The Last Breath (Pumuzi ya Mwisho) - 5
Johnson alionekana kuwa katika maumivu makali kupindukia,
mguu na mkono wake wa kushoto ulikuwa umevimba ni kama vile alikuwa amevunjika.
Ni katikati ya pori wakiwa wawili tu Johnson na mwanaye
Melania, hakuna kitu kinachosikika zaidi ya milio ya ndege tu inayosikika
pamoja na mabaki ya ndege yakiwa yamepatapakaa kila mahali, Melania anaangua
kilio hajui nini chakufanya.
Je, nini kitaendelea? Johnson atakufa? Melania je ataokolewa
na nani?
SONGA NAYO
DAD!DAD!DAD!” (baba!Baba!Baba!) alianza kumwita baba yake
huku akimtingisha kwa nguvu nyingi, akafurahi kuona amejigeuza, upande mmoja wa
uso wake ulikuwa umevimba sana na mkono wa kushoto umepinda, ishara kwamba
ulikuwa umevunjika.
“Dad!” (baba!) Melania akaita tena.
Johnson akafumbua macho akiwa katika hali ya utupu kichwani
mwake, hakuelewa chochote kilichokuwa kikiendelea, kwa dakika kadhaa alibaki
hivyo akiwa amemkodolea mwanaye macho. Dakika kama kumi hivi baadaye kumbumbu
zikaanza kumrejea, akapiga kelele kwa sauti ya juu, alipojaribu kunyanyuka
akagundua pia mguu wake wa kushoto ulikuwa umepinda na kugeukia nyuma, nao
ulikuwa umevunjika huku ukiwa umevimba kupindukia.
“Thanks God we are alive!”(Ahsante Mungu tupo hai!)
alipomaliza tu kusema kauli hiyo akaanguka chini, macho yake yakafunikwa na
giza, kiasi kikubwa sana cha damu kilikuwa kimepotea, hivyo kila aliposimama
damu kidogo aliyokuwa nayo ilishindwa kupandisha mlima kwenda kichwani na
kujikuta akizimia.
Melania hakuwa na la kufanya zaidi ya kuendelea kuomba
akimshukuru Mungu kwa muujiza uliofanyika, baba yake akiwa katika hali hiyo ya
kutokuwa na fahamu, ghafla alisikia sauti
za mtu akiongea nyuma yake, akageuka na kukutana na sura ya mwanamke wa
Kizungu ambaye uso wake ulikuwa umepasukapasuka na kujawa na damu iliyoganda.
“Sorry for what happened!” (Pole kwa kilichotokea!)
“My father is dying!” (Baba yangu anakufa!) Melania alilia
na kumfanya mwanamke huyo atambae mpaka mahali walipokuwa.
Bahati nzuri mwanamke huyo alikuwa daktari, akamgusa Johnson
kifuani na kugundua alikuwa bado anapumua, moyo wake ukipiga vizuri. Alichoamua
kufanya ni kumnyanyua sehemu za miguuni ili damu itiririke kwenda kichwani,
kitendo hicho hakikuchukua muda mrefu sana, Johnson akafumbua macho tena.
“He is anaemic, to little blood, that is why he is
fainting!” (ana damu kidogo, ndiyo maana anazimia!)
“Will he be alright?” (Je, atapona?)
“God knows, everything here is a miracle, I can’t believe I
am alive and everyone else except us, is dead!”(Mungu anajua, kila kitu
kilichoko hapa ni muujiza, siwezi kuamini niko hai na watu wote isipokuwa sisi,
wamekufa!) aliongea mwanamke huyo, ghafla naye akaanguka chini.
Johnson aliyekuwa kimya, akanyanyuka na kusogea karibu ya
mwanamke huyo na kumnyanyua miguu akisaidiana na Melania, damu ikatiririka kwenda kichwani na muda
mfupi baadaye akafumbua macho, wote isipokuwa Melania, wakawa wanaongea wakiwa
wamelala kwa hofu ya kuzimia wakisimama.
Kila kitu mahali walipokuwa kilitisha, ukimya wa ajabu,
mabaki ya ndege, miti mirefu na giza ingawa ilikuwa ni asubuhi, maiti
zilizotapakaa kila mahali na viungo vya wanadamu vilivyokatika! Hakuna hata
mmoja wao aliyewahi kufikiria jambo hilo linaweza kuwapata, lakini sasa ndiyo
hali waliyokuwemo, hilo halikuwa na ubishi.
“I am also alive!”(mimi pia ni mzima!) ghafla walisikia
sauti ya msichana ikiongea nyuma yao, awali walifikiri ilikuwa ni maiti,
wakatambaa mpaka sehemu hiyo.
“Thank the Lord you are one among the few!”(Mshukuru Mungu
wewe ni mmoja kati ya wachache!)
“To be involved in a plane crash and be alive!”(kuwemo
katika ajali ya ndege kuanguka na bado
ukawa mzima!)
“True!”(kweli!)
Walipomchunguza vizuri waligundua sehemu ya mguu wa msichana
huyo yote ilikuwa haifanyi kazi, alikuwa amepooza kuanzia kiunoni kwenda chini
akiwa katika maumivu makali kupindukia sehemu za bega la kulia. Walimuuliza
maswali mengi alikuwa ni mtu wa wapi, akasema kwao ilikuwa ni sehemu za Kisumu
huko Kenya.
“Tunaondokaje hapa?” Johnson aliuliza.
“Sijui tutaondokaje.” Mwanamke wa Kizungu ambaye katika mazungumzo yao alijitambulisha kama
Joanna alijibu.
“Itabidi tu tutambae taratibu maana tukisimama, tutazimia!”
