SURPRISE YA AIBU - 03
Nilijipaka dawa yangu tena kwenye nyonyo na kutoka bila kitu mwilini na kwenda chumba cha mzungu mwingine aliyekuwa akinisubiri kwa hamu sana.
Kama kawaida baada ya kupanda kitandani nilimuomba anyonye matiti na yeye alinyonya baada ya muda alilegea na kummaliza kama mwenzake.
Kumbe wakati nammalizia yule mzungu wa pili mzungu wa tatu sijui alishtukia vipi nilimuona akija huku akimwita mwenzake kwa sauti ya juu.
“Mr Rich kuwamakini Mr Rich kuwa makini.”
Kwa haraka niliteremka kitandani na kujificha nyuma ya mlango, aliingia na bastora mkononi akili yake ikiwa kwa mwenzake ambaye nilikuwa nimeisha msafirisha kuzimu. Nilijua nimekufa kwa vile sikuwa na ujanja wowote wa kujiokoa kwa mzungu yule aliyekuwa na siraha mkono pili hata mwili wake kama angenikamata basi ningefia mkononi kwake.
Nikiwa natetemeka mpaka haja ndogo ilinitoka baada ya kuona akimpima mwenzake mapigo ya moyo. Niliona ile ndiyo nafasi yangu ya kutoka mbio, nilikurupuka nyuma ya mlango na yeye alimuacha mwenzake na kunifuata. Kwa vile nilijua mlango umefungwa nilijitahidi kuufunga ule mlango ili nimfungie ndani. Wakati huo yule mzungu alikuwa akija mbio, nilifanikiwa kuufunga ule mlango na kumfanya ajigonge mlangoni na kuanguka chini.
Alianguka kwa kishindo, nilifunga mlango kwa komeo kwa nje kisha nilichungulia ndani na kumuona amelala chini damu zikimtoka kichwani. Nilikwenda mpaka jikoni na kufanikiwa kupata kisu kikubwa ambacho nilirudi nacho na kuufungua mlango wakati huo roho ya damu ilinijaa.
Nilimfuata chini alipolala huku nikiwa na hasira niliteremsha mapigo mfurulizo ya kifuani mpaka alipotulia. Nilinyanyuka na kujifuta damu kisha nilivaa nguo zangu. Nilianza kupekua kila kona na kufanikiwa kupata dola laki nne, nilizifunga vizuri kisha nilichukua bastora hadi kwenye banda la mbwa na kuwaua mbwa wote na kwenda kwenye moja la gari lao na kutoka nalo.
Mlinzi alipoangalia ndani ya gari na kuniona mimi alishtuka na kunihoji:
“Vipi mbona unatoka na gari?”
“Siyo juu yako fungua geti,” nilimjibu kwa sauti ya ukali.
“Kazi yangu ni ulinzi nina haki ya kuuliza,” mlinzi naye alikuwa mbishi.
“Sikiliza we kidampa hebu fungua geti kabla sijakupoteza!” nilimtisha afungue mlango.
“Siwezi mpaka nipate ruhusa ya mabosi wangu.”
Niliona kama ananichelesha nilichukua bastora iliyokuwa pembeni yangu na kumshuti. Niliteremka haraka na kwenda kufungua geti kisha nilirudi kwenye gari na kuliondoa kwa kasi.
Nilitembea huku moyo wangu ukiwa na hasira ya kunywa damu ya mtu.Nilikwenda na gari hadi mjini ambako nililiacha njiani na kuchukua teksi iliyonipeleka nyumbani. Kwa wasiwasi wa kukamatwa sikutoka ndani kwa siku tatu huku nikisikiliza taarifa kwenye vyombo vya habari ambavyo vililipoti vifo vya wazungu watatu na mlinzi wao waliouawa kinyama na mtu asiyejulikana.
Nilitulia kwa muda wa mwezi mzima nikiwa mtu wa kujificha ikiwemo kuhama nilipokuwa nakaa na kuhamia nje ya mji. Baada ya hali kutulia nilianza msako wa mkuu wa polisi na hakimu. Nilifuatilia nyendo zao na kujua kila mmoja anakunywa wapi.
