akitandaza soka maridadi iliyowafanya wapenzi walipuke mayowe muda wote kwa pasi za uhakika za Shuku ambazo zilimfikia mlengwa na kumfanya Lily aonesha umahiri wa wepesi wa nyonga yake kuiwahi mipira yote iliyopigwa na Shuku na kuufanya mchezo uwe wa ufundi zaidi kuliko nguvu.
Lily alikuwa wa kwanza kugeuka golini kuokota mpira baada ya gonga safi za hapa na pale zilizompelekea kusogea mbele ya goli na Shuku kuuchopu mpira uliomfanya anyooshe mbavu bila mafanikio ya kuugusa mpira, goli lile lilimfanya amsifie mfungaji kwa goli tamu alilofungwa na shuku kwa kumng’ang’ania kwa nguvu kuliacha dafu limwage maji baada ya kupasuka.
“Be..be..be....beeeee,” Lily alipagawa baada ya siku za nyuma kuchezewa na teja kwa muda mrefu lakini siku ile alikutana na mwanaume wa shoka mwenye kuijua kazi yake uwanjani. Aliitafuna midomo kama kamwagiwa kopo la asali.
“Niite Shuku baby,” Shuku alimwambia huku akimpa uhuru Lily alifuahie utamu wa maji ya dafu yaliyokuwa yakimwagika kwa kumng’ang’ania shingoni.
“Shuku...Umeniweza...siamini ...siamini.. Shuku kumbe nilikosa raha hizi jamani, ulikuwa wapi Shuku? Mungu kakupendelea kila kitu mbona nitafaidi Lily mimi.”
Baada ya kutulia Shuku naye alianza kulitafuta bao la kusawazisha kwa kutumia mashuti ya mbali ambayo kwa mara nyingine yalimpeleka Lily marketi kwa kuvunja yai la pili baada ya kuangukia banda la kuku.
“Shu..shu ..ku we..we..we..kiboko haki ya na..nani lingine hi.. hi..hiloooo.”
Lily alisema kwa sauti ya kudeka safari hii Shuku akufanya fair play alianzisha mpira mara moja kwani naye alianza kuiona pwani hivyo hakutaka kushusha stimu iliyokuwa inapanda kama sumu ya nyoka.
Baada ya kuwatoroka  mabeki na kuukuta mpira ambao Lily aliamini ni off side, mwanaume aliingia nao kwa kasi huku akimfungasha tela Lily aliyekwenda kumkatia ndani ya wavu kiliwa bao moja la Shuku huku Lily naye akipasua yai la tatu.
Wote walitulia kama mkwezi mwizi aliyedondoka kwenye mnazi na kufikia kiuno na kumfanya atulie hata kama mwenye mnazi angetokea asingeweza kumkimbia. Walitulia kwa muda kama wamepakwa nta kwa muda.
Baada ya kila mtu dafu lake kukata maji, alimuachia mwenzake na kujilaza pembeni ya mwenzake. Moyoni bado Shuku aliona kama yupo ndotoni kulala hoteli ya gharama na mtoto mzuri tena mwenye kuijua kazi yake. Lily naye aliamini baada ya kuhangaika sana pale alikuwa amefika mwisho wa reli aliuapia moyo wake atampa mwili wake mwanaume mwingine zaidi ya shuku.
Siku ile waliimalizia pale mpaka siku ya pili Shuku alimrudisha Lilly nyumbani kwao, walipofika Shuku alifungua gari kwa juu na kutoka nje na kwenda kukaa mbele ya gari ili aagane na mpenzi wake.
“Kwa hiyo bebi?” Lilly aliuliza.
“Tutaonana jioni.”
“Si utanifuata?”
“Wewe ulitakaje?”
“Nataka unifuate bebi.”
“Hakuna tatizo.”
“Bebi katika maisha yangu sijawahi kuinjoi kama jana.”
“Huo ni mwanzo tu bebi.”
“Kwa nini usinioe kabisa.”
“Ni haraka sana.”
“Basi bebi utakuwa na mwanamke mwingine zaidi yangu.”
“Sina mwanamke mwingine bebi bahati hiyo umekuangukia wewe tu.”
“Mmh! Bebi basi nioe nijue unayosema ni kweli.”
“Bebi bado hujaniakikishia nipo peke yangu kwa vile nimekukuta na mtu.”
“Nakuapia yule mshenzi hapa atapaona kama kituo cha polisi na muuza bangi.”
“Ni mapema sana, bebi si ndiyo tumeanza haraka ya nini?”
“Bebi nina hamu ya kuolewa na wewe.”
“Nimekusikia, basi jioni kodi gari uje home.”
“Si umekubali nitanifuata imekuwaje tena, bebi hunipendi.”
“Nakupenda mpaka nasikia maumivu.”
“Sasa kwa nini usinifuate, bebi unajua mtaa huu wanajifanya wanajua sana ukinifuata wataniheshimu.”
“Mbona mtaa wenyewe haupo kivilee?”
“Kuna vicheche fulani wana waume zao wenye nazo, hivyo basi huja na vigari vyao kutukonga.”
“Wanazo kunishinda mimi?”
“Hawakufikii lakini lazima wajue mimi ni matawi  ya juu.”
“Wana gari kama hili?”
“Noo, wana Prado za milioni 75.”
“Basi bebi jioni nitawafunika wote.”
“Kweli bebi?”
“Sasa chagua nije na gari la milioni mia moja au mia mbili.”
“Bebi la mia mbili ili wakome kabisa.”
“Basi poa, nataka wajue wewe si mtu wa kuchezea pia nataka niivunje nyumba yenu na kujenda bonge la bangaruu simulizi la kitaa.”
“Bebi nijengee yangu ile nyumba ya familia watanidhurumu.”
“Basi nitakujengea Masaki unasemaje?”
“Yaani nitafurahi ile mbaya.”
“Na gari la milioni mia moja.”
“Jamani bebi yaani nakuahidi hata yule Mpemba aliyeniahidi kuninunulia Lav4 nampiga chini.”
“La4 nini bwana zile gari za wanafunzi.”
“Umeona eeeh!”
“Basi bebi jiite mwanamke mwenye bahati.”
