ad

ad

KUMEKUCHA YANGA SC, TWITE AONGEZA MKATABA

Mlinzi kiraka wa timu ya Young Africans Mbuyu Junior Twite leo ameongeza mkataba mpya
wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu ya Yanga baada ya kufikia makubaliano na
uongozi na kupata majibu ya Shirikisho la Soka nchini TFF juu ya idadi ya wachezaji wa
kimataifa kwa msimu ujao 2014/2015.
Usajili wa Twite umefanyika leo makao makuu ya klabu ya Yanga chini ya Katibu Mkuu Bw
 Beno Njovu ambapo mchezaji amesema ataendelea kujitolea kwa uwezo wake kuisaidia timu yake ya Yanga.

Katibu Mkuu wa Young Africans Beno Njovu amesema wameingia mkataba wa mwaka
 mmoja na Twite baada ya pande zote kukubaliana, hivyo kuanzia sasa Twite ataendelea
 kuwa mchezaji wetu kwa msimu ujao wa 2014/2015 na kusisitiza kuwa usajili ndio umeanza sasa.

Akiongea mara baada ya kuweka sahihi kwenye mkataba wake mpya Twite amesema
anajisikia furaha kuendelea kuwa mchezaji wa Yanga, kwani anafurahia maisha ya
 Jangwani, wapenzi, washabiki, viongozi na wachezaji ni marafiki/ndugu ndani na nje ya Uwanja.

Aidha Twite amesema Yanga ni miongoni mwa timu kubwa barani Afrika, zenye
 washabiki na waachama wengi hivyo wangu ni fahari kuendelea kuitumika timu hii
 ambayo tangu kujiunga nayo nimekua nikijtoa kwa moyo wangu wote kusaka mafanikio.

Mbuyu Twite amekua ni mchezaji wa Young Africans kwa kipindi cha miaka miwili
 tangu Julai 2012 alposajiliwa huku katika kipindi hicho chote akiwa ni mchezaji wa
kikosi cha kwanza ambapo msimu uliopita aliweza kuisadia timu yake kutwaa
Ubingwa wa Lig Kuu ya Vodacom na msimu huu kushika nafasi ya pili.

No comments

Powered by Blogger.