REAL MADRID YAITANDIKA BAYERN MUNICH 4-0 NA KUIVUA UBINGWA WA ULAYA
Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kuhusu
Bayern Munich baada ya usiku huu kutandikwa mabao 4-0 na Real Madrid
katika Nusu Fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa nyumbani kwao, Allianz Arena mjini Munich, Ujerumani.
Bayern wamevuliwa ubingwa wa Ulaya kwa kipigo cha jumla cha mabao 5-0, baada ya awali kuchapwa 1-0 Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid katika Nusu Fainali ya kwanza na Real inaingia Fainali kwa mara ya kwanza baada ya miaka 12, ambako itakutana na ama Chelsea au majirani zao Atletico Madrid ya Hispania pia.

Shujaa wa Real alikuwa ni Sergio Ramos aliyefunga mabao mawili, la
kwanza dakika ya 16 pasi ya Luka Modric na la pili dakika ya 20 pasi ya
Pepe kabla ya Mwanasoka wa Bora Dunia, Cristiano Ronaldo kumaliza kazi
kwa kufunga mabao mawili dakika ya 34 pasi ya Gareth Bale na dakika ya
89.
Bayern Munich: Neuer, Lahm, Dante, Boateng, Alaba,
Schweinsteiger, Kroos, Ribery/Gotze dk73, Muller/Pizarro dk73 na Robben,
Mandzukic/Martinez dk46.
Real Madrid: Casillas, Carvajal, Pepe, Ramos/Varane
dk75, Coentrao, Alonso, Modric, Di Maria/Casemiro dk84, Ronaldo, Bale na
Benzema/Isco dk80.
Post a Comment