BONGO MUVI WAFUNIKA KWA MAUNO
MASTAA wa kike katika tasnia ya filamu Bongo
Sabrina Rupia ‘Cathy’, Salma Salim ‘Sandra’ na Rose Ndauka juzi walikuwa
kivutio kwa wananchi waishio maeneo ya Kinondoni jijini Dar baada ya
kushindana kuzungusha nyonga.
Mastaa hao walifanya tukio hilo katika sherehe za kuwasimika ukamanda
wa vijana Tawi la CCM Bwawani ililopo maeneo hayo wakati walipopagawa
na vikorombwezo vya Msaga Sumu katika wimbo wa taarab.
“Dah kumbe mastaa wetu wana fani nyingi,
angalia mauno yale utafikiri hawana mifupa sehemu za kiunoni,” alisikika
akisema njemba moja lililokuwa likishuhudia shoo hiyo ya bure.
Staa wa filamu Bongo, Salma Salim ‘Sandra’.

Post a Comment