Pia niliona kuwapata siyo kazi kutokana na tabia zao za unywaji na kupenda wanawake. Niliona nianze na hakimu kwa kujua polisi msako wake ni mkubwa kuliko wa hakimu. Hakimu alikuwa akikaa maeneo ya Mikocheni na alikuwa akipenda kunywa kwenye baa moja maarufu iliyopo Kinondoni.
Niliamua kumfuatilia nyendo zake ambazo nilizielewa, siku moja nilimkuta kwenye baa hiyo akiwa amekaa peke yake akinywa bia yake huku akichati na simu. Kwa vile nilikuwa nimevaa kiutata niliamini kila mwanaume alitamani kuwa na mimi. Nilisogelea meza yake na kumsalimia:
“Habari za saizi?”
Kabla ya kuitikia alinyanyua uso na kunitazama kisha alishusha pumzi ndefu na kusema:
“Ooh! Sorry, karibu mrembo.”
“Hapana nakusalimia,” nililegeza sauti.
“Ooh! Nzuri mrembo karibu.”
“Asante, vipi una mtu hapa?”
“Nipo peke yangu karibu mtoto mzuri.”
Nilikaa na kujifanya natoa simu kwenye mkoba na kujifanya nasoma kitu kumbe ilikuwa kumlia pozi.
“Mmh! Binti unatumia kinywaji gani? Aliniuliza baada ya uhudumu kuja kusimama mbele ya meza yetu.
“Heinken.”
“Na nini mrembo?”
“Kwanza hiyo inatosha kuanzia mi si mnywaji sana.”
Baada ya vinywaji kuletwa nilitulia na kunywa kistaarabu, kitu kilichomfanya hakimu kutaka kunijua zaidi.
“We ni mgeni?”
“Si sana.”
“Mwenyeji wa wapi?”
“Arusha.”
“Ooh! Nimefurahi kuwa na wewe nina imani leo tutakuwa pamoja.”
“Mmh! Na mkeo?” nilijifanya kulia wivu.
“Mke wangu nikirudi kwangu, sasa hivi mimi nipo na wewe mtoto mzuri.”
“Mmh! Kama hivyo basi wewe tu,” nilijifanya kulegea.
Baada ya chakula tulikubaliana kwenda nyumba ya wageni si kwa kulala kwa mapenzi ya muda mfupi kwa kisingizio nipo kwa baba yangu mdogo siruhusiwi kulala nje. Tulitoka pamoja kwenye gari lake na kuingia, nilipata wazo la haraka la kumuulia ndani ya gari ili kufuta ushahidi.
Baada ya kutoka eneo la baa niliacha gari liende mbele kidogo na kumuomba alisimamishe pembeni.
“Kuna nini sweet?”
“Nina hamu mpenzi naomba uninyonye matiti kidogo uzipunguze.”
“Vumilia nitazishusha sasa hivi.”
“Hapana ninyonye,” nilisema huku nikizitoa matiti yangu ambazo yalimbabaisha na kukubali kupaki gari pembeni na kuanza kuyanyonya matiti yangu. Japokuwa alinipandisha mzuka lakini lengo langu lilikuwa roho yake.
Aliendelea kulinyonya kwa ufundi mkubwa sana mpaka nikajikuta namaliza haja zangu bila kupenda, lakini lengo langu kwa siku ile halikuwa hilo zaidi ya roho yake. Baada ya kunyonya kwa muda nilimuona akianza kulegea na kuliachia ziwa kisha alijilaza pembeni.
Nilimtikisa na kugundua amelegea nilichukua mto ndogo ndani ya gari na kumziba nao usoni kwa kumkandamiza kwa nguvu. Kwa vile hakuwa na nguvu hakuweza kunizuia nilimbana mpaka alipopoteza uhai nilimlaza pembeni na kuteremka zangu kwenye gari, nilifunga mlango na kuondoka zangu.
Nilitembea haraka mpaka mbele na kukodi bodaboda mpaka Magomeni ambako nilikodi teksi mpaka nyumbani. Nilitulia ndani sikilizia kwenye vyombo vya habari vitaripoti vipi kifo kile. Taarifa ya asubuhi kwenye radio zote zilielezea Hakimu Kiondo alivyokutwa amekufa kwenye gari lake.
