RIWAYA: SIKU YA GRADUATION...SEHEMU YA TANO
SEHEMU YA TANO
Siku zilizidi kuyoyoma kuelekea kwenye Graduation ya kina Ramla, siku ambayo mbali ya kuhitimu masomo yake pia alikua akijiandaa kuvishwa pete ya Mwanaume wake PABLO MWAKI wakati huo huo hii ndo siku iliyopangwa kwa ajili ya kutekeleza azma ya kutuua mimi na Ntahondi tukiwa hukuhuku Msituni, Hasira zilinipamba kichwani kila nikikumbuka jinsi nilivyokutana na Ramla kwa mara ya kwanza, nikamtoa Tabora na kumleta Jijini Dar Es Salaam, nikikumbuka gharama kubwa nilizokua nikizitumia kwa ajili ya kumlipia ada, malazi na Chakula bila ya kusahau jinsi nilivyokua nikituma pesa za matumizi kwa mama yake Mzazi aliebaki Tabora halafu Leo amenisaliti kisa kapata Mwanaume Tajiri na Maarufu kuliko mimi mbaya zaidi na Mama yake nilietegemea angekua ndie kimbilio langu nae kaingiwa na Tamaa ya pesa na kutaka tu Mwanae aolewe na Tajiri huyu..
Tangu aondoke yule Baunsa mweupe anaemtaka kimapenzi Ntahondi tuliendelea kuishi chini ya ulinzi mkali japokua hali ya mateso kwa sasa haikuwepo tena bila shaka ni kutokana na maelekezo waliyoachiwa vijana hawa kutoka kwa jamaa huyo anaemzengea Ntahondi, tulikua tunakula chakula ambacho kiasi ni kizuri ukilinganisha na kile tulichokua tukipewa awali, pia maji ya kunywa na kuoga tulipatiwa na hata Malazi yetu kwa sasa yalikua yana ahueni kiasi, tuliendelea kulala Chumba kimoja mimi na Ntahondi kwa kipindi chote hicho na Tuliitumia ipasavyo nafasi hii kila siku kujipanga kisawa sawa juu ya kuutekeleza mpango wetu wa kutoroka, Kila mara tulijikumbusha mipango hiyo tukihisi hiyo ndiyo njia pekee ya kutuokoa mule ndani. ilikua ni kitu kigeni kwa Mtoto wa kiume kulala chumba kimoja na mtoto wa kike, tena mtoto mweyewe ameumbika kisawa sawa Bila ya kupata hisia za mihemko ya kimapenzi Lakini kwetu haikua hivyo kila mtu alikua busy akiumiza kichwa namna ya kujiokoa ukizingatia siku za Jamaa kurudi zilikua zimekaribia..
Siku tano zilitimu tangu Njemba ile iende mjini kuonana na PABLO MWAKI Hivyo tukawa tayari tukijua siku hiyo ilikua ndo siku tuliyokua tukisubiri, Ntahondi alijitahidi kujiweka katika hali ya Urembo ili kuzidi kumchanganya jamaa atakaporejea japokua hakua katika kiwango kile cha IFM Kutokana na hali ya mazingira.. Tuliendelea kumsubiri yule Baunsa bila mafanikio ya kumuona mpaka usiku ukaingia Tukaingia kulala tukiwa na kiu ya kuutekeleza mpango wetu, Tulilala mpaka asubuhi mapema sana tuliposhtushwa na Sauti za watu wakicheka kwa shangwe nje ya Mjengo ule uliojaa kila hali ya kutisha na kuogofya, nilipojaribu kusikiliza ili nijue kua zilikua ni cheko za nini hasa niliisikia Sauti ya Baunsa aliekua mjini kwa siku sita sasa na bila shaka alikua akipokelewa na vijana wake baada ya kuingia akitokea mjini, nikainuka pole pole na kwenda mpaka katika kitanda cha Ntahondi, nikamuamsha na kumpa taarifa za ujio wa Jamaa ili awe tayari kukabiliana nae, kisha nikarudi kitandani kwangu na kujifunika shuka halafu nikatulia kama vile niko katika usingizi mzito..
