RIWAYA: SIKU YA GRADUATION...SEHEMU YA SITA (6)
Mwanga wa chumbani ulikua ni hafifu mno hivyo ilikua ni hali nzuri kwangu kuzidi kujiamini, sasa nikatambaa mpaka mbele ya kitanda kasha nikasimama ghafla. niliposimama tu jamaa akshtuka nae akaruka kutoka kitandani na kunirukia, me nikamkwepa hapo hapo mapambano yakaanza nikafyatua Risasi moja lakini ikamkosa jamaa alikua ni mwepesi wa viungo kuliko hata nilivyotegemea, akaenda upande wa nyuma wa kitanda nikapiga risasi ya pili nayo ikamkosa, hapo sasa hali ya tafrani ilizidi kupamba chumbani mule, nilikua naogopa kufyatua Risasi hovyo nikihofia kumdhuru Ntahondi ambae nae alikua kitndani hapo, niikaanza kuhaha sasa maana nilijua ndani ya pisto ile hapakua na Risasi zaidi ya tano ghafla nikasikia mlango wa chumbani umepigwa kwa nguvu na jamaa mwingine akaingia nilipogeuka kumuangalia ni nani hiyo ndo ilikua mistake ya kwanza Baunsa yule alinirukia na kunipiga ngumi ya kichwa nikaenda mpaka chini, pistol ikaniponyoka ikarukia kitandani.. nikaanza kazi ya mchezo wa ngumi na watu wawili sasa lakini kutokana na ile hali Mwanga mule ndani ikanisaidia kidogo maana baunsa alikua anpiga hovyo mpaka anampiga mlinzi wake..
Mpambano ulichukua takribani dakika sita ndipo nilipohamia upande wa pili karibu na kitanda na haraka Ntahondi akanipa tena ile Pistol nilipoishika tu nikamuelekezea yule Mlinzi
"Weka Silaha chini!!!" niliongea kwa ukali, wakati huo Ntahondi analia akiwa amesimama upande wa kiti kile chenye Bunduki, Mlinzi akawa bado ameshikilia vema Bunduki yake basi hapo hapo sikumkawiza nikamdungua Risasi ya karibu ya kifuani upande wa bega la kulia akaanguka chini huku akipiga kele kali za maumivu, nilipogeuka kwa Baunsa huyu nikamfyatulia Risasi Loo salaleee Risasi zilikua zimekwisha na jamaa akaligundua hilo sasa ikawa kizaa zaa mule ndani wote macho yetu yako kwenye Bunduki ya huyu Mlinzi sasa...
Ngumi zikaanza tena kwa kasi ya ajabu, kiukweli jamaa alikua akinizidia nguvu sana tu tatizo alikua kahamaki hivyo nikawa naitumia hiyo fursa kumpa mapigo ya kumshtukiza, nikiwa nagalagazana nae pale sakafuni wakati huo huyu mlinzi analia kwa maumivu makali ya Risasi, baunsa hyu akanizidia nguvu na kuniweka chini kisha akaanza kunipa makonde ya kichwa mpaka nikataka kupoteza fahamu, hapo hapo Ntahondi akaja kwa kasi ya ajabu akiwa amenyanyua kiti kidogo cha chuma na kupiga nach yule jamaa kichwani jamaa alitoa sauti moja tu kali na kisha akaenda mpaka chini akapoteza fahamu
Nikanyanyuka haraka na kujifuta damu zilizokua zikinitoka puani na upande wa kisogoni nilikua nimepasakua baada kuanguka pale chini, hara haraka tukachukua Bunduki zote mbili ile ya Mlinzi na ile ya huyu baunsa iliyokua kwenye kiti kisha tukatoka haraka mule ndani, tukaenda mpaka Getini hapakua na mtu mwingine tukafungua Geti kisha tukatoka nje kabisa na kuanza kukimbia hovyo kama kuku aliekatwa kichwa, maana hatukujua tuko wapi na tunaenda wapi, hatukujua ni mkoa gani ule wala ni wilaya gani ukizingatia na giza nene lililokutanda Msitu ule ni hatari lakini hatukukata tamaa tukaendelea kukimbia kwa kwenda mbele tu..
Tulikimbia kwa umbali mrefu tukiwa peku, majani magumu almaarufu kama Magugu yalitupasuapasua miguu, ikafika mahali Ntahondi akawa analia huku akilalama kua pumzi zimemuishia hivyo hawezi kukimbia tena, akagoma kukimbi akilalamika amechoka sana, pia miguuni alikua akivuja damu zilizotakona na kuchomwa na visiki vikavu vya miti mule Msituni na mbaya zaidi hakukua na dalili hata ya Nyumba moja licha ya umbali tuliokimbia karibu kilometa tano,Nilijaribu kumbembeleza ajikaze tuendelee na safari lakini ilishindikana Binti alikua hajiwezi ikanibidi sasa nimbebe mgongoni na safari ikaendelea japo nami nilikua hoi bin taabani ila nilijikaza tu..
