MONALISA AMWANDALIA TYSON SAPRAIZI
Staa wa Bongo Movie, Yvonne Cherry ‘Monalisa’
STAA wa Bongo Movie,
Yvonne Cherry ‘Monalisa’ amefunguka kuwa bado anamkumbuka sana aliyewahi
kuwa mumewe, marehemu George Tyson hivyo atafanya kitu kwa ajili ya
kumuenzi.
Akizungumza na mwandishi wetu siku ya Arobaini ya Tyson, Monalisa
alisema daima ataendelea kumkumbuka na kumuombea Tyson na ameona kuna
umuhimu wa kufanya kitu ambacho kitakuwa kumbukumbu maalum ya marehemu
ambacho ni siri yake.
“Kifo cha Tyson ni kama vile sinema, daima namuombea nakumkumbuka
siku zote. Siku chache baada ya hii Arobaini, nitafanya kitu ili
kumuenzi,” alisema Monalisa.
Arobaini ya Tyson aliyefariki kwa ajali ilifanyika wikiendi iliyopita nyumbani kwa Monalisa,
Arobaini ya Tyson aliyefariki kwa ajali ilifanyika wikiendi iliyopita nyumbani kwa Monalisa,

Post a Comment