ad

ad

CHOMBEZO: MPANGAJI SEHEMU -14

 ILIPOISHIA...
“Huyu ni mgeni,ni mdogo wake George,katoka Dar. Kafika hapa jana usiku wa saa tatu. Anaitwa Prince”.Mzee yule akanitambulisha kwa wanawe ambao mimi nilishaanza kupiga nao stori kidogo kidogo.
“Karibu Prince”.Nikakaribishwa na mabinti wale kwa wao kupokezana kusema karibu Prince.
“Ehee. Prince. Hawa ni wanangu,huyu mkubwa anaitwa Farida Donyo,huyu anaemfata anaitwa Sheila naye ni Donyo na huyu wa mwisho anaitwa Lilian.
SONGA NAYO HAPA

Sasa kitu nilichoona kama mtego kwangu ni pale kifuani,ha ha haaa,nyie watu dunia hii wamebarikiwa sana kwa maujanja. Alikuwa hajafunga vifungo hadi juu,hivyo alifanya yale matiti yake makubwa yanaonekana vizuri sana. Yalikuwa yamevimba halafu yanang’aa kutokana na ule weupe aliokuwa amebarikiwa na MUNGU.
Nilibaki nimechutama pale nilipokuwa natafuta bandeji,lakini sikuchutama bure,bali nilikuwa namuangalia yeye na uzuri wake aliopewa na muumba.
“Mbona umetulia?”.Aliniuliza huku akiwa ametabasamu.
“Nakuangalia wewe unayeingia nyumba ya watu bila hodi”.Nikamjibu.
“Hamna bwana. Samahani kwa hilo. Vipi umepata bandeji”.Aliniuliza.
“Yap. Ndiyo hii hapa nimeipata”.Nilimjibu baada ya kufungua droo moja ya kabati lile lililobeba TV na kukuta hiyo bandeji.
“Okey. Sasa si unanisaidia kubandika?”.Aliniuliza swali la mtego huku anatoa ile khanga yake na kumbakiza na lile gauni la jinzi.
Teheee. Acheni Adam adanganyike tu! kwa Hawa, wanawake wanavishawishi bwana.
Unajua nini? Lile gauni alilivaa lilikuwa linaishia magotini.Kitendo cha kutoa khanga na kisha kukaa kwenye kochi,kilifanya lile gauni kuvutika kwa juu na kuonesha upaja wake ulionona kama umepakwa mafuta ya kula.
“Nitakubandika tu!Mbona rahisi”.Nilimjibu na kumfuata pale alipo na kuibandika ile bandeji.Wakati nambandika alikuwa natoa visauti fulani sijui ni vya raha au maumivu au uchokozi tu! sababu vilikuwa kama vina nisisimua kamanda. Nilipomuangalia usoni,alikuwa kalegeza macho utadhani ananyonywa pango.
Nilijifikiria kwanza kabla sijafanya maamuzi. Kwanza kabisa,ni siku ya kwanza tu!ndo nimefika,lakini huyu manzi anaanza kuleta ishu zake mazee.
Pili nikaona huyu anataka aniletee kesi kama za wakina Tuse,na zaidi nikaona labda ni kicheche hivyo anakitu anataka anifanyie au labda ni mtego ili nifumaniwe.
Mawazo hayo yalipitishwa kwa haraka na bunge la kichwa changu,na nikaona njia mbadala ni kumuacha kama alivyo,kisha nianze kutafuta marafiki ambao watanipa data za familia ile.
Niliichukua khanga yake na kumfunika maungio yake mazuri na mororo.Kisha kamanda nikatabasamu na kukaa karibu yake ili asihisi vibaya.
“Nikuwekee filamu gani”.Niliongea naye kwa upole ili ajisikie amani ya moyo.
“Hauna ile ya Romeo and Juliet?”.Aliniuliza huku akiwa na aibu kidogo.
“Ile ninayo. Kuna CD nilitoka nazo Dar,ipo hiyo. Si ile ya Leonard Decaprio?”Nilimjibu na kumuuliza ili nipate uhakika.
“Sijui ndio huyo. Yule aliye-act Titanic”.Alinipa uhakika zaidi.
“Okey. Ndio huyo. Ninayo collection yake”.Nilimjibu na kunyanyuka pale kochini na kuelekea chumbani ambapo baada ya dakika kadhaa nilitoka na albamu ya kuhifadhia CD.
Niliitoa CD anayohitaji na kisha nikaiweka na kuanza kuangalia naye tukiwa wote pale kwenye kochi.Yahitaji uvumilivu sana kuwa karibu na mtoto kama yule ambaye unajua wazi alikuja kwa ajili ya mchezo lakini ukamzingua.
Nilimshukuru MUNGU sana pale mdogo wake alipomuita kwenda kuandaa chakula cha usiku kwani angesipoitwa,nahisi uvumilivu ungenishinda. Mapozi niliyokuwa nawekewa,daah! Kama mtego basi niliutegua hasaa. Namshukuru MAULANA kwa kunifanikishia hilo.
****************