Tulizidi kutembea umbali mrefu japo ilikua ni shida lakini tulijikaza, mara kwa mara tulikua tukipumzika njiani kisha tukiendelea na safari ndefu isiyojulika tuendako, baada ya Ntahondi kupata tena nguvu tukaanza tena kukimbia kuelekea hovyo hovyo tu mpaka hatimea kwa mbali tukaanza kuona kama dalili ya makazi ya watu, tulipozidi kusogea tuliona majaruba yaliyolimwa mahindi na vitu kama karanga vile hatukuweza kuona vizuri kutokana na giza totoro lililotawala maeneo yale, tulipokaribia tukaanza kuona nyumba zilizoezekwa kwa nyasi, hii ilikua ni ishara sasa kua japo tumefika kwenye makazi ya watu ila hapaku mjini kabisa, hatukujali sie tulichokua tukikililia ni ni msaada tu kutoka kwa Raia wema, tulipofika maeneo yale palikua kimya sana bila shaka watu walikua wamelala, kwa kukadiria ilikua ni mida ya saa tisa za usiku, tulijaribu kujadiliana kama tuwagongee wenyeji kisha wakitufungulia ndo tujieleze kwao na kuomba msaada lakini hatukufanya hivyo tukihofia kua wasingweza kumfungulia mtu wasiemjua na ingeleta madhara kwetu kama tungepigiwa kelele za wizi..
Tukaenda mpaka kwenye nyumba nyingeine ambayo ilikuahaina milango tukaingia mule ndani, ilikua ni kama sehemu wanayoitumia kwa kupikia, kulikua na majiko ya kienyeji, pia kulikua na viroba kama vitano hivi vyenye mabunzi ya mahindi, tukaamua kua tulale mule mpaka asubuhi kisha wenye wakija tutawaeleza tatizo letu, Naam tukaribu kulala lakini usingizi haukupita kabisa pengine kutokana na woga tuliokua nao, ikichagizwa na mbu wengi waliotusshambulia mule jikoni, baada kama ya nusu saa tulisikia mlio wa piki piki zikija kwa kasi tukaamka na kusikiliza milio ile ikua ikielekea wapi na baada ya dakika kadhaa tulikubaliana wote kua ni pikipiki za zilikua zikija kule tulipo, tukasimama haraka nikamshauri Ntahondi kua tuingie ndani ya mifuko ile yenye mabunzi ya mahindi ili tujifiche kama hatari ile itaku ni yetu..
Naam nikampakia Ntahondi katika kiroba kimoja kisha nikakiegesha vizuri ukutani kisha nikamsisitiza atulie, nami nikafanya hivyo hivyo kwenye kiroba kingine kilichokua nyuma ya jiko la kupikia, baada ya dakika kama tano sauti zile za pikpiki zilizidi kuja maeneo yale na kisha zikasimama maeneo yale ya kijiji kisha nikasikia Sauti za watu wakiongea kwa kufokezana, sikujua ni kina nanii?! baada ya Muda niliisikia Sauti ya yule Baunsa aliekua amezimia kule Mjengoni akimgongea mwenye nyumba
"Mjumbe Fungua haraka kabla sijakichoma moto hiki kibanda chako" hofu sasa ikazidi kutanda moyoni mwangu, nilijilaumu sana kwa kumuacha bila ya kummalizia Yule Baunsa, baada ya muda nikawa naona mwanga wa tochi ukimulika nje na baada ya mazungumzo marefu ya huyo mjumbe kisha wakaanza kuongoza wakija kule jikoni
"Kuna majambazi watatu mmoja mwanamke wamekuja kutuvamia kule kwenye godauni letu la nafaka wamemuua mlinzi na mimi wamenijeruhi sana, tazama damu zote hizi, kama mmewahifadhi naomba muwataje Laa sivyo mtajuta" Ilikua ni sauti ya yule Baunsa, kisha wakaja mpaka kule Jikoni
"Hii mifuko a nini?" aliuliza baunsa
"Ni mabunzi ya mahindi hua tukipukuchua mahindi ndo tuyaweka humo"
"Zungu hebu pekua pekua humo kwenye hiyo mifuko kama hakuna kitu twende na huko wanakolala"
mwanga mkali wa tochi uliendelea kumulika ndani chumba hiki cha wazi, kasha nikasikia mlio wa mifuko ile ya Sandarusi, nikaanza kulia kwa moyoni sasa nikijua tunakamatwa tena..
ITAENDELEA SIKU YA KESHO HAPA HAPA
LIKE PAGE YETU HAPA ==>www.facebook.com/2jiachie
Post a Comment