“Au kuna ndege za uokoaji zitapita? Maana haiwezekani ndege
ikaanguka halafu isitafutwe!”
“Kwa hapa msituni ndege ilipoangukia tena katikati ya miti
mikubwa namna hii bondeni, si rahisi mabaki ya ndege kuonekana.”
“Pengine wanayo mitambo.”
“Hata kama ni mtambo hawawezi kuona, msitu ni mkubwa mno,
cha maana hapa ni kuondoka kwa kutembea taratibu.”
“Na Nyambura je?” Joanna aliuliza akimaanisha msichana wa
Kenya.
“Msiniache hapa nife peke yangu!”
Johnson alibaki kimya kwa karibu dakika tano akitafakari juu
ya nini cha kufanya, ni kweli msichana huyo alikuwa kikwazo sababu hakuwa na
uwezo wa kutembea na wao wasingeweza kubaki eneo hilo hilo bila chakula wala
maji. Ingawa yeye alikuwa na maumivu makali kwenye mguu na mkono uliovunjika,
alikuwa tayari kutambaa mpaka sehemu ambako pengine wangeweza kukutana na
msaada, au sehemu ya wazi ambako helkopta zingepita na wao kupunga mashati yao
hewani ili waonekane. Pamoja na hayo yote, wasingeweza kumwacha Nyambura.
“Sasa tunafanyaje?” Joanna aliuliza.
“Twende tukitambaa naye kwa makalio tukiwa tumembeba kwenye
mapaja.”
“Mguu wako?”
“Nitaufunga na miti kwa kutumia suruali yangu, najua
nitakuwa na maumivu makali lakini ni bora kuumia ili tuendelee na safari mpaka
sehemu ya usalama, vinginevyo hapa tutakufa.”
Wakakubaliana na Johnson akakata vipande vya miti na kwa
msaada wa Melania na Joanna walimfunga mguu na mkono, wakitumia suruali na
shati lake, akabaki na nguo ya ndani peke yake, zoezi hilo lilipokamilika
wakampakata Nyambura miguuni na kuanza kutambaa taratibu, hakuna safari ya
taratibu kama hiyo, lakini walikuwa na tumaini kwamba mbele wangepata msaada.
Walipita katikati ya misitu, wakipishana na nyoka wakubwa
ambao wangeweza kuwauma na kufa kwa sumu, lakini haikuwa hivyo Mungu alikuwa
pamoja nao, hicho ndicho walichokiamini. Kwa siku nzima walitambaa, Johnson
akiwa kwenye maumivu makali, usiku ulipoingia walilala hapo hapo ulipoingilia,
asubuhi ya siku iliyofuata walipomwamsha Nyambura, hakuamka, alishafariki!
Hawakuwa na la kufanya, wote walilia kwa uchungu lakini
mwisho wakaamua kuuacha mwili wake na kusonga mbele. Siku nzima waliendelea
kutambaa bila kutokeza sehemu yoyote ya wazi, njaa ikiwasumbua, chakula chao
kikiwa matunda ya mwitu ambayo wala hawakujua yalikuwa ni sumu au la! Ili mradi
waliwaona Sokwe wakila, nao kikawa chakula chao.
Siku ya tatu, Joanna alikuwa hoi, akawa anazimia mara nyingi
kiasi cha kufanya safari ishindwe kuendelea,
mwisho ikashindikana kabisa, naye akafariki! Wakabaki Johnson na mwanaye
Melania, wakilia kwa uchungu nao wakiwa hawana uhakika kama wangeweza kutoboa
hadi upande wa pili wa msitu mnene wa Congo.
Wakauacha mwili wa Joanna porini na kuendelea na safari,
Johnson sasa akitembea kwa fimbo na aliposikia kizunguzungu aliketi. Kwa wiki
nzima walitembea bila kukutana na msaada wowote, Johnson akachoka pia, akawa
hana tena la kufanya zaidi ya kubaki amelala sehemu moja, kizunguzungu
alichokuwa nacho hakikumwezesha hata kufumbua macho, huku mguu wake ukiwa
umevimba kama kinu.
“Mwanangu! Sitaweza tena, kama nikifa wewe endelea,
utakutana na mkono wa Mungu mahali fulani, niangalie nitakapopumua pumzi ya
mwisho na kutulia, ujue mimi nimeondoka. Kama ukifanikiwa kuokolewa, msalimie
sana mama yako, mwambie nimekufa nikijuta ni kwa nini sikumsikiliza.”
“Baba usiseme hivyo!”
“Inaniuma Melania, lakini basi tena.”
Haukupita muda mrefu sana, giza likawa limeingia na Johnson
akapumua pumzi ndefu na kutulia, Melania akajua tayari baba yake amefariki!
Machozi yakaanza kumtoka, hakujua angewezaje kuendelea na safari bila baba
yake, alikuwa mtoto mdogo wa miaka mitano, katikati ya msitu wa Congo. Naye
alijua mwisho wake ulikuwa umewadia,
ghafla akamulikwa na tochi nyingi sana usoni, alipogeuka kuangalia,
macho yake yalikutana na watu wenye sura za kutisha, weusi, wenye macho mekundu, baadhi wakiwa vifua wazi, wawili
wakiwa wamevalia sare za kijeshi lakini wote wakiwa na bunduki.
Wakamshika na kumvuta hadi pembeni ambako walimlaza chali
ardhini, wakamgandamiza mikono na miguu juu ya ardhi, kisha mmoja wao akaanza
kuvua suruali, ishara kwamba walitaka kumwingilia kimwili. Melania alikuwa
akilia huku akimwita baba yake lakini hakupata msaada wowote.
Je, nini kitaendelea? Fuatilia siku ya Jumatatu katika
gazeti la Championi Jumatatu

Post a Comment