ad

ad

RIWAYA: SIKU YA GRADUATION...SEHEMU YA NNE

SEHEMU YA NNE
TULIVYOKUTANA NA RAMLA

Ilikua ni mwaka 2009, Mwaka mmoja tangu nipate kazi kwenye kampuni ya KIGWAZA inayojishughulisha na Upakiaji na upakuaji mizigo bandarini kama Muhasibu nikachukua likizo fupi kwa ajili ya kwenda kumsalimu Mama yangu mzazi Bi Shammy Naufal aishiye Tabora, niliifurahia sana safari hii kwakua ilikua ni muda mrefu sana sijaenda nyumbani hivyo nilitaraji kuonana na Mama yangu kipenzi, Ndugu zangu, na Marafiki zangu ambao tulikua tukikaa wote kijiweni tukibadilishani story kadha wa kadha..

Niliwasili TABORA majira ya saa kumi na mbili jioni, nilipokelewa na wadogo zangu waliokuja Stand ya Mabasi kunipokea kisha tukaondoka mpaka nyumbani ambako nilipokelewa kwa shangwe na Mama na ndugu wengine waliokua pale nyumbani, ilikua ni siku ya furaha sana kwangu, kama kawaida ya wageni mambo kama Jogoo huusika kwa asilia mia wakati wa mduara wa chakula cha usiku na kila aina ya vinywaji ilipofika Saa sita kasoro(usiku) niliondoka na kwenda Chumbani kwa Mdogo wangu wa kiume na kujiandaa kwa ajili ya kulala..

Asubuhi ya siku iliyofuata niliamka mapema, na baada ya kuoga na kupata kifungua kinywa nikajipumzisha kidogo pale ukumbini na kisha nikamuaga Mama kua ninaenda kijiweni kuwasalimia jamaa zangu kisha kuna Mzigo nilipewa na Mke wa Boss wangu ili niupeleke kwa dada yake anaishi Mtaa wa Rufita anaitwa Bi Ayman Gamba, baada ya hapo nikaanza kujongea kijiweni ambako pia nilipokelewa kwa furaha sana na washikaji zangu wa kitambo niliowaacha wakati naenda Dsm, tukiwa katikati ya Story alikatiza binti mmoja ana mirindimo mithili ya Mjaluo, Mrembo, Mrefu, sio Mweupe wala si mweusi, Hips kama ameficha panya, , yaani kama we ni Rijali lazima ungegeuka mara mbili kumtazama. Huyo si mwingine alikua ni RAMLA

Baada ya kuwaulizia washikaji kuhusu binti huyu waliniambia kua anakaa mtaa wa Rufita, kuhusu shughuli zake niliambiwa kua anafanya kazi za msimu katika ofisi za ATTT! Nilitamani kujua mengi zaidi yamuhusuyo binti huyu lakini washikaji walibadili mada na tukaendelea na Story zangu baada ya muda mrefu niliwaaga jamaa ili niende sasa nikamtafute huyo Bi Ayman wa mitaa ya Rufita maana nilikua sipaju anapokaa, nikachukua boda boda kisha nikaondoka zangu, nilipofika Rufita maeneo niliyoelekezwa tukasimaa kisha nikateremka kwenye boda boda ili nimuulize mmoja wa vijana aliekua upande wa pili wa bara bara lakini kabla sijavuka akatokea msichana mmoja katika nyumba niliyokua nimesimama akamwaga maji nje nilipogeuka na kumuangalia alikua ni yule binti mrembo aliepita kule kijiweni

Kabla sijasema chochote akaniwahi yeye kwa kunisalimiA
"Mambo"
"Poa, mzima wewe?
"Me mzima, mara tu umefika huku?" hili swali likanishtua nikahisi amenifananisha lakini kabla sijamjibu chochote akaniwahi kwa swali jingine
"Kwani wewe si nilikupita na jamaa zako mmekaa kule Minazi mikinda?" nikajua hakua akibahatisha
"Duh una kumbukumbu sana, yeah ni mimi. sasa mie naomba kukuuliza, napaulizia kwa kwa Bi Ayman Gamba!!" akacheka kidogo kisha akanijibu kwa Pozz
"na unaeongea nae hapa ni binti yake aitwae Ramla, karibu ndani" wote tukacheka na kisha tukaangia ndani, nikamuomba yule dereva wa boda boda anisubiri kidogo

