ad

ad

BREAKING NEWS; FRANK DOMAYO NAYE AANGUKA MIAKA MIWILI AZAM FC

KIUNGO mkabaji wa Yanga SC, Frank Domayo amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na mabingwa wapya wa Tanzania Bara, Azam FC
 jioni ya leo mjini Mbeya.

Domayo amesaini Azam FC baada ya kumaliza Mkataba wake wa 

miaka miwili na Yanga SC, ambayo alijiunga nayo akitokea JKT Ruvu miaka miwi iliyopita.
 
 Kutoka Jangwani hadi Chamazi; Frank Domayo akisaini 
Mkataba wa Azam FC leo

Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa Mohamed ‘Father’ amesema 
katika kuendelea kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu
 ujao wamepiga hatua nyingine kwa kumsaini Domayo.
Frank Domayo akitia dole gumba, maana yake ni mchezaji 

mpya wa Azam FC

“Kama unavyojua, baada ya kumaliza msimu vizuri tukiwa 

mabingwa wa Bara, tuligundua mapungufu kwenye kikosi chetu na 
kwa ushauri wa mwalimu wetu (Joseph Marius Omog) ndiyo tunayafanyia kazi,”alisema Father.

Domayo anakuwa mchezaji wa wa pili ndani ya siku mbili kusajiliwa na 

Azam FC kutoka mabingwa wa zamani na mabingwa wa kihistoria 
Tanzania Bara, Yanga SC baada ya jana klabu hiyo kumsaini 
mshambuliaji Mrundi Didier Kavumbangu.

CHANZO: BIN ZUBEIRY 

No comments

Powered by Blogger.