ad

ad

MALINZI, MWANA FA WAZUA MJADALA MTANDAONI, WAJIBIZANA

MWANA FA


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, mapema wiki hii alijikuta 
akijibizana hoja na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ juu ya mwelekeo
 wa timu ya taifa, Taifa Stars, mara baada ya matokeo ya mabao 2-2 dhidi ya Msumbiji 
kwenye 
Uwanja wa Taifa jijini Dar, Jumapili iliyopita.


Mwana FA ambaye ni mdau mkubwa wa soka, alitoa hoja kwa Malinzi katika mtandao wa Twitter, ambapo alilalamika juu ya mahudhurio hafifu ya mashabiki katika mechi, ambapo ilielezwa yalitokana na ukubwa wa kiingilio kilichopangwa na TFF, lakini Malinzi alipinga
 hoja hiyo.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.
Sehemu ya majibizano yao ilikuwa hivi:
Mwana FA: Mheshimiwa Jamal Malinzi, nadhani hii kauli inatufaa na sisi...mahudhurio
 hafifu yanashusha morali za wachezaji wetu.
Malinzi: Mwana FA timu yoyote isiposhinda visingizio huwa havikosekani, Tanzania vs Zimbabwe waliingia watu 8,000 tu na tukashinda, juzi waliingia 20,000 tukapata sare.
Mwana FA: Jamal Malinzi siyo lazima kushinda kila siku, kama mwanamichezo naelewa,
 ni kuhusu kutengeneza mazingira 'yanayowabeba' wapenzi na wachezaji wetu.
Baada ya hapo, Malinzi hakutaka tena kuendelea na mjadala huo licha ya wadau wengine kuendelea kutoa maoni mtandaoni hapo, ambapo wengi wao walionekana kuitupia lawama TFF kutokana na kuweka kiingilio cha chini kuwa shilingi 7,000 ambacho walikilalamikia kuwa
 ni kikubwa. 
CHANZO: SALEHJEMBE.COM

No comments

Powered by Blogger.