RIWAYA: SIKU YA GRADUATION...SEHEMU YA TISA
SEHEMU YA TISA
Baada ya kuagana na Wazee pale kijini safari ya kuelekea mjini ikaanza, Tulitembea kwa umbali mrefu bila ya kuona nyumba zingine tofauti na zile za awali tulipokua tumepata hifadhi, sikuweza kutambua tulikua katika kijiji gani kwa maana sikupata hata nafasi ya kufanya hivyo kutokana na Shauku na kiu yangu ya kufika mjini ili nijue nini kinafuata ili kuona haki ikitendeka , Hamu yangu kuu ni kuona Ramla na huyo hawara yake Pablo Mwaki wakiadhirika mbele ya macho yangu kwa uovu na unyama waliotutendea japo hatukustahiki kutendewa yale,
Wakati safari ikiendelea nilikua nikitafakari na kujenga darasa huru kichwani mwangu kufuatia kadhia hii iliyotukumba, japo nimepata taabu na kuteseka sana bado kuna vitu nilivichukulia kama sehemu ya darasa kubwa katika maisha yangu na katika maisha ya mtu mwngine yeyote atakaebahatika kuipata kwa kina simulizi ya haya yaliyotokea, kila nilipomuangali Ntahondi ambae alionekana kua bado hajamini kua walau sasa tuko kwenye mikono salama nilifikiri mambo mengi sana, nilianza sasa kuitambu a Nguvu ya Wanawake katika baadhi ya mambo muhimu, niliamini kua bila Ntahondi nisingekua pale muda ule..
Safari ilikua ndefu na sasa hatimae tukatokea katika wilaya ya bagamoyo mkoa wa pwani na hapo ndipo nikaanza kupata picha sasa ya Muelekeo wa tunapotoka na tunapoelekea, Gari ilishika kasi barabara kuu ya kuelekea sasa jijini Dar Es Salaam, nilifarijika sana kuanza kuyaona mandhari ya mji ambayo kwangu sikutegemea tena kuyaona maana kuponyoka kwa wale Maharami ni sawa na Ngamia kupenya kwenye Tundu la sindano, Mwl Honde kila alipojaribu kutuongelesha tulimjibu tu ili mradi tumemjibu lakini kila mtu alikua akiwaza yake kichwani.. kilichonishtua zaidi ni pale Honde alipotuambia kua kwa sasa Ramla ni mjamzito na kila mtu ameshajua pale chuoni, ni mimba ya Pablo. Japo siku na hamu tena ya kua na Ramla ila roho ilizidi kuniuma tu..
Baada ya Safari Ndefu tuliingia sasa jijini Dar na moja kwa moja msafara ukaendelea kwa kasi kuelekea maeneo ya Msasani, na baada ya magurudumu ya Gari kuzunguka kwa kasi nzuri tu hatime breki zilipigwa mbele ya Nyumba moja kubwa, Nzuri, na ya kifakhari iliyo zungushiwa Fance kubwa iliyonakshiwa kwa kila aina ya mapambo, baada ya kusimama pale akateremka Mwl Honde na kwenda moja kwa moja Getini kuongea na Askari walinzi waliokua pale Mlangoni kasha baada ya mazungumzo yao mafupi walifungu geti kasha gari yetu ikaingizwa ndani, tulipofika ndani ya geti hili kubwa Tukapokelewa na kijana mmoja Mrefu, maji ya kunde, aliyeonekana kujazia vizuri misuli yake licha ya Suti aliyokua ameivaa lakini bado alionekana vema kua ni mwana mazoezi mzuri tu, baada ya kutupokea akatuongoza ndani kabisa ya Mjengo ule
Tulietembea katika korido ndefu mpaka katikati ambako wote tulisimama na kisha kijana huyo mwenye Suti nyeusi akagonga Kengele, wakati huu sasa tulia wane tu Mimi, Ntahondi, Mwl Honde, na huyu kijana alievaa suti nyeusi, wale Askari walibaki nje wakiwa pamoja na Oscar na baada ya kama dakika mbili hivi mlango ukafunguka kisha tukaingia ndani, tulpofika ndani tukapokelewa na watu waliokua mule ndani, kwa haraka haraka niliweza kuwatambua wawili tu kwa kua nilikua nikiwaona mara kadhaa kwenye vyombo vya habari, wakwanza alikua ni Mhe Abraha Honde waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzani, na wapili ailiku ni Mhe Stanley Kalokola KalokolaWaziri wa Mambo ya ndani, huyu watatu sikumtmbua kwa haraka. Baada ya mapokezi hayo tukakaribishwa kwenye viti kasha tukaketi, Waheshimiwa hawa walionekana kuumizwa na kusononeshwa na kitendo kile cha sisi kuteswa kikatili kiasi kile maana hapo tulipokua tulikua Tumepauka vuu kama nyani, michiirizi ya damu ikiwa imeganda mwilini, mimi nikiwa na jeraha kubwa kichwa nillolipata wakati ule tunakirikishana na Yule Baunsa kule Msituni, Ntahondi akiwa kaumia zaidi miguuni kutokana na kukanyaga visiki vikavu vya miti wakati tunakimbia kule Porini,
