SHILOLE: NILIPONASA SASA SIPINDUI
STAA wa filamu na mduara Bongo, Zuwena Mohamed
‘Shishi Baby’ amefunguka kuwa amenasa vilivyo katika penzi la msanii
mwenzake, Nuhu Mziwanda hatarajii kuachika.
Staa
wa filamu na mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shishi Baby’ akiwa kwenye
pozi la kimahaba na mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la Nuhu Mziwanda.
Akipiga stori na paparazi wetu, Shishi alisema yupo tayari kuolewa na
Mziwanda kwani anampenda na ndiyo ubavu wake kutokana na vile ambavyo
amekuwa akimwonesha mapenzi ya kweli tofauti na wapenzi wake wote
waliopita.
“Huyu ndiye shemeji yenu, ndiye mume
wangu mtarajiwa, ninampenda na yeye ananipenda kwa hiyo Mungu akijalia
soon tutakamilisha taratibu za ndoa,’’ alisema Shishi Baby.
Nuhu na Shishi.
Post a Comment