ad

ad

BEYOND LOVE- (ZAIDI YA MAPENZI) SEHEMU YA 11 MPAKA YA 20



Beyond love-11

Wakiendelea na maongezi, mlango wa chumba cha wagonjwa mahututi ulifunguliwa, muuguzi akatokeza nje akionyesha wasiwasi mwingi na kumuomba daktari aingie haraka chumbani kwani mgonjwa tayari alikuwa amekufa! Daktari huyo aliyejulikana kwa jina la Dk. Mbisse  aliingia ndani haraka akimuacha mama yake Mariam,   muda mfupi baadaye mama huyo alianguka chini na kupoteza fahamu, ikabidi watu waliokuja naye wambebe juu juu mpaka idara  ya wagonjwa  wa nje ambako daktari alipomuona tu alionyesha wasiwasi  na kuanza kuuliza maswali huku akimuangalia mgonjwa usoni.
Je, nini kitatokea?  Mariam amekufa? Mama yake Je? Kinaendelea nini kwenye maisha ya Tom huko machimboni? SONGA  NAYO.
  
                                                                              
“Mh!” Daktari aliguna tena na kuzidi kuwatia wasiwasi watu waliompeleka mama yake Mariam kwenye chumba chake, hisia kwamba alikuwa amepoteza uhai zilianza kuwaingia vichwani mwao, wakiwa nje waliendelea kusikiliza kupitia dirishani kila kitu kilichoendelea.
“Shinikizo lake liko juu sana, sijawahi kuona presha ya aina hii, ni lazima aanzishiwe dawa sasa hivi vinginevyo atapasuka mshipa kichwani, inavyoonekana ni mgonjwa wa presha wa muda mrefu ila alikuwa hajitambui!” Sauti ya daktari iliwafikiwa majirani waliokuwa wameketi nje kwenye benchi wakisubili kupewa maelezo.
“Dawa gani tunamuanzishia daktari?”
“Mpeni Rosartan na Aprinox haraka iwezekanavyo, halafu muendelee kumpima shinikizo lake kila baada ya nusu saa na nipewe taarifa, kama kuna tatizo lolote niiteni haraka iwezekanvyo, mmenisikia?” Daktari aliuliza.
“Ndio daktari!”
“Haya mpelekeni chumba cha wagonjwa mahututi haraka iwezekanavyo!”
“Sawa daktari!”
 Mama yake Mariam akashushwa kitandani na kulazwa juu  ya machela kisha kusukumwa kuelekea chumba cha wagonjwa mahututi, majirani na marafiki wakifuata nyuma kutaka kufamu kilichotokea. Walifurahi baada ya wauguzi kuwaeleza kwamba mama yake Mariam alikuwa hajafa, bali shinikizo lake la damu lilikuwa limepanda mno, hivyo lilihitaji kushushwa ili aweze kurejewa na fahamu zake.
Chumba cha wagonjwa mahututi mama yake Mariam alilazwa kwenye moja ya vitanda vilivyokuwemo, akawekewa mashine ya hewa ya Oksijeni  iliyofunika pua na mdomo wake kisha dawa zilizoandikwa na daktari zikaanza kutolewa  kwenye njia ya mshipa na vidonge. Kitanda  kilichokuwa jirani na mahali alipolazwa mama huyo, palikuwa na pazia la rangi ya kijani lililozungushwa kwenye kitanda  huku madaktari na wauguzi wakionekana kuhangaika, baadaye Dk. Mbisse alitokeza  nje na kumuona mama yake Mariam.
“Mh! Huyu mama si nilikuwa naongea naye hapo nje?”
“Ndio!”
”Imekuwaje tena?”
“Baada ya kuongea naye tu  alianguka chini na kupoteza fahamu!”
“Farida makosa yak ohayo!”
“Kwanini daktari?”
“Ulitoa ujumbe vibaya, nadhani alifikiri mtoto wake amekufa,  siku nyingine ukiwa unatoa taarifa za aina hiyo lazima uangalie kwanza mazingira, mgonjwa alikuwa amepoteza fahamu tu wewe ukafikiria amekufa halafu ukaniita kwa kusema “Daktari mgonjwa amekufa!”  Hiyo ni kinyume cha taaluma, siku nyingine usifanyi  hivyo, sawa?” Dk Mbisse aliongea kwa sauti ya chini.
“Sawa daktari nimesikia, sitarudia tena!”
“Hebu nimuangalie kidogo!” Dk Mbisse aliongea akikisogelea kitanda cha mama yake Mariam, alipokifikia alianza kumpima shinikizo la damu, hata yeye alipomaliza pia aliguna na kumpigia simu daktari aliyemuona kwa mara ya kwanza,  wakajadiliana na kukubaliana kuongeza dozi ya dawa kwani shinikizo lilikuwa juu mno. 
*********
Mama yake Mariam alirejewa na fahamu masaa sabini na mbili baadaye, ikiwa katikati ya usiku, akaangaza macho yake huku na kule chumbani akijaribu kutaka kuelewa ni wapi alipokuwa. Fahamu hazikumwijia upesi mpaka alipouona mrija  wa dripu  ukiteremka na kuingia kwenye mshipa wa mkono wake, hapo ndipo akaelewa kwamba alikuwa hospitali. Kikohozi kikamkaba na kujikuta akikohoa, hicho ndicho kilimfanya mtu aliyekuwa kando yake azinduke usingizini, macho yao yakagongana na mtu huyo akatoa tabasamu.
“Pole sana mke wangu, ndio Dunia ilivyo!”
“Baba Mariam!”
“Naam           mke wangu!”
“Nisamehe kwa yote yaliyotokea, sikumruhusu Mariam atoke, aliiba gari nikiwa usingizini!”
“Usijali hayo mke wangu yamekwishatokea!”
“Yuko wapi Mariam?”


*********
Machimboni Tom aliendelea na maisha yake, kazi yake kubwa ikiwa ni kuosha mabaki ya mchanga wa dhahabu ulioachwa na matajiri akitumia madini ya Zebaki, kiasi kidogo cha fedha kilichopatikana alikitumia kwa chakula na kumtumia mama yake matumizi! Hakuwa na mahali pa kulala, siku zote usiku ulipoingia alilala kando ya mto karibu kabisa na mahali alipofanyia kazi zake. Haikuwa rahisi kwa mtu yoyote kuelewa alikuwa kijana mwenye uwezo mkubwa darasani, aliamua kukatisha masomo sababu ya umasikini, jambo hilo wala hakutaka kuliongelea akiwa na marafiki zake.
Alikuwa mkimya kupita kiasi, asiye na maneno mengi wala ugomvi na vijana wenzake jambo ambalo kwa machimboni lilikuwa ni kawaida,  karibu kila kijana alitembea na kisu na wengi walikuwa wamejaa majeraha miilini mwao sababu ya kuchomana visu! Hapakuwa na kituo cha polisi wala mahali pa kutoa malalamiko mtu alipoonewa, wanawake walifanyiwa unyanyasaji wa kutisha wakibakwa mbele za watu lakini hakuna aliyechukua hatua, hayo ndiyo yalikuwa maisha ya machimboni ambayo Tom alilazimika kuishi ndani yake sababu alikuwa akitafuta mafanikio  baada ya njia ya kupitia shule kushindikana.
“Naweza,  naweza kufanikiwa pia kwa njia hii, kuna watu wengi tu Duniani walioacha shule na wakafanikiwa, ni kweli shule ni muhimu lakini inaposhindikana si mwisho wa kila jambo, bado upo uwezekano wa kufanikiwa kama binadamu akitumia akili yake!” Hayo ndiyo yalikuwa mawazo yake kila siku asubuhi kabla ya kwenda kazini,  hakuwa amekata tamaa na aliamini siku moja angepata mafanikio makubwa sana na kurejea tena Dar es Salaam ambako angemtafuta tena Mariam mpaka ampate na kumuonyesha kwamba kitendo cha kumkimbia akiwa na shida hakikuwa cha kiungwana hata kidogo.
“Ipo tu siku  changudoa yule atanitambua! Nitamuonyesha mie ni nani, yeye si anajidai na utajiri wa baba yake, mimi nitakuwa nazo zangu mwenyewe, hivi sasa naamini Duniani hakuna mapenzi ya kweli, watu wanadanganyana tu, kwa jinsi Mariam alivyokuwa akiniambia maneno mazuri vile, kumbe yote yalikuwa kamba? Siamini, sitampenda mwanamke tena, naapa!” Tom alisema moyoni mwake akiosha mchanga kando ya mto, bado   chuki  dhidi ya Mariam  iliula moyo wake,    alimchukia msichana huyo kuliko kitu kingine chochote chini  ya jua la Mungu.
Je, nini kitaendelea

KUPATA SIMULIZI TAMU ZAIDI JIUNGE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK
 LIKE HAPA >>>>>>>>www.facebook.com/2jiachie


Beyond Love -12
Tom alifanya kazi kwa nguvu akiwa na usongo wa kupata utajiri ili siku moja arejee  Dar es Salaam na kumwonyesha Mariam kwamba maisha na mafanikio yalikuwa ni kwa kila mtu, si  kwa watoto wa matajiri peke yao. Ndio maana alikuwa na nidhamu katika kila fedha aliyoipata,  hakujishirikisha katika mambo mabaya kama ulevi na uvutaji wa bangi,  ambayo yalifanywa karibu na vijana wote wa machimboni.
Je, nini kitaendelea?  Tom atafanikiwa? Mariam yu hai au amekufa? SONGA NAYO…

“Yeke mura! Mang’ana?” (Vipi mshkaji mambo?) Tom alimsalimia Mwita kulipokucha asubuhi wakijaanda kuondoka kwenye kibanda chao kidogo kwenye  mto kuendelea na kazi yao ya kuosha Marudio.
“Maia!” (Safi tu)

Ilikuwa ni saa kumi na mbili asubuhi,   wote watatu  wakaamshana na kuanza kuondoka kuelekea mtoni, kila mmoja wao akiwa na uchungu moyoni mwake,  wote walikuwa ni watoto wa masikini waliotamani sana kufanikiwa katika maisha yao, wakiwa njiani  Tom aliwaeleza mambo mbalimbali aliyoyasoma kwenye vitabu vya watu waliofanikiwa kama Donald Trump, Robert Kiyosaki  na Bill Gates, alieleza kwa lugha rahisi ili   wapate kumwelewa na pia wasigundue kwamba alikuwa  na elimu kuwazidi, jambo ambalo hakutaka kabisa ligundulike, siku zote alitaka kufanana na watu waliomzunguka ili iwe rahisi kufanya nao kazi.
“Ili ufanikiwe ni lazima uwe na ndoto, ninaposema ndoto simaanishi kulala na kuota, uwe unatamani kuwa kama mtu fulani na ufanye kazi kwa nguvu kufikia kiwango hicho cha maisha, uwe tayari kupitia kwenye dhiki zote alizozipitia mtu huyo, tatizo letu tunatamani kuwa kama  Yesu Kristo lakini hatupo tayari kusulubishwa msalabani,  tunataka kwenda Mbinguni lakini hatuko tayari kufa… wewe Mwita unataka uwe kama nani maishani mwako?”
 “Gachuma!” Mwita alitamka kwa ujasiri, Gachuma alikuwa mfanyabiashara maarufu sana miongoni mwa kabila la Wakurya, wengi walimchukulia kama mfano wa kuigwa.
“Uko tayari kupitia matatizo yote aliyoyapitia Gachuma?”
“Sana tu”
“Wewe Gimonge unataka kuwa kama nani?”
“Kuna rijamaa rimoja ra Mwanza rinaitwa Rikishimba” Gimonge alisema kwa Kiswahili chenye lafudhi ya Kikurya akimtaja mfanyabiashara  mmoja wa Mwanza

Wote walikuwa na ndoto  za  kufikia hatua fulani maishani mwake,   kila siku asubuhi mpaka jioni waliongea mafanikio, magari mazuri, wanawake wazuri,  nyumba nzuri,  nguo nzuri pamoja na heshima ambayo wangepewa kama wangefanya vizuri maishani mwao. Walijiona wadogo ambao kesho yake wangekuwa wakubwa, hawakufanya mchezo hasa Tom ambaye kila alipomfikiria mama yake nyumbani machozi yalimtoka,  alitamani sana kubadilisha maisha ya mama yake ili naye apate kuheshimiwa na majirani waliombeza na kumdharau kwamba yeye na mume wake walikimbilia mjini ambako maisha yaliwashinda.

Kidogo alichopata Tom alikitumia na  mama yake,  sehemu nyingine akatunza kama akiba akiwa na lengo la kufungua biashara ndogo machimboni lakini hakufanikiwa, kwani   fedha ilipoongezeka  na kufikia mtaji wa kufungua duka,   alipata taarifa kwamba mama yake ni mgonjwa, akaondoka machimboni kwenda kumwona. Hali aliyomkuta nayo ilikuwa ya kusikitisha, alikuwa amepungua kupita kiasi na miguu imevimba, uso wake ukiwa mweupe na mashavu yametuna na macho yakiwa na rangi ya njano.
“Pole mama”
“Ahsante mwanangu,  hali yangu si nzuri, ni bora umekuja ili unipeleke hospitali”
“Hakuna shida mama, nina fedha kidogo hapa ambayo nimepata, bila shaka  itakusaidia!”
“Ahsante sana mwanangu”

Walikubali na siku iliyofuata Tom alikodisha baiskeli na kumbeba mama yake mpaka Tarime  Mjini ambako alimpeleka hospitali ya Wilaya, uchunguzi ukafanyika na kugundua kwamba mama huyo alikuwa na tatizo   kwenye Wengu lake, lilikuwa limepanuka na kuongezeka ukubwa, jambo lililofanya liwe na uwezo usio wa kawaida wa kuvunjavunja chembechembe za damu.
“Kwa kitaalam hali hii inaitwa Splenomegally!” daktari alimwambia Tom mbele ya mama yake.
“Atapona?”
“Atapona lakini itachukua muda mrefu, kwa hivi sasa itabidi alazwe wodini kuongezewa damu na pia tufanye uchunguzi zaidi kutafuta sababu ni kwanini Wengu limevimba!” Dk. Richard Mitiro alimwambia  Tom ambaye uso wake ulionyesha kukata tamaa.
“Itagharimu shilingi ngapi matibabu yake?”
“Si fedha nyingi, lakini atahitahi mtu wa kumwongezea damu”
“Nina shilingi elfu hamsini tu,  ila damu ninayo nyingi”
“Zinatosha, ngoja niandike kwenye fomu  uende maabara kupima damu tuone kama inafaa kumwongezea mama yako”
“Sawa daktari”

Mama alichukuliwa na kwenda kulazwa wodini,  Tom akapelekwa maabara ambako  damu yake ilichukuliwa na kuchunguzwa ikilinganishwa na ya mama yake ambayo pia ilichukuliwa baadaye na kuonyesha alikuwa na uwezo wa kumtolea chupa tatu, mchana wa siku hiyo hiyo akatoa damu na mama yake akaanza kuongezewa mpaka siku iliyofuata jioni ndio zoezi hilo likakamilika. Tom alishindwa kuondoka,  ikabidi  abaki na  mama yake hospitali kwa muda wa wiki nzima  majibu yalipotoka na kuonyesha kuvimba kwake kwa Wengu kulisababishwa na tatizo  kubwa kwenye damu yake.
“Itabidi umpeleke Mwanza!”
“Mwanza? Daktari, Mwanza?” aliuliza kwa mshangao mkubwa.
“Ndio kijana”
“Hauwezi kunisaidia tu hapa hapa? Sina uwezo wa kumpeleka mama Mwanza kwa matibabu”
“Kauze hata ng’ombe!”
“Hatuna ng’ombe hata mmoja daktari”
“Inabidi ujitahidi, hali ya mama si nzuri, anahitaji uchunguzi wa kina zaidi ya uwezo tulionao hapa Tarime, hospitali ya Bugando itafaa zaidi maana wao wana vifaa vikubwa kuliko tulivyonavyo sisi”
“Ninaelewa daktari, tatizo fedha”
“Kawaone ndugu nyumbani”
“Sina ndugu”
“Sijawahi kuona Mkurya asiye na ndugu”
“Wazazi wangu walitengwa”
“Na nani?”
“Na ndugu zao”
“Sababu?”
“Walikimbilia mjini wakaacha kuwasiliana nao, baba alipougua na kufariki ndio tukarudi huku na mimi ndiye mtoto pekee kwa wazazi wangu”
“Nakushauri ukafanye mpango,” daktari alizidi kusisitiza.

