CHOMBEZO: MPANGAJI SEHEMU 16
ILIPOISHIA
Baada ya
kuanika akanifata pale nilipo na kisha akaanza kuongea maneno ambayo,dah!
Sikudhani mtoto kama yule angeweza kuyanena.
“Nasikia
unamla dada”.Alianza.
“Mh!We Shei
unawehuka?”.Ilibidi niulize.
“We sema tu!
Unamla dada?’.Alikazia.
Songa nayo..
“Embu
kaendelee kufua”.Nilimkatisha maswali yake.
“Basi
sasa,mimi nilikuwa nataka kukusaidia jambo lakini yaonekana huna
mpango”.Aliongea huku ananiacha pale peke yangu.
“We Shei
embu rudi rafiki yangu”.Nilimwita.Naye bila hiyana akarudi.
“Niambie
kuna nini?”.Nilimuuliza.
“Sema
kwanza. Unamgonga au humgongi”.Kicheko kilinibana hasa nikiangalia anayeniambia
hayo.
“Poa.
Nimefanya naye. Kuna nini kwani?”.Nilimjibu na kumtupia swali.
“Ulitumia
ndomu?”.Swali lingine lilikuja kwangu.
“Sasa
wadhani mimi namuamini msichana kama yule hadi nisitumie kinga?Kinga sitatumia
kwa mtu nayejua hana tabia za ajabu”.Nilimjibu.
“Ahaaa. Hapo
basi,hilo muhimu sana. Yule ni dada yangu lakini kuwa makini naye,unaweza
kuzikwa. Hapo kaenda viwanja,akirudi yupo bwii”.Aliongea Sheila na kuondoka
eneo lile kwa ajili ya kwenda kumalizia kufua.
Maneno yake
yalikuwa kama yameamsha jambo na kutaka kulijua zaidi. Nikasema lazima
nijitahidi ili nihakikishe maneno yale kutoka kwa Sheila.
Basi siku
hiyo nilikaa nje kwa muda mrefu kuliko siku zote ili tu! Nimuone huyo Farida na
muda anaorudi na kuhakikisha maneno ya Sheila.
Ndipo mida
ya saa nne na nusu za usiku,nilisikia mtu kama ananyata kuingia eneo lile la nyumbani.
Na mimi niliposikia hivyo,nilijificha kwa pembeni kidogo ili nisionekane pale
atakapotokeza.
Mara
nilimuona Farida akiwa kavalia kimini kimoja matata sana na brazia moja ya
ajabu mno.
Kile kimini
kiliishia juu ya mapaja,hali ambayo kama akiinama basi nguo yake ya ndani
ingeonekana,wakati huo ile brazia ilikuwa ni kama chandarua,yaani ilikuwa
inamatobo matobo halafu ndani hakuvaa kitu chochote. Hali hiyo ilifanya chuchu
zake zitoke nje kupitia yale matobo ya brazia aliyovaa.
Aliangalia
huko na huko kisha alitoa kimkoba chake na kunyofoa khanga mbili. Moja aliivaa
chini na nyingine aliitanda kwa juu. Na baada ya kufanikiwa hilo,alienda hadi
lilipo-dirisha lao na kuanza kumuita Sheila kwa sauti ya chini,na baada ya
Sheila kuitika,aliulizwa kama baba yake yupo. Akajibiwa hayupo,na ndipo ahueni
ya Farida iliposikika kwa kushusha pumzi moja ndefu.
Mimi kama
kawaida yangu,huwa sipendi sana kumficha mtu. Baada ya Farida kutoka pale
dirishani,alienda hadi ulipo-mlango wao wa sebuleni. Na mimi niliona huo ni
muda muafaka wa kujifichua mahala nilipokuwepo.
Kwa mbwembwe
nyingi nilianza kwa kupiga mruzi wangu uleule ambao haulewekagi ni wimbo gani
unaimbwa katika ara ile ya mruzi.
Nilimuona
kama kashtuka lakini alijitahidi kuficha hisia zile na kunifata hadi pale
nilipokuwa nazuga napiga mruzi.
“Kwani P
ulikuwa hapa muda mrefu eeh”.Aliniuliza swali ambalo wakati linakuja lilikuja
na harufu ya pombe.
“Unakunywa
na pombe mwenzetu?”.Nilimuuliza swali badala ya kujibu swali.
“Aaagh.
Imetokea tu leo,nikajikuta nimekunywa”.Alinijibu huku akiangalia pembeni kama
mtu atafutaye kitu pale nje.
“Mmmh,kwa
hiyo na hayo mavazi ya ndani nayo utasema umetokea tu! Kuyavaa,si ndio
mama?”.Nilimuuliza swali lingine.
“Daah!
Yaonekana ulinisubiri kitambo,kama mzazi wangu vile”.Alinijibu Farida kwa
maneno ambayo yalikuwa yana nia ya kuanzisha vurugu.
Sikuwa na
wasiwasi na shombo zake bali nilimchukulia kama
mtu asiyejielewa afanyalo. Nilimuangalia usoni kwa macho yaliyojaa
hasira zilizochanganyika na huruma juu ya maisha yake, na yeye aliniangalia kwa
macho yake ambayo yalikuwa makavu na tayari kwa ajili ya vurumai. Wakati huo
Sheila alishafungua mlango na kubaki mlangoni akitutazama tunachofanya.