Tulipofika ndani tulipokelewa na Bi mkubwa mmoja mnene na mweupe, na baada ya kusalimiana nae Ramla alinitambulisha kua ndie Bi Ayman Gamba, nikamsabahi na baada ya kumsabahi nikamueleza kilichonipeleka
"Mama mimi natokea Dar japo asili yangu ni wa hapa hapa Tabora, nimepewa mzigo huu kutoka kwa mke wa Boss wangu kaniambia nimkabidhi dada yake" aliupokea mzigo na kunishukuru sana Kisha me nikaaga zangu, wakati naondoka Ramla akaniwahi na kunitania
"Umeshamaliza shida zako hata hauniagi eeh?"
"Nilijua uko nje, haya nakusubiri unisindikize" Binti yule akanifuata kama ananisindikiza vile nikaona kama nyota ya Jaa imeniangukia, tukawa tunatoka nje huku tupiga story mbili tatu japo hazikua za msingi na baada ya utani wa hapa na pale tukaagana, Lakini kabla sijaondoka nikamchombeza kua anipe namba yake kama hatojali, nae bila ajizi akaishika simu yangu aina ya Sumsung akaandika namba yake halafu akaji beep baada ya hapo tukaagana kwa tabasamu kila upande... ISHARA NZURI

Niliporejea nyumbani akili ikawa ni kwa Ramla tu, ilipofika usiku tukaanza kuwasiliana kwa msg, tulitaniana, tulisifiana, daah basi sikulala siku hiyo,, kwa kifupi Ramla alikua ni binti mrembo alieumbika kike, anapendeza machoni, hali ilikua hivyo kwa karibu siku tatu mfulilizo mwishowe kijana wa Kinyamwezi nikajitosa kutamka maneno matatmu ya kuomba hifadhi ya nafsi yangu katika bustani ang'avu la moyo wake, Haikua kazi rahisi sana kutokana na mbwembwe na mapozz niliyokutana nayo kwake, haikunifanya nikatae tamaa nikaendelea kila siku kumgasi Mwishowe Mtoto Ramla akinielewa na kunikaribisha sio tu sebuleni bali mpaka chini ya uvungu wa moyo wake, ikawa ni mapenzi moto moto mpaka kizunguzungu!!, Ndani ya wiki kama mbili tu za mapenzi yetu moto moto muda wangu wa kurudi Dar ulifika na nikawa sina budi kuondoka..

Nakumbuka tuliagana siku hiyo kwa furaha iliyojawa na majonzi maana Ramla alikua akilia akihisi nitamsahau nikfika mjini lakini nilimbembeleza na kumuahidi kua nikifika Dar baada ya wiki mwezi mmoja ningemtumia nauli aje ili nimfanyie mpango wa Shule maana alikua amenieleza mambo mengi kuhusu Familia yao kua wanaishi maisha ya tabu na dhiki tangu baba yake Mzazi alipoikimbia Familia yeye akiwa mdogo sana, Alinieleza kua aliishia kidato cha nne hivyo alitamani sana kuendelea na masomo lakini hali ya kiuchumi haikua nzuri kwao na Mama yake hataki Ramla aende Dar kwa huyo mama yake mdogo mke wa Boss wangu Mr Jimmy kwa kua yule alibadilishwa dini na Jimmy na kuolewa hivyo anahofia kua kama akiienda kukaa kule nae ataweza kushawishiwa kufanya mambo kama hayo..

Baada ya mwezi mmoja nikawasiliana na Ramla nikamtumia pesa za nauli kwa ajili ya kuja Dar na pia nikamuongezea pesa za kumuachia Mama yake pale nyumbani ili asipate taabu siku za mwanzo, kweli baada ya siku kama tatu hivi akaja Dar, ilikua ni kazi kubwa kwangu ya kumtoa tongo tongo za macho kwa kumtembeza kila kona ya Jiji hili la maraha ili nae auone mji, na baadae nilimtafutia chuo pale IFM akawa anaishi pale pale katika Hostel nilijipa majukumu ya kumuhudumia kila kitu pia ilibidi sasa mama yake ajue kila kitu kua kwa sasa mimi ndie niko na mwanae na ndie ninae msomesha chuo ikabidi sasa nipeleke kwao na Barua ya Uchumba ili akimaliza chuo tu nimuoe, nikawa sasa namuhudumia mpaka na mama mkwe pindi apatwapo na matatizo. nashukuru Mungu Mama huyu aliniheshimu na kunithamini sana, japo Ramla alikua anenda kwa mama yake mdogo mke wa Boss wangu Mr Jimmy lakini ilikua ni mara moja moja sana...