Alichokifanya Tom ni kuondoka ofisini kwa daktari na kwenda moja kwa moja kitandani kwa mama yake, hakutaka kulia wala kuonyesha udhaifu lakini mama  yake aligundua na kumuuliza ni kwa sababu gani alikuwa kwenye hali hiyo ya masikitiko, akashindwa kumficha na kulazimika kuuweka ukweli wote wazi kwamba walitakiwa kwenda Mwanza kwa uchunguzi zaidi! Mama yake alibubujikwa na machozi ya uchungu, hakuwa ametarajia kabisa taarifa kama hizo kwani alifahamu hawakuwa na uwezo wa kufanya jambo hilo.
“Tutatoa wapi fedha?”
“Sijui mama, lakini nashauri tuondoke kwenda nyumbani, nikakuache ili mimi nikimbie machimboni Nyamongo kujaribu kuhangaika, labda naweza kufanikisha kwa msaada wa Mungu” aliongea Tom, safari hii alishindwa kuyazuia machozi, mashavu yake yakalowa na mama yake kuanza kuyafuta.
“Usijali mwanangu,  Mungu yupo!”
“Sitaki ufe mama, sitaki kubaki peke yangu”
“Mungu atasaidia”

KUPATA SIMULIZI TAMU ZAIDI JIUNGE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK
 LIKE HAPA >>>>>>>>www.facebook.com/2jiachie

Jioni ya siku hiyo hiyo kwa baiskeli ya kukodi Tom alimbeba mama  yake na kumrejesha nyumbani ingawa hali yake ilikuwa bado dhaifu, huko  hawakulala usiku mzima wakiwa wameangaliana, Tom akiwa na wasiwasi sana na maisha ya mama yake! Hakutaka afe na aliamini ilikuwepo njia ya kulifanya jambo hilo. Kulipokucha, ingawa kwa shingo upande, Tom aliaga na kumwacha mama yake akiwa amelala hoi kitandani, hakuwa na uhakika kama wakati wa kurudi angemkuta akiwa hai lakini ilibidi afanye hivyo kwani kuendelea kumwangalia peke yake kitandani isingesaidia.
“Mama acha tu niende, utajitahidi kidogo kidogo kuwa unanyanyuka na kupika, lazima nikatafute fedha, nitakuwa nakuja mara kwa mara kukuona, nikipata kiasi cha kutosha tu nitakuja nikupeleke hospitali!” Tom alisema maneno hayo akibubujikwa na machozi, kwake kilichokuwa kikitokea kilikuwa ni sawa na kumuaga mama yake kwa mara ya mwisho,  ndani ya moyo wake alifahamu siku atakaporejea angekuta maiti imelala  kitandani ikiwa imeharibika! Mawazo hayo yalimfanya afumbe macho kwa kuogopa.
“Nenda tu mwanangu, lililopangwa na Mungu hatuwezi kulibadilisha”
“Ahsante mama,  buriani”
“Buriani mwanangu”
Tom akatoka na kufunga mlango nyuma yake kisha kuanza kutembea kwa unyonge akipita porini mpaka akafika machimboni Nyamongo,  hakuwakuta Mwita na Gimonge kambini kwao, akaelewa tayari walikuwa kazini mtoni wakiosha marudio! Akazidi kutembea mikono akiwa ameshika nyuma,  machozi yakimbubujika mpaka mtoni ambako hakuwakuta Mwita na Gimonge jambo ambalo halikuwa la kawaida na kulikuwa na watu wachache sana mtoni siku hiyo, akazidi kushangaa. Muda mfupi baadaye akapita mtu mmoja na kulazimika kumsimamisha.
“Wako kwenye shimo namba tatu!”
“Kuna nini?”
“Limetema vibaya mno, watu wote hivi sasa wana fedha!”
“Mungu wangu!” Tom alitamka neno hilo na kuanza kukimbia kuelekea kwenye shimo aliloambiwa, hakuna kitu alichohitaji  katika maisha yake wakati huo kama kupata fedha ili aweze kumpeleka mama yake hospitali,  alijisikia mwenye bahati mbaya kutokuwepo wakati shimo hilo likitema dhahabu.

Alikuta kundi kubwa la watu likiwa zimezunguka shimo hilo,  hali ilikuwa tofauti kabisa  na alivyotarajia kwani  mahali ambako watu wengi walikuwa wamepata fedha  alitegemea kuwa na vicheko na furaha lakini wengi  wa watu walikuwa  wakitokwa na machozi! Moyo wake ukashtuka, hata hivyo akapenya katikati ya watu kwenda mbele ambako alikuta miili  kumi ikiwa imelazwa chini, muda huo huo akaguswa begani, alipogeuza kichwa chake alikutana na Mwita, mashavu yake yakiwa yamelowa na machozi.
“Vipi tena?”
“Mwenzetu kafa!”
“Nani?”
“Gimonge”
“Kimetokea nini?”
“Shimo limetitia na  kuwabana watu ndani yake, bahati mbaya yeye na vijana wengine ndio walikuwemo!”
“Ha! Dhahabu zimo?”
“Nyingi mno lakini watu wameogopa kuingia kwa sababu linaendelea kutitia taratibu!”
“Wee! Kwa hiyo hata nikiingia sasa hivi dhahabu zimo?”
“Ndio”
“Hebu nipe hiyo RPG yako pamoja na  tochi!” Tom alimwomba Mwita vifaa vya kuchimbia, kichwani mwake taswira ya mama yake mzazi akiwa kitandani akiteseka kwa maumivu huku akisubiri kifo kwa sababu hapakuwa na fedha ilimwijia.
“Za nini?”
“Wewe nipe tu”
Mwita bila kujiuliza mara mbili alimkabidhi Tom vifaa vyake, katikati hali ambayo hakuitarajia alishangaa kumwona rafiki yake akikimbia mbio katikati ya watu na kwenda moja kwa moja kuzama ndani ya shimo lililokuwa likititia, watu wakashika mikono kichwani mwao katika hali ya mshangao, mtu mwenye akili timamu asingeweza kufanya jambo la aina hiyo wakati maiti kumi zilikuwa zimelala chini. Muda huo huo shimo likaanza kutitia,  watu wote wakakimbia kwenda pembeni kuepusha maisha yao.
Je,  nini kitatokea?  Tom atanusurika au ndio mwisho wake?

KUPATA SIMULIZI TAMU ZAIDI JIUNGE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK
 LIKE HAPA >>>>>>>>www.facebook.com/2jiachie

Beyond love -13

Kumuacha mama yake afe kwasababu ya fedha wakati aliambiwa kwamba dhahabu ilikuwa inatoka ingawa shimo lilikuwa likititia, halikumuingilia akilini mwake kabisa. Aliona ni bora afe akijaribu kuliko kumpoteza mama yake ambaye alitakiwa kuwa na fedha za kumtibu.
Huku watu wakishangaa ujasiri aliokuwa nao, Mwita alichukua tochi pamoja na RPG yake, kisha akaingia shimoni! Muda huo huo likaanza kutitia! Watu wakaanza kukimbia ili kukoa maisha yao! Je, nini kitatokea? Tom atapona? SONGA NAYO...

Kwa masaa kadhaa shimo liliendelea kutitia hali iliyowatia hofu sana wachimbaji waliokuwa jirani na mashimo hayo, hawakuhitaji akili nyingi sana kufahamu kwamba Tom alikuwa ameshafariki na hataonekana tena!
Watu walihuzunika sana, walishindwa kuelewa ni kwanini Tom alikuwa kujitoa kafara kiasi kile, kila alikuwa akizungumza lake. Walishindwa kuelewa ni akili ya aina gani aliyoitumia kuingia shimoni wakati alikuwa akiona maiti zimelala juu ya mashimo hayo baada ya kutitia.
“Lakini kwanini hamkumzuia?” Mmmoja wa vijana waliokuwa wakijadiliana alisema.
“Huu ni uzembe wa hali ya juu,” mwingine akadakia.
“Au mlimdanganya?”
“Hapana, aliingia mwenyewe!”
“Kwanini mlimuachia?”
“Hakuna aliyekuwa akijua nia yake, aliomba tochi na RPG kisha ghafla tukashangaa anakimbilia shimoni, akaingia!”
“Mh! Lakini huyu jamaa mjinga sana!”
“Sana, ni kama alikuwa akitaka kufa!”
Mazungumzo yale yaliwaumiza sana mwita na Gimonge, hawakuona kama walikuwa na sababu ya kuendelea kuyasikiliza. Walichokifanya ni kuchepuka pembeni kama wanajadilina jambo fulani kisha baadaye wakaondoka na kwenda nyumbani.
“Vipi kaka, unadhani jamaa atapona kweli?” Mwita alikuwa wa kwanza kumuuliza rafiki yake Gimonge.
“Sidhani, kwa hali ilivyo?”
“Eh...!”
“Siyo rahisi kutoka akiwa hai!”
“Sasa?”
“Nafikiri cha kufanya hapo ni kwenda kujaribu kama tutaweza kumtoa, lakini ikishindikana hadi kesho, ni wazi kwamba atakuwa amekufa!”
“Akifa itakuwaje ndugu yangu?”
“Hakuna kitu kingine zaidi ya kwenda kumweleza mama yake hali halisi!”
“Sawa!”
“Turudi machimboni!”
“Twende!”
Waliporudi machimboni hali ilizidi kuwa mbaya kwani shimo lilizidi kutitia, hapakuwa na matumani ya Tom kutoka akiwa mzima. Kila mtu aliamini Tom alikuwa amekufa.
******
Asubuhi ya siku iliyofuata Gimonge na Tom walikuwa safarini kwenda kwa mama yake na Tom kumpa taarifa za msiba wa mwanaye. Kila mmoja alikuwa hafahamu jinsi gani mama yake Tom angezipokea taarifa hizo kwa majonzi.
Hadi kufikia saa nane walikuwa wameshafika nyumbani kwa mama yake na Tom ambaye walimkuta akiwa hoi kitandani.
“Shikamoo mama!”
“Marhaba wanangu, hamjambo?”
“Hatujambo, pole sana kwa kuumwa!” Mwita akamwambia.
“Ahsante, hata hivyo nimeshazoea, hapa nasubiri siku yangu ya kufa tu, najua sitapona!”
“Usiseme hivyo mama, Mungu yupo na wewe, amini kwamba kwake kila kitu kinawezekana!”
“Vipi mbona mpo hivyo?” Mama Tom aliwauliza baada ya kuona wana majonzi ingawa walikuwa wakijaribu kuyaficha.
“Hakuna kitu!”
“Semeni tu wanangu, hamuweza kunificha!” Mama Toma akasema kwa uchungu, tayari alishahisi kwamba kulikuwa na tatizo!
“Mwambie...” Mwita akamwambia Gimonge.
“Mwambie wewe!”
“Hapana mwambie wewe!” Waliendelea kubishana kwa muda mrefu sana, kiasi mama Tom akazidisha wasiwasi.
“Ni nini lakini wanangu, ni vyema mkaniambia kuliko kubishana, maana hata kama mtachelewa kuniambia lakini lazima mwishoni mtaniambia tu!”
“Mama...Tom amefariki!”
“Unasema?”
“Tom amefariki mama, hatuna haja ya kukuficha!”
“Ilikuwaje?”
“Alisikia shimo linatoa madini, yeye akaingia ingawa lilikuwa linatitia, tangu jana hajatoka na tumeshatoa maiti nyingi lakini yake hatujaiona!”
“Tom mwanangu unaondoka na kuniacha mama yako nakufa! Unakufa kabla hujaiona maiti yangu....Eeeh Mungu naomba umpokee mwanangu, najua na mimi nitamfuata muda siyo mrefu!” Mama Tom alilia sana lakini baadaye akawaomba wale vijana aongozane nao Nyamongo.
“Kufanya nini tena?” Mwita akamwuliza.
“Nataka kuona mahali mwanangu alipolala!”
“Lakini unaumwa mama!”
“Najua lakini nitajikaza, lazima nione mahali mwanangu alipolala kabla na mimi sijafa!”
“Mama kwa hali yako hutaweza kutembea!”
“Mtatumia machela kunibeba!” Hawakuwa na sababu ya kubishana naye tena, wakakubaliana naye.
Machela ikatengezezwa jioni ile ile na siku iliyofuata walimbeba na kuanza safari ya kwenda Nyamongo. Walifika jioni majira ya saa 10:15.
“Nipekeni machimboni!”
“Kwanini tusiende asubuhi?”
“Siwezi kulala kabla ya kuona mahali alipolala mwanangu, lazima nione leo hii hii!” Hakuna aliyepingana naye, walijua ni kiasi gani alikuwa na uchungu.
Wakambeba na kuongoza moja kwa moja machimboni. Walipofika, mama Tom aliangalia shimo alilofia mwanaye huku machozi yakimtoka. Alionekana akiwa kimya kwa sekunde chache kisha akafuta machozi yake na kugeuza shingo na kuwatizama watu waliokuwa wamezunguka eneo lile.
“MWANANGU HAJAFA! TOM YUPO HAI?” Mama Tom akasema kwa sauti kubwa.
“Mama hivi unaona hapo kuna mtu atakayeweza kutoka akiwa hai?”
“Nasema Tom hajafa!” Yalikuwa maneno ambayo yaliyowachanganya wengi, hakuna aliyeweza kujua sababu za mama huyo kukazania kwamba mwanaye hakufa.
Kitu akabaki ameduwaa.
****
Pamoja na kukandamizwa na mchanga akiwa ardhini, Tom alikuwa akijitahidi kuchimba kidogo kidogo kwenye mwamba ili aweze kutoka. Pamoja na mateso yote aliyokuwa akiyapata ya kukosa pumzi, hata mara moja hakuachia mfuko wake wa salufeti uliokuwa na dhahabu.
Alijitahidi sana kujiokoa lakini pumzi ilikuwa ikimuishia, akilini mwake alikuwa akihuzunika sana kufa na kumuacha mama yake akiwa katika hali ngumu.
“Najua mama yangu utateseka sana, lakini hakuna jinsi naamini ni mipango ya Mungu, siwezi kuzuia kifo changu ikiwa Mungu mwenyewe wa mbinguni atakuwa amenipangia, sina ujanja tena, naelekea kifo changu sasa!” Tom akajisemea moyoni mwake.
Hakuwa na kitu cha kubadilisha ukweli kwamba alikuwa anakufa! Kitu pekee kilichokuja akini mwake ilikuwa ni kutafuta toba kwa Mungu wake. Kwanza aliamua kumsamehe Mariamu, hakutaka kufa akiwa na kinyongo na watu. Baada ya hapo akakumbuka sala ya Baba Yetu, akaanza kusali ili akifa aende Mbinguni.
‘Baba yetu uliye Mbinguni,
Jina lako litukuzwe,
Ufalme wako uje,
Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani,
Kama yatimizwavyo huko mbinguni,
Utupe leo riziki zetu,
Utusamehe makosa yetu,
Kama tunavyowasamehe waliotukosea,
Usitutie majaribuni,
Bali utuokoe na yule muovu,
Kwakuwa ufalme ni wako,
Na nguvu,
Na utukufu,
Hata milele,
Amen.’
Alipomaliza sala hiyo akavuta pumzi ndefu sana kisha akazishusha taratibu akihisi kifua kumbana. Akayafumbua macho yake kisha akaufungua ule mfuko wa salufeti, akasikia mapigo ya mopyo wake yakipiga paaa!
“HAPANA, LAZIMA JAMBO FULANI LIFANYIKE NIWEZE KUTOKA HUMU SHIMONI! NIKITOKA LAZIMA NITAKUWA TAJIRI MKUBWA NA HATA MAMA YANGU ATAPONA! MUNGU ALIYENIUMBA AMBAYE NILIKUWA NAMUOMBA MUDA MFUPI ULIOPITA NDIYE ATAKAYENITOA HUMU SHIMONI NIKIWA HAI!” Tom akawaza akilia kwa uchungu.

Je, Tom atafanikiwa kutoka au atafia shimoni?