Vyanzo vya habari vilisema alionekana ameongozana na mwanamke mmoja mrembo na kwenda kwenye gari lake na baadaye gari lake kuonekana hatua chache na baa aliyokuwa akinywa.
Polisi walisema wanamsaka mwanamke aliyetoka naye japo ilikuwa vigumu kunigundua kwa vile hakuna hata mmoja aliyekuwa akinifahamu pia alikuwa mgeni maeneo yale. Baada kufanikisha kifo cha Hakimu nilitulia kwa miezi mingine miwili kujipanga kwa ajili ya kummaliza mkuu ya kituo ambaye wakati huo alikuwa OCD katika wilaya moja mkoani Morogoro.
Mwanamke baada ya kujipanga nilifunga safari mpaka Morogoro na kupanga kwenye hoteli moja yenye hadhi mkoni Morogoro. Nilianza kumfuatilia OCD Mzizire kwa siku tatu na kugundua bado wana tabia zilezile za kunywa kwenye baa kubwa pia kupenda watoto wazuri.
Baada ya kujua baa anayokunywa nilikwenda siku moja kwenye ile baa na kutafuta siti ya karibu na alipokuwa amekaa na wapambe wake wakinywa. Nilimwita mhudumu.
“Habari dada.”
“Nzuri, karibu.”
“Asante, samahani dada yangu.”
“Bila samahani.”
”Eti mzee Mzizire anakunywa kinywaji gani?”
“Serengeti.”
“Na wenzake?”
“Kuna anayetumia ndovu, konyagi na Tusker.”
“Kila mmoja mpe tatutatu mwambie mzee Mzizire ofa yangu kwake.”
“Sawa.”
“Shilingi ngapi?”
“Usiwe na wasi nitakwambia baada ya kuhudumia, wewe je, huagizi?”
“Mi niletee Heinken moja.”
“Baridi, moto?”
“Moto hali ya hapa ni baridi.”
“Dada barudi ipo wapi wewe mgeni?”
“Si sana.”
Yule msichana aliondoka na kunifanya niendelee kumtazama kwa uchu mzee Mzizire, kila nilipokumbuka alivyonifanyia moyo uliniuma na sikutaka kumsamehe hata kidogo, kwa tabia zake za kuwakandamiza wanawake na kuwatetea wazungu waliowafanya vibaya wanawake kwa kuwafanyisha mapenzi na mbwa na mwisho wa siku wanafungwa wao bila kosa.
Baada ya muda nilimuona yule mhudumu akiweka tlei la vinywaji kwenye meza. Nilimuona akiuliza, mhudumu alinionesha mimi ambaye alimpokea kwa tabasamu kali. Niliwaona wote wakinishuku kwa kushika vifuani vyao nami nilijibu kwa kushika changu kuonesha nikubali.
Alipotoka pale aliniletea heinken yangu na kunifungulia na kutaka kuniwekea kwenye glasi, nilimkataza na kujiwekea mwenyewe na kupiga funda moja na kutulia. Nilifanya kuangalia chini ili niwape nafasi ya kuusanifu uzuri wangu ambao ulinifanya nijiamini muda wote.
Siku zote huwa naamini wakubwa ndiyo wanapenda kujipendelea kizuri lazima wakitake wao. Baada ya muda yule dada alikuja na bei nne na kutaka kuziweka juu ya meza yangu.
“Vipi dada?” nilimuuliza.
”Mzee amesema nikuhudumia nikupe chochote unachokitaka.”
“Mwambie asante, leo sijisikii kunywa sana, sina uhakika hata kama bia hii moja nitamaliza.”
“Dada si ungechukua hata kama hunywi ungenipa mimi mdogo wako.”
“Usiwe na wasiwasi we rudisha nitakupa elfu kumi ya matumizi unasemaje?”
“Duh! Dada yangu utaokoa maana leo hali ni mbaya.”
Nilifungua mkoba wangu na kuchukua noti ya elfu kumi na kumpa.
“Hii ya nini?”
“Yako.”
“Na bili?”
“Hujaniambia kiasi gani pia hujawaongezea bia nyingine.”
“Kwa hiyo niwaambiaje kuhusu bia hizi?”
“Mwambie kama nilivyokwambia kuwa sijisikii kunywa bia leo, labda kesho nitaungana nao.”