Hazikupita hata dakika tano nikasikia mlango wa Chumbani kwetu ukifunguliwa, niliendelea kujifanya nimelala, kisha nikamsikia Baunsa akimuamsha Ntahondi na kumsalimia
"Hujambo binti? una lala mpaka saa hizi?"
"Sijambo, nilikua nimeshaamka ila usingizi ukanipitia tena"
"Vipi hakuna mtu yeyete aliekusumbueni tangu nilipoondoka?"
"hakuna alietusumbua, nashukuru"
"Usiogope sema kama mlipata tabu yoyote, hawa ni vijana walio chini yangu hawapaswi kukiuka maagizo yoyote nayotoa mimi" Jamaa aliendelea kujizolea masifa lukuki kutoka kwa Ntanhondi, wakati huo mie bado nimejifunika shuka yangu halafu nimetulia tuli, Ntahondi aliendelea kukataa kwa sauti ya laini na mahaba kiasi kwamba hata mimi sasa nilianza kupata 'vibration', baada ya mazungumzo hayo mafupi jamaa akuambia Ntahondi amfuate, Binti akainuka wakaanza kutoka nje, nikamsikia jamaa akiuliza
"Huyu Bwege nae kalala tu kama yuko kwa baba yake humu" akimaanisha mimi
Sikujua wamekwenda wapi, ikanibidi na mimi niamke niwe tayari kwa lolote nilikaa kama dakika Ishirini bila kupata hata dalili ya kinachoendelea huko kisha kwa mbali nikasikia sauti za nyayo za miguu zikija usawa wa chumbani kwetu, nikajiegesha ukutani nikijifanya kama ndo nimetoka kuamka, nikasikia mlango ukifunguliwa na Ntahondi akaingia, mkoni ameshika sahani yenye Mkate uliopakwa Blueband na jam na mkono mwingine amebeba kikombe kikubwa cha chai ya maziwa, akanisogelea huku akiwa na tabasamu na kunikabidhi kifungua kinywa hicho, nikakipokea na kisha nikamuuliza
"Imekuaje huko?"
"Jamaa kanipeleka hadi chumbani kwake anakolala, akanipa chai ninywe, wakati nakunywa akaanza kuniuliza kama nimeafiki suala lake, na mie kwa mapozi nikamkubalia, kweli kuna wanaume wanatamaa ya Ngono Eti ndani ya Dakika tano tu nimeishaitwa majina yote mazuri mara baby, mara sweat, mara dia Hivyo tumekubaliana kua Leo jioni wake wataondoka na kwenda mitaa ya mbele huko kuna 'center' ya kijiji hivyo atabaki yeye tu kama mlinzi kwahiyo nitaenda kulala nae Chumbani kwake" baada ya maelezo hayo tukaanza sasa kuboresha mipango yetu upya ya namna ya kufanya mashambulizi na kisha kutokomea,
Kilichozidi kunifariji ni maneno ya kijasiri na kishujaa ambayo ki ukweli sikutegea kuyasikia yakitoka kinywani mwa mtoto wa kike tena mdogo kama huyu,
"Huu ni mpambano wa kuokoa roho zetu ikibidi hata kwa kutoa roho ya yeyote atakaekua mbele yetu hivyo inabidi tuwe makini, tuna aslimia 99 ya kufanikiwa kutoroka mpaka sasa ila pia tuna asilimia moja tu ya kushindwa kutekeleza mpango huu hivyo tusiiruhusu asilimia hii ikazizidi asilimia 99" Ntahondi alikua akiongea kwa maneno makali huku akionesha kujiamni, kisha akaendelea kua
"Nilipoingia chumbani kwake nimemuona akiwa na bunduki mbili, moja kubwa akiwa kaining'iniza juu ya kiti kilichopo karibu na kitanda, nyingine ni Ndogo(Pistol) alikua kaining'iniza usawa wa kiuononi kwenye suruali yake hivyo nikiwa nae chumbani we uwe tayari tayari, kwaku huyu Shetani anaonesha ni mtu wa tamaa ya mapenzi me nitamlaghai mpaka nihakikishe amelainika kama mgonjwa wa degedege, ukisikia tu nakohoa kwa sauti kubwa ujue picha iko tayari hapo hapo usichelewe uje fasta mlango sitaufunga nitauegesha tu hivyo ukifika we unaingia moja kwa moja" nilikua nikimsikiliza kwa makini mdada huyu akiwa hana hata chembe ya woga usoni mwake, nikamuuliza
"Sasa vipi kwa bahati mbaya nikishaingia halafu hizo bunduki nisizione?"