KUPATA SIMULIZI TAMU ZAIDI JIUNGE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK
 LIKE HAPA >>>>>>>>www.facebook.com/2jiachie


Beyond Love -14

Tom yupo shimoni akiwa hana uwezo wa kupumua vizuri, anaomba sala ya ‘baba Yetu’, akiamini ingemsaidia kabla ya kifo chake. Lakini alipomaliza sala hiyo na kuangalia dhahabu iliyokuwa kwenye mfuko wake, aliumia sana moyo wake.
Alijipa matumaini ya kutoka, akiamini kufanikiwa kwake kutoka kungekuwa mwisho wa maisha ya kifukara na mateso. Akamuomba Mungu kwa mara nyingine amsaidie kutoka akiwa hai. Je, atafanikiwa? SONGA NAYO...


Maneno ya mama yake Tom yaliwashangaza sana watu wengi waliokuwa machimboni, wengi walimpuuza! Isingewezekana mtu kuwa shimoni kwa siku tatu halafu akawa mzima. Maneno ya mama Tom yalikuwa sawa na usiku wa giza.
“Mh!” Mmoja aliguna.
“Vipi?”
“Huyu mama anazeeka vibaya!”
“Kweli!”
“Lakini damu nzito kuliko maji ndugu zangu, huwezi kujua kwanini huyu mama anaamini mwanaye hajafa, maana kama angekuwa amekufa, angeona ishara yoyote moyoni mwake,” kijana mmoja alisema kwa sauti kubwa, mama Tom akamsikia.
“Nisikilizeni jamani, Tom hajafa! Nina uhakika huo, moyo wangu hauniambii kabisa kwamba mwanangu amekufa!” Mama Tom akasema huku machozi yakimtoka kwa uchungu.
“Jamani sasa tufanyeje?” Mmoja wa vijana waliokuwa pale machimboni alisema.
“Nafikiri ni vyema kama tukiendelea kuchimba, huenda tukampata!”
“Sawa!” Vijana wakaitikia na kazi ya kuanza kuchimba ikaanza.
Gimonge na Mwita walikuwa wakiongoza wenzao kuchimba pembeni ya shimo ambalo Tom alikuwepo! Walichimba kwa muda mrefu sana bila mafanikio. Kila walipotaka kuacha, mama Tom alipiga kelele akisema kwamba wanamuacha mwanaye afie ndani ya shimo.
“Lakini juhudi zetu mama umeziona, Tom hawezi kuwa hai katika hili shimo! Ni maiti ngapi tumezitoa? Shimo lenyewe linazidi kutitia, siyo rahisi Tom akawa mzima mama, amini ninachokuambia!” Gimonge akamwambia mama Tom.
“Hapana...hapana...mimi ni mtu mzima wanangu, ninachowaambia ni kwamba Tom hajafa na ni vyema kama mkiendelea na juhudi za kuchimba, mwananu yupo hai ingawa atakuwa na hali mbaya sana!”
“Kwahiyo?”
“Endeleeni kuchimba!”
“Sawa mama, hatuna budi kukuridhisha!” Kazi ya kuendelea kuchimba ikaendelea.
Wengi wa vijana waliokuwa wakichimba walikuwa wakifanya hivyo kwa ajili ya kumridhisha mama Tom tu, lakini hawakuwa na matumaini ya kumtoa Tom akiwa mzima.
*******
Hewa ilizidi kumuishia Tom. Njaa, kiu na joto vilizidi kumsumbua lakini kila alipochungulia kwenye mfuko wake uliokuwa na dhahabu zinazong’aa alijiona ana kila sababu ya kujitahidi sana ili aweze kutoka akiwa salama akafurahie utajiri.
Tom aliendelea kupagua majbali pamoja na mchanga kwa mikono akielekea kutoka juu kupitia upande wa pili wa shimo. Alijitahidi sana kutoka eneno ambalo lilikuwa likititia, aliendelea kufanya hivyo kwa muda mrefu hadi aliposikia ardhi ikitingishika!
Alihisi kama kulikuwa na mtu akilima au akichimba kitu chini ya ardhi aliyokuwemo. Hapo alijua huenda shimo lilitaka kutitia tena! Akajisogeza pembeni zaidi kupisha mtetemeko na kishindo alichokuwa akikisikia. Ghafla akashangaa kuona sululu ikitita na kutoa pembeni ya sehemu aliyokuwemo, tobo likaonekana!
Tom hakuamini!
Alikuwa ni Gimonge, Mwita na vijana wengine wakichimba. Tom akapata furaha ya ajabu sana. Akaaza kupumua kwa kasi ya ajabu sana.
“...Huyu hapa!” Mwita akapaza sauti yake.
“Nani?”
“Tom!”
Mama yake Tom aliposikia hivyo alitamani kuamka kumfuata lakini alishindwa, aliishia kulia kwa sauti kubwa. Tom akabebwa na kutolewa hadi juu ambapo alianza kupepewa! Wakati yote hayo yakifanyika, hakuwa tayari kuuachia mfuko wake wa dhahabu uliokuwa mkononi mwake. Mwita alipotaka kumsaidia, alishangaa Tom akikataa.
“Wewe umechoka sana, acha nikusaidie!”
“Hapana, nitabeba mwenyewe!”
“Mamamaaaaaaa......” Tom alipaza sauti baada ya kumuona mama yake akiwa amelala kwenye machela, huku macho yake yakiwa yamejaa machozi.
“Tom mwananguuuuuuuu.....” mama Tom naye akapaza sauti yake.
“Pole sana mwanangu!” Ilikuwa ni mapema sana wewe kufa, napaswa mimi nitangulie kwanza, nikuache ukihangaikia maisha yako.
“Mama Mungu amesikia kilio chetu mama, utaishi maisha ya furaha katika kipindi chote ulichobakisha duniani! Mama tumeuaga umasikini...” Tom akasema huku akimfungulia mama yake ule mfuko wa slufeti uliokuwa na dhahabu!
Mama yake Tom hakuamini macho yake, akamkumbatia mwanaye wakilia kwa furaha. Katika vitu ambavyo Tom hakujaribu kabisa kuvifanya ni pamoja na kuuachia ule mfuko aliokuwa ameushika! Isingekuwa rahisi kufanya jambo la hatari kiasi hicho, alikumbatiana na mama yake, lakini mfuko wake ukiwa mkononi mwake.
Kilichofanyika baada ya hapo ilikuwa ni Tom kuandaliwa uji mwepesi kisha akapewa akanywa na kupata nguvu, baada ya hapo akapewa maji ya kunywa.
Hakutaka kulala kijijini Nyamongo, baada ya kupata nguvu wakakodisha Landrover iliyowapeleka hadi mjini ambapo Tom aliuza dhahabu kidogo, fedha aliyopata aliwagawia Mwita na Gimonge kisha kiasi kilichobaki alikitumia kama nauli ya kwenda Nairobi kuuza madini yake.
Alipofika Nairobi alikwenda moja kwa moja kwa Sonara wa Kimataifa kuuza madini yake. Hakuamini macho yake pale alipokabidhiwa kiasi cha shilingi bilioni 7 za Tanzania, Tom akashika kiasi hicho kikubwa cha fedha akiwa na umri wa miaka 20. Kitu kilichokuwa akilini mwake kilikuwa ni afya ya mama yake.
Mara moja akakodi ndege na kwenda nayo hadi nyumbani kwao ambapo alimchukua mama yake na kumpeleka Nairobi kupata matibabu. Alimpeleka katika hospitali kubwa iliyosifika Afrika Mashariki nzima kwa kutoa tiba za uhakika ingawa walikuwa gharama za hospitali hiyo zilikuwa kubwa sana.
Baada ya vipimo kufanyika na mama Tom kupewa kulazwa, Tom aliitwa ofisini kwa daktari na kupewa majibu ya vipimo vya mama yake ikiwa ni pamoja na gharama za matibabu.
“Huyu mgonjwa ni nani wako?”
“Mama yangu!”
“Mama yako?”
“Ndiyo!”
“Pole sana mwanangu!”
“Nashukuru, hivi anasumbuliwa na nini?”
“Anasumbuliwa na uboho wa kweye mifupa!”
“Ni nini hiyo na inakuwaje?”
“Hiyo kitalaamu tunaita Bone Marrow, ambayo huathiri ute wa kwenye mifupa hivyo kusababisha upungufu wa nguvu za kuzalisha chembe hai nyeupe za damu na hapo ndio chanzo cha tatizo hilo kutokea!”
“Sasa?”
“Ni matibabu tu!”
“Atapona?”
“Ni matumaini yetu, lakini anatakiwa kufanyiwa ukarabati katika mifupa yake, kitaalamu tunaita Bone Marrow Transplant!”
“Naomba afanyiwe mapema tafadhali!”
“Tatizo ni gharama yake, sijui kama utaweza kumudu!”
“Ni kiasi gani?”
“Milioni 40 za Kenya!”
“Zitakuwa kiasi gani kwa fedha za Tanzania?”
“Milioni 400!”
“Hakuna shida, nipo tayari kutoa kiasi chochote kwa ajili ya mama yangu! Fedha haina thamani aliyonayo mama yangu!” Tom alisema akionyesha huzuni sana.
“Hakuna tabu, acha tukaanze hiyo kazi leo hii!”
“Nitashukuru sana dokta, kazi njema!”
Matibabu ya mama Tom yalianza mara moja, wiki mbili baadaye aliruhusiwa baada ya hali yake kutengemaa. Alipewa dawa kwa ajili ya kutumia nyumbani. Safari hii hawakurudi kijijini walipokuwa, badala yake walikwenda Dar es Salaam.
Tom akafungua akaunti katika Benki ya CRDB Tawi la Lumumba na kuhifadhi fedha zake. Akaanza mipango ya maisha yake mapya. Alinunua nyumba nyingi sana jijini Dar es Salaam na Kibaha. Akateua nyumba moja iliyopo Mbezi Beach kwa ajili ya kuishi na mama yake.
Katika nyumba hiyo kubwa ya kifahari, waliishi yeye, mama yake na msichana wa kazi tu! Tom akawa maarufu Dar es Salaam nzima, akaanza kutoa misaada katika Vituo vya Watoto Yatima. Akawa anadhamini michezo mbalimbali, jina lake likawa kubwa Dar es Salaam nzima, jina lake likabadilika, hakuitwa Tom tena, sasa alijulikana kwa jina jipya.
Alikuwa akiitwa Papaa Bill, likiwa ni kifupisho cha jina  Bill Gates, bilionea wa Marekani. Jina lake likawa maarufu katika nyimbo za Dansi na Bongo Fleva. Tom (Papaa Bill) akaanza kufanya biashara mbalimbali jijini Dar es Salaam na Afrika Mashariki, safari za kwenda nje ya nchi zikawa haziishi. Jina lake likazidi kuwa kubwa sana, akawa Mjasiriamali aliyealikwa kufundisha katika vyuo, shule, makanisa na Jumuiya mbalimbali juu ya elimu ya Ujasiriamali na jinsi alivyoweza kupata utajiri na kudumu nao. Tom akaawa Papaa Bill kwelikweli! Utajiri wake ukaongezeka maradufu.
Jioni moja akiwa mezani wanapata chakula cha usiku na mama yake, alimweleza juu ya mkutano aliotakiwa kuufanya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam siku iliyofuata. Mama yake alimtia moyo sana.
“Itakuwa saa ngapi?”
“Ni semina ya siku nzima, nashindwa kuelewa itakuwaje, maana chuo kizima watakuwa wakinisikiliza!”
“Tatizo lipo wapi mwanangu, mbona mara nyingi umekuwa ukienda kutoa semina kwa watu?”
“Siyo Chuo Kikuu mama, kwanza ni wengi halafu pili ni wasomi, natakiwa kuandaa pointi za msingi sana kuweza kuwateka watu wenye elimu kunizidi mimi!”
“Usiwe na wasiwasi mwanangu, Mungu atakutangulia!”
“Ahsante sana mama! Nakupenda sana!”
“Nakupenda pia Tom!”
“Siamini kama umepona mama, lakini moyo wangu unaumi sana kula mafanikio haya bila baba. Ingekuwa furaha sana baba naye angekuwa nasi, sijui kwanini Mungu alimchukua mapema kiasi kile?!” Tom  alisema machozi yakimlengalenga.
“...Mwanangu...Mungu hufanya kila jambo kwa makusudi yake, amini kwamba ana sababu za kumchukua baba yako...usijiumize mwanangu, Mungu atatutia nguvu! Hata hivyo ukianza kumlaumu kwa kumuita utakuwa unamkufuru! Kaka ni yeye ndiye aliyemuumba, kwanini asiamue kumchukua kwa wakati wake? Mwanangu umesahau kwamba sote tunaelekea huko huko na siku moja tutakutana naye? Tulia mwanangu, usijali tutakutana naye siku moja!” Mama Tom alisema kwa uchungu sana akimwangalia mwanaye.
“Sawa mama!” Tom akaitika kwa upole, hakuweza kukaa zaidi, Tom akaingia chumbani kwake kulala na mama yake pia.
******
Ukumbi wa Nkurumah  ulikuwa umejaa wanafunzi wengi sana pamoja na Wahadhiri wakimsikiliza kwa makini Papaa Bill (Tom) alivyoweza kupata utajiri. Historia ya maisha yake iliwahunisha wengi.
Haikuwa rahisi watu kuamini kwamba Papaa Bill na fedha zake aliwahi kupitia maisha ya taabu kiasi kile. Baadhi yao hasa wanawake walishindwa kuzuia machozi yao, wakajikuta wakilia kwa huzuni wakati wakimsikiliza Papaa Bill.
“Hata jina la Papaa Bill, nilipewa hapa mjini baada ya kuwa maarufu na utajiri nilionao. Jina langu halisi ni Tom!” Papaa Bill alisema watu walimsikiliza makini.
Hakuna hata mmoja aliyekuwa akikohoa, kila alitaka kusikia kila neno lililotoka kichwani mwa Papaa Bill.
******
“Tom?!” Msichana mmoja aliyekuwa katikati ya wanafunzi alisema kwa sauti huku akioonyesha kushtuka sana.
“Vipi?”
“Namfahamu huyu Tom!”
“Acha kujipendekeza, mara hii unasema unamfahamu? Au kwasababu umeona ni tajiri?”
“Niache bwana, namfahamu naamini akiniona atanikumbuka!” Msichana huyo alisema maneno hayo huku akikazana kwenda mbele aliposimama Bill akihutubia.
Hakujali kama maneno yale yalisikika au lah, shida yake ilikuwa kuonana na Bill. Akajipenyeza katikati ya watu hadi akafika mbele kabisa aliposimama Bill, alishtuka sana kumuona msichana huyo.
”Mariam?!”
“Tom?!”
“Ni wewe?”
 “Ndiyo!”
“Wewe ni mtu mbaya sana!”

Je, nini kitatokea?
KUPATA SIMULIZI TAMU ZAIDI JIUNGE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK
 LIKE HAPA >>>>>>>>www.facebook.com/2jiachie


  
Beyond love -15

Anamwangalia kwa jicho la hasira huku kumbukumbu mbaya zikimjia akilini mwake. Tom anamwambia Mariam ni mtu mbaya sana. Ni maneno makali yaliyomwingia sana Mariam. Je, nini kitatokea? SONGA NAYO...