*****
Wakati tukiwa katikati ya mazungumzo na Ntahondi ghafla mlango ukafunguliwa kwa kasi kisha akiingi Mtu mmoja mnene bila Shaka alikua ndo PABLO MWAKI Maana mimi sikua nikimjua kwa sura zaidi ya kumjua kwa sifa zake tu...
Baada ya mlango ule kufunguliwa kwa kasi aliingia kijana mmoja Mnene, Mweupe, hakua mrefu sana ila ana kimo kiasi chake, niliendelea kuamini kua huyu ndie PABLO MWAKI Tajiri alieamua kuvunja penzi langu kwa Ramla kwa kutumia Ukwasi aliokua nao na hatimae kuniteka na kuagiza vijana wake wanitese na hatimae waniue. Baada ya Njemba hii kusogea mpaka pale chini tulipokua tumekaa tukijaribu kuwaza na kuwazua njia ya kujiokoa kutoka katika mikono ya mabaradhuli hawa, alipofika akauliza huku akiniangalia usoni
"We ndie Naufal?"
"Ndio"
"Ni nani Mwingine zaidi ya huyu Ntahondi anaejua kua ulikua na matatizo na PABLO?" nikamjibu tena
"Hakuna anaejua mkuu" baada ya hapo akaja upande wangu wa kushoto Kisha akamuangalia Ntahondi usoni kisha akasema kwa kebehi na dharau
"Ntahondi, Mrembo wa IFM" Kisha akauliza kwa sauti Nyepesi
"Ni nani mwingine uliempa story za PABLO zaidi ya huyu Naufal?"
"Hakuna anaejua". Baada ya maswali hayo jamaa akatoka nje...

Tulibaku tumepigwa na butwaa huku tukiangaliana, binafsi nilijua fika kua walichotaka kufahamu ni nani mwingine anapaswa kutekwa kabla hajavujisha taarifa zozote zinazoendelea kati yangu na PABLO Ili watakapotuua mambo yao yaendelee kubaki kua ni Siri. ndani ya dakika kadhaa waliingia tena mule ndani vijana wengine wawili wakiwa na kamba mikononi walipofika wakaniinua na kunifunga kamba mikononi na kisha kunining'iniza juu kama mbuzi anaesubiri kuchunwa, kisha wakaja kwa Ntahondi nae wakampeleka mpaka pembezoni mwa kitanda cha Simenti ambacho hua nalalia mimi, kuna kiti maalum kwa ajili ya kupewa mateso ya Umeme nae wakamfunga kisawa sawa halafu wakatoka nje vijana wale...

Tulikaa katika hali ile ya Sintofahamu huku kila mmoja akiwaza yake juu ya nini tulikua tunakuja kufanyiwa, sikuamini kama ndo tulikua tunauliwa kwa kua nilishadokezwa na Ntahondi kua Tungeuawa siku ya Graduation ya kina Ramla ambayo ingefanyika miezi miwili baadae.. nikiwa naendelea kusali sala zote mpaka sasa nikawa nachanganya dua maana nilijikuta Eti nasoma dua ya kuchinjia kuku anhaa Usiombee Matatizo yakufike kooni, Ghafla akaingia tena yule Bonge aliekuja kutuhoji maswali, mara hii akiwa amevalia kihatari hatari, alikua amevaa Bukta ya Jeanz, tishert nyepesi, mikononi aevaa Gloves, aliingia na Kebo(waya) maalum kwa ajili ya kutolea adhabu, sindano ndefu sikujua ni ya nini, mawe ya kupimia uzito kwenye mizani, na vifaa vingine vingi ambavyo sikuelewa na vya nini?, nilipogeuka upande wangu wa kulia nilimuona Ntahondi maskini akilia kwa Uchungu sana..

