PENNY: SITAKI KUMSIKIA DIAMOND
ZILIPENDWA wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’,
Penniel Mungilwa ‘Penny’, amefunguka kuwa hataki kumsikia mpenzi wake huyo
wa zamani kwa madai kuwa amefungua ukurasa mpya wa uhusiano na mtu ambaye
hata hivyo hakuwa tayari kumweka wazi.
Penny alisema hayo hivi karibuni jijini Dar wakati akizungumza na gazeti hili lililotaka kujua anazungumziaje tuzo saba za Kilimanjaro alizojizolea Diamond ambapo majibu yaliyopatikana yalikuwa: “Wanaotakiwa kuzungumzia hili ni mkewe na ndugu zake, mimi sitaki.”
Alipoulizwa mke wa Diamond ni nani alisema: “Mnamjua” na kuicha historia ikibaki kuwa
Penny na msanii huyo waliwahi kuwa katika mapenzi mazito ya njiwa kabla ya kumwagana
na mwanamuziki huyo kumrudia mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu, ambaye mwenyewe anapenda aitwe mke mtarajiwa. Hahahaha!

Post a Comment