Yalikuwa maneno makali sana yaliyomchoma moyo Mariam, hakuelewa sababu iliyomfanya Tom amwambie yeye ni mtu mbaya! Aliamini alikuwa mtu mwema sana katika maisha ya Tom, hasa kutokana na ukweli kwamba alishapata matatizo makubwa sana kutokana na kumsadia Tom.
Mariam akamwangalia Tom kwa macho ya mshangao, watu wakiwa kimya kuangalia kilichotokea, kuna waliochukizwa na kitendo cha Mariam kwenda mbele kwani kiliharibu mtiririko mzima wa semina.
“Tom, mimi ni mtu mbaya?”
“Yeah! Wewe ni mtu mbaya sana katika maisha yangu! Naona sasa umeona thamani yangu baada ya kusikia nimekuwa tajiri! Unajua baadhi ya watu wenye uwezo huwa mnajisahau sana, mnaona kama utajiri ni kwa ajili yenu na maisha ya shida ni ya watu wa chini siku zote!
“Mungu huyo huyo aliyewapa ninyi utajiri, ambao ulininyanyasa na kutoa thamani ya utu wangu, ndiye aliyenibariki na hivi sasa nina fedha!” Tom alisema kwa uchungu sana.
“Usiseme hivyo Tom!”
“Kumbe nisemeje?”
“Hujui yaliyotokea, nina habari mbaya sana!”
“Sawa...niache kwanza nimalize semina, hayo mambo mengine yafuate baadaye!”
“Sawa!” Mariam akaitika kwa shingo upande, huku machozi yakimtoka machoni mwake.
Akaondoka na kwenda kukaa mahali alipokuwa mwanzoni. Furaha yake ikatoweka kabisa, hakuwa na amani tena, shida yake ilikuwa kuhakikishiwa kuwa na mwanaume aliyempenda, Tom!
Hakuna aliyekuwa akifahamu kilichokuwa kikiendelea, ilikuwa ni siri ya Tom na Mariam peke yao, wao ndiyo waliojua kilichokuwa kikiendelea. Semina ikaendelea ambapo Tom alieleza siri ya mafanikio ya utajiri wake na jinsi anavyoweza kutunza fedha na kuendelea kuwa tajiri.
“Tatizo siyo kupata fedha, kikubwa ni jinsi gani ambavyo unatumia fedha zako! Labda niwaeleze jambo moja, baada ya kupata kiasi kikubwa cha fedha ni rahisi sana fedha hizo kupuputika kwa matumizi ambayo siyo ya lazima.
“Hata ukiwa na fedha nyingi kiasi gani? Kama hutatulia na kupanga mikakati, basi lazima mwisho wa siku utalia. Jambo la kwanza kabisa katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio ni nidhamu ya fedha!
“Lazima fedha iheshimiwe, usiamini una fedha nyingi sana kiasi cha kuanza matumizi ambayo siyo ya lazima. Nidhamu ya fedha inaanzia unapokuwa na kiasi kidogo kwanza, matumizi yako yapoje?
“Hupaswi kuidharau shilingi mia, maana ni mwanzo wa kuelekea kwenye elfu moja. Anza sasa kuwa na nidhamu ya fedha, utaona faida yake. Jambo lingine ni kuweka mikakati ya nini ufanye huku utafiti ukiwa silaha ya kila jambo linalohitaji fedha kabla ya kulifanya.
“Fanya utafiti wako kwanza, ni kweli ukitoa fedha zako hazitapotea? Ni kweli ni biashara nzuri inayolipa? Unaweza kufanya utafiti kwa wengine ambao wamewahi au wanafanya biashara ambayo inafanana na hiyo unayotarajia kuifanya kabla ya kuingia kwenye biashara husika.
“Tunza fedha, nenda kwa mahesabu, kila kitu kifanyike kwa rekodi, utaona mafanikio yake. Ndugu zangu, kama nilivyotangulia kusema awali kwamba, kupata fedha au utajiri siyo jambo gumu sana, lakini kinachowashinda wengi ni jinsi gani ya kuweza kudumu na huo utajiri bila kutetereka. Kwangu mimi naamini tunaweza na si imani yangu kwamba kuna mmoja kati yenu atashindwa kuwa na nidhamu ya fedha ili mwisho wa siku aweze kupata utajiri!” Tom alisema akishangiliwa.
Watu walikuwa makini sana kumsikiliza kwa kila alichokuwa akiongea, kwa wanafunzi pamoja na Wahadhiri wa Chuo Kikuu, ilikuwa faraja kubwa sana kwao kupata semina elekezi juu ya kufikia mafanikio.
Tom alikuwa na fedha nyingi sana, alikuwa tajiri mwenye uwezo mkubwa wa fedha na mwenye mali zinazoendelea kuzaliana. Ukiachana na maduka mbalimbali aliyokuwa amefungua jijini Dar es Salaam, Arusha, Mbeya, Tanga, Moshi, Mwanza na Dodoma alikuwa akimiliki kampuni ya kuuza na kununua madini mbalimbali iliyoitwa Tom Minerals Ltd iliyokuwa eneo la Posta jijini Dar es Salaam.
Alimjengea mama yake nyumba ya kifahari Musoma ambapo alimwekea mifugo na maduka ambayo aliyasimamia. Maisha ya kubahatisha yakawa yamefutika kabisa, mama yake Tom akaishi maisha ya kitajiri yaliyojaa furaha na amani.
Tom alikuwa akilipwa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa saa kila anaposimama kutoa semina na ushuhuda wa maisha yake. Kila siku alikuwa akiendelea kukua na kukua!
Baada ya kumaliza semina, Tom akiongozwa na wapambe wake, walitoka wakiliendea gari lake. Mariam alikuwa akimfuata na kumuita jina lake lakini Tom hakugeuka. Alipolifikia gari lake, akafunguliwa mlango na kuingia.
Mariam akaendelea kulia akiomba asikilizwe, hata hivyo maneno yale Tom hakuyasikia kwakuwa alifunga vioo vyote. Mariam alipozidi kulia, Tom akafungua dirisha moja na kumwangalia kwa jicho la huruma.
“Hebu mwacheni, mruhusuni aje!” Tom akasema, wapambe wake hawakuwa na kipingamizi tena, wakamruhusu   Mariam ambaye alisogelea gari la Tom akizidi kulia.
“Mfungulieni mlango!” Tom akaagiza.
Mlango ukafunguliwa, Mariam akaingia ndani ya gari, mlango ukafungwa na vioo vikapandishwa. Tom akawasha kiyoyozi kisha akafungulia redio yake kwa sauti ya chini sana.
“Nini kipya unataka kunieleza Mariam? Nimeshakuambia wewe  ni mtu mbaya sana katika maisha yangu, sioni kama kuna sababu ya kuendelea kusumbuana. Haiwezekani kipindi nikiwa na matatizo unikatae halafu sasa hivi nina mafanikio ndiyo unajifanya unanililia. Huo naufananisha na unafiki! Acha unafiki Mariam!” Tom akasema kwa hasira ya wazi akimtizama Mariam machoni.
“Hapana Tom, nakupenda sana Tom wangu, Mungu ndiye shahidi wa ninac hokiongea. Nilitaka kupoteza maisha yangu kwasababu yako! Hujui kilichotokea!”
“Kwani ulipatwa na nini?”
“Siku ile wakati narudi kutoka hospitalini, nilipata ajali mbaya ya gari, nikakimbizwa hospitalini na kulazwa. Nilikuwa na hali mbaya sana maana nilipoteza kabisa fahamu kwa miaka mitano!
“Nililala kitandani kwa muda wote huo nikiwa sijui kinachoendelea, ni kama nilikuwa nimekufa! Nilipata majereha makubwa sana katika ubongo wangu hivyo kushindwa kupata fahamu katika kipindi chote hicho. Niliteseka sana, lakini nilipopata fahamu na hali yangu kurejea kawaida ndipo nikarudi tena hapa chuo, ndiyo maana unaniona nina umri mkubwa zaidi kuliko wanafunzi wengine!” Mariam alisema huku machozi yakitiririka machoni mwake kwa kasi sana.
“Pole sana Mariam, nakupenda sana Mariam!”
“Hata mimi Tom, sijaona mwanaume mwingine zaidi yako, sikuambii haya kwasababu ya utajiri ulionao sasa, kumbuka hata kipindi ulipokuwa huna kitu nilikuwa nakupenda kwa mapenzi haya haya ninayokupenda leo!
“Nirudishe moyoni mwako tafadhali, nipe nafasi nyingine Tom, naamini kwa kuwa na wewe  maisha yangu yatakuwa ya furaha tena baada ya kuishi bila kuwa na furaha kwa miaka mingi sasa!” Mariam akamwambia Tom.
“Lakini umeshachelewa!”
“Kivipi?”
“Subiri!”
Tom akatoa simu yake mfukoni kisha akabonyeza namba fulani, akaanza kuzungumza na mtu. Dakika moja baadaye, msichana mrembo sana mwenye sifa zote za kuitwa mrembo akaingia kwenye gari ya Tom. Alikuwa mrefu, mwenye hips pana, makalio makubwa yaliyobebwa na kiuno chembamba sana.
Msichana huyo alikuwa amevaa suruali nyepesi nyeusi, blauzi ya pink pamoja na viatu vya wazi vyenye rangi ya pinki. Macho yake yalifunikwa kwa miwani kubwa ya giza! Alikuwa na midomo minene, iliyopambwa na mafuta maalum ya kupambia midomo, nyusi zilizochongwa kwa ustadi wa hali ya juu zilizochorwa kwa wanja mweusi zilizidisha uzuri wake.
Alikuwa msichana mrembo kwelikweli, manukato yake yalikaribia kupasua pua za Mariam! Yalikuwa manukato ya bei mbaya yenye harufu nzuri kuliko kawaida. Alipofika aliketi na kumtizama Mariam kwa dharau.
“Unasemaje Tom?” Msichana huyo akasema akionekana kuchukizwa na Mariam kuingia kwenye gari la Tom.
“Nataka kukutambulisha!”
“Sawa...”
“Mariam huyu ni mchumba wangu mpenzi ninayempenda sana, anaitwa Juliana. Ndiye mwanamke niliyenaye kwasasa ambaye kwakweli nampenda sana. Tupo mbioni kufunga ndoa ili tuishi kama mke na mume!” Tom akamwambia Mariam. Alipomaliza akamgeukia Juliana.
“Juliana, huyu anaitwa Mariam, alikuwa mpenzi wangu wa zamani kabla sijakutana na wewe!”
“Mh! Kumbe ulikuwa na mwanamke mbaya hivi? Ulifikiria nini lakini kuwa na uhusiano naye? Huyu ni kama alikuwa anakusababishia nuksi tu, katika maisha yako? Huyu ni takataka tu, hastahili kabisa kuwa na wewe!” Juliana akasema huku akifungua mlango tayari kwa  kurudi kwenye gari lake.
“Tom mimi mbaya, takataka? Ndiyo umeamua kumuita mwanamke wako ili anitukane? Sawa bwana, Mungu yupo!” Mariam akasema akilia sana.
Muda huo huo akashuka kwenye gari na kukimbia akielekea mtoni. Hakuna aliyejua alichokifuata.

Je, nini kitatokea? Mariam amefuata nini mtoni?


Beyond Love -16

Huyu alikuwa msichana mzuri aliyefikia kilele cha urembo lakini tatizo alikuwa mwenye dharau sana. Alimtizama Mariam kuanzia juu hadi chini kisha akamgeukia Tom na kumwambia; “Mh! Kumbe ulikuwa na mwanamke mbaya hivi? Ulifikiria nini lakini kuwa na uhusiano naye? Huyu ni kama alikuwa anakusababishia nuksi tu, katika maisha yako? Huyu ni takataka tu, hastahili kabisa kuwa na wewe!” Mariam aliumizwa sana na maneno yale.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO....  
KUPATA SIMULIZI TAMU ZAIDI JIUNGE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK
 LIKE HAPA >>>>>>>>www.facebook.com/2jiachie


Maneno yale kutoka kwa Juliana yalikuwa sumu kali kwa Mariam, kwanza alijiangalia kuanzia chini hadi juu, kisha akamwangalia na Juliana baadaye akayarudisha macho yake kwa Tom, hakuamini alichosikia, aliona kama alikuwa katikati ya ndoto kali na huenda muda wowote angezinduka.
Alishuka haraka sana kwenye gari kisha akapiga hatua za haraka akielekea katika mto uliokuwa chini ya Jengo la Utawala. Kila mtu alimshangaa, alionekana kama mwendawazimu.
Kilichokuwa kikimuuma zaidi ni kitendo cha kumsaidia Tom kwa moyo wake, tena wakati akirudi kutoka kumpeleka baba yake na Tom hospitalini akapata ajali ambayo ilimlaza kitandani kwa miaka kadhaa.
Hakuona thamani yake tena, kila kitu alikiona kichungu, hakuwa na hamu ya kuendelea kuishi duniani. Alipofika mtoni alikaa chini akiwaza jinsi gani atakavyoweza kumaliza hasira zake, haikuwa rahisi kupata jibu la haraka. Tom alikuwa amempa kovu ambalo lisingepona kabisa.
“Nimemkosea nini mimi jamani, kosa langu ni nini? Kwanini ananinyanyasa kiasi hiki? Kwanini ananikosesha amani kiasi hiki? Amenionaje kwanza, yaani napoteza kabisa mwelekeo wa maisha yangu!” Mariam akawaza.
Aliendelea kulia akiwa hajui la kufanya, maisha yake sasa yalishakuwa machungu. Lakini baada ya kuwaza muda mrefu, akapata jibu; jibu lenyewe lilikuwa baya sana. Aliwaza kujiua!
“Ndiyo lazima nife...sioni sababu ya kuendelea kuishi katika dunia yenye tabu kiasi hiki, dunia yenye watu wenye roho mbaya ambao hawataki kuangalia thamani ya maisha ya wenzao, bora nife!” Mariam aliwaza akifikiria njia nzuri ya kujitoa uhai bila maumivu.
“Watu wanaojinyonga mara nyingi hutamani kukata kamba, lazima nifikirie njia nzuri ambayo haitaniumiza, lazima niondoke duniani kimya kimya, tena bila maumivu makali. Nataka kufa taratibu...ndiyo bora nife, hakuna sababu ya kuendelea kuishi nikiteseka!” Aliwaza Mariam.
Alidhamiria kufa, lakini hakutaka kusikia maumivu wakati roho yake ikitengana na mwili, lakini alikuwa akiwaza sana njia ya kujiua! Ni njia gani hiyo? Hakuwa na majibu, lakini ilikuwa lazima ipatikane.
* * * * *
Watu walikuwa wamezunguka gari la Tom wakisikiliza mzozo uliokuwa ukiendelea kati yake na Juliana, tayari Juliana alishaanza kuleta fujo baada ya kumuona Mariam, alilalamika kwamba eti alikuwa akidhalilishwa!
“Nimekwambia ni msichana wangu wa zamani, kwani kuna tatizo gani?”
“Wewe huoni tatizo?”
“Lipi? Sioni tatizo mimi!”
“Sasa sikiliza, wakati mwingine sipendi na sitaki unifanyie ujinga kama wa leo, tafadhali sana Tom, na kama hunitaki ni bora ukaniambia ukweli ili nijue moja!”
“Usiseme hivyo mpenzi wangu!”
“Kumbe nisemeje?”
“Sikiliza tuachana na haya mambo, tunaonyesha picha mbaya, nenda kwenye gari lako tuondoke!”
“Siendi kabla haya mambo hayajaisha!”
“Unataka yaisheje?”
“Kwani wewe unafikiriaje?”
“Basi twende tutazungumza nyumbani!”
“Sawa!” Juliana akajibu kwa hasira kisha akatoka na kwenda kwenye gari lake.
Kila jicho la watu waliokuwepo mahali pale lilikuwa likimwangalia Juliana. Alikuwa mwanamke mzuri sana kwa mwanaume yeyote rijali. Alikuwa mrefu, mwenye hips pana, makalio ya kumtosha na mwendo wake ulizidi kuwakosha raha wanaume.
“Mh! Huyu msichana mzuri sana jamani!” Mmoja wa watu waliomuona akipita alisema.
“Ni kweli kaka! Kweli pesa ni kila kitu, yaani ukiwa na pesa unaweza kuwa na mwanamke yeyote umtakaye!”
“Hivi umemuona vizuri usoni?”
“Ndiyo, ana macho mazuri ajabu, halafu anajua kuyatumia! Hakyanani huyu nikimpata chumbani, hakuna kulala yaani usiku mzima ni kupeana maraha tu!”
“Mh! Mshkaji sasa wewe umefika mbali!”
“Hakuna umbali wowote, ni mambo ya kawaida sana kwa mwanaume yeyote mwenye viungo vyote vizima mwilini!”
“Umeshinda kaka!” Hayo yalikuwa mazungumzo ya vijana wawili waliokuwa wakimtizama Juliana aliyekuwa akitembea kwa maringo akielea gari lililokuwa limeegeshwa karibu na la Tom.
Alipolifikia akafungua mlango na kuingia, Tom akafunga mlango wa gari, kisha akamwambia dereva aondoe gari! Tom akaondoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
******
Utajiri wa Tom ukawa gumzo kwa wanafunzi wa chuo, stori zote siku hiyo zilikuwa zikimhusu Tom! Kila mtu alikuwa akimmiminia sifa kutokana na uwezo mkubwa kifedha aliokuwa nao. Tom alikuwa mfano wa kuigwa.
“Lakini ana maendeleo sana!” Mmoja wa wasichana waliokuwa wakijadiliana kuhusu Tom alisema.
“Sana, halafu ana mwanamke mzuri sana!”
“Yaani acha tu, yaani ndiyo upate bahati ya kuwa na boyfriend kama yeye mh! Yaani mji mbona ungechimbika?”
“Lakini hapana bwana, watu wenye fedha wana matatizo yao bwana, waone hivyo hivyo!”
“Matatizo gani?”
“Kufungua zipu!”
“Tena ni viboko ile mbaya!”
“Ukiamua kuwa naye, lazima ukubali kuteswa, kutukanwa na kuchangia na wengine, lakini ukiwa na yale mambo ya kupenda umependa utake kuwa mwenyewe, thubutu haiwezi kutokea! Wanaume wenye pesa zao tabu tupu, asikudanganye mtu!” Walizungumza kwa muda mrefu sana wasichana hao, lakini baadaye mmojawao akamkumbuka Mariam.
“Halafu nilimuona kama Mariam akimfuata mbele wakati jamaa akitoa mada!”
“Eti alikuwa anamwambia anamkumbuka!”
“Mh! Mie sikuona jamani, ikawaje?”
“Jamaa akamtolea nje!”
“Si nilisikia baadaye alipotoka nje alimfuata tena?”
“Enhee! Lakini yaliyomkuta huko balaa!”
“Ilikuwaje?”
“Alimfuata jamaa, akamfungulia mlango, baadaye Tom akamuita mwanamke wake! Mzuri huyo asikuambie mtu. Basi bwana, sijui walikuwa wakizungumza nini, nikashangaa Mariam akitoka kwa hasira na kuondoka zake!” Lilian, mmoja wa wasichana hao alisema.
“Akaenda wapi?” Pamela akauliza.
“Kakimbilia huko chini!”
“Wapi?”
“Mtoni!”
“Alikuwa katika hali gani?”
“Kama amekasirika hivi, maana inaonekana aliambia kitu kilichomuuza sana!”
“Mungu wangu!”
“Mbona umeshtuka?”
“Yaani mnaona ni jambo dogo hilo, tunaweza kumpoteza mwenzetu kwa mzaha hivi hivi!” Pamela akasema huku akikimbia.
Wenzake nao walimfuata wakikimbia hadi mtoni. Baada ya kutafuta kwa muda, walifanikiwa kumuona Mariam akiwa amelala chini akilia. Wakati mwingine alikuwa akjipigiza chini kwa hasira.
“Mariam vipi?” Pamela akamuuliza.
“Niache rafiki yangu!”
“Kwanini nikuache, niambie kuna nini?”
“Nina matatizo makubwa sana!”
“Matatizo gani tena?”
“Si unakumbuka niliwahi kukusimulia kuhusu maisha yangu?”
“Nakumbuka sana!”
“Unakumbuka kwamba nililala kuitandani kwa zaidi ya miaka minne nikiwa nimepoteza fahamu!”
“Nakumbuka!”
“Sijui kama unakumbuka sababu iliyonisababuishia matatizo yote hayo!”
“Ulisema...nakumbuka Mariam!”
“Ilikuwa ni nini?”
“Mapenzi...” Pamela akasema kwa sauti ya taratibu sana.
“Mwanaume mwenyewe ni Tom!”
“Tom?!”
“Ndiyo! Tom ndiyo chanzo cha matatizo yote hayo, lakini leo hii naambulia matusi!”
“Tom amekutukana?”
“Siyo yeye!”
“Sasa mbona umesema ni Tom?”
“Ni Juliana!”
“Juliana ndiyo nani?”
“Mwanamke wake, yule aliyekuja naye!”
“Mbona siamini kama anaweza kukutukana? Amekuambiaje?”
“Eti mimi mbaya, sina hadhi ya kuwa na Tom, yaani mimi mbaya...mimi mbaya? Sina hadhi ya kuwa na Tom? Siamini macho yangu, siamini kabisa, naona ni bora nife!” Mariam alipomaliza kusema maneno hayo akaanguka chini kama mzigo!
Akapoteza fahamu. Wakajaribu kumtingisha lakini hakushtuka, macho yake yakaanza kulegea pole pole kisha akayafumba kabisa, ute mwepesi ukaanza kumtoka kinywani mwake, shingo yake ikalegea kabisa. Mariam hakujigusa tena.
Wakapiga kelele za kuomba msaada.

