The Last Breath (Pumzi ya Mwisho) - 8
Muandishi:Eric Shigongo
KIENDACHO kikizunguka, hurudi kikizunguka. Mwisho wa Nabii Joshua (Mateo) umefika baada ya uovu mkubwa aliokuwa anaufanya kwa kivuli cha dini, kufichuka na kuushangaza ulimwengu.
Inabainika kuwa Nabii Joshua aliyekuwa akimiliki kanisa la kisasa lenye waumini lukuki, hakuwa mtumishi halisi wa Mungu kama alivyokuwa anawadanganya watu, bali alikuwa ni mhalifu mkubwa wa kuogopwa, aliyekuwa akitumia kigezo cha dini kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya na nyara za serikali.
Kazi kubwa iliyofanywa na Cecilia na Ceciliana waliokuwa wakilipiza kisasi kwa wote waliohusika na vifo vya wazazi wao, Mwanaisha na Bahanooz, ndiyo inayofichua mambo yote. Wasichana hao wanafanikiwa kuwaua watu wote walioshirikiana na Mateo katika matukio yaliyosababisha vifo vya wazazi wao.
Hans Kekule, Alfred Gwakisa, Laizer Ole Nangale, Mathias Kivuyo na Jamal Isango wanauawa kwa mikono ya Cecilia na Ceciliana na mwisho wanamalizia kwa Mateo ambaye wanamjeruhi vibaya kwa kumchoma visu viwili, kifuani na shingoni.
Analazwa Hospitali ya Muhimbili akiwa amepooza mwili wote isipokuwa kichwa tu. Ni hapo ndipo siri kubwa iliyokuwa imejifichwa kwenye maisha ya Mateo ilipoanza kufichuka, baada ya kudungwa sindano ya kumpumbaza akili, anaeleza kila kitu kilichokuwa kimejificha kwenye maisha yake.
Majasusi wa kimataifa na wapelelezi wa ndani wanagundua shehena kubwa ya madawa ya kulevya, meno ya tembo, fedha bandia na magari ya wizi, vyote vikiwa vimefichwa kwenye vyumba vya chini ya ardhi kanisani na nyumbani kwake. Pia inabainika kuwa alikuwa akimiliki genge kubwa la ujambazi.
Taarifa hizo zinaposambaa, watu wanahamia upande wa Cecilia na Ceciliana na kuwaona kama mashujaa wanaostahili kupongezwa.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
HSANTE Mungu kwa miujiza yako,” alisema Cecilia na kumkumbatia mwenzake kwa nguvu, wakaendelea kutokwa na machozi ya furaha huku wakimshukuru sana Zambi kwa kuwa nao bega kwa bega katika shida na raha.
Baada ya muda, walitolewa kwenye chumba hicho na kupelekwa kwenye ukumbi wa mahakama ambako walikuta tayari umati mkubwa wa watu ukiwa umetulia. Walipopandishwa kizimbani, minong’ono mingi ilisikika, utulivu uliokuwepo mahakamani ukapotea kwa muda mpaka hakimu alipoanza kuingia.
Watu wote walisimama wakati jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo akiingia na jopo lake, wakakaa kisha watu wote mahakamani nao wakakaa, wakiwa na shauku kubwa ya kusikiliza kitakachoamuliwa na mahakama.
Utaratibu wa kawaida wa kuendesha kesi ulianza, mwendesha mashtaka wa serikali akaanza kwa kuwasomea mashtaka Cecilia na Ceciliana ambao walikuwa wamesimama kizimbani, wakiwa wameshikana mikono.
Baada ya kumaliza kuwasomea mashtaka yote yaliyokuwa yanawakabili, mwendesha mashtaka alipeleka faili kwa hakimu na kulikabidhi kisha akarudi na kukaa sehemu yake. Ukimya wa ajabu ulifuatia, kitu pekee kilichosikika zilikuwa ni kelele za karatasi zilizokuwa kwenye faili la kesi lililokuwa linapekuliwa na jaji.
Baada ya ukimya uliodumu kwa takribani dakika mbili, hakimu alirekebisha miwani yake na kuinua uso wake kuwatazama Cecilia na Ceciliana. Akaanza kuwahoji lakini kama walivyokuwa wameelekezwa na Zambi, hawakujibu chochote na kumuachia kazi hiyo wakili wao aliyekuwa akiwatetea.
Wakili wao alifanya kazi yake kikamilifu na baada ya kumaliza kujibu maswali yote ya hakimu, alienda kukaa kwenye kiti chake, hakimu akawa anaandika maelezo hayo kwenye faili kisha akawapa nafasi mawakili wa upande wa mashtaka ambao walianza nao kutoa maelezo yao.
Mjadala mkali ukazuka baina ya mawakili wa pande zote mbili, upande mmoja ukiwatetea Cecilia na Ceciliana wakati upande mwingine ukiwakandamiza. Baada ya mawakili kubishana sana kwa hoja, kila mmoja akitetea upande wake, hatimaye jaji alihitimisha shughuli za kimahakama na kuiahirisha kesi hiyo mpaka baada ya siku tatu nyingine ambapo ndiyo ilipangwa iwe siku ya hukumu.
