KOMBE LA DUNIA: CAMEROON YAFUMULIWA 4-0 NA KUTUPWA NJE
CAMEROON
imekuwa timu ya kwanza ya Afrika kuaga Kombe la Dunia na ya pili kwa
ujumla baada ya waliokuwa mabingwa watetezi, Hispania.
Hiyo
inafuatia kuchapwa mabao 4-0 usiku huu na Croatia katika mchezo wa
Kundi A mjini Manaus, Brazil, ambao ilimpoteza kwa kadi nyekundu kiungo
wake Alex Song aliyemchezea rafu Mario Mandzukic dakika ya 40.
Cameroon
imebakiza mchezo mmoja na wenyeji Brazil ikiwa haina pointi, wakati
tayari Brazil na Mexico kila moja ina pointi nne na Croatia ina pointi
tatu.

Punguza kasi: Danijel Pranjic akimkwatua Benjamin Moukandjo katuka mchezo huo
Brazil
lazima ipate japo sare katika mchezo wa mwisho ili kujihakikishia
kuingia 16 Bora- maana yake Cameroon wanaweza kurejea Younde bila
ushindi.
Mabao
yaliyowazamisha Simba Wasiofungika usiku huu yametiwa kimiani na Olic
dakika ya 11, Perisic dakika ya 48 na Mandzukic mawili, dakika ya 61 na
73, wakati Song alitolewa dakika ya 40.
Kikosi
cha Cameroon kilikuwa; Itanjde, Mbia, Chedjou/Nounkeu dk46, N’Koulou,
Assou-Ekotto, Song, Matip, Enoh, Moukandjo, Aboubakar/Webo dk70 na
Choupo/Salli.
Croatia;
Pletikosa, Srna, Lovren, Corluka, Pranjic, Rakitic, Modric,
Sammir/Kovacic dk70, Perisic/Rebic dk78, Mandzukic na Olic/Eduardo
dk69.
Kiungo wa zamani wa Arsenal, Alex Song akitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Mario Mandzukic

Post a Comment