ad

ad

SUAREZ AOMBA RADHI KWA KUMNG'ATA CHIELLINI,

 
 
MSHAMBULIAJI Luis Suarez amepoza shutuma dhidi yake baada ya Jumatatu usiku kuomba radihi kwa kumng'ata Giorgio Chiellini na ameahidi kutorudia kufanya kosa kama hilo - huku Barcelona ikipiga hatua zaidi katika kuwania saini yake.
 
Siku nne baadea ya kufungiwa miezi minne na ameambia FIFA kwamba tukio hilo lilitokea katika mechi ya Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Italua mjini Natal lilitokana na kushindwa kujizuia.
 
Mshambuliaji huyo wa Liverpool ameibuka kikamilifu na kujutia kosa lake. Lakini kuomba kwake radihi kunakuja katika wiki ambayo habari zimevuma mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anatakiwa kwa dau la Pauni Milioni 80 Nou Camp.
 
Gary Lineker, mshambuliaji wa zamani wa Barcelona, amesema klabu hiyo ya Katalunya imemuambia Suarez bombe msamaha kama wanataka waendelee na jitihada za kumnunua.
Msamaha: Hatimaye Luis Suarez amoeba radihi kwa kumng'ata beki wa Italian wiki iliyopita

No comments

Powered by Blogger.