Dakika 17 zamuondoa Wambura Simba
KAMATI ya Uchaguzi ya Simba chini ya Mwenyekiti
Damas Ndumbaro, imemuondoa rasmi mgombea wa nafasi ya urais Simba,
Michael Wambura, kama ilivyokuwa imeandikwa kwenye gazeti hili, juzi
Jumatatu.
Wagombea wengine waliokuwa wamewekewa pingamizi, wote wamefanikiwa kuendelea katika hatua inayofuata. Ndumbaro ambaye alitumia dakika 17 kusoma hukumu ya Wambura, alilazimika kufanya hivyo kutokana na ufafanuzi mrefu ulioandaliwa kuhusiana na suala la Wambura ambaye aliwekewa mapingamizi saba, lakini ni mawili ndiyo yaliyomponza na kuondolewa na kuwaacha Andrew Tupa na Evans Aveva katika kuwania urais.
Ndumbaro alitaja mapingamizi mawili yaliyomuondoa Wambura kuwa ni kitendo chake cha kuipeleka Simba SC mahakamani katika kesi Namba 100/2010 iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kinyume na Ibara ya 11 (1) (e), (2), 12(3) na 55 ya Katiba ya Simba ya mwaka 2010.
“Pingamizi la pili kamati imepokea ushahidi na kuridhisha kuwa Mei 5, 2010, kupitia kikao halali, Kamati ya Utendaji ya Simba ilimsimamisha uanachama Wambura kwa tuhuma za kuipeleka Simba mahakamani katika kesi tajwa.
“Baada ya kusimamishwa uanachama na kamati ya utendaji kwa mujibu wa ibara 12(1), (2) & (3) ya Katiba ya Simba mwaka 2010, jambo hilo lilipaswa kupelekwa katika mkutano mkuu ili utoe adhabu au msamaha. Kwa mujibu wa Katiba ya Simba, Ibara ya 55, adhabu ya kosa hilo ni kufukuzwa uanachama. Si kamati ya utendaji wala mwekewa pingamizi aliyepeleka suala hili katika mkutano mkuu ili litolewe uamuzi,” alisema Ndumbaro.
Kuhusu barua ya msamaha, Ndumbaro alisema: “Kamati ilipokea barua tatu kutoka kwa Wambura, kuhusu uanachama wake Simba, ya kwanza iliandikwa Novemba 6, 2012 kwenda kwa mwenyekiti wa Simba.
“Barua hiyo inakiri kosa la kuipeleka Simba makahamani na kuahidi kuwa hatarudia tena, ya pili kutoka kwa Mwenyekiti wa Simba ya 15/09/2012, Ref. No. SSL/20/9/12, kukiri kupokea barua kutoka kwa Wambura na kuahidi kuwa suala hilo litafanyiwa kazi, ingawa kamati ilibaini kuwa barua ya kujibu imeandikwa takribani miezi miwili kabla ya ile ya awali, jambo ambalo haliwezekani.
“Na ya tatu ni ya 25/9/1012, kumb. SSC 28/9/12 ambayo inasema Simba haina tatizo na Wambura, lakini uhalali wa barua hiyo una shaka kubwa sana kiasi cha kamati kuamua ipelekwe kwenye mamlaka husika kwa hatua zaidi.
“Hivyo basi, kamati imejiridhisha kuwa, maamuzi ya Kamati ya Utendaji ya Mei 5, 2010 ya kumsimamisha Wambura bado yanaendelea na yana nguvu za kisheria kwa sababu hakuna maamuzi yoyote ya mkutano mkuu yaliyobatilisha hatua hiyo.”
Mara baada ya kumalizika kwa hukumu hizo, wanachama wa Simba waliokuwepo wakati Ndumbaro anazungumza kwenye makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Posta jijini Dar, waliibuka na kutangaza kwenda mahakamani kudai haki ya Wambura baada ya kuondolewa kwenye kinyang’anyiro hicho.
“Haiwezekani, sisi tukiwa kama wanachama halali wa Simba na wenye mapenzi na timu hii tutalipeleka hili suala TFF na kama tutashindwa basi tutaenda Fifa na huko pia tutashindwa basi tutaenda mahakamani,” alisema mmoja wa wanachama hao aliyejitambulisha kwa jina la Bosi Matola mwenye kadi namba 080.CHANZO NI CHAMPIONI

Post a Comment