“Haya dada, asante sana.”
Yule mhudumu aliondoka na kuniacha nikiibembeleza bia yangu ambayo niliiweka kuzugia tu kwa siku ile sikuwa mnywaji kabisa zaidi ya kumtamani Mr Mzizire kama Simba mwenye njaa aliyemuona Swali akinywa maji pembeni yake.
Baada ya muda yule mhudumu alinifuata na kuniletea kimemo toka kwa Mr Mzizire.
Sorry mrembo tunaweza kuwa pamoja leo?
Baada ya kukisoma nilitabasamu kumfanya aliyeleta ujumbe ambaye nilijua alikuwa akinifuatilia kujua nitaupokeaje. Tabasamu langu lilikuwa la kwanza kumpa matumaini.
Baada ya kusoma nilimuomba kalamu mhudumu na kunipa na kugeuza kalatasi kwa nyuma na kuandika.
Kwa leo au kwa siku zote?
Nilimpa mhudumu aliyempelekea baada ya kusoma naye aliandika kikalatasi kingine.
Nimekupenda sana nina imani itakuwa siku zote.
Nilipoletewa nilisoma na kumjibu.
Sawa, lakini sipendi kuchezewa na wanaume! Nilijifanya kutoa onyo.
Mhudumu alichukua ujumbe ule na kumpelekea baada ya kuusoma alijibu:
Nimekuelewa, naomba tuzungumze faragha.
Baada ya kuletewa niliusoma na kumjibu:
Hakuna tatizo.
Baada ya kupelekewa jibu langu, niliona akijadiliana na mpambe wake baada ya muda nilimuona yule mpambe akija nilipokuwa nimekaa na kuniinamia.
“Samahani naomba unifuate.”
“Sawa ngoja nilipe kwanza.”
“Hapana mzee atalipa.”
“Hapana, vinywaji hivi nimeagiza mimi.”
Baada ya kulipa nilitoka na yule mpambe aliyenipeleka mpaka kwenye hoteli moja iliyokuwa nje kidogo ya mji. Moyo wangu ulijawa furaha baada ya kuona mtego wangu umenasa kirahisi tofauti na nilivyofikiria. Jamaa baada ya kunifikisha chumbani aliniacha na kuondoka.
Baada ya kuondoka nilibakia chumbani peke yangu nikiwa katika wakati mgumu wa kutimiza nilicho dhamilia. Wasiwasi wangu ulikuwa kujulikana mimi ndiye muuaji hivyo kunifanya nishikwe mara moja na kukamatwa kabla sijafika mbali.
Nilijikuta nikiingiwa wasiwasi kuhusiana na mpango wangu kwa vile kama ningemuua basi ningekatatwa mara moja. Wazo la kumuua siku ile sikutaka kulitekeleza kwa vile mazingira yalikuwa tata kwa kujua wapambe wake hawakuwa mbali niliamini baada ya kuonekana natoka lazima watamfuatilia na wakimkuta amekufa msako wake ungekuwa mkubwa na mimi nisingefika mbali lazima wangenikamata.
Siku zote niliamini mpango mzuri ni kati yangu na adui yangu asiwepo wa tatu mwenye kujua mpango ule ambaye anaweza kuwa shahidi wa kuweza kunitia hatiani. Nilikubali siku ile nifanye mapenzi tu bila kuingiza kitu chochote huku nikiapa kujituma ili kumfanya aombe tukutane siku nyingine.
Nikiwa katika ya mawazo mkuu wa polisi wa wilaya OCD mzee Mzizire aliingia na kuja moja kwa moja nilipokuwa nimejilaza kwenye kochi.
“Niambie mpenzi wangu?”
“Mmh! Nakusikiliza wewe.”
“Mimi ninalo zaidi ya kuhitaji mapenzi yako.”
“Lakini kweli unanipenda au unanitamani?” nilijifanya kujibalaguza huku nimelegeza macho na sauti.
“Siyo siri mrembo, sijawahi kumpenda mtu kwa haraka hivi kama nilivyokupenda wewe.”
“Muongo! Unanidanganya unataka kunichelea tu leo kisha uniache,” nilijifanya kudeka.
“Kweli kabisa nakupenda kwa dhati wala si kukuchezea.”
“Kweli?”