Je,nini kitatokea? Mariam amekufa? Mapenzi ya Tom na Juliana yatafikia wapi? Vipi kuhusu mama yake Tom huko kijijijini?


Beyond Love- 17

Kitendo cha mwanamke wa Tom, Juliana kumtukana Mariam, kilimuumiza sana! Alijikuta akijiona hana thamani tena, hakuyatamani maisha. Akatoka mbio akielekea mtoni chini ya daraja ambapo alianza kuwaza huku akilia machozi.
Baadaye Pamela na wenzake wanamfuata mtoni alipokuwa amekimbilia ambapo wanamkuta akiwa katika hali mbaya sana akilia kwa uchungu. Baadaye Mariam alilegea na kuanza kutokwa na mapovu mdomoni kabla ya kupoteza fahamu.
Je, nini kitatokea? SONGA NAYO...


Dakika kumi tu baadaye tayari watu walikuwa wameshajaa katika eneo lile. Hawakuwa na sababu ya kuuliza kilichotokea kwani hali aliyokuwa nayo Mariam pale chini iliwahuzunisha sana, mara moja akabebwa juu juu na kupelekwa eneo la Utawala.
“Nini kimetokea?” Mmoja wa wanafunzi aliuliza.
“Hayo siyo maswali kinachotakiwa sasa hivi ni kumuwahisha hospitali kwanza!”
“Lakini ni vizuri tukafahamu!”
“Ndiyo maana nimesema tumpeleke kwanza hospitali!” Pamela akaendelea kusisitiza.
Pamela na wenzake wakaongoza moja kwa moja hadi ofisini  kwa Mkuu wa Chuo ambapo alitoa taarifa na  gari likatolewa mara moja. Muda mfupi baadaye safari ya kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikaanza. Hawakuchukua muda mrefu sana kufika hospitalini hapo wakitumia Barabara ya Sam Nujoma baadaye Ali Hassan Mwinyi kisha walipofika eneo la Daraja la Salender wakakata kulia wakielekea Hospitali ya Muhimbili.
Hawakuwa na sababu ya kukaa mapokezi, moja kwa moja  aliweka juu ya machela na kusukumwa  kuelekea wodini.
“Nini kimempata?” Mmoja wa wauguzi aliuliza.
“Alianguka!”
“Kwanini?”
“Alipatwa na mshtuko!”
“Wa?”
“Ni mambo ya uhusiano!”
“Kawaida ya wasichana!”
“Naomba utusaidie apone!”
“Usijali hii ndio kazi yetu, mmesema mnatokea wapi?’
“Chuo Kikuu!”
“Tulisikia Papaa Bill alikuwa anatoa semina ya Ujasiriamali pale!”
“Ndiyo,  tena yeye ndiye amesababisha yote haya!”
“Kivipi?”
“Aliwahi kuwa mpenzi wa Mariam!”
“Mungu wangu!”
“Kwa hiyo alivyokuja pale alikuja na mwanamke mwingine anayeitwa Juliana. Hata hivyo Mariam alivyomfuata alimtambulisha kwamba ana mpenzi mwingine, mbaya zaidi Juliana alimtukana Mariam hiyo ndiyo sababu iliyosababisha matatizo  yote haya!”
“Poleni sana, kwani Papaa Bill alikuwa hajui kwamba Mariam alikuwepo chuoni?”
“Alikuwa hajui!”
“Mbona sielewi kivipi?”
“Walipotezana muda mrefu sana na hata hivyo Papaa Bill alivyokuja Mariam hakujua kama ndiye mpenzi wake wa zamani!”
“Kwanini asijue?”
“Papaa Bill siyo jina lake halisi!”
“Kumbe anaitwa nani?”
“Tom!”
“Ok nimeanza kuelewa, tupeni nafasi kidogo tufanye kazi yetu!”
Pamela na wenzake wakatoka nje na kuwaachia wauguzi waendelee na kazi ya kumpatia matibabu Mariam. Jopo la madaktari watatu walikuwa bize kuhakikisha hali ya Mariam inakuwa nzuri.  Kazi ya kupandisha mapigo yake ya  moyo ilianza mara moja na matumaini yakaanza kuonekana.
Baadaye Muuguzi aliyekuwa akizungumza na akina Pamela  alitoka nje uso wake ukionyesha alikuwa na jambo la kuzungumza nao. Macho yake yalionyesha wasiwasi mwingi jambo ambalo liliwazidishia hofu Pamela na wanafunzi wengine waliokuwepo.
“Muuguzi nini kinaendelea huko ndani?” Pamela alikuwa wa kwanza kuuliza.
“Punguzeni hofu, Mariam anaendelea vizuri!”
“Ameamka?”
“Bado lakini hali si mbaya!”
“Ahsante Mungu!”
“Mnaweza  kwenda na kurejea kesho asubuhi!”
“Ahsante sana na Mungu akubariki!”
“Nanyi pia!”
****
Majina ya Tom na Mariam yalikuwa gumzo  chuo kizima, kila kona walikuwa wakizungumziwa wao,  hakuna hata mmoja aliyeelewa siri iliyokuwepo kati yao. Wengi walimwonea huruma sana Mariam lakini kuna ambao walimwona kama mtumwa wa mapenzi anayemng’ang’ania Tom kwa sababu ya fedha alizokuwa nazo.
Kilichokuwa nyuma ya pazia hakuna aliyekifahamu kwani ilikuwa ni siri kubwa iliyojificha katikati ya moyo wa Mariam ambaye alimweleza siri hiyo rafiki yake pekee Pamela.
“Hivi anaendeleaje Mariam?”
“Hajambo!”
“Ametoka?”
“Bado ila ameshapata fahamu!”
“Mh!”
“Mbona unaguna?”
“Sababu iliyompeleka hospitali!”
“Sasa hiyo ni ya kuuliza?’
“Ndiyo kila mtu anajua alianguka lakini sababu ya kuanguka kwake ndiyo inayonitatiza!”
“Si mapenzi?” Mwingine akadakia.
“Ishu sio mapenzi bali ni nani anayempenda!”
“Jamani huyu naye si Papaa Bill!”
“Sasa haoni kama hawaendani naye?”
“Msiingilie mambo ya watu hivi mnajua nguvu ya mapenzi ninyi?” Pamela aliuliza kwa ukali.
“Rafiki yako naye amezidi kujipendekeza kwa watu wenye fedha zao,  halafu anajifanya mgumu utafikiri binti mlokole, hajawahi kusimama na mwanaume hata siku moja lakini hii inashangaza mpaka akazimia?”
“Ndiyo maana nasema hamfahamu kitu kinachoendelea hivyo kaeni kimya!”
“Sasa kama  unajua si utuambie?”
“Ya ngoswe muachie ngoswe mwenyewe mmekuja kusoma au kujua ya watu?”
“Mh! Na wewe una majibu...shauri yako wewe mwendekeze tu huyo shoga yako!”
“Fyuuuu bakini  na umbea wenu!” Pamela akasema huku akisonya na kuondoka zake.

***
Siku tatu baadaye Muuguzi aliyekuwa akipita raundi  ya asubuhi alishangazwa na hali ya Mariam ambaye alikuwa ameanza kufumbua macho na kupepesa huku na kule. Mara moja muuguzi akasogea  katika kitanda cha Mariam kisha akaketi.
“Pole!”
“Ahsante!”
“Unajisikiaje sasa?”
“Sijambo, kwani hapa ni wapi?”
“Hospitali!”
“Hospitali?”
“Ndiyo!”
“Nililetwa hapa kufanya nini?”
“Uliletwa hapa ukiwa hujitambui umepoteza fahamu!”
“Mungu wangu!” Akili ya Mariam ikafanya kazi kwa haraka. Akavuta kumbukumbu tataribu.

Nataka kwenda kwa Tom...
Napanda kwenye gari lake...
Namkumbusha mimi ni nani...
Ananiambia ana mchumba...
Baadaye anamwita...
Ni mwanamke mrembo sana...
Anaonekana ana dharau...
Anavuta midomo yake...
Ananiambia mimi ni mwanamke mbaya...
Mimi mbaya?...
Nakimbilia chini ya daraja, nalia...
Pamela
“No! Haiwezekani Tom kwanini unanitesa kiasi hiki Tom? Mimi ni mwanamke mbaya kiasi hicho? Nimelala hospitali kwa miaka mitano kwa sababu ya kukuokoa uhai wa baba yako lakini haukujali yote hayo unaniletea mwanamke anitusi. Tom! Kwanini mimi?” Pale pale Mariam alianza kulia baada ya kukumbuka picha nzima ya tukio lote lilivyokuwa.
“Pole sana binti haya ndiyo maisha!”
“Lakini inaniuma sana!”
“Najua lakini usijali, Mungu atakupa mwanaume mwingine!”
“Dada, si kama Tom wangu niliyempenda na kujitoa kwake!”
“Jitahidi tu!”
“Siwezi,  siwezi nimekaa miaka yote hiyo nikimsubiri yeye, sikujua alipoelekea  sasa amerudi namhitaji!”
“Mariam!”
“Bee!”
“Wewe hivi sasa ni mgonjwa unahitaji kutulia na kufikiria afya yako kwanza!”
“Najua, lakini inaniuma sana!”
“Pole sana!”
“Ahsante!” Muda huo huo Pamela akaingia akiwa na maua mkononi mwake.
“Mariam umezinduka?” Pamela aliuliza kwa mshangao.
“Ndiyo namshukuru Mungu!”
“Pole, unaendeleaje sasa?”
“Nasikia vizuri!”
“Utapona usijali!”
Walizungumza mambo mengi  na Mariam kuhusu tukio zima lilivyokuwa na jinsi wanafunzi wanavyomchukulia. Pamela alitumia muda mwingi sana kumshauri na kumfanya ajisikie kawaida. Ilikuwa  kazi ngumu  lakini  aliimudu ipasavyo.
Wiki moja baadaye ikiwa  ni baada ya Mariam kupata Ushauri Nasaha kwa  madaktari hali yake ilirejea vizuri na alikuwa tayari  kuishi bila Tom. Akarejea chuoni na kuendelea na masomo kama kawaida.
***
Mapenzi ya Tom na Juliana yalipamba moto huku mipango ya ndoa ikiwa katika hatua za mwisho kabisa. Tayari ndoa yao ilishaandikishwa Kanisani na ilitarajiwa kufungwa wiki moja baadaye. Tom akapata safari ya ghafla kikazi ya kwenda Arusha. Alishindwa ni jinsi gani angemweleza Juliana akamwelewa juu ya safari hiyo lakini ilikuwa ni lazima amweleze.
Alichokifanya ni kuwahi nyumbani kisha akaoga pamoja na mpenzi wake baadaye wakaungana pamoja mezani kwa chakula cha usiku. Tom aliona hiyo ndiyo ilikuwa nafasi pekee ya kumweleza mchumba wake juu ya safari iliyokuwa mbele yake. Hata hivyo alisita.
“Darling inaonekana kuna  kitu kinakutatiza leo!”
“Ahaaa, hapana usijali mpenzi nipo sawa tu!”
“Nakujua vizuri sana mpenzi wangu si kawaida yako kuwa hivyo!”
“Ni kweli mpenzi lakini nafikiria ni namna gani utakavypokea ujumbe ninaotaka kukueleza!”
“Ni ujumbe gani, hata kama ni mbaya nieleze tu!”
“Nimepata safari ya ghafla ya kwenda Arusha kesho mchana!”
“Kuna nini tena?”
“Akina Jamali wameniita, kuna tatizo kidogo kule kwenye ofisi yangu ya kule sina budi kwenda ili nikalitatue, hata hivyo kesho kutwa tu nitakuwa hapa!”
“Mh! Darling nitabaki na nani?  Kumbuka zimebaki siku chache tu kabla ya ndoa yetu!”
“Sasa?”
“Siyo vizuri kusafiri!”
“Hizo ni imani tu, ondoa shaka mpenzi wangu wewe umeshakuwa wangu tayari!”
“Sawa, lakini usizidishe kesho kutwa!”
“Usijali”
Siku  iliyofuata Tom alijiandaa kwa safari ya kwenda Arusha na baadaye akiwa safarini kuelekea Uwanja wa Ndege akapigiwa simu na kufahamishwa kwamba tatizo lilishatatuliwa,  kwa maana hiyo hakuhitajika tena kwenda huko. Tom alifurahi lakini aliamua kumshtukiza mkewe.
Akaondoka na kwenda  kwa marafiki zake Msasani,  alikaa huko mpaka saa tano za usiku ndipo aliporejea nyumbani. Baada ya mlinzi kumfungulia aliegesha gari mahali pazuri kisha akafungua mlango mkubwa na kwenda moja kwa moja chumbani kwake. Macho yake hayakutaka kumeza yalichokiona mbele yake.
Juliana alikuwa na mwanaume kitandani, tena rafiki mkubwa wa Tom aliyeitwa Joseph. Tom aliyatoa macho bila kuamini alichokiona, akafikiria siku ya ndoa yake, akafikiria  jinsi alivyoalika wageni wengi, akawaza juu ya gharama alizozitumia kuandaa sherehe hiyo,  akachanganyikiwa.
“Juliana...Joseph,  mnanifanyia hivi?” Tom alisema maneno hayo akitetemeka. Ghafla akaanguka chini kama mzigo, puuu!
Picha ya Mariam ikamjia kichwani  mwake. Akapoteza fahamu.

