WALICHOSEMA UKAWA KWA WAANDISHI WA HABARI DODOMA APRIL 17 2014
Baada ya
kugoma na kuamua kutoka nje ya bunge la katiba Dodoma kikundi cha umoja
wa katiba ya Wananchi (UKAWA) kimekutana na waandishi wa habari April
17 2014 na kuyazungumza haya yanayofata hapa chini.
Profesa Ibrahim Lipumba:‘Tumekubaliana
kwamba siku ya Jumamosi kwa pamoja Wabunge wote ambao hatuna dharura
tutakua tumekwenda Zanzibar kwenye mkutano wa hadhara kuanzia saa nne
asubuhi, tutaondoka na boti asubuhi saa moja kuelekea Zanzibar na
tutaeleza yaliyojiri katika bunge hili maalum’
‘Baada
ya hapo tutaendelea na mikutano nchi nzima kujulisha Wananchi msimamo
wetu ambao ni rahisi, uko wazi kwamba Rais aliunda tume ya katiba katika
utaratibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba itayokusanya maoni ya
Wananchi lakini katika yale mapendekezo ambayo yamekuja ukawa ni mjadala
wa matusi, kejeli, lugha za kibaguzi na kutaja Wapemba, Waarabu,
Wakongo na Wahindi, viongozi wapo na hamna aliewakanya tena ndio
wanawapigia makofi’
Freeman Mbowe:
‘Tume iliundwa kuratibu zoezi kupata mawazo ya Wananchi kufanya utafiti
ambao uliipa tume rejea maalum ya kufata, tume haikukusanya tu maoni ya
Wananchi bali ilifanya pia tafiti nyingi na ilikua na timu kubwa tu ya
watu makini na mahiri na ikaonekana muafaka wa muungano wa kudumu ni
serikali tatu’
‘Kinachofanyika
pale bungeni ni kutulazimisha kuondoka kwenye msingi wa ile rasimu na
kuzusha rasimu mpya ambayo inapendekeza mfumo wa serikali mbili, mfumo
ambao haujafanyiwa utafiti na haujatolewa maoni na Wananchi, je
tumeletewa nyaraka za kutosha za kujadili serikali mbili?’
‘Ni
dhahiri kama tunataka kuvunja ule msingi wa rasimu iliyoletwa na
Warioba turudi kutengeneza rasimu nyingine ambayo ina mfumo
wanaopendekeza wao lakini hatuwezi kupitia mgongo wa tume ya Warioba
kwenye msingi wa rasimu iliyoletwa ya serikali tatu alafu tukajadili
mfumo wa serikali mbili, hata wajumbe hawana mamlaka hayo’
‘Hatuwezi
kushiriki katika majadiliano yenye matusi, kejeli, dharau na kupotosha
umma…. kauli zinatolewa na viongozi zinapindishwa, wabunge wa upande
wetu wakitoa mawazo yao na kueleza ukweli… unageuzwa kuwa karaha,
kututaka sisi tuendelee kushiriki katika udhalilishaji ule hakika
hatuwezi… je tutapata tutakachokitaka?
‘Kuna
njia nyingi za kuitafuta haki, haki inaweza kutafutwa ndani ya bunge au
nje ya bunge, kazi yetu kama vyama vya siasa ni kuweka shinikizo na
kujenga hoja za shinikizo, kama tumeshapeleka maoni yetu hayaheshimiwi
huna busara yoyote unaweza kutumia kwenye genge la watu kama wale ambao
wamekaririshwa maneno’
‘Wao
wanatulaumu sisi UKAWA tunakaa tunaweka misimamo lakini wao wanakuja
ndani ya bunge kujadili mambo ambayo wamejadili wao, na wanajadili
Waziri mkuu akiwa miongoni mwao’ – Freeman Mbowe.
CHANZO NI MILLARDAYO.COM
Post a Comment