“Hata mimi naona, ndiyo maana siku ile nilikupa namba yangu bila kukuhoji kwa vile nilijua nimelamba dume.”
“Baadaye basi.”
“Pouwa bebi.”
Shuku naye alijifanya kauzu japo hakuzoea alidendeka na Lilly mbele za watu. Baada ya kuachiana Lilly alikimbilia kwao akiwa amevimba kichwa na kujiona ana bahati kuliko kiumbe chochote cha kike.
Shuku alirudi kwenye gari lake na kupiga honi kabla hajaondoka kitu kilichomfanya Lilly ageuke nyuma, alibusu kwa kulipeperusha busu, naye Lilly alilipokea. Kisha aliwasha gari na kuondoka kwa kasi huku akitimua vumbi.
Shuku alikuwa bado haamini kilichotokea kumpata mtoto mzuri kulala hoteli ya bei mbaya. Moyoni aliomba aikute Vogue lipo nyumbani ili akazidi kumkonga Lilly na kuwatesa wavimba macho wote.
Alipofika nyumbani alimkuta MJ akitoka kuoga akiwa ameongozana na msichana mwingine mkali.
“Vipi mzee?” MJ alimuuliza Shuku.
“Poa tu mkubwa.”
“Ndo unarudi nini?”
“Wee acha.”
“Kwa nini?”
“Wakubwa unafaidi, mambo niliyokutanana nayo sikuyategemea, bila umatemate huwezi kula raha kama zile.”
“Vipi mtoto?”
“Yuko bomba kila idara.”
“Mbona hukuja naye?”
“Jioni, nimempitisha kwao abadili nguo, nitamfuata baadaye.”
“Kwa nini hukumpitisha kwenye maduka ya nguo mkabadili, au mkwanja umekwisha?”
“Bado upo mwingi tu.”
“Mlikwenda wapi?”
“Sijui.. hoteli ya Serena.”
“Usiniambie!”
“Wee acha wakubwa wacha mfaidi.”
“Umelala chumba cha shilingi ngapi?”
“VIP.”
“Weweee.”
“Si umeniambia nitumie niwezavyo.”
“Mtoto kasemaje?”
“Mambo niliyomfanyia kachanganyikiwa, mara ooh nioe si mtaki mwanaume mwingine.”
“Ndoa noma, ukioa dunia itakucheka.”
“Kwa nini?”
“Watoto wazuri kama hawa utamuachia nani?”
“Lakini mimi bado siwazi mwingine zaidi ya Lilly.”
“Demu wako anaitwa Lilly?”
“Ndo maana yake.”
“Basi mzee kazi kwako mi nabadili nguo natoka mara moja kuna mzigo umeingia.”
“Poa,” Shuku alipotaka kuondoka alikumbuka kitu.
“MJ nimekumbuka kitu.”
“Kitu gani?”
“Vipi Vogue utatumia leo?”
”Hapana, nitatumia hummer”
“Mmh! Hummer na Vogue lipi la bei mbaya?”
“Chezea Hummer wewe?”
“Basi mimi nilijua Vogue ndiyo matawi.”
“Imechelewa kujua.”
“Basi leo nitamfuata mtoto na Vogue siku nyingine nitafunga kazi kwa hummer.”
“Wewe tu.”
Shuku kwa vile alikuwa amechoka baada ya kushindana na kilichowashinda wahenga na wahenguzi kinyama cha hamu kisichoisha hamu, alikwenda kulala na kumuacha MJ akijiandaa kutoka na mtoto mzuri.
                                               ****
Majira ya saa kumi na moja jioni Shuku aliamka kitandani na kwenda kuoga tayari kumfuata Lily Temeke. Baada ya kutimba pamba kali, alitoka nje na kwenda kuchukua Vogue kwa ajili ya kwenda kumkonga mpenzi wake na wavimba macho wa mtaa ule.
Wakati akitoka alikutana na MJ akiingia, ilibidi asubiri kwanza aingie swahibu wake ndipo naye atoke. Baada ya MJ kuingiza gari ndani aliteremka na demu mwingine mkali kuliko aliyelala naye.
“Vipi mzee hujatoka?” MJ alimuuliza Shuku.
“Ndo natoka nimelala sana.”
“Poa utanikuta, huyu ni shemeji yako Angel,” MJ alimtambulisha demu wake.
“Ooh! Nimefurahi, mambo shemu?” Shuku alimsalimia kwa kumpa mkono.
“Poa, mbona wageni tunakuja wenyeji mnaondoka?” Angel alionekana mcheshi.
“Narudi sasa hivi.”
“Mmh! Sijui kama atanikuta.”
“Acha hizo, mbona hata nusu saa haichukui nitakuwa nimerudi.”
“Haya baba umeshinda, niletee zawadi tu.”
“Umepata, zawadi gani?”
“Yoyote itakayo ona inalingana na hadhi ya shemeji yako,” Angel alisema huku akijishebedua.
Shuku aliingia kwenye gari lake na kuondoka kumuwahi Lily ambaye aliamini ana kimuhemuhe cha kumsubiri kwa hamu. Akiwa njiani alijikuta akijiuliza ubadilishaji wa MJ watoto wazuri, alijiuliza watoto wakali kama wale anawatoa wapi. Kilichomshangaza toka afike hakukuwa na msichana aliyejirudia.
Alijiuliza hizo nguvu ya kugawa dozi kila kukicha anazitoa wapi. Lakini kwake pamoja na kuwaona wanawake wazuri pengine kumzidi hata Lily, lakini kwake Lily penzi lake lilikuwa limefika mwisho kama reli iliyogota Kigoma.
Alipofika maeneo Temeke Mikoroshini alikutana na lile gari lililotumiwa na mjanja wa Lily. Alishtuka na kutupa macho ndani ya gari labda Lily kaondoka, lakini ndani alikuwepo msela peke yake.
Alijiuliza imekuwaje huko baada ya msela kurudi peke yake, alipofika alisimamisha gari kwa makeke na kumpigia honi Lily. Alimuona Lily akichungulia na kurudi ndani alishindwa kumuelewa. Alipiga tena honi lakini safari ile hakutoka kabisa.
Aliamua kutoka nje ili Lily amuone, baada ya kusimama mbele ya gari Lily alitoka mbio na kwenda kijitupa kifuani kwa Shuku na kuanza kulia.
“Vipi bebi?”