Je, nini kitaendelea?
KUPATA SIMULIZI TAMU ZAIDI JIUNGE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK
 LIKE HAPA >>>>>>>>www.facebook.com/2jiachie



Beyond Love- 18
Wiki moja kabla ya Tom kufunga ndoa na Juliana, Tom anamfumania Juliana akifanya mapenzi na rafiki yake wa karibu aitwaye Joseph. Tom haamini kilichotokea, anajikuta akianguka chini na kupoteza fahamu. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...
Kilikuwa chumba kizuri kuliko kawaida, dari lilikuwa limepigwa rangi nyeupe, chini kukiwa na zulia la manyoya laini lenye rangi nyeupe, ukuta ulikuwa umepigwa rangi nyeupe, mashuka nayo yalikuwa meupe kabisa huku feni iliyokuwa juu ikisambaza hewa nzuri chumbani mle ikiwa nyeupe!
Kila kitu kilikuwa cheupe! Macho yake yalikuwa yakizunguka kila kona ndani ya chumba hicho bila kujua alikuwa mahali gani, baadaye akataka kuamka, lakini akashindwa! Alishindwa kwasababu alihisi maumivu katika mkono wake wa kuume, ni hapo alipogundua kwamba mkono wake ulikuwa umetobolewa na dawa iliyokuwa ikitokea kwenye drip ilikuwa ikiingia katika mishipa yake ya damu!
Huyu ni Tom au Papaa Bill kama alivyojulikana na wengi, hapo akili yake ikafanya kazi ipasavyo. Akagundua kwamba alikuwa hospitalini! Anaumwa nini? Ni swali ambalo alijiuliza bila kupata jibu sahihi. Baadaye alipogeuza uso wake akamuona Muuguzi akiwa amesimama mbele yake. Akatabasamu.
“Pole sana kaka!”
“Ahsante sana!”
“Unajisikiaje sasa?”
“Vizuri, kuna nini?”
“Unaumwa!”
“Na nini?”
“Huwezi kukumbuka, ulipoteza fahamu!”
“Hapa ni hospitali gani?”
“Ocean Road!”
“Umesema Ocean Road?”
“Ndiyo!”
“Nani alinileta?”
“Juliana!”
“Nani?”
“Juliana!”
“Umesema Juliana?”
“Ndiyo!”
Hapo picha nzima ikamjia, akakumbuka tukio zima la fumanizi kati ya Juliana na Joseph, moyo wake ulisononeka sana. Machozi yakaanza kutiririka machoni mwake kama maji yatiririkavyo katika kijito kilichopo mlimani. Moyo wake ulipata majeraha makubwa sana, hakuwa tayari kupata maumivu makali kiasi kile, akamchukia sana Juliana.
“Kwani vipi kaka?”
“Dada dunia hii...dunia dada!”
“Imefanya nini? Kwanza ni nini kilitokea?”
“Dada nimeamini unaweza kuwa na fedha nyingi sana lakini ukakosa mapenzi ya dhati kutoka kwa mtu mwenye penzi la dhati!”
“Unamaanisha nini kaka yangu?”
“Dada ninavyokuambia wiki ijayo nilitakiwa kufunga ndoa na mpenzi wangu wa moyo Juliana, lakini alichonifanyia siwezi kusahau katika maisha yangu yote!”
“Amefanya nini?”
“Si ulisema Juliana ndiye aliyenileta hapa?”
“Ndiyo!”
“Basi huyo mwanamke ndiye ambaye nilikuwa natarajia kufunga naye ndoa wiki ijayo, lakini nimemfumania na mwanaume mwingine, mbaya zaidi ni rafiki yangu wa karibu ambaye ninamsaidia vitu vingi ikiwemo pesa!”
“Pole sana Mungu atakusaidia!”
“Nashukuru sana dada yangu! Hivi, nilizimia kwa muda mrefu sana?”
“Siyo sana, uliletwa jana usiku na sasa ni saa saba na nusu mchana!”
“Yaani nimepoteza fahamu kwa masaa yote hayo?”
“Ndiyo, lakini usijali hali yako sasa inaendelea vizuri na utapata nafuu, usijali!”
“Nashukuru sana!”
Yule Muuguzi akaondoka na kumuacha Tom akiwa amelala peke yake kitandani, akili yake ikiwachambua wanawake wawili; Juliana na Mariam! Moyo wake ulikuwa unamuuma sana kwa makosa aliyomfanyia mpenzi wake wa zamani Mariam, hakuona kama alistahili kufanyiwa yale. Alishanza kuamini kwamba laana ya Mariam ndiyo iliyokuwa ikiusambaratisha uhusiano wake na Juliana.
Ilikuwa lazima atumie akili nyingi sana, ndivyo alivyofanya. Hakutakiwa kuwa na papara katika hali ngumu aliyokuwa nayo, alipaswa kuwa makini, mwenye mawazo endelevu katika matatizo aliyokuwa nayo. Busara zake zilikuwa zinahitajika sana kwa wakati.
“Ndiyo...lazima niwe makini sana hapa, nikicheza hapa naweza kupoteza muelekeo wa maisha yangu! Napaswa kuwa mjanja huku nikiiacha akili yangu ichanganue mambo kwa nafasi, vinginevyo nitakuwa nakaribisha machozi tena katika maisha yangu, jambo ambalo napingana nalo kwa nguvu zote!” Aliwaza Tom.
“Lakini hapa sina ujanja tena, nimeamini hakuna mapenzi ya kweli, ni bora nikarudiana na Mariam wangu, ambaye ana mapenzi ya dhati na mimi, kwanza alinipenda kabla sijawa na kitu, kwanini nisiamini kama ananipenda?
“Nisidanganyike na hawa wasichana wa mjini, watanipotezea mwelekeo wa maisha yangu, nitakuja kulia halafu niishie kuchekwa na wabaya wangu. Mariam...Mariam wangu, tafadhali sikia kilio changu, ni kweli nimekukosea, lakini lazima ukumbuke hii dunia ina vishawishi vingi sana.
“Nilipoteza mawasiliano na wewe mpenzi wangu, sikujua kama ulipata matatizo makubwa kiasi ulichonieleza. Akili yangu ilinituma kwamba umeamua kunisusa na kumuacha baba yangu afe wakati wewe ukiwa katika matatizo makubwa.
“Nisamehe tafadhali, nisamehe mpenzi wangu na ninakuomba unikaribishe katika himaya ya mapenzi yako tena. Nisamehe mpenzi wangu, kukosea ni ukamilifu wa binadamu...tafadhali....nipo chini ya miguu yako....” akiwa anawaza hayo, ghafla mlango wa wodi aliyokuwa amelazwa ukafunguliwa.
Macho yake yakakutana na ya Juliana akimwangalia kwa huzuni huku machozi yakianza kumlengalenga! Mikononi mwake alikuwa amebeba maua mazuri yenye rangi nyeupe. Akasogea hadi kitandani alipokuwa amelala Tom, akapiga magoti chini huku mikono yake iliyobeba maua akiwa ameielekeza kwa Tom. Muda wote huo Tom alikuwa kimya akimtizama, hakunyanyua mdomo wake wala kufanya jambo lolote zaidi ya kumwangalia.
“Najua nimekukosea sana mpenzi wangu, kumbuka kwamba mimi ni binadamu, naomba unisamehe!” Juliana akasema akilia kwa uchungu.
“Nikusamehe?” Tom akauliza kwa sauti ya upole sana.
“Ndiyo naomba unisamehe mpenzi wangu, kwanza kumbuka kwamba Joseph alinilazimisha, nilipoona anazidi kuning’ang’ania nikamwacha!”
“Kwahiyo kila mtu akija kukulazimisha wakati mimi sipo utakuwa tayari kufanya naye uchafu kama mliofanya na Joseph siyo?”
“Sina maana hiyo mpenzi wangu!”
“Kumbe una maana gani?”
“Nilipitiwa mpenzi wangu, naomba unisamehe tafadhali!”
“Naomba kukuuliza swali moja la msingi sana!”
“Nakusikia!”
“Unafahamu kwamba wiki ijayo tutatakiwa kupanda madhabahuni kufunga ndoa?”
“Najua!”
“Sasa kuna ndoa gani ambayo kabla hata haijafungwa imeshaanza kuwa na usaliti?”
“Mpenzi wangu kumbuka tutaingia aibu sana kama tusipofunga, tumealika watu wengi sana na isitoshe wanatuheshimu sana, sasa tutaficha wapi nyuso zetu mpenzi wangu?”
“Jiulize wewe utauficha wapi uso wako siyo mimi!”
“Najua sweetie ndiyo maana nakuomba msamaha! Kumbuka wazazi wangu wananipenda na kuniamini sana, wakisikia nimefanya mambo haya itakuwa aibu kubwa sana kwangu na kwa familia nzima kwa ujumla, naomba unisamehe tafadhali!”
“Sawa, nimeshakusamehe!” Tom akasema huku akilia, maumivu aliyokuwa nayo moyoni mwake yalikuwa makali sana.
“Kweli Tom? Umenisamehe kweli mpenzi wangu?”
“Niamini mpenzi, ni kweli nimekusamehe!”
“Nashukuru sana kusikia hivyo!” 
“Hata mimi pia, lakini lazima uwe makini na jambo moja!”
“Nakusikia mpenzi wangu!”
“Siku nikukufumania kwa mara nyingine, ujue itakuwa ndiyo mwisho wa penzi letu!”
“Nimekuelewa!”
“Siyo uelewe pekee, uweke akilini mwako na uhakikishe hurudii kosa hilo tena!”
“Nakuahidi mpenzi wangu!” Juliana akaondoka hospitalini pale akiwa na furaha sana.
Taratibu za sherehe zikaendelea kama kawaida,  Juliana alikuwa na hamu sana ya kufunga ndoa na Tom, alikuwa kijana mwenye mafanikio makubwa sana. Ndoa yao ilipangwa kufungwa kifahari sana, kwanza ingefungiwa katikati ya bahari wakiwa kwenye meli na sherehe nzima ya ndoa yao ingemalizikia huko. Furaha yake ikarejea kwa mara ya pili.
“Nashukuru sana Mungu amenisaidia, Tom wangu amenisamehe, nilikuwa na mashaka sana juu ya mpenzi wangu, sikuwa na uhakika wa kurudi tena katika himaya yake, hasa ndoa ambayo ilitaka kuingia dosari.
“Lakini na mimi nimezidi tamaa, Joseph ana nini kiasi cha kunichanganya akili yangu kiasi kile? Hata hivyo, sina sababu ya kuwaza mambo yaliyopita, acha niyaache yaliyopita yaende zake na mimi nibaki na maisha yangu nikisubiria ndoa yangu iliyopo mbele yangu!” Juliana akawaza huku akitabsamu.
*****
Siku iliyofuata Tom aliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya afya yake kutengemaa, Juliana ndiye aliyeenda kumchukua hospitalini na kumrudisha nyumbani, njiani wakizungumza mambo mengi yaliyohusu ndoa yao.
Kila mmoja alionekana kuwa na hamu sana na ndoa yao, wakawa wanakwenda Kanisani kwa ajili ya Mafundisho ya Ndoa kama kawaida, wageni wengi walikuwa wamealikwa kwa ajili ya kwenda kushuhudia ndoa hiyo ya aina yake iliyopangwa kufanyika kwenye meli.
Kila kitu kilikwenda sawa ingawa Tom alikuwa na maumivu makali sana katika moyo wake, alikuwa akiwaza sana juu ya mabaya aliyofanyiwa na Juliana. Siku aliyomkuta Joseph ambaye alikuwa rafiki yake kipenzi kifuani mwa Juliana, ilijirudia akilini mwake kila wakati huku akihisi maumivu makali sana ya mapenzi.
Walishirikiana kwa kila kitu, lakini Tom alikataa kufanya mapenzi na Juliana kwa kisingizio kwamba anasubiri hadi siku ya ndoa.
“Lakini mbona tumekuwa tukifanya siku zote hizo?”
“Siyo sababu!”
“Ni sababu!”
“Siyo sababu mpenzi wangu, unajua hata kama tumemkosea Mungu kwa siku zote hizo, halafu tumekuja kugundua baadaye kwamba tulikuwa tunamkosea ni vizuri tukabadilika!”
“Hapana...!”
“Nataka niwe na wewe mpenzi wangu, kumbuka siku ya ndoa huwa na mshawasha wake, isitoshe tutakwenda fungate, huoni kwamba itakuwa siku nzuri kwa sisi kufanya mapenzi tena,  halafu isitoshe wakati huo tutaita tendo la ndoa nadhani itakuwa nzuri sana!”
“Sawa lakini moyo wangu bado una maswali mengi sana!”
“Maswali ya nini?”
“Nahisi kama kuna kitu kinaendelea moyoni mwako!”
“Acha wasiwasi wako mpenzi wangu, nini hicho kinaendelea moyoni mwangu?”
“Basi tuachane na hayo!”
“Sawa basi, tulale!”
“Mwaaa!” Wakapeana mabusu motomoto na kulala.
*******
Zikiwa zimebaki siku tatu tu kabla ya ndoa ya Tom na Juliana, huku vyombo mbalimbali vya habari vikitangaza na kuandika juu ya ndoa hiyo ya aina yake nchini Tanzania, Tom alikuwa mwenye mawazo mengi sana. Ni kweli alikuwa akimpenda sana mpenzi wake Juliana, lakini kitendo cha usaliti kiliendelea kusafiri akilini mwake siku zote tangu siku ya tukio lile na baadaye kulazwa.
Alihisi moyo wake ulikuwa unakosa kitu muhimu sana, alimhitaji sana Mariam wake hata kama asingemuoa. Alichokifanya ni kuandaa kadi kwa ajili ya Mariam kisha akampigia simu na kumtaka aonane naye.
“Umesema unaitwa nani?”
“Thomas!”
“Tom?”
“Ndiyo!”
“Unataka kuonana na mimi?”
“Ndiyo!”
“Kuna nini?”
“Ni vizuri tuonane, siwezi kuzungumza kwenye simu!”
“Namba yangu ni nani amekupa?”
“Hilo siyo la muhimu kujua kama ambalo linanifanya nikuite!”
“Tukutane wapi sasa?”
“Nitakuja Mlimani City!”
“Wapi sasa?”
“Samaki Samaki!”
“Sawa, saa ngapi?”
“Saa mbili kamili usiku nitakuwa hapo!”
“Huwezi kufanya mapema zaidi?”
“Muda huo ni mzuri zaidi kutokana na aina ya maongezi niliyonayo!”
“Ok!”
“Kazi njema!”
Moyo wa Mariam ulilipuka sana, hakujua Tom alikuwa na kitu gani cha kumwambia hasa ukizingatia alikuwa akisikia kila kukicha juu ya maandalizi ya ndoa yake. Hata hivyo, aliisubiri jioni hiyo kwa hamu kubwa sana, alihisi kama mshale wa sekunde hautembei ipasavyo. Ikawa saa la kwanza, la pili hatimaye saa moja na nusu ilipofika alikuwa kwenye teksi akielekea Mlimani City kukutana na Tom.
Alifika Mlimani City saa 1:48 za usiku, akiamini alikuwa amewahi sana lakini cha ajabu alimkuta Tom akiwa anamsubiri kwa hamu kubwa sana. Mariam akamsogelea sehemu aliyokuwa amekaa akitetemeka kwa woga, hakuamini kama aliyekuwa amekaa mbele yake alikuwa Tom.
“Habari yako mrembo?” Tom akamsalimia.
“Nzuri! Mbona tumekaa sehemu ya wazi kiasi hiki? Kumbuka wewe ni mtu maarufu na isitoshe ndoa yako ipo mbioni kufungwa, huogopi wapiga picha wa udaku?”
“Wapo wanaosimamia hilo, siyo rahisi kupigwa picha, vijana wangu wapo kazini!”
“Sawa basi, sema ulikuwa unasemaje?” Mariam akauliza akiwa mtulivu sana.
Tom hakuongea chochote zaidi ya kutoa kadi na kumkabidhi. Mariam akaifungua na kuisoma, ilikuwa ni kadi ya mwaliko wa harusi yake ambayo ilikuwa inafanyika siku tatu zilizofuata.
“Umeamua kuja kunitukana? Hujatosheka na mateso uliyonipa?”
“Tulia mrembo huwezi kujua nina maana gani, lakini naomba usiache kuja, nina bonge la surprise kwa ajili yako!”
“Surprise?”
“Ndiyo, niamini tafadhali, naomba usipuuze!”
“Lakini wewe siku hiyo ndiyo unaoa na unafahamu kabisa ni kiasi gani nakupenda, unataka niumie moyo wangu kwa mara nyingine?”
“Sina maana hiyo Mariam, nakuomba uje halafu nakuhakikishia furaha. Amini siku hiyo itakuwa ya furaha kuliko zote zilizowahi kutokea katika maisha yako!” Tom alitumia kila aina ya maneno matamu kumshawishi, mwishowe akakubali.
Akatoa bahasha ya khaki ambayo ndani ilikuwa na milioni moja, akamkabidhi kama nauli. Mariam akakubali kufika kwenye harusi ya Tom.
******
Watu walikuwa wamefurika ndani ya meli, wakisubiria kwa hamu kubwa sana ndoa ya Julina na Tom ambayo ilikuwa ya aina yake. Ibada iliendelea kama kawaida, baadaye Mchungaji akawaita Tom na Juliana mbele kwa ajili ya kuwafungisha ndoa. Watu walipiga vigelegele na makofi wakiwashangilia.
“Je, Bi. Juliana David Mongara, umekubali kuolewa na Bw. Thomas Chacha, awe mumeo, kwenye shida na raha, taabu na matatizo? Umpende, kumtunza na kumheshimu siku zote za maisha yako, hadi kifo kiwatenganishe?” Mchungaji Samwel Kiswele aliuliza.
“Ndiyo Mungu anisaidie!” Juliana akajibu akimtizama Tom machoni mwake, moyo wake bado ulikuwa na wasiwasi mwingi.
Baada ya hapo Mchungaji Kiswele akamgeukia Tom na kumuuliza; “Je, Bw. Thomas Chacha, umekubali kumuoa Bi.  Juliana David Mongara, awe mkeo, kwenye shida na raha, taabu na matatizo? Umpende, kumtunza na kumheshimu siku zote za maisha yako, hadi kifo kiwatenganishe?” Hilo lilikuwa swali gumu sana kwa Tom, akamwangalia Juliana usoni kisha akarudisha macho yake kwa waalikwa, yakagongana na ya Mariam.
Machozi yakaanza kumtoka.
“HAPANA MCHUNGAJI SIPO TAYARI!” Watu wote wakapingwa na butwaa. Juliana akiwa haamini alichokisikia, Tom akatoka mbio na kwenda kumshika Mariam mkono, ambaye mpaka wakati huo alikuwa haelewi kinachoendelea, akamwongoza hadi mbele. Akatoa pete iliyokuwa mfukoni mwake, kisha akachukua kidole cha Mariam na kumvalisha.
“Kuanzia sasa, wewe ndiye mchumba wangu na ninakuahidi sitakutesa katika siku zote za maisha yako! Tumuombe Mungu siku ya ndoa yetu ifike. Sherehe hii ni kwa ajili ya kumvalisha mchumba wangu Mariam pete ya uchumba, aliyonifanyia Juliana yanatosha!” maneno hayo yalipenya moja kwa moja masikioni mwa Juliana, hakuamini alichosikia,
Ghafla akahisi kizunguzungu, akaanza kuporomoka taratibu, mwisho akaanguka chini kama mzigo.
Je, nini kitaendelea? Nini kitampata Juliana?
KUPATA SIMULIZI TAMU ZAIDI JIUNGE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK
 LIKE HAPA >>>>>>>>www.facebook.com/2jiachie


