JACK PATRICK AANGUA KILIO KORTINI... BAADA YA KUPANDISHWA WACHINA WAMZOMEA
HATIMAYE
modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ amepandishwa
kortini kwa mara ya kwanza huko Macau nchini China, Aprili 10, mwaka huu
kwa kukutwa na madawa ya kulevya tumboni aina ya heroin kete 57 au kilo
1.

Jack alipandishwa kwenye korti hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu alipokamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’ Desemba mwaka jana akitokea Bongo kupitia Thailand na kuingia nchini humo.
ILIKUWAJE?
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilichopo Macau, Jack alifikia hatua hiyo dakika 15 baada ya kupanda kizimbani na kukutana na nyuso za Wachina tu zikimwangilia.

Kikaendelea: “Unajua kwa kawaida mtu anapopanda kizimbani mara zote
anafarijika sana endapo atawaona anaowafahamu, hasa ndugu zake ambao
watafika kumtia moyo, sasa yeye hakulipata hilo.”
DAKIKA 10 ZATUMIKA KUMSOMEA MASHITAKA
Kuna madai kwamba, msoma mashitaka wa mahakama hiyo alitumia
dakika 10 kutokana na taratibu za kisheria za huko huku akitakiwa kusema
ndiyo au hapana tu kabla keshi hiyo kupigwa kalenda hadi Mei 23, mwaka huu.
KUNA MADAI ALIZOMEWA
Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, mbali na kukutana na upweke huo
mahakamani, pia Jack alipata kisanga kingine pale baadhi ya raia wa nchi hiyo
walipomzomea kwa sauti ya chini wakati akitoka kortini.
Inadaiwa kuwa, kwa Wachina kumzomea au kumsema vibaya mtu
aliyedakwa na madawa ya kulevya ni kawaida kwani hakuna biashara,
inapigwa vita nchini humo kama ya unga wakiamini unaangamiza nguvu kazi ya kizazi kijacho.
NDUGU WADAIWA KUMKATIA MAWASILIANO
Habari nyingine kutoka chanzo chetu zilidai kwamba, kwa sasa Jack
amebaki yeye na Mungu wake baada ya nduguze waishio Bongo kumkatia mawasiliano kwa kile walichodai kuwa kitendo alichokifanya kimeiaibisha familia nzima.
“Unajua
ndugu zake walikata mawasiliano kabisa? Nchi nzima au tuseme dunia
nzima kilio ni jinsi vijana wanavyoharibika kwa madawa ya kulevya, sasa kule
kubainika kwamba
Jack alibeba unga tumboni kwenda kuuza kumeifanya familia kujisikia vibaya sana,”
kiliongeza chanzo hicho kikiomba chondechonde kisitajwe gazetini.
KAMA ATARUDI BONGO SALAMA
Habari zaidi zinadai kwamba modo huyo ambaye pia ni Miss Ilala No 3, 2005,
aliwahi kumwambia mshirika wake mmoja akiwa mahabusu kwamba, kama
atabahatika kurejea Bongo salama,
atakwenda kupiga dua juu ya kaburi la mama yake ili amsimamie katika kumwondolea
nuksi kama siyo mabalaa. Baba wa Jack anadaiwa kuishi nje ya nchi.
TUJIKUMBUSHE
Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Macau
nchini China akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou,
Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China ambako ilidaiwa ndiko
alikokuwa anafikisha unga huo.
Ilidaiwa kuwa miongoni mwa mambo yaliyochangia kukamatwa kwake ni
kuonesha uso wenye uchovu, kuanza kuwa na hali mbaya ya mwili, kushindwa
kujibu maswali vizuri na hati yake ya kusafiria, yaani ‘passport’ kukutwa
imegongwa mihuri ya kuingia nchini humo kila mara jambo ambalo wakaguzi
waliliona si la kawaida
kwa msichana kama yeye.
CHANZO NI GLOBAL PULISHERS
LIKE PAGE YETU HAPA ==> www.facebook.com/2jiachie
Kete zinazosadikiwa kukutwa na modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ akiwa amezimeza
1
yakiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 223 huku ishu kubwa kwa
muda wote aliokuwa mahakamani ikiwa ni kuangua kilio kila wakati.Jack alipandishwa kwenye korti hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu alipokamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’ Desemba mwaka jana akitokea Bongo kupitia Thailand na kuingia nchini humo.
ILIKUWAJE?
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilichopo Macau, Jack alifikia hatua hiyo dakika 15 baada ya kupanda kizimbani na kukutana na nyuso za Wachina tu zikimwangilia.

Akiwa chini ya ulinzi wa polisi akipelekwa selo.
“Yeye
alijua angekuta Wabongo au hata watu weusi wakimpa kampani, lakini
matokeo yake alikutana na sura za Wachina tu,” kilisema chanzo chetu.Kikaendelea: “Unajua kwa kawaida mtu anapopanda kizimbani mara zote
anafarijika sana endapo atawaona anaowafahamu, hasa ndugu zake ambao
watafika kumtia moyo, sasa yeye hakulipata hilo.”
DAKIKA 10 ZATUMIKA KUMSOMEA MASHITAKA
Kuna madai kwamba, msoma mashitaka wa mahakama hiyo alitumia
dakika 10 kutokana na taratibu za kisheria za huko huku akitakiwa kusema
ndiyo au hapana tu kabla keshi hiyo kupigwa kalenda hadi Mei 23, mwaka huu.
KUNA MADAI ALIZOMEWAChanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, mbali na kukutana na upweke huo
mahakamani, pia Jack alipata kisanga kingine pale baadhi ya raia wa nchi hiyo
walipomzomea kwa sauti ya chini wakati akitoka kortini.
Inadaiwa kuwa, kwa Wachina kumzomea au kumsema vibaya mtu
aliyedakwa na madawa ya kulevya ni kawaida kwani hakuna biashara,
inapigwa vita nchini humo kama ya unga wakiamini unaangamiza nguvu kazi ya kizazi kijacho.
NDUGU WADAIWA KUMKATIA MAWASILIANO
Habari nyingine kutoka chanzo chetu zilidai kwamba, kwa sasa Jack
amebaki yeye na Mungu wake baada ya nduguze waishio Bongo kumkatia mawasiliano kwa kile walichodai kuwa kitendo alichokifanya kimeiaibisha familia nzima.
“Unajua
ndugu zake walikata mawasiliano kabisa? Nchi nzima au tuseme dunianzima kilio ni jinsi vijana wanavyoharibika kwa madawa ya kulevya, sasa kule

Post a Comment