Njemba ile ikaja usawa wangu na kuniuliza
"Umekataa kutaja mtu anaejua kuhusu suala hili huko nje?!" nikajibu huku nikitokwa na Machozi
"Siwezi kukudanganya kaka, hakuna anaejua", akahamia kwa Ntahondi nae akamuuliza swali kama langu kilichonishangaza na ule ujasiri wa Ntahondi pale alipojibu pengine akiwa ameshakata tamaa ya kuishi tena
"Tumechoka na mateso yenu ni bora mkatuaa tu" majibu yale yalimkera Njemba yule nikashangaa akipiga ngumi za nguvu kama anampiga mwanaume, Ntahondi alikua akilia kwa sauti ya Uchungu sana, nilishindwa kuendelea kumuangalia tukio lile nikawa nimefumba macho, nilipofumbua macho nilimuona Ntahondi akiwa anavuja damu uso mzima..

Kisha Njemba hii ikahamia kwangu, ilipofika haikuuliza kitu, ilikua ni adhabu juu ya adhabu, nilichapwa sana na waya, nikawa nachomwa na ile sindano kwenye Ncha za vodole vyangu, Kijana huyu aliendelea kunipiga bila ya kunipa mapumziko huku akinisisitiza nitaje mtu anaejua mkasa huu, nililia huku nikijitetea kua hakuna anaejua, baada ya kipigo cha muda mrefu kilichoniacha na maumivu makali na majeraha, Baunsa huyu akarudi kwa Ntahondi ma kuanza kumpa sasa mateso ya Shot ya Umeme Ntahondi alikua akipiga kelele nyingi sana! nikaanza kupoteza matumaini kama angeweza kustahmili ukali wa mateso yale na Pengine angemtaja Mwl Honde ambae bila Shaka ndie mtu aliebaki huko uraiani akijaribu kutupigania..

Tuliteswa kwa kiwango cha ajabu bila ya kutaja chochote walichotaka na baadae kijana yule akatoka nje akiwa anavuja jasho sana kwa kazi nzito ya utesaji dhidi ya viumbe wasiokua na hatia, dakika kumi baadae wakaja vijana wale waliotufunga kamba kisha wakatufungua tukiwa hoi, tulikaa kama saa moja hivi wakatuletea chakula kidogo sana na maji, ikabidi mie nijifanye nimeshiba ili tu ale Ntahondi peke yake maana chakula kilikua kidogo kiasi kwamba kisingemtosha hata mtoto mdogo Lakini Ntahondi ane aligoma kula peke yako ikabidi tule hivyo hivyo wote wawili baada ya hapo tukalala mpaka asubuhi

Hali ya mateso iliendelea kila siku jioni na huku tukiambiwa kua wangeacha kututesa kama tutawataja japo watu wawili wanaojua habari ile kua mimi na PABLO Tunagombania Mwanamke ambae ili nao watiwe nguvuni wasije wakavujisha siri itakayokusababisha Serikali pengine ianze kumchunguza PABLO na hatimae kumtia nguvuni, Siku moja alikua huyu Baunsa anaetutesa kila siku na kumchukua Ntahondi kisha akaondka nae na sikujua alipompeleka, nilibaki na hofu kubwa nikijua kua huko pengine Ntahondi ataadhibiwa sana mpaka atatoa taarifa za watu wanaojua sakata hili, pia niljua kua wangeweza hata kumuua huko kama angeendelea na msimamo wa kutotaja mtu hata mmoja, Lakini nashukuru Mungu ilipofika saa moja na nusu jioni Ntahondi alirudishwa ikiwa saa zima limepita tangu waondoke nae..

"Vipi uko salama kweli? nilijua wameenda kukuua" nilimuuliza Ntahondi, nae akajibu
"Niko salama wangu, mie mwenyewe nilijua sitakukuta tena Thanx God tuko salama", nikaendelea kumuhoji kilichojiri huko, nae bila ya kusita akaanza kutiririka
"Mwenzangu sasa hapa we have to do something, kwa kifupi huyu jamaa kaniambia ananitaka kimapenzi na endapo nitamkubali hatokua anatutesa tena na tutapewa chakula kizuri kila siku na atajitahidi kutufanyia mpango wa kutoroka kabla ya siku ya Graduation ambayo ndo imepangwa kua PABLO Atakuja kutuua" Nilijikuta nimeshusha Pumzi nzito, nikiwa sina cha kushauri maana kutoroshwa nataka, lakini sitaki binti huyu audhalilishe mwili wake kwa kumpa Rushwa ya penzi mtu asiemjua vema, pengine ni muathirika wa magonjwa mbali mbali ikiwemo Ukimwi, pia inawezekana ni tama zake tu za ngono lakini wala asitutoroshe. nikiwa bado sijajua cha kushauri Ntahondi akendelea kufunguka kua
"Na ameniambia kua Leo anaenda mjini kuonana na PABLO hivyo ataacha maagizo kwa vijana wake kua watupe chakula kizur na maji na atakaa huko kwa muda wa siku tano tu halafu atarudi hivyo akirudi kasema siku hiyo atakuja kulinda yeye peke na hawa vijana wake wataenda mjini kutembea hivyo siku hiyo ndo nikalale nae..

