ad

ad

TOROJO BAMIA (Winga teleza) - 03


“Namaanisha kuwa hapa umefika sitaki uondoke, nataka kukurudisha katika ujana nakuona umezeeka kama unavuta sigara kali.”
“Kuna documenti zangu redio tivi kochi  kitandani na vitu vichache.”
“Vitu vyote achana navyo utahamia hapa.”
“Nitashukuru lakini pale nadaiwa fedha ya mwaka mzima.”
“Shilingi ngapi?”
“Laki moja tatu na sitini.” Shuku aliongeza fedha nyingi makusudi wakati chumba alikuwa akili elfu kumi yeye aliongeza elfu ishirini kila mwezi. Nia yake kulipia miaka mitatu kwa vile asingemuamini mtu moja kwa moja.
“Okay, basi nitakupa ukalipe, unajua kudrive gari?”
“Ndiyo lakini sina leseni.”
“Nitakukatia.”
MJ alinyanyua simu na kumpigia mkuu wa polisi barabarani kumuomba leseni yenye jina la John Shuku.
“Sasa pumzika baadaye utakwenda kulipia chumba na kuchukua documenti zako kisha vitu vyote vya ndani vitoe sadaka kwa mahirani zako.”
“Hakuna tatizo.”
“Basi utakwena kupiga picha ya haraka kisha utazipeleka kesho utaipata.”
“Nitashukuru.”
“Sasa tukaoge ili uuage umaskini.”
Shuku alipelekwa kuoga, baada ya kuoga alipelekwa kwenye chumba kilichokuwa na kila kitu ndani.
“Hiki ndicho chumba chako.”
“Asante sana ndugu yangu.”
“Hizo nguo nina imani zitakutosha aliyekuwepo huku unalingana naye mwili.”
“Asante.”
“Mimi nipo sebuleni kuna demu wangu anakuja muda si mrefu.”
“Poa.”
Shuku alibadili nguo kwa kuvaa bukta kubwa na singland kama mcheza basket ball, alitoka sebuleni na kumkuta rafiki yake akiangali mkanda wa blue printi.
“Mbona unaangali mkanda huu muda huu?” Shuku aliuliza.
“Kwani muda wake saa ngapi?”
“Usiku.”
“Acha ushamba mkanda huu unaungalia muda wowote, na mimi navutia kasi kuna mtoto si wakawaida ataingia muda si mrefu.”
Shuku hakujibu naye kwenye sofa liningine na kujilaza kula kupupwe cha kiyoyozi naye alikula kideo.
“Shuku una demu?” MJ alimuuliza rafiki yake bila kumtazama.
“Sina.”
“Huna! Una matatizo gani?”
“Sina tatizo  basi nimeamua.”
“Hapana Shuku lazima utakuwa na tatizo, kwa nini usiwe na mpenzi wakati dunia ya leo imejaa wanawake wazuri wanaotafuta wanaume hata kwa kuwahonga.”
“Hao wazuri wanagharama, wa kuhonga sijapata.”
“Kwa hiyo hata wa siku mojamoja huna?”
“Nikiwa nimezichanga nakwenda Kimboka au Sewa najipigia juu kwa juu tunaachana, wale hawana gharama sijui wameishiwa lotion au kwenda salon mkilipana na kumalizana hamjui tena hawana gharama ya guest kwenye kichochoro anapandisha nguo wewe unamwaga mzigo mnaachana.”
“Mmh! Sikwezi.”
“Kawaida, nami ningekuwa nazo ningetafuta mrembo mmoja wa kula naye bata kama wewe.”
“Usiwe na wasiwasi changu chako nitahakikisha raha ulizozikosa unazipata hapa.”
“Nitashukuru, vipi wewe hujaona?”
“Nioe watoto wote wazuri na watamu nimuachie nani?”
“Kwa hiyo huna mke?”
“Sina.”
’Ila?”

ITAENDELEA KESHO HAPAHAPA

1.SOMA SEHEU YA KWANZA YA SIMULIZI HII HAPA >>>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-01.html
2. SEHEU YA 2: >>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-02.html

: Utamu ndio kwanza unazidi kukolea. Bado sehemu kibao kuweza kuisha chombezo hili la aina yake . Kamwe usithubutu kusimuliwa hii simulizi ingia ujisomee mwenyewe hapa hapa uwanja wa simulizi pekee.

:: SHARE nyingi na COMMENT bila kusahau LIKE ndizo zinafanya Chombezo hili kuwa likitoka kila siku na kwa muda muafaka hapa www.facebook.com/2jiachie pekee. Hakika si ya kukosa hii.

Wanaotakiwa kusoma chombezo hili ni kuanzia +18 tu!
Hairuhusiwi kunakili. Au kutoa hata neno kuhamishia kwenye kitabu,tamthiliya ama wall ya facebook,twitter,whatsapp na sehemu nyingine pasipo idhini ya 2JIAHIE utashitakiwa!!.

TUKUTANE HAPA SIKU YA KESHO



No comments

Powered by Blogger.