: Utamu ndio kwanza unazidi kukolea. Bado sehemu kibao kuweza kuisha chombezo hili la aina yake . Kamwe usithubutu kusimuliwa hii simulizi ingia ujisomee mwenyewe hapa hapa uwanja wa simulizi pekee.


” ITAENDELEA KESHO HAPAHAPA

KAMA ULIKOSA SEHEMU ZA NYUMA SOMAHAPA
SOMA SEHEU YA KWANZA >>>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-01.html
SEHEMU YA 2: ==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-02.html
SEHEMU YA 3:==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-03.html
SEHEMU YA 4:==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-04.html
SEHEMU YA 5==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-05.html
SEHEMU YA 6: ==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-06.html
SEHEMU YA 7==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-07.htm
SEHEMU YA 8==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-08.html
SEHEMU YA 9==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-09.html

:: SHARE nyingi na COMMENT bila kusahau LIKE ndizo zinafanya Chombezo hili kuwa likitoka kila siku na kwa muda muafaka hapa www.facebook.com/2jiachie pekee. Hakika si ya kukosa hii.

Wanaotakiwa kusoma chombezo hili ni kuanzia +18 tu!
Hairuhusiwi kunakili. Au kutoa hata neno kuhamishia kwenye kitabu,tamthiliya ama wall ya facebook,twitter,whatsapp na sehemu nyingine pasipo idhini ya 2JIAHIE utashitakiwa!!.

No comments

Powered by Blogger.