ad

ad

Boko Haram waonyesha wasichana waliotekwa


Wasichana ambao kundi la Boko Haram liliwateka nyara
Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekahu amesema
 kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya Nigeria wataachiliwa huru.
 

Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo, kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika kipindi
 cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara.
 

Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake miamoja wakiwa 
wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa 
wanawake hao ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.
 

Walitekwa nyara kutoka katika shule yao mjini Chibok, 
Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo
Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano 

utakaotafuta njia za kupambana na Boko Haram

No comments

Powered by Blogger.