"Mimi kwakua nitakua humo humo chumbani nikau namuangalia anavyoweka kila kitu hivyo kama asipoweka maeneo hayo nilipoziona mwanzo nitaona ameweka wapi hivyo nitakupa Ishara ya haraka mahali zilipo halafu wewe utaenda moja kwa moja kuchukua, na ukishaichukua usichelewe kumfyatua" Tulipanga kila kitu mpaka mwisho tukawa tumekaa tu tunasisitizana kua makini..
Hatimae jioni ikafika, ilikua ni majira ya saa moja magharibi, hali ilikua tulivu kabisa na giza lilikua limeanza kutinga kwa kasi bila shaka ni kutokana mazingira msituni kule.. Tukiwa chumbani mimi na Ntahondi tuliwaona wale vijana wawili wakitokomea kwa mbali kupitia matundu ya dirisha wakitokomea Hivyo tukawa tayari kukabiliana na Ibilisi huyu altakaebakia peke yake, Tuliendelea kukaa mule ndani kwa muda mrefu tu mpaka ilipotimu majira ya kama saa tatu usiku tukasikia mlango wa chumbani kwetu ukifunguliwa kisha akaaingi kijana mmoja akiwa na Bunduki yake mkononi kisha akamwimbi Ntohondi "Boss anakuita chumbani kwake"
"Ok nakuja" alijibu Ntahondi kisha kijana yule akatoka nje ya chumba kile, ile hali ilitushtua sana maana tuliamini kua hakukua na mtu mwingine yeyote ndani ya mjengo ule Lakini sasa dalili sio nzuri kumbe kuna huyu kijana alieonekana ni Mlinzi pia, Ntahondi akasimama huku akiwa na mfadhaiko usoni, nikampa moyo na kumwambia
"Nenda, fanya kama tulivyokubaliana, kuhusu huyu kijana ondoa Shaka tutajua namna ya kumkabili ila mipango yote ni kama tulivyopanga" Ntahondi alitikisa kichwa kuashiria ameafiki Kisha akatoka na kwenda chumbani kwa Baunsa..
Kadri muda ulivyozidi kwenda niliendelea kupata nguvu ya kupambana, japo kibinaadamu mapigo ya moyo hayakuacha kwenda kasi, jasho jembamba liliendelea kunitiririka mwilini, kilichozidi kunitia hofu ni hali ile ya ukimya sikusikia Sauti ya Ntahondi akikohoa kama tulivyokubaliana na sasa imeshakua takribani saa moja tangu aende kule chumbani kwa Baunsa yule, nilipojaribu kucungulia nje usawa wa getini japo ilikua ni mbali na chumba hiki nilimuona yule kijana mlinzi akiwa amekaa kwenye kiti kama vile mtu aliepitiwa na usingizi, nikataka kutoka na kwenda chumbani aliko Ntahondi lakini kengere ya hatari ikalia kichwani mwangu nikakumbuka jinsi Ntahondi alivyonisisitiza kua nisiende mpaka nikimsikia anakoho kwa nguvu, ikanibidi Nishushe pumzi kisha nirudi mpaka kitandani na kujitupia..