Tukiwa katikati ya majadiliano ya nini cha kufanya, Mlango ukafunguliwa akaingia mmoja kati ya wale vijana ambao hua wanatufunga kamba kabla ya kuanza kuteswa. lakini safari hii aliingia akiwa na Ndoo mbili za maji, akaziweka chini kisha akatoka nje na kurudi na Mfuko mweusi una nguo na shuka ndani yake kisha akasema kila mtu akaoge kisha avae nguo halafu tusubiri chakula cha usiku, yaani sikuamini kinachotokea maana karibu mwezi na Nusu sasa sijaoga zaidi ya kumwagiwa maji ili nizinduke baada ya kuzimia kutokana na kuzidiwa na kichapo kikali nachopewa mara kwa mara halikadhalika Ntahondi. tukaaingia kuoga zamu kwa zamu na baada ya kupata maji ngozi sasa walau ilionekana ni ya kibinaadamu japo nilikua na vidonda vilivyotokana na moto niliokua naunguzwa kwa kutumia Misumari na Sindano zilizowivishwa kwenye moto, Ndani ya mfuko kila mtu alivaa nguo alizozikuta kutokana na jinsia yake na pia kulikua na shuka mbili za kujifunika, Ntahondi alikua na upele mwingi usoni uliotokana na Mbu waliokua wakituuma siku zote tulipokua tukilala kwenye simenti bila hata ya Shuka..

Baada ya kumaliza kuoga kijana yule kijana akatuijia na kutupeleka kwenye chumba kingine kilichokua na vitanda vidogo viwili na meza moja iliyokua na chakula juu, kisha akatuambia "Mkimaliza kula kila mtu alale kwenye kitanda chake" kisha akatoka zake, nilibaki nikimtazama Ntahondi kwa macho ya mshangao wa kila kinachoendelea, walau sasa tulifarijka kwa huduma mpya tulizopewa, sikua na Furaha sana kwakua niliamini kua siku tano zijazo itampasa Ntahondi awajibike kuzilipa huduma hizi kwa kumuhonga Rushwa ya Ngono yule Baunsa mweupe, baada ya Chakula tulipumzika na kisha tukaendelea na majadiliano yetu..

Nilianza mimi kutoa ushauri wa nini cha kufanya ambapo Ntahondi aliuafiki kisawasawa ushauri huu
"Sasa huu ndo muda wetu wa kutoroka, muda wa kuokoa maisha yetu, cha kufanya tuwe majasiri kwa kila hatua, kwakua siku hiyo ambayo jamaa anataka ulale nae atakua peke yake humu kama Mlinzi itatupasa tuitumie fursa hiyo kumzidi akili, tumtie nguvuni sisi na hatimae tuondoka humu ndani"
"Kwahiyo tutamuwekea sumu au? "
"Humu ndani hatuwezi kupata sumu kirahisi hivyo"
"Kwahiyo tutafanyaje? "
"Itabidi tujue Bunduki yake anaiweka wapi ili ukiwa nae kitandani mie nitaingia ghafla na kuichukuanajua kutumia Bunduki ipasavyo na hapo hapo sitamkawiza nitausambaza Ubongo wake na safari itaanza, cha msingi ukishaingia nae tu Chumbani hakikisha hamjafunga mlango"
"Naufal hiyo ni hatari sana, una uhakika kua unajua kutumia Bunduki wewe? "
"Ondoa shaka, mie zamani nilikua naenda Porini kuwinda na kaka yangu huko nijifundisha kutumia Bunduki za aina nyingi tofauti"
Ntahondi aliinuka kwa fu...raha na kunikumbatia kwa wazo zuri nililitoa, na hapo tukaanza kujiandaa tu na utekelezaji...INAENDELEA HAPA HAPA
 LIKE PAGE YETU HAPA ==>www.facebook.com/2jiachie

No comments

Powered by Blogger.