“Kweli kabisa, unataka nikufanyie kitu gani uamini nakupenda?”
“Unipende tu wala sitaki kitu kingine.”
“Wewe ni mgeni hapa?”
“Ndiyo.”
“Unatokea wapi?”
“ Arusha.”
“Ooh! Vizuri na hapa Morogoro umefikia wapi?”
“Nipo katika mapumziko tu.”
“Unafanya kazi?”
“Ndiyo.”
“Ipi?”
“Kwenye kampuni ya utalii.”
“Upo likizo?”
“Ndiyo, leo ni siku ya tano, ila kesho nitakuwa Dar ambako nitakaa siku mbili na kwenda Zanzibar kidogo kisha nitaenda Mwanza na kurudi Arusha, kidogo nitakuwa nimeosha macho.”
“Duh! Inaonekama utalii imekukaa sana.”
“Upo ndani ya damu yangu.”
“Kwa nini usimalize likizo yako hapa ili tuwe pamoja, nitakupangia kwenye hoteli hii kwa muda wote utaokuwa hapa.”
“Asante, kwa vile nimeishapanga ratiba zangu, nitakutafutia nafasi yako hata ya kusema uongo kazini kuwa nauguliwa hivyo nitakuja unifiche unifaidi.”
“Basi ondoka kesho kutwa.”
“Hapana naomba kesho uniache niondoke, naweza kuacha kwenda Mwanza nikarudi kwako niache niende Dar na Zanzibar.”
“Mmh! Sawa.”
Baada ya kukubaliana tuliondoana nguo zetu kwa kupeana msaada kisha tulikwenda kuoga na kurudi kitandani ambako nilimpa raha kamili zilizomfanganya mzee wa watu. Kwa vile nilikuwa mzoefu wa kukutana na wanaume pia nilijua kuitaka hela ya mwanaume ambaye alikuwa akiitoa bila kusita hata tuliyokubaliana lazima uiongeze kwa penzi ninalompa.
“Mpenzi kwa nini kesho usihahirishe safari yako, kwa penzi unalonipa sijawahi kupewa sema unataka nikupe nini ili usiondoke.”
Nilitaka kumwambia naitaka roho yake, lakini ilibakia siri yangu ambayo niliijua mimi na Mungu wangu. Niliendelea kumpa vitu vipya mtoto wa kike huku nikikataa kila alichotaka kunipa kujifanya sina tamaa kumbe naitaka roho yake.
“Mpenzi sihitaji chochote bali penzi lako.”
“Penzi umepata, nakuahidi kukujengea nyumba na kukununulia gari hata kesho.”
“Nimekuelewa mpenzi wangu ila nina ombi moja kwako.”
“Ombi gani mpenzi wangu?”
“Kwa vile kesho nitakuwa Dar, naomba uje hata jioni tuwe pamoja, nimefurahia penzi lako naomba niwe nyumba yako ndogo,” nilizidi kumtia ujinga.
“Umeipata hata ukitaka nimfukuze mke wangu nipo radhi.”
“Hapana mkeo usimfukuze bali mimi nipo radhi kuwa nyumba ndogo lakini naomba uniheshimu tu.”
“Nakuhahidi kukuheshimu zaidi ya heshima hata ukitaka nikupikie na kukufulia.”
“Hapana sivyo hivyo nataka utambue mimi kuanzia leo ni mpenzi wako.”
“Jamani Bebi au nipige kelele kuonesha nimekubali.”
“Basi nimekuelewa lakini hajajibu ombi langu.”
“Lipi bebi?”
“La mimi na wewe kuwa kesho Dar.”
“Kumbe hilo, usiwe na wasi nakuahidi mpaka saa kumi na mbili jioni nitakuwa Dar, unataka tuwe hoteli gani?”
“Sea Cliff.”
“Hakuna tatizo mpenzi wangu.”
“Nimefurahi kusikia hivyo, naomba fedha ya hoteli nilipe mimi.”
“Naomba mpenzi wangu nilipe mimi.”
Sikutaka kulazimisha nilimkubalia na kunieleza asubuhi kabla ya mimi kuondoka atakodi yeye chumba ili nikifika nifikie kwenye hicho chumba.
