KOMBE LA DUNIA NI LEO: BRAZIL VS CROATIA
Rio de Janeiro, Brazil
WENYEJI Brazil leo Alhamisi watakuwa na kibarua pevu cha kuhakikisha wanaanza vyema michuano ya Kombe la Dunia ambapo wanatarajiwa kufungua pazia kwa kumenyana na timu ya taifa ya Croatia kwenye Uwanja wa Rio de Janeiro mjini hapa.
WENYEJI Brazil leo Alhamisi watakuwa na kibarua pevu cha kuhakikisha wanaanza vyema michuano ya Kombe la Dunia ambapo wanatarajiwa kufungua pazia kwa kumenyana na timu ya taifa ya Croatia kwenye Uwanja wa Rio de Janeiro mjini hapa.
Ikumbukwe
kuwa Croatia inayonolewa na Niko Kovač, haijawahi kuifunga Brazil zaidi ya
kuambulia sare na vipigo hivyo leo inatarajiwa kuwa mechi ya kukata na shoka
inayotarajiwa kuanza mishale ya saa 5 usiku.
Mara ya
mwisho timu hizo zilipokutana kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2006 iliyofanyika
nchini Ujerumani, Brazil iliichapa
Croatia bao 1-0 lililotupiwa kimiani na kiungo Ricardo Kaka ambaye mwaka huu
hajaitwa katika timu hiyo.
Tayari
mshambuliaji tegemeo wa Brazil, Neymar dos Santos, amesharejea uwanjani na
ameahidi kufanya makubwa kwenye mechi ya leo.
Kwa upande
wa Croatia kupitia kwa kocha wao Niko amesema kikosi chake hakitapaki basi
kwenye mchezo wa leo ambao wenyeji wanapewa nafasi kubwa ya kushinda.
Wachezaji tegemeo Brazil: Neymar, David Luiz, Dani Alves,
Fred, Ramires, Paulinho, Marcelo, Willian, Hulk, Dante, Thiago Silva na kipa
Julio Cesar.
Wachezaji tegemeo Croatia:
Darijo Srna, Dejan Lovren, Vedran Corluka,
Danijel Pranjic, Luka Modric,
Mario Mandzukic, Ivica Olic, Eduardo.
Post a Comment