KOMBE LA DUNIA: HISPANIA YAVULIWA UBINGWA WA DUNIA NA KUTUPWA NJE
AIBU
gani hii! Hispania imevuliwa ubingwa wa dunia usiku huu baada ya
kuchapwa mabao 2-0 na Chile katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa Maracana,
Rio de Jeneiro, Brazil.
Maana
yake, Hispania watacheza mechi ya kukamilisha ratiba dhidi ya Australia
kisha kurejea nyumbani mapema, wakiiacha michuano bado mibichi kabisa.
Mabao yaliyoizamisha Hispania 'SIKU YA JANA' yamefungwa na
Eduardo
Vargas dakika ya 19 na Charles Aranguiz dakika ya 43 - hivyo
ukijumlisha na kipigo cha 5-1 walichopewa na Uholanzi maana yake hawana
maisha tena katika Fainali za Brazi 2014.
Uholanzi
na Chile zote zina pointi sita kila moja, wakati Australia na Hispania
hazina pointi. Kwa Chile ushindi wa leo ni sawa na kulipa kisasa cha
kufungwa 2-1 nchini Afrika Kusini mwaka 2010 katika mchezo wa mwisho wa
kundi kwenye michuano hiyo.
Mwanzo mzuri: Eduardo Vargas akishangilia baada ya kuifungia Chile bao la kwanza dhidi ya Hispania
Kocha
Vicente Del Bosque atajutia uamuzi wa kuendelea kumpanga kipa Iker
Casillas, kwani kwa mara nyingine leo amefungwa mabao ya ‘kibwege’.
Kikosi
cha Hispania kilikuwa; Casillas, Azpilicueta, Martinez, Ramos, Alba,
Busquets, Alonso/Koke dk46, Silva, Iniesta, Pedro/Cazorla dk77 na
Costa/Torres dk64.
Chile;
Bravo, Medel, Silva, Jara, Isla, Aranguiz/Gutierrez dk64, Diaz, Mena,
Vidal/Carmona dk88, Vargas/Valdivia dk85 na Sanchez.
Amekwisha: Vargas akimtungua kiulaini kipa aliyechuja Iker Casillas


Post a Comment