“Hongera kwa
maneno yako matamu. Lakini nimeona kila kitu. Umependeza sana kwa yale mavazi,ila
nashangaa kwa nini uliamua kuvaa mikhanga”.Niliongea huku bado macho yangu
yakiwa usoni pake.
“Hayo
hayakuhusu babu wee. Jali biashara zako na si kukaa kwa kaka yako na kusubiri
kumuona Farida kavaaje au anafanya nini. Baridi limekupiga kutwa nzima,kisa
unamsubiri mwana wa Donya. Utakufa na Athima mtoto wa kiume,unaelelewa na ndugu
zako. Tafuta vyako bwege wewe,msyuuu”.Aliongea Farida kwa nyodo na kunifanya
nichanue tabasamu la kejeli kutokana na maneno yake yaliyomalizika kwa msonyo
mrefu kutoka kinywani kwake.
16 SEHEMU YA
“Ohooo.
Kumbe na wewe una kidomodomo eeh. Pole sana binti,kama ulidhani mimi nitakuja
juu,umebugi sana. Na jambo usilolijua,litakusumbua sana. Na mwisho wa siku
utabaki unasonya misonyo tu!. Endelea na kazi yako ya umalaya,si ndio
inakufanya ulete dharau na kuniona mimi bwege?Kwa kuwa wewe unatafuta kwa
kutumia mwili wako na mimi nakaa kwa kaka yangu bila kazi,si ndio
eeh”.Niliongea huku nampa mgongo kwa ajili ya kuingia ndani kwangu.
“Wewe
unadhani Mwana FA aliimba bure? Ingekuwa vipi kama kungekuwa hakuna malaya,si
ubakaji ungeongezeka kwa kasi ya ajabu. Acha niwe malaya ili niwalinde wadogo
zangu wasibakwe kwa kuwamaliza hamu wanaume wenye tabia hizo. Usidhani malaya
kaumbwa ili awe malaya,saa nyingine ni maisha tu!”.Maneno hayo yalinikumbusha maneno
ya Mama Tuse na Tuse mwenyewe.
Niligeuka
nikamwangalia sana Farida,kisha nilitikisa kichwa kwa masikitiko na kurudi tena
pale niliposimama mwanzo.
“Hivi wewe
Farida,hapa kwa baba yako umekosa nini wewe?Utake nini usipewe? Utake uende
wapi ukataliwe? Na wewe unadiriki kusema eti hukupenda kuwa malaya?Unafanya kwa
sababu ya jambo?
Jambo gani
ambalo unalifanya linaleta faida kwa baba yako? Hao uanaosema unawalinda
wasibakwe,wewe uliwahi kubakwa hapo mwanzo?Wewe ulilindwa na nani ili
usibakwe?Embu acha chenga,tena bahati yako,ungekuwa anga zangu ningekuchapa
viboko kwa kuwashushia heshma wazazi wako waliokulea kwa kila hali huku
wakihakikisha unapata kila kitu muhimu.
Nimekutana
na malaya mimi,malaya ambao kama wangekuwa ni wewe,sidhani kama wangefanya
yale. Wanamalengo kuliko hata ya mtu ambaye si malaya. Eti na wewe unasema
hukupenda,tamaa za mwili na vitu vikubwa,zitakuponza wewe”.Niliongea kwa hasira
sana maneno hayo,na yeye alitambua kuwa nimepata moto hivyo alikaa kimya bila
kusema chochote hadi pale nilipoingia ndani kwangu na kusikia mlango wao
ukifungwa.
****************
Kesho yake
Farida hakutoka nje kwa sababu ya aibu. Na mimi nilishukuru sana kwani maneno
yangu yawezekana yalimuingia ipasavyo.
Siku ikapita
bila kumwona na hatimaye wiki ikakata pia bila kumwona bali kumsikia akimuita
mdogo wake,ila nahisi alikuwa anatoka,sema akiniona anakimbia au kujificha.
“Atajua
mwenyewe.Meseji sent”. Ni maneno niliyojisemea siku moja baada ya kuona kimya
chake kikiwa kikubwa.
******************
Kwa upande wangu, muda wa kukaa pale nyumbani
kwa kaka,ulibaki kama wiki mbili na nilikuwa tayari kwa kuondoka baada ya wiki
hizo.
Nilianza
kuwaaga pale nyumbani hasa wale niliyokuwa nawaona. Tulikuwa tumezoeana
sana,hasa utani wangu ndiyo kama chachu kwao ya kuwa wanyonge baada ya kusikia
naondoka.
Wakati
nimebakiza wiki moja niondoke pale nyumbani,likatokeza tatizo kubwa jingine.
Hili ni tatizo kubwa kuliko matatizo yote niliyowahi kuyapata maishani mwangu.
Tatizo hili naweza sema ndilo haswaa,lililonifanya nione Arusha chungu na mbaya
sana kuliko mikoa yote niliyowahi kutembelea.
MPANGAJI sehemu ya 17 itaendelea tena kesho.

Post a Comment