Baada ya kuketi tu kijana huyu alianza kututambulisha kwa waheshimiwa hawa, na hapo ndipo nikamjua huyu mtu wa tatu, aliitwa Mhe Florent Samwel ndie Mkurugenzi mkuu wa idara ya Usalama wa taifa baada ya hapo nae akajitambulisha kwetu kua ni Captein John Makala, kilinishangaza kijana huyu alionekana kutujua vizuri maana alipomaliza kutupa utambulisho wao sasa akatutambulisha sisi kwa Mhe Waziri kwa kututaja majina mpaka na ubini, alianza kwa kunitaja mimi kua ni Naufal Mpodobakshi kisha akafuatia kwa Ntahondi Salum na baada ya hapo akamuachia nafasi ya kuongea Mhe Waziri Mkuu ambae akaanza kuongea kwa utulivu mkubwa
“Kwanza poleni sana kwa matatizo yaliyowakuta, hizo ni changamoto katika maisha ya kila mwanadamu na ili mkabiliane nazo inabidi kwanza mzikubali, Matatizo yaliyowakuta pia yametusaidia sisi kuzidi kumpeleleza sana huyo anaedhaniwa kuhusuika na matatizo haya na sasa tunavitu vingi sana tumevipata kama ushahidi wa umafia na uharamia wa huyu mtu” ila kabla hatujafika mbali zaidi hebu tuambieni ilikuaje huko mlikotekwa maana wewe Naufal huku pia una kesi ya kujibu kuhusu tuhuma za kukutwa na mwili wa Yule dereva wa Tax alieuwa“ Nikaanza mimi kuelezea Story nzima jinsi ilivyokua, kwa kweli hadithi ilikua ni ndefu ya kuumiza na kusisimua nilielezea kwa ufasaha bila kuruka hata nukta moja, story hii ilionekana kumuingia sana Mhe Waziri wa Mambo ya ndani nikaona anaingiza mokono mfukoni na kutoa Leso kisha akawa anafuta machozi, ksha baada ya hapo ikawa zamu ya Ntahondi ambae aliongea mengi sana mpaka siku aliyokamatwa na kuteswa kinyama japo alishindwa kuimalizia story hii akaanza kulia, ikabidi Waziri Mkuu ambembeleze na kasha akaanza sasa kuonge waziri wa mambo ya ndani
“Huyu Pablo ni mtu hatari sana, ana pesa chafu nyingi zisizojulikana hata amezipata wapi lakini kwa uchunguzi wa kina tulioufanya tuligundua kua huyu bwana mwaka 1998 alifungwa jela kwa kosa la mauaji ya Muuza Madini kutoka mererani, inasemekana alimuua na kumdhulumu pesa nyingi sana Lakini mwaka 2000 alikata rufaa na kushinda kesi yake ambayo nasikia alihonga pesa nyingi sana kwa baadhi ya mahakimu, baada ya kurudi huku uraiani akawa anajihusisha sana na Biashara za wizi wa magari kabla ya kuanza kujihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya. Mtu huyu ni hatari sana amewanunua watu wengi sana katika vitengo tofauti ambao ni vibaraka wake kila kona, anao mapolisi, waandishi wa habari, mahakimu, nk na kesi zote za mauaji aliyoyafanya tuna ushahidi wote juu ya meza, sasa na hiyo ya kumuua huyo dereva wa Tax nayo tunaiingiza kwenye List” Mhe Waziri alikua akiongea kwa hasira sana iliyotamalaki usoni machoni mwake
“Habari tulizo nazo ni kwamba zimebaki wiki mbili tu ifanyike hiyo Graduation ambapo PABLO anataka kumvisha pete ya Uchumba huyo binti aitwae Ramla ambae nae anapaswa kukamatwa kwa kushiriki tendo haram la utekaji, mauaji na utesaji, hivyo mipango inasukwa ya kuwakamata siku hiyo na kuwapeleka mbele ya vyombo vya Sheria, na siku hiyo itapaswa na ninyi wawili muwepo hapo japo mtaku ndani ya gari maalum mpaka mtakapohitajika, tutakua na ulinzi mkali sana eneo hilo kwa sababu PABLO ni mtu hatari sana na anashirikiana na baadhi ya Maofisa wa Polisi wasio waadilfu, mipango yote inatakiwa ifanyike kwa uangalifu na usiri mkubwa, hata ndugu zenu hawapaswi kujua kua mko hapa;;” kisha akamiliza kuongea, nilimuelewa vizuri huyu Waziri alikua akijaribu kututahadharisha juu ya Nguvu za Pablo na inaonekana siku hiyo inawezekana akaja na vijana wake wa kazi ni mwisho tukashindwa kumtia nguvuni..
