MALINZI ASIMAMISHA UCHAGUZI SIMBA SC
SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limesimamisha mchakato wa uchaguzi wa klabu ya
Simba SC hadi hapo klabu hiyo itakapounda Kamati ya Maadili ambayo
itasikiliza masuala ya kimaadili kuelekea uchaguzi huo.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesimamisha uchaguzi wa Simba SC
Akizungumza
na Waandishi wa Habari makao makuu ya TFF, katikati ya Jiji la Dar es
Salaam mchana wa leo, rais wa TFF, Jamal Emil Malinzi amesema kwamba
Simba SC inatakiwa kuwa imekwishaunda Kamati ya Maadili hadi kufika Juni
30, mwaka huu.
Malinzi
amesema kwamba hatua hiyo imefuatia TFF kupokea malalamiko mengi juu ya
ukiukwaji wa maadili kwa baadhi ya wagombea na wanachama wa klabu hiyo.
Malinzi
amesema kwamba baada ya kuundwa kwa Kamati hiyo Maadili itasikiliza
malalamiko yote ya kimaadili yanayougubika mchakato wa udhaguzi huo,
ambao awali ulipangwa kufanyika Juni 29, mwaka huu.
Malinzi
amesema kwamba kwa sasa Kamati ya Utendaji ya Simba SC iliyopo
madarakani chini ya Mwenyeiiti wake, Alhaj Ismail Aden Rage itaendelea
kuiongoza klabu hiyo hadi hapo mchakato wa uchaguzi utakapokamilika.

Post a Comment