Beyond Love- 19
Ikiwa imebaki wiki moja tu kabla ya ndoa ya Juliana na Tom, Juliana anamsaliti Tom kwa kutembea na rafiki yake wa karibu sana aitwaye Joseph! Tom anashuhudia kwa macho yake jinsi mpenzi wake aliyempenda Juliana akifanya uchafu katika kitanda chao.
Haikuwa rahisi kuvumilika, Tom akaanguka chini kama mzigo! Baadaye akazinduka akiwa katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam. Muda mfupi baadaye anatoekea Juliana ambaye analia na kuomba msamaha.
Tom anakubali kumsamehe na wanakubalina kufungua ukurasa mpya! Taratibu za ndoa zinaendelea kama kawaida, ingawa akilini mwa Tom kulikuwa na kitu kingine zaidi, alipanga kumuumiza Juliana siku ya ndoa yao.
Alichokifanya ni kukutana na mpenzi wake wa zamani Mariam ambapo alimuomba sana asiache kuhudhuria hasuri yake ambayo ilipangwa kufanyikiwa ndani ya meli katikati ya Bahari ya Hindi. Mariam anakataa lakini baada ya kumshawishi kwa muda mrefu akakubali.
Siku ya ndoa, Juliana alipoulizwa na Mchungaji kama alikuwa tayari kuolewa na Tom alikubali, lakini Tom alipoulizwa kama alikuwa tayari kumuoa Juliana alikataa. Muda mfupi baadaye akamwita Mariam mbele na kumvalisha pete ya uchumba mbele za wageni waalikwa.
Watu walishangaa sana, Juliana akashikwa na uchungu mwingi sana, akashindwa kuzuia hisia zake, akaanguka chini na kupoteza fahamu. Je, nini kitatokea? SONGA NAYO....

Ukumbi mzima ulikuwa kelele tupu, utulivu uliokuwepo awali ulitoweka ghafla. Kulikuwa na makundi mawili katika kelele zile, wapo waliokuwa wakimsapoti Tom na wengine waliokuwa wakipingana naye. Waliokubaliana na Tom ni wale waliokuwa wakifahamu vizuri historia yake na Mariam.
Mama yake Tom hakuamini kilichotokea, akaenda mbele haraka akimfuata mwanaye. Wakati huo huo wengine walikuwa wakimchukua Juliana na kumpeleka kwenye chumba cha Huduma ya Kwanza kwa ajili ya kumhudumia.
Dakika moja baadaye mama Tom alikuwa ameshafika mbele baada ya kujipenyeza katikati ya watu waliokuwa wakizozana kutokana na tukio lililokuwa limetokea siku hiyo. Tom hakuwa na habari kabisa na mama yake, aliendelea kumkumbatia Marima huku machozi yakimtoka.
Mariam hakuamini kabisa kilichokuwa kikitokea, alihisi kama alikuwa katika njozi kali na pengine baada ya muda mfupi angezinduka. Hata hivyo baada ya kutingisha kichwa chake kwa nguvu aligundua kwamba hakuwa anaota kama alivyokuwa akifikiria.
“Tom mwananu, umefanya nini?” Mama Tom akamuuliza mwanaye.
“Unaaminisha nini mama?”
“Kwanini unatuharibia sherehe?”
“Sijaharibu sherehe mama, sherehe iliyopo hapa ni ya kumvalisha pete ya uchumba Mariam, hiyo ndoa yangu na Juliana haipo na wala sitaki kuisikia!”
“Kwanini hukusema mapema kuliko kuja kumuaibisha mwenzio na familia yake?”
“Ilikuwa lazima nifanye mama!”
“Kwanini unasema hivyo?”
“Naomba MC anipe kipaza sauti nitoe sababu za msingi za mimi kukataa kumuoa Juliana dakika za mwisho, najua mnanihukumu bure na hiyo ni kwasababu hamjui kilichotokea. Nipeni nafasi niseme ukweli!” Tom akasema akimtizama mama yake kwa makini sana.
Mama Tom akatoka na kumfuata MC ambapo alimuomba kipaza sauti na kumpelekea Tom ambaye bila kuchelewa alianza kuzungumza.
“Najua wengi mnanilaumu kwa kitendo changu cha kukataa kumuoa Juliana, lakini naamini nikiwapa sababu za msingi mtanionea huruma. Hata wewe mama yangu ambaye umekuja hapa mbele na kunisema kwamba nimekuabisha, utagundua kuwa Juliana ndiye aliyekuabisha.
“Naamini hata wazazi wa Juliana na ndugu zake wote watajua wazi kwamba mtoto wao ndiye aliyeleta aibu hii katika hii sherehe. Juliana hafai kabisa, ni mwanamke mwenye sura ya kike lakini siyo mke.
“Nilimpenda sana Juliana, moyo wangu nikamkabidhi yeye  nikiamini kwamba angekuwa furaha ya maisha yangu, lakini imekuja kuwa tofauti. Juliana ameniumiza sana, amenitesa na nina uhakika alidhamiria kuniua,” Tom alikuwa akizungumza kwa hisia sana huku ukumbi mzima ukiwa makini kumsikiliza atakachokiongea.
Mpaka wakati huo, bado Tom alikuwa hajataja sababu ya msingi ya kuachana na Juliana, hivyo watu walikuwa na shauku kubwa sana ya kutaka kujua atakachokiongea.
“Wengi wenu mnafahamu kwamba wiki moja iliyopita nilikuwa nimelazwa, lakini hamjui sababu ya mimi kulazwa, ila leo nataka kuwaelezeni ukweli kwamba Juliana ndiyo cha mimi kulazwa. Nilianguka na kupoteza fahamu baada ya kumfumania Juliana akifanya mapenzi na rafiki yangu wa karibu sana Joseph!” Tom aliposema hivyo ukumbi mzima ulipigwa na butwaa.
“Aaaaaah!” Wati wote walisikika wakiguna.
“Ni maumivu kiasi gani aliyonipa Juliana? Ni nani ambaye angeweza kuvumilia maumivu hayo? Baada ya mambo hayo kutokea, niliamua kutulia, nikawaza kwa makini sana hatua ya kuchukua. Nilijua hakuna atakayenielewa kama ningehairisha ndoa.
“Kitu cha msingi ambacho kilikuwa kichwani mwangu ni kuacha taratibu zote ziendelee lakini akilini nikijua kwamba itakuwa ni sherehe ya kumvalisha Mariam pete ya uchumba na siyo ya ndoa yangu na Juliana. Nilikumbuka mengi aliyonifanyia Mariam, nikasikia uchungu sana.
“Mariam alinisaidia sana wakati nikiwa na shida, aliiba gari lao na kumpeleka baba yangu hospitalini akiwa hoi usiku wa manane. Kwa bahati mbaya wakati anarudi  nyumbani, alipata ajali mbaya na kulala kitandani akiwa hajitambui kwa zaidi ya miaka minne!
“Yote hayo alifanya kwa ajili yangu, sikuwa na zawadi nyingine ya kumpa zaidi ya penzi la kweli kwake. Hiyo ndiyo zawadi ya pekee ambayo naona inamfaa kwa wema wote alionitendea. Mariam alikuwa katika hatari ya kufa, kupoteza fahamu kwa zaidi ya miaka minne ni nusu ya kufa, inawapasa wote mfahamu kwamba Mariam alikuwa katika hatari hiyo kwa ajili ya penzi lake kwangu!
“Kwanini nimuumize tena? kwanini nimtese tena? Pamoja na utajiri nilionao sasa, usaliti wa Juliana ulinifanya nikumbuke maisha yangu ya dhiki na taabu. Ni kitu gani alichokikosa kwangu hadi aanze kutembea na Joseph? Huyo Joseph ana nini ambacho mimi sina? Kwa hakika Juliana alinipa kidonda kikubwa sana katika moyo wangu lakini sasa nimeshapata tiba.
“Mariam ni tiba tosha katika maisha yangu. Naomba sherehe iendelee lakini ikumbukwe kwamba ni sherehe ya kumvalisha mchumba wangu Mariam pete, ni matumaini yangu kwamba siku chache zijazo, mtashuhudia ndoa yetu nzuri sana, itakayopendeza!” Tom alisema watu wakiwa kimya kabisa kumsikiliza.
Maneno aliyoongea yalikuwa makali san, watu wote walimwonea huruma, lakini wapo waliompongeza kwa ujasiri wake.
“Ana moyo sana huyu mtoto!” Mama mmoja aliyealikwa alimwambia mwenzake.
“Ni kweli, kama ni mtu mwingine asingeweza kuvumilia!”
“Lakini kuna kitu nahisi!”
“Kitu gani?”
“Unajua kwa jinsi Mariam alivyomsaidia, ilikuwa lazima arudiane naye siku moja!”
“Kwanini unasema hivyo?”
“Mapenzi yana nguvu sana ndugu yangu, kama mtu aliweza kuhatarisha uhai wake kwa sababu ya mapenzi, unadhani uhusiano wa aina hiyo unaweza kufa hivyo?”
“Kweli kabisa, mwacheni Mungu aitwe Mungu!”
“Yeye ni kila kitu, akisema iwe na inakuwa hivyo, akisema hapana, inakuwa hapana. Hakika yeye ni mwema!” Kila mtu alikuwa akiongea lake latika ukumbi huo uliokuwa kwenye Meli.
Sherehe ikaendelea kama kawaida, ingawa utaratibu haukuwepo na hakuwa na utaratibu wa kutoa zawadi. Walishauriwa warudi nazo kwanza hadi siku ya ndoa ya Mariam na Tom. Watu walikunywa, kula na kusaza.
“Tom!” Mariam alimwita walipokuwa wamejibanza kwenye eneo lenye giza totoro.
“Nakusikiliza mpenzi!”
“Umenishangaza sana!”
“Kwanini?”
“Sikutegemea!”
“Hata mimi pia, lakini leo nimeamini kwamba Mungu yupo na akipanga lake hakuna yeyote chini ya jua anayeweza kupangua. Nakuhakikishia Mariam, Mungu alipanga mimi niishi na wewe!”
“Ni kweli mpenzi wangu, tumetoka mbali!”
“Kweli kabisa, nakuhakikishia utafurahia maisha siku zote za uhai wako ukiwa na mimi. nataka kulipa fadhila zote kwako, nataka kukuonyesha kulala kwako kitandani kwa zaidi ya miaka minne ukiwa huna kumbukumbu ya chochote kinachoendele haikuwa bure!”
“Nitashukuru sana mpenzi wangu!”
“Mariam mpenzi!” Tom akaita kwa sauti iliyojaa mahaba.
“Naomba unifanyie kitu kimoja....”
“Sema tu, mpenzi!”
“Naomba unibusu!”
“Hilo tu, sema lingine!”
“Siyo zaidi ya busu lako!”
“Haya bwana! Mmwaaaaaaaaa...” Mariama akamuangushia Tom busu maridhawa kabisa.
“Ahsante sana mpenzi!”
Baada ya sherehe kuisha, meli ilirudi hadi Bandarini na kutia nanga, watu wakashuka na kutawanyika. Tom akampeleka Mariam Hotelini kwake. Mapenzi yao yakarudi upya, yalikuwa motomoto.
******
Mwezi mmoja baadaye taratibu zote zilikuwa zimeshakamilika. Tom alitambulishwa rasmi nyumbani kwa akina Mariam kama mchumba wa Mariam, wazazi wa Mariam hawakuwa na kipingimizi. Waliruhusu watoto wao waendelee na mapenzi yao kutoakana na ukweli kwamba walianza kupendana muda mrefu kabla wakati wanasoma.
Mipango ya ndoa ikafanyika haraka sana, ilipangwa kufanyika ndoa ya kifahari kuliko kawaida. Kama ilivyokuwa wakati akitaka kufunga ndoa na Juliana ndivyo alivyofanya pia safari hii, aliamua kufunga ndoa yake katikati ya Bahari ya Hindi, wakiwa kwenye meli.
Ndivyo ilivyokuwa, siku ya harusi ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa ilifika, waalikwa walikuwa ni wengi sana. Mariam na Tom walikuwa haamini kabisa kilichotokea, walikuwa na nyuso za furaha sana kufunga ndoa yao.
Mchungaji akawaita mbele wakiwa na wapambe wao, ambapo mara moja shughuli ya kuwafungisha ndoa ikaanza.
Je, Bw. Thomas Chacha, umekubali kumuoa Bi.  Mariam Isaya, awe mkeo, kwenye shida na raha, taabu na matatizo? Umpende, kumtunza na kumheshimu siku zote za maisha yako, hadi kifo kiwatenganishe?” Hilo lilikuwa swali rahisi sana kwa Tom, akamwangalia Mariam usoni kisha akarudisha macho yake kwa waalikwa, baada ya hapo akajibu.
“Ndiyo, Mungu anisaidie!” Ukumbi mzima ukapiga vigelegele na makofi kwa furaha.
Baada ya Tom kujibu, Mchungaji aliyekuwa akifungisha ndoa akamgeukia Mariam na kumuuliza; “Je, Bi. Mariam Isaya, umekubali kuolewa na Bw. Thomas Chacha, awe mumeo, kwenye shida na raha, taabu na matatizo? Umpende, kumtunza na kumheshimu siku zote za maisha yako, hadi kifo kiwatenganishe?”  Mchungaji akamuuliza lakini Mariam hakujibu.
Mchungaji akaamua kuuliza kwa mara ya pili, bado Mariam alikuwa kimya. Ghafla Mariam akaanza kutoa miguno ya taratibu, baadaye akashindwa kujizuia na kuanza kuangua kilio. Tom akashtuka sana, hata waalikwa nao walipigwa na butwaa.
“Mariam kuna nini?”
“Hakuna!”
“Mbona hujibu maswali ya Mchungaji!”
“Hapana...”
“Hapana nini?” Tom akazidi kumuuliza akiwa haelewi kinachoendelea. Mariam alizidi kulia.