Baada ya mazungumzo haya Waziri mkuu akamwambia mdogo wake Mwl Honde kua atupeleke vyumbani tukaoge na kubadili nguo kasha tupewe chakula halafu tupumzike na kwamba yeye angerudi pale kesho yake, Laikini kabla hatujatoka tukaombwa tupige Picha kama ushahidi wa kila tukio linaloendelea sasa, tukapiga picha tukiwa vile vile na damu zetu kasha tukatoka kwenda vyumbani tulikopelekwa na Mwl Honde, baada ya kuoga, kubadili Nguo, na kupata chakula cha nguvu tulikaa pamoja Seating Room tukiwa Mimi, Ntahondi na Mwl Honde ambae alijaribu kutufurahisha na kututoa hofu kabisa kua tupo sehemu yenye usala mkubwa na kwamba hakuna yeyote atakaeweza kuja kutudhuru mahala pale baada masaa kama mawili Mwalimu Honde akatuaga na kuondoka zake..
Tuliishi mule ndani kwa Raha mustarehe, tukiwa na amani na furaha, huku tukiisubiri kwa hamu SIKU YA GRADUATION, Japo huku sisi tukiisubiri siku hiyo kwa lengo la kuustaajabisha umma kwa kuwatia nguvuni Pablo mwaki, Ramla, na wapambe wao, hali ilikua tofauti huko Nje ambako Graduation hii ilionekana kusubiriwa kwa hamu na watu wengi wakiwamo wanafunzi, waalimu, na watu wengine ili kushuhudia tukio lilosisimua wengi la kitenda cha PABLO Mwaki kumvisha pete ya uchumba Ramla.. amaa kweli pesa ilipasua mlima nasikia tayari mwaki alishakua kawalipa na baadhi ya waandishi wa habari kutoka katika baadhi vya vyombo vya habari kwa ajili ya kuripoti tukio hilo
Tukiwa mule ndani Ntahondi mara kwa mara alikua akilalamika kua asingeweza kuendelea kuishi peke yake kule Chumbani kwani kila ikifika usiku mkubwa alikua akishtuka na kuogopa sana, ikabidi siku moja ikabidi aje kulala huku kwangu kwa kua vyumba vyetu vilikua karibu karibu, Tuliendelea kuishi na kulala pamoja japo sasa Uzalendo ukanishinda nikajikuta nasema jambo
“Ntahondi, kuna jambo nataka kukuambia“
“Niambie tu Naufal“
“Mimi na wewe tumeteseka sana, na tumeumizwa sana na mkasa huu wote, naamini Mungu alikua na agenda yake kutukutanisha kua karibu zaidi“
“Ni kweli kabisa“
“Sababu ya mateso yote haya ni mapenzi lakini pamoja na hayo huu sio mwisho wa kupenda“
“Ni kweli, na mie nakuombea kwa Mungu umpate mwingine mwenye mapenzi ya dhati akufute machozi ya kila kilichokikumba“
“Mie nahisi tayari nimeshampata mwenye mapenzi ya dhati“ baada ya neon hilo tukajikuta tumecheka wote kasha akaniuliza swali la kichokozi
“Nani tena huyo mwenzetu? “
“Ni Ntahondi“ nilijikaza na kutamka tu, Ntahondi akabaki ananiangalia kama mtu ambae hakufikiria kitu hicho, nikaona niendelee kutoa maneno kuntu ili anielewe
“Ntahondi naamini kuna kitu cha ziada mpaka Mungu kutukutanisha ki mtindo huu, naomba unikubalie, na kama utanielewa nataka tukimaliza tu zoezi la kumtia nguvuni Mwaki na muuaji mwenzie Ramla nikuvishe Pete ya Uchumba na hapo sasa tujiandae rasmi kwa ajili ya Ndoa“ Ntahondi alionesha wasiwasi mkubwa wa kukubali jambo hili ila baada ya maongezi marefu tulifikia muafaka na kukubaliana kufunga ndoa...
ITAENDELEA SIKU YA KESHO HAPA HAPA
LIKE PAGE YETU HAPA ==>www.facebook.com/2jiachie

Post a Comment