Ni baada ya wiki mbili sasa. Tayari nilikuwa mwenyeji wa Arusha hasa eneo lile la fire. Kule ilipo shule ya Themi ndipo nilikuwa na marafiki wengi,huku kule Daraja Mbili nikiwa naenda sana kuangalia wasanii wadogo ambao kwa pale Arusha walikuwa wengi sana kwa kule.
Pale karibu na nyumbani,nilikuwa nimepata rafiki wengi sana,lakini Gasper ndiye alikuwa rafiki yangu mkubwa kutokana na umri wake na hata alipokuwa anasoma. Alikuwa ni kijana mdogo tu! Lakini alikuwa mjanja sana. Yeye alikuwa anasoma shule moja ya kimataifa pale Arusha,kwa hiyo zile tabia za kichalii chalii alikuwa hana. Tabia kama kujiingiza kwenye makundi ya kihuni na uvutaji bangi ambayo ilikuwa kitu cha kawaida sana kwa wana Arusha,Gasper alikuwa hana.

“Kaka vipi. Ushakula mtoto hata mmoja hapo?”.Siku moja jioni Gasper aliniuliza baada ya Farida na wadogo zake kutoka kuangalia filamu.
“Ha ha haaa. Mimi hata sijui tabia zao dogo. Wasije wakanidhuru bure”.Nilimjibu Gasper.
“Hamna,uoga wako tu! Mbona wasafi hao. Yaani kama pesa mpya”.Alinijibu kwa kunipa moyo.
“Ina maana wewe unawajua hawa tabia zao?”.Nikamuuliza.
“Mimi tena. Data za huu mtaa wote ninazo”.
“Acha bwana. Embu niambie kuhusu huyu dada mtu,kwa sababu ndiye anayenitega-tega”.
“Huyo ni kicheche,siwezi kukudanganya,ila haka katoto kengine,kametulia balaa”.
“Ukicheche wake nini huyu Farida,mbona sijawahi kumuona?”.
“Ha ha haa. Huyu katulia sasa hivi tu! Baba yake alimtishia kumpeleka kijijini kwao ndo maana katulia. Anakikundi kimoja cha wenzake,wanajiita MADUU WA UKWELI,wapo wanne, wanaongozwa na dada mmoja anaitwa Cindy. Hao ni nouma,wakivaa hivi wakiwa wanatafuta mabwana,utasema wanaenda bichi”.Gasper alikuwa akiongea huku akiwa siriaz kitu kilichonifanya niamini asilimia zote.
“Daaah! Kwa hiyo ningeuingia hapa eeh. Maana alikuwa ananitega,sema nilikuwa nategua”.Nikamwambia Gasper.
“Hapo umejitahidi,ila si wa kumuacha huyu. Batua kichizi,tena anaonekana anahamu balaa. Ujue muda ajatoka mtaani,yaani katulia sana. Baba yake aliwafata wale wanamuharibu na kuwapiga mkwara,hadi leo wakimuona wanamkimbia. Nasikia ilikuwa mshikemshike balaa. Wanasema dingