AKU, SIJAVUNJA NDOA YA DIDA –JOKATE
Mtangazaji wa Kipindi cha The One Show, Jokate Mwegelo ‘Jojo’
amefunguka kuwa hahusiki na kuvunjika kwa ndoa ya Khadija Shaibu ‘Dida’
kwani ni mshikaji wake na wanaheshimiana.
Mtangazaji wa Kipindi cha The One Show, Jokate Mwegelo ‘Jojo’.
Akijibu tuhuma kuwa, yeye anahusika na kuparaganyika kwa ndoa hiyo
kufuatia ‘ku-fall in love’ kwa mume wa Dida, Edzen Jumanne ambaye ni
mtangazaji mwenzake, Jokate alisema:
'Dida' akiwa na Ezden.
“Yaani watu wanapenda kuungaunga maneno kweli, jamani mimi siwezi
hata siku moja kuwa na Edzen, ni mfanyakazi mwenzangu halafu Dida ni
mshikaji wangu siwezi kabisa, tena wasitake kunitibulia.”

Post a Comment