MSHINDI WA ‘CHEMSHA BONGO YA BRAZIL’ AKABIDHIWA CHAKE
Afisa Masoko wa Azam TV, Shah Mrisho (kulia) akimkabidhi zawadi zake Afande Jamila.
Afande Jamila baada ya kukabidhiwa zawadi zake.
Akiwa na tabasamu wakati akihojiwa na wanahabari.
Afisa
Masoko wa Global Publishers, wachezashaji wa Bahati Nasibu hiyo,
Innocent Mafuru, akiongea na wanahabari baada ya mshindi kukabidhiwa
chake.
Afisa Masoko wa Azam TV, Shah Mrisho, akiwaeleza jambo wanahabari (hawapo pichani).
MSHINDI wa Chemsha Bongo
ya Brazil inayoendeshwa na gazeti la Championi, Afande Jamila Omari
Mkele, leo amekabidhiwa king'amuzi na dishi kutoka Azam TV pamoja na
televisheni ya kisasa (flat screen) kutoka kampuni ya Sony baada ya
kushinda shindano hilo.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika
ofisi za Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Amani,
Risasi, Ijumaa, Championi na Ijumaa Wikienda.
PICHA : RICHARD BUKOS / GPL
Post a Comment