Haikuwa kawaida kwa kesi kuendeshwa harakaharaka kiasi hicho lakini ilibidi iwe hivyo kutokana na shinikizo kubwa lililokuwepo kutoka kwa wananchi. Baada ya hapo, jaji aligonga nyundo mezani kisha akasimama na kuondoka akifuatiwa na jopo lake.
Watu ambao kwa muda mrefu walikuwa kimya kabisa wakifuatilia mwenendo wa kesi hiyo, nao walisimama na baadhi wakasikika wakipaza sauti na kuitaka mahakama kuwaachilia wasichana hao kwani kazi waliyoifanya ilikuwa kubwa na inayostahili pongezi.
“Hao wanaojiita wanausalama wenyewe wameshindwa kugundua uovu mkubwa uliokuwa unafanywa na Mateo kwa kipindi kirefu, leo hawa wasichana wameweza halafu mnataka kuwafunga, hii siyo haki kabisa, waachiwe huru,” alisema mtu mmoja nje ya mahakama hiyo kwa sauti kubwa, akaungwa mkono na wenzake waliomshangilia kwa nguvu na kuendelea kusisitiza kuwa Cecilia na Ceciliana walikuwa mashujaa.
Polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia na wale wa magereza, walikuwa na kazi ya ziada ya kuwatuliza watu waliokuwa wamefurika nje ya mahakama hiyo. Hata hivyo, hakuna bomu la machozi hata moja lililolipuliwa wala hakuna mtu aliyepigwa au kukamatwa na polisi kutokana na amri iliyokuwa imetoka ngazi za juu.
Cecilia na Ceciliana wakapakizwa kwenye karandinga na kuondolewa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali, huku wakisindikizwa na magari sita yaliyokuwa yamejaa askari wenye silaha.
Wakati karandinga likiondoka, umati uliokuwa umefurika mahakamani hapo ulikuwa ukiwashangilia Cecilia na Ceciliana huku kila mmoja akiwapongeza kwa kuweza kumdhibiti Mateo na majambazi wenzake.
Japokuwa walikuwa kwenye matatizo makubwa, hali hiyo iliwafariji mno Cecilia na Ceciliana hasa baada ya kugundua kuwa watu wengi walikuwa upande wao na hawakuwa wakiwachukia tena kama ilivyokuwa mwanzo kutokana na kuujua ukweli.
Msafara uliendelea kukatiza mitaa ya Jiji la Dar es Salaam na hatimaye ukawasili gerezani ambapo waliteremshwa na kuingizwa ndani chini ya ulinzi mkali. Akili za Cecilia na Ceciliana zilikuwa zimebadilika mno, ile hatia kubwa waliyokuwa nayo ndani ya mioyo yao, sasa ilibadilika na wakawa na matumaini makubwa ya kurudi uraiani.
***
“Kwani nini kimekwamisha? Mimi nilitegemea leo ndiyo wangeachiwa huru?”
“Hapana bwana Zambi, kwani wewe hujui taratibu za kisheria?”
“Nazijua lakini si uliitwa ikulu leo? Mimi nilijua ukirudi tu basi kila kitu kitakuwa kimekwisha.”
“Ni kweli niliitwa ikulu, jambo jema ni kwamba mheshimiwa rais ameonyesha kuguswa sana na hii kesi, anawasikitikia sana Cecilia na Ceciliana na ameahidi kuwa yupo tayari kuwasaidia.”
“Ooh! Imekuwa habari njema sana lakini atawasaidia lini? Wanangu wanaendelea kuteseka gerezani na kama ujuavyo hali ya kule ilivyo.”
“Kuwa na subira, nilishakuahidi hata kabla mheshimiwa rais hajaliingilia kati hili suala. Acha mahakama ifanye kazi yake kwanza, kuna mpango maalum tumeshauandaa lakini kwa sasa hatuwezi kuiingilia mahakama.”
“Kwani mmepanga kufanya nini?”
“Acha kesi iendelee mpaka hukumu itolewe kisha baada ya hapo, badala ya kutumikia hukumu watakayopewa wataachiwa kwa msamaha maalum kutoka kwa rais, ameshasaini kila kitu, tunachokisubiri ni hukumu tu.”
“Unasema kweli?”
“Kweli kabisa, kwa nini nikudanganye?”
“Ooh! Ahsante Mungu,” alisema Zambi huku akimkumbatia kwa nguvu mwendesha mashtaka mkuu, ndani ya ofisi yake.
***
Nisingependa kumaliza hadithi hii ya leo bila kukumbusha jambo muhimu la kutoa maisha yako kwa Mungu. Maisha tuliyonayo hapa duniani ni mafupi sana, yanapita kama maua yachanuavyo na kunyauka. Wengi unaowafahamu wamekufa lakini wewe unapumua, ni vyema basi kufikiria maisha baada ya kifo.
Kila siku jiulize: “Hivi nikifa leo nitakwenda jehanam au peponi?” Kila mmoja wetu analo jibu lake, bila shaka sote tungependa kwenda peponi. Kama hivyo ndivyo, basi tiketi ya kwenda huko ni matendo mema na kujiepusha na uovu.
Tukumbuke mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele.
Je, nini kitaendelea? Usikose kufuatilia Jumatatu kwenye Gazeti la Championi Jumatatu.
LIKE PAGE YETU HAPA ==>www.facebook.com/2jiachie

Post a Comment