Je, kuna nini? Kwanini Mariam analia?
Beyond Love- 20
Tom haamini macho yake alipomkuta mpenzi wake ambaye walikuwa na mipango ya kufunga ndoa, Juliana akimsaliti, tena na rafiki yake wa karibu aliyeitwa Joseph.
Lilikuwa tukio lililomsononesha sana, hali iliyomsababishia simanzi, kabla ya kuanguka chini na kupoteza fahamu. Baadaye anazinduka akiwa katika Hospitali ya Ocean Road, ambapo Juliana anakuwa wa kwanza kuonana naye na kumuomba msamaha.
Tom anakubali kumsamehe na wanakubaliana kufungua ukurasa mpya! Taratibu za ndoa zinaendelea kama kawaida, ingawa akilini mwa Tom kulikuwa na kitu kingine zaidi, alipanga kumuumiza Juliana siku ya ndoa yao.

Akafanya mpango wa kukutana na mpenzi wake wa zamani Mariam ambapo alimuomba sana asiache kuhudhuria harusi yake ambayo ilipangwa kufanyikiwa ndani ya meli katikati ya Bahari ya Hindi. Mariam anakataa lakini baada ya kumshawishi kwa muda mrefu akakubali.

Siku ya ndoa, Juliana alipoulizwa na Mchungaji kama alikuwa tayari kuolewa na Tom alikubali, lakini Tom alipoulizwa kama alikuwa tayari kumuoa Juliana alikataa. Muda mfupi baadaye akamwita Mariam mbele na kumvalisha pete ya uchumba mbele za wageni waalikwa.

Siku chache mbele, Mariam na Tom wakaamua kufunga ndoa! Kama ilivyokuwa awali,  ndoa yao ilifungwa katikati ya bahari, kwenye meli. Kitu cha kushangaza, Mariam alipoulizwa na Mchungaji kama alikuwa tayari kuolewa na Tom, alinyamaza.

Baadaye akaanza kulia kabisa. Tom alipomuuliza kama kulikuwa na tatizo lolote, Mariam hakujibu. Je, nini kitatokea? SONGA NAYO....

Kitendo cha Mariam kukataa kujibu swali la Mchungaji kama alikuwa tayari kuolewa na Tom au lah, kilimchanganya sana Tom, alishaanza kuhisi mchezo mchafu ulikuwa ukichezwa nyuma ya pazia. Ukimya wa Mariam ukazidi kumchanganya.

Hata hivyo alikosa raha zaidi baada ya kushangaa Mariam akianza kulia, hapo akili yake ikaenda mbali zaidi, alianza kufikiria kwamba, inawezekana Mariam alilazimishwa kumuumiza siku ya ndoa yao ili ampe maumivu lakini yeye hakuwa tayari.

Zote hizo zilikuwa hisia zilizoutawala ubongo wake, lakini mwenye majibu sahihi alikuwa ni Mariam pekee, alitakiwa kutumia kila njia anayoifahamu ili aweze kujua kilichokuwa kikiendelea. Akamgeukia Mariam wake ili amuulize kwa ajili ya kupata uhakika zaidi, tayari akili yake ilishabadilika, alipoteza matumaini ya kuwa na Mariam tena.

“Kuna nini Mariam?”

“Nishakujibu Tom.”

“Kwamba?”

“Sina tatizo.”

“Mbona unashindwa kumjibu Mchungaji, hujui kwamba ni wewe ndiye unayesubiriwa ili ndoa iweze kufungwa?”

“Najua...”

“Sasa?”

“Nashindwa kuamini kabisa.” Marim akasema akionekana kuwa na hofu sana na maneno aliyokuwa akiyaongea.

“Huamini nini tena? Kwani kuna nini?”

“Nashindwa kuzuia hisia zangu Tom, nimeshindwa kabisa.”

“Hisia za nini tena?”

“Machozi Tom, unajua wewe ndiye mwanaume pekee ambaye nilikukabidhi moyo wangu, siamini kabisa kwamba nimeweza kuwa na wewe tena katika ndoa!” Mariam akasema machozi yakizidi kumtoka.

“Amini mpenzi wangu...mwambie basi Mchungaji aendelee kwanza, haya mambo mengine tutazungumza wenyewe baadaye,” Tom alisema akiwa haamini kama Mariam hatamkataa, akili yake ilimtuma moja kwa moja kwamba lazima Marim angemkataa ili amuumize kama ambavyo yeye alivyomuumiza siku alipokutana naye Chuo Kikuu alipokwenda kutoa semina ya Ujasiriamali. 

“Mchungaji unaweza kuendelea....” Mariam akamwambia Mchungaji.

“Nini kilitokea?” Mchungaji akauliza.

“Hakuna...” Mariam akajibu.

“Hpana...kuna kitu mnanificha. Kama kuna tatizo liwekeni wazi.”

“Hakuna Mchungaji, niamini mimi, hakuna kitu kingine zaidi ya furaha. Siamini kabisa kwamba leo naolewa na Thomas.”

“Hilo tu.”

“Kwani dogo Mchungaji? Kuolewa na mwanaume ambaye unampenda kwa moyo wako wote, nafikiri ni jambo la baraka sana!”

“Ni kweli kabisa, sasa naweza kuendelea Mariam?’

“Bila shaka.” Maram akajibu akionyesha tabasamu pana kabisa lililochanua vyema usoni mwake.

Muda wote huo Kanisa lilikuwa kimya kabisa, wakisubiri kitakachoendelea. Baadaye Mchungaji akamgeukia Mariam, ambaye sasa machozi yake yalishafutika na alikuwa akitabasamu muda wote kwa furaha. Mchungaji akamuuliza; “Je, Bi. Mariam Isaya, umekubali kuolewa na Bw. Thomas Chacha, awe mumeo, kwenye shida na raha, taabu na matatizo? Umpende, kumtunza na kumheshimu siku zote za maisha yako, hadi kifo kiwatenganishe?” Mchungaji akauliza, safari hii akiwa mtulivu sana.

“Ndiyo, Mungu anisaidie!” Mariam alipojibu jibu hilo, ukumbi mzima ulilipuka kwa vigelegele, makofi na vifijo.

Tom hakuamini kama ni kweli Marim alikuwa ameamua kuolewa naye. Aliendelea kuwa na mashaka hadi pale waliposaini pamoja katika vyeti vya ndoa. Baada ya hapo sherehe iliendelea hadi usiku kabisa ambapo meli ilirudi hadi Bandarini, ikatia nanga, wageni wakaanza kushuka na kwenda kuingia moja kwa moja kwenye magari kwa safari ya kurudi majumbani mwao.

Ilikuwa sherehe iliyopendeza sana, huo ukawa mwanzo wa maisha mapya ya ndoa, kati ya Tom na Mariam. 

********

Maisha yao ya ndoa yalikuwa ya furaha sana, lakini tatizo lilikuwa moja tu, Tom alikuwa mtu wa starehe sana. Kila siku alikuwa haishi kwenda kwenye majumba ya starehe na kurudi usiku wa manane. Kisingizio chake siku zote kikawa ni kazi nyingi alizonazo.

Ingawa Mariam alikuwa na elimu nzuri, lakini Tom alimzuia kufanya kazi kwa kisingizio kwamba atamdharau. Siku zote Mariam alikuwa akijitahidi sana kumuelewesha Tom juu ya hilo lakini hakumuelewa.

“Na kwanini unalazimisha sana kufanya kazi?”

“Napenda mume wangu.”

Kuna unachokosa kutoka kwangu?”

“Sina maana hiyo.”

“Sasa kwanini unang’ang’ania kufanya kazi? Mimi nina uwezo na ninakutimizia kila kitu, nini kinachokufanya utafute kazi?”

“Ni vizuri kila mmoja akatoka, unajua ninapokaa hapa ndani nalemaa.”

“Unalemazwa na nini?”

“Lakini kwanini nimesoma sasa kama nilikuwa sina haja na kazi? Elimu yangu inanisaidia nini kama sitaitumikia jamii?”

“Hiyo jamii na mimi, ni nani mwenye umuhimu zaidi kwako?”

“Ni wewe mume wangu.”

“Basi sihitaji ufanye kazi.”

“Nimekuelewa ila kuna kitu kingine nataka tuzungumze.”

“Juu ya nini tena?”

“Tom mume wangu, umekuwa ukichelewa sana kurudi nyumbai, wakatiu mwingine unanikuta nimeshalala kabisa, uwe unajitahidi basi kuwahi kidogo!”

“Mariam una nini leo? Kwanza niwahi kuja kufanya nini? Mimi napika?”

“Hupiki, lakini unatakiwa kuja kula na mimi, ndiyo mapenzi hayo mume hayo mume wangu.”

“Nimekuelewa!” Tom akajibu kwa kifupi kisha akaondoka.

Maisha yao hayakuwa na furaha kama ilivyokuwa mwanzo, Tom alikuwa hana muda maalum wa kurudi nyumbani. Mbaya zaidi alirudi akiwa amelewa sana na hakutaka kula chakula cha mkewe. Jambo hilo lilimkosesha sana raha Mariam lakini hakuwa na jinsi, aliamua kuvumilia akiamini siku moja angebadilika.

*******

Ilikuwa siku ya Jumamosi usiku, ndani ya Ukumbi wa 56 Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Watu walikuwa wamejaa sana kushuhudia uzinduzi wa albamu mpya ya Bendi ya Kigingi Music Band ambapo pia mbali na uzinduzi wa albamu yao mpya, pia walikuwa wakiwatambulisha wanamuziki wapya walionunuwa na Tom ambaye ambaye alikuwa akiitwa Papaa Bill.

Pesa haikuwa tatizo, Papaa Bill (Tom) aliwanunua wanamuziki hao kutoka nchini Congo ambapo walikuwa wakifanya kazi katika bendi kongwe za muziki nchini humo, lakini kwa fedha alizokuwa nazo Papaa Bill, aliweza kuwaleta Tanzania na kuwalipa fedha nyingi sana.

Baadhi ya watu walikuwa wakimsikia tu Papaa Bill kwenye vyombo vya habari hasa magazeti na redio, lakini walikuwa hawajawahi kumuona. Kati ya hao alikuwa ni Mayasa. Msichana ambaye alikuwa na hamu kubwa sana ya kumuona Tom.

Mayasa alikuwa na nia zaidi ya kumfahamu, yeye alipanga kumuweka mkononi mwake. Pamoja na kusikia kwamba alikuwa na mke, lakini kwake halikuwa tatizo, alishaandaa mbinu za kutosha kwa ajili ya kumsana Tom. Huyu ni Mayasa wa Mbagala jijini Dar es Salaam.

Usiku huo alikuwa amevalia gauni jepesi sana linaloonesha kila kitu ndani! Kwa mwanaume yeyote ambaye hana matatizo, ilikuwa lazima ashtuke sana pindi atakapokutanisha uso wake na Mayasa. Kiasili alikuwa maji ya kunde, lakini mkorogo ulifanya kazi yake ambapo alionekana mweupe sana isipokuwa kwenye viungio vya ugoko wa miguuni na mikono, ambapo kutokana na ngozi kuwa ngumu sana, haikuweza kuchunika kwa mkorogo!

“Leo lazima nimuone huyo Papaa Bill!” Rafiki yake na Mayasa alisema.

“Bora wewe unayetaka kumuona, miye naondoka naye kabisa...” Mayasa alisema akionyesha kuwa na nyodo za wazi kabisa.

“Haya tuone. Unafikiri Papaa Bill ni sawa na hao wanaume wako wa Mbagala, huyu ni matawi ya juu.”

“Sasa nitajua kama Mbagala ipo Dar es Salaam au Lindi?” Mayasa alisema akionyesha kujiamini sana.

Dakika chache baadaye, wakati wakiendelea na mazungumzo yao, Mc wa siku hiyo, alisimamisha muziki kwanza kisha akamuomba Papaa Bill atoke mbele ya jukwaa ili awatambulishe wanamuziki wapya. Papaa Bill akatoka.

“Ninayo heshima kubwa sana, kumkaribisha Papaa Bill a.k.a Tom ili aje awatambulishe wanamuziki wetu wapya. Kwa taarifa tu ni kwamba, pamoja na kwamba yeye ndiye anayewalipa wanamuziki hao mishahara pamoja na kuwanunua, pia ndiye aliyeenda kuwachukua mwenyewe Congo!” Mc aliposema maneno hayo, ukumbi mzima ukashangilia.

Tom ‘Papaa Bill’ akapanda jukwaani kwa mbwebwe sana, jioni hiyo alikuwa amevalia suruali yake ya jeans ya rangi ya blue na fulana ya kubana ya rangi nyeupe. Mikononi na shingoni alichafuka cheni za madini ya fedha!

“Sina mengi ya kuongea, naomba niwatambulishe wanamuziki wetu wageni ambayo mimi mweny....” Tom alishindwa kumalizia sentesi yake, baada ya kugonganisha macho yake na Mayasa.

“Haki ya nani tena, sijawahi kukutana na mwanamke mzuri kiasi hiki! Mh...wa wapi huyu?” Tom aliwaza akiwa amezidiwa vilivyo na hisia kali za mapenzi.

Kwa hali aliyokuwa nayo, alikuwa tayari kumsaliti Mariam wake.

“Naitwa Tom....bila shaka mimi ni Tom a.k.a Papaa Bill...namuhitaji huyu mwanamke, ni lazima nilale naye, lazima...” Tom akawaza huku akimtizama kwa matamanio.

Wakati huo Mayasa ndiyo akazidisha vituko, akapandisha gauni lake juu zaidi na kuacha sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa wazi. Tom akasikiza mwili wake ukipiga shoti!
Je, nini kitatokea? Tom amejikuta akimtamani Mayasa ghafla bila kujua kwamba Mayasa naye alikuwa akimuwinda.

KUPATA SIMULIZI TAMU ZAIDI JIUNGE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK
 LIKE HAPA >>>>>>>>www.facebook.com/2jiachie


No comments

Powered by Blogger.