TUZO ZA MTV: WEMA, DIAMOND WACHAFUA HALI YA HEWA
JAMBO limezua jambo. Pamoja na kuanza kwa kishindo safari yake ya kuelekea
Afrika Kusini ‘Sauz’ kwa ajili ya fainali za kuwania Tuzo za MTV Africa (MAMA),
mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na baby wake, Wema Isaac Sepetu
wamechafua hali ya hewa.
Billicanas.
Pamoja na kufanya makamuzi ya kufa mtu kwenye shoo ya kuwatambulisha
wasaniiwanaowania tuzo hizo kwenye Ukumbi wa Bilicanas uliopo Posta, Dar, Diamond
hakumpandisha Wema stejini kama kawaida yake, jambo lililozua kizaazaa.
Kuna muda mashabiki wake walipiga kelele wakimtaka Wema apande stejini lakini
hakufanya hivyo.
Awali Diamond alipanda stejini mishale ya saa 8:00 akipishwa na msanii kutoka Sauz,
Jigger ambaye alikuwepo kwa ajili ya kutoa sapoti kwa Mbongo Fleva huyo.
Msauz huyo alifanya shoo ya dakika 20 kisha akampisha Diamond ambaye aliingia na
Kibao cha Uswazi Take Away Remix, ambacho ndani yake amemfagilia
Halima Haroun ‘Kimwana’ ambaye ni hasimu wa mpenzi wake, Wema.
Baada ya kumaliza wimbo huo ndipo baadhi ya mashabiki wakasikika wakimwambia
Diamond ampandishe Wema la sivyo watakinukisha.
Ishu hiyo iliendelea hadi jamaa aliposhuka stejini hapo.
Wakati Diamond akiendelea kufanya makamuzi yake hayo, Wema na Halima Kimwana wote walikuwepo ukumbini hapo na kwa bahati nzuri kama si mbaya walijikuta wote wakimshangilia Diamond, tena wakiwa VIP ya juu ambapo walikuwa wakiingia watu maalum.
Mwanahabari wetu aliwashuhudia wawili hao walipogeukiana kila mmoja alionekana kumwekea mwenzake uso wa mbuzi.
Hali hiyo ilidumu hadi Diamond alipomaliza shoo yake na Wema kushuka na kumuacha Halima Kimwana.
Baada ya shughuli za shoo Diamond alibaki na Halima Kimwana wakicheza disco.
Kufuatia hali hiyo kwenye mitandao ya kijamii usiku huohuo, kuliibuka maneno mengi
kutoka kila upande kuwa shoo ya Diamond ilichafuliwa na Wema na Halima Kimwana ambaye alidaiwa alijipanga kwenda kumfanyia fujo Wema kwa kuwa yupo upande wa Penniel Mungilwa ‘Penny’.
CHANZO: IJUMAA WIKIENDA/GPL

Post a Comment