Baada ya kama nusu saa tena nikiwa nimejilaza pale kitandani nikamsikia Ntahondi akikohoa kwa sauti kubwa kama vile mtu aliepaliwa na machicha ya nazi hapo hapo nikasimama haraka, nikaenda mpaka dirishani tena na kumchungulia yule Mlinzi kule Getini nae alikua maekaa vile vile, nikaufungua mlabgo wa chumba taratibu kisha nikatoka haraka nikiwa na kisu mkononi, kisu hiki ilikikuta pale kwenye korido juu ya pipa kubwa la maji, nikaenda mpaka kwenye chumba cha nne kutoka kile chetu, hapo ndipo walipokua Ntahondi na Huyu haramia, nilipofika mlango tu nikajaribu kuusukuma mlango wa chumbani LAA HAULA Mlango ulikua umefungwa kwa ndani, nikazidi kupata hofu nisijue la kufanya, lakini nikiwa bado sijajua nifanye nini nikamsikia Ntahondi akimwambia yule jamaa ampele msalani akajisaidie, nikashusha pumzi kisha nikarudi fasta mpaka chumbani kwetu halafu nikwa nachungulia kwa jicho moja kupitia kwenye pazia nyepesi aliyokua mlangoni..
Baada ya dakika mbili hivi nikwaona wakitoka chumbani wakielekea upande wa pili wa korido ile ndefu ambako ndiko kuna vyoo, jamaa huyo akiwa maevaa bukta huku akiwa kidali wazi, na Ramla akiwa amejifunga khanga. walipokatiza tu kuingia Maliwatoni mimi nikatumia mwanya huo haraka nikaenda mpaka pale mlangoni walipotoka nikaingia mule chumbani, nikakuta chumba cha kawaida tu, kukiwa na mwanga hafifu wa taa za kichina, haraka hara nikaanza kupepesa macho huku na kule nikitafuta silaha, 'HAMAD' Nikaiona Bunduki ikiwa pale pale kwenye kiti kilichopo mbele ya kitanda, nikaiacha na kwenda mbele tena kwenye suruali yake ya jinzi aliyokua kaitundika kwenye msumari ukutani, nilipoigeuza upande wa pili nikaiona Pistol yake nikachukua haraka kisha nikaenda mpaka pale kitandani halafu nikaingia chini ya kitanda(uvunguni) kitendo cha kama sekunde kadhaa nikwasikia wanaingia ndani..
"Funga mlango hua vizuri, unatakiwa kua makini usipende kulala bila ya kufunga mlango" ni sauti ya Baunsa akimwambia Ntahondo, nikiwa chini ya uvungu wa kitanda niliona miguu ya huyo Baunsa akienda mpaka usawa wa kiti na kuishika Bunduki yake, nikawa naomba dua zangu zote ili asiende kule alikotundika suruali yake maana angekuta hakuna Pisto yake haipo ingeanza mtanange, baada Ntahondi kutoka usawa wa malangoni karudi mpaka pale kitandani akapanda kisha akakohoa tena kwa nguvu nadhani hakujua kama tayari nipo ndani hivyo ilikua ni ishara tena ya kuniita, nikaendelea kutilia tuli, nikaiona sasa miguu ya huyu Baunsa akija mpaka kitandani nae akapanda kitandani kisha baada ya mazungumzo yao ya hapa na pale nikasikia sasa sauti za mahaba hasa hasa kutoka kwa kidume huyu hapo hapo nikaanza kutambaa taratibu kwa Tumbo mpaka mwisho kitanda wakati huo nikiwa tayari nimeshaikoki Pistol yangu kidole cha shahada kikiwa 'attention' kwenye 'trigger' kwa ajili ya kufyatua risasi muda wowote..
*****
ITAENDELEA SIKU YA KESHO HAPA HAPA
LIKE PAGE YETU HAPA ==>www.facebook.com/2jiachie

Post a Comment