Siku ile tulilala mpaka siku ya pili alfajiri aliponiaga anakwenda nyumbani kuvaa sare ya kazi ili aingie kazini na saa tisa alasiri ataondoka Moro kuja Dar.
Kabla ya kuondoka alibuku chumba Sea Cliff hoteli na kuniuliza aandike jina la nani.
Ili kupoteza ushahidi nilimwambia aandike jina lake, baada ya kupata chumba namba 215 kwa jina Kaka Mkubwa aliondoka na kuniacha nimejilaza kitandani ili kujiandaa kurudi Dar huku nikifurahia mpango wangu umekwenda vizuri. Nilitamani kupige vigelegele vya furaha. Moyo mwingine uliingia huruma kumuua mzee kama yule aliyekuwa na familia nilijikuta kwenye wakati mgumu wa maamuzi yangu.
Niliondoka Morogoro na basi majira ya saa moja kasoro asubuhi na kufika Dar saa tatu na kukodi teksi hadi kwangu. Nilipofika nilijipumzisha kwa kuoga na kujilaza, majira ya saa kumi na mbili niliamka na kuoga ili kujiandaa kwenda Sea Cliff hoteli kumsubiri mtu wangu ili nimalize kazi ilibaki ili kufanya mambo mengine.
Baada ya kujiandaa na kuchukua vifaa vyangu vya kazi nilikodi teksi hadi Sea Cliff , nilifika majira ya saa moja na nusu tofauti na muda tuliokubaliana wa saa kumi na mbili kasoro. Kwa vile mzee Mzizire alikuwa ameisha chukua chumba nilikwenda moja kwa moja mapokezi na kuomba funguo, nilimkuta dada mmoja mrembo.
“Habari dada?”
“Nzuri, karibu.”
“Asante, naomba ufunguo wa chumba namba 215.”
Yule msichana alipekua kitabu na kuniuliza.
“Samahani dada mbona chumba hiki kimechukuliwa na mtu anayeitwa Kaka Mkubwa?”
“Ndiye mpenzi wangu, chumba hiki tumechukua kwa kubuku kwa simu alfajiri ya leo.”
“Ooh! Mpenzi ndo unafika,” sauti nyuma ilinishtua ilikuwa ya mzee Mzizire.
Niligeuka mzimamzima na kwenda kujitupa kifuani kwake, kwa usanii niliokuwa natumia hata ungekuwa na moyo mgumu kiasi gani angekubali nampenda sana.
Kwangu hakikuwa kitu kigeni kwa vile ile ndiyo kazi yangu iliyokuwa ikinipatia kipato, hivyo nilikuwa najua jinsi na kumpumbaza mwanaume na kuamini nampenda kumbe nina yangu.
“Waaawooo mpenzi,” nilijifanya kuchanganyikiwa.
“Waaawoo.”
“Yaani ndo nafika na kukutana na maswali kama polisi,” nilijifanya kudeka.
“Jamani dada yangu sasa ningetoa chumba bila kuwa na uhakika?” msichana wa mapokezi alijitetea.
“Basi mpenzi, vipi umefika zamani?”
“Kama ningefika zamani si ningeumbuka.”
“Basi yameisha, tunaomba ufunguo,” mzee Mzizire alisema.
Tulipewa ufunguo na kuelekea kwenye vyumba tukiwa tumekumbatiana mtoto wa kike nilideka kuonesha nimemmisi sana. Tulikwenda mpaka chumbani na kujilaza kitandani kabla ya kwenda kuoga. Wakati mwenzangu akiwaza mapenzi mimi nilikuwa naitamani roho yake ambayo niliamini sehemu ile ilikuwa nzuri sana isiyo na ushahidi.
Tulipotoka kuoga sikuhitaji auchezee mwili wangu tena kwa vile pale nilikuwa na kazi moja naye. Baada ya kutoka kuoga nilipaka dawa yangu kwenye matiti na kumuomba anyonye.
“Mpenzi..mpenzi naomba uninyonye matiti nisikie raha.”
Fuatilia HAPA SIKU YA KESHO.
ENDELEA USHARE NA KUTEMBELEA HAPA KWA SIMULIZI ZOTE UTAZIKUTA HAPA >>www.2jiachie.com/search/label/Simulizi?max-results=7

Post a Comment