RIWAYA: SIKU YA GRADUATION...SEHEMU YA NANE
SEHEMU NANE
"eehh hujambo?..."
"Sijambo Shikamoo mzee.."
"Marhaba"
"Kuna nini Baba mbona asubuhi asubuhi, kuna usalama kweli?"
"Usala upo, Hebu kwanza niambie yule Binti alietekwa huko mjini anaitwa nani vile?!" wote tulikua tumetega masikio kwenye simu ya Nokia ya Tochi na kwakua Mzee huyu alikua ameeweka Loud Speaker hivyo tuliyanasa mazungumzo yao kisawa sawa..
"Anaitwa Ntahondi, kwani kuna nini Baba?" watu wote tukaangaliana usoni, Mzee Ngozi alimuangalia yule kijana aliekua anampa maelekezo kua wanataka kuturejesha kule Godown, tena alikua akimuangali kwa jicho lilionesha kumsuta kwa upuuzi waliokua wakitaka kuufanya,Wakati huo Mzee Banzi alikua akiendelea kuongea na simu na mwanae alieko Dar japo hatukumjua ni nani!
"Sasa sikia huyo Ntahondi tuko nae hapa kijijini, ameumizwa sana na yuko na kijana mwingine hivi nae kaumizwa sana maeneo ya kichwani, sasa fanya hima kachukue Polisi uje nao huku kijijini haraka"
"Baba mbona kama sikuelewi? una uhakika ni Ntahondi? na we umemjuaje?"
"Sasa hutaki? hebu ongea nae huyu hapa" Mzee Banzi kampa simu Ntahondi ili aongee na huyo mwanae, nilitamani niidake mie ile simu ili nijaribu kutumia akli nimshawishi huyo kijana asiende Polisi na badala yake nijaribu kumpa utaratibu wa kuwapata ndugu zetu kwanza maana nilikua najua kua PABLO MWAKI ana nguvu sana ya pesa hivyo atakua kaishawanunu askari wengi tu wanaoweza kutugeuka na kutupoteza kabisa ili kuficha ushahidi,
"Hallow.." aliongea Ntahondi sasa
"Eeeh We Ntahondi?"
"Ndio we ni nani?"
"Mie ni Oscar mlinzi hapa chuoni kwenu IFM, Pole sana na matatizo, imekuaje sasa?"
"Ahsante nimekufahamu, hatuwezi kuongea mengi kwa sasa ila tuko hapa kijijini kwenu tumefika baada ya kuwatoroka wale waliotuteka, naomba umfuate haraka Mwl Honde umpe hii habari kisha umpe utupigie simu tumpe maelekezo ya kwenda Polisi kutoa taarifa" hapo hapo simu ikakata nilifarijika kidogo sasa kwa kua Ntahondi nae katumi mbinu nilioitaka mimi maana nae alijua tu wakitoa taarifa ya kawaida tu kituoni huenda wakazipata Askari wapambe wa MWAKI halafu itakua blaa jipya kwetu
Baada ya simu kukatika wazee wale wakatuambia tuinuke pale chini tulipokua tumekalishwa kisha wakaanza kujadili kwa hofu kubwa juu ya hili tukio, Mzee Ngozi alizidi kuonekana na hekma sana mbele ya hawa wana kijiji wenzie, baada ya hapo wakatuchukua mpaka katika nyumba iliyokua mbele kidogo ya kichuguu kikubwa kiliconekana mpaka kuizidi urefu nyumba, tulipokua mule ndani tulijaribu kuwasimulia japo kwa mukhtasar tu mkasa huu uliotukumba, wazee wale walionesha kukunwa sana na stori hii. wakati tukiendelea kujadiliana ghafla simu ya Mzee Banzi ikaita tena.. akapokea
"Hallow.."
"Eeh baba, sasa tunakuja huko muda si mrefu ila msimuambie mtu yeyote hii habari kwani nasikia huyo alie wateka ana pesa na anajuana askari wengi sana hivyo isije ikwaletea tabu hapo"
"Hakuna mtu ajuaje zaidi yetu sisi na wewe huko mjini"
"Haya hebu mpe simu huyo dada.." Mzee akamsogelea Ntahondi na kumpa simu
"Hallow Ntahondi are you oky?" ilikua ni Sauti ya Mwl Honde sasa. maskini Ntahondi akashindwa kujikaza na kuanza kulia
"NO Usilie sasa, tuko njiani tunakuja huko, uko na nani?"
"Niko na Naufal"
"Wewe!!!?.. are you sure?" Inaonesha Mwl Honde hakutegemea kabisa kusikia jambo lile, kabla Ntahondi hajajibu tena simu ikakatika, kuangalia hivi ilikua imeishiwa charge, hatukusikitika sana kwani tulikua tunajua sasa tuko katika mikono salama kiasi
Tuliendelea kukaa pale mpaka majira ya mchana hivi nadhani ilikua ni saa nne kutokana na Jua lilivyokua likizidi kua kuongezeka hapo kwa mbaali tukaanza kusikia sauti ya gari ikija upande wetu, Ntahondi masikini akasimama na kutaka kujificha akijua pengine ni wale mabedui wa Pablo Mwaki wanarudu tena, tulipochungulia nje tuliona Gari aina ya kama ya Range Rover ikiwa imepaki nje ya Nchumba iliyokua mbali kidogo na pale tulipo, kisha wakashuka vijana watatu wakiwa na Bunduki wakiwa wamevalia kiraia, kisha wakashuka tena watu wawili nilipowaangalia vizuri niliwajua alikua ni Mwl Honde, na Oscar Mlinzi wa pale chuoni kwa kina Ramla na Ntahondi ambae pia kumbe ni Mtoto wa Mzee Banzi..
Nikamsikia Mzee Banzi akimwambia Mzee Ngozi "wanajua tuko kwangu," kisha mzee Ngozi nae akamjibu "Haya basi tuwasogelee" tukasimama na kuanza kutoka nje ya Nyumba ile tuliokua tumekaa, tukiwa tuko mbele, muda wote hu kule ndani tulikua pamoja na wale wazee wawili wa mwanzo walionesha kua na shaka na sisi na kutaka kuturudisha mikononi mwa Maharamia wale PABLO hawakua wakichangia chochote nadhani walikua wakijilaumu kwa kila walichotaka kutufanyia. Tulipowakaribia akina Honde nikamuona Honde akija kwa kasi upande wetu na kisha akanifuata na kunikumbati huku akitokwa na machozi, kisha akaenda kumkumbatia Ntahondi, baada ya hapo tukaingia Ndani kwa Mzee Banzi..
Tulipofika ndani akaanza kuongea Mwl Honde
"Wazee tunawashukuru sana kwanza kwa kila jitihada zenu mlizozifanya za kuhakikisha mnawatunza vijana hawa na kututafuta sisi mpaka tumefika hapa, pili tunawaomba radhi kwa kila aina ya usumbufu mlioupata tangu mlipokua na hawa vijana hapa" kisha akaendelea tena baada kuvuta Pumzi
"Mimi ni naitwa Stephen Honde hawa watatu ni askari kitengo maalum , " nilishukuru Mungu kimoyo moyo kusikia maneno haya ya Mwl Honde kwakua sasa niliamini ukombozi hauoko mbali
Kisha Honde akanigeukia na kuniambia kua
"sasa tunaondoka na kwenda moja kwa moja mpaka kwa Mhe Waziri mkuu mtakaa pale kwa mahojiano maalum" baada ya kuongea maneno hayo Honde aliwasisitiza wazee hawa wasitoe ile siri popote kisha akawapa pesa kama shukrani kisha akawaaga kwa ahadi kwamba atarudi tena kuzungumza nao siku nyingine, Wazee hawa walishukuru sana na kuahidi kua watatupa ushirikiano wowote kama utahitajika. Tukanyuka na kuingia kwenye gari kwa ajili ya Safari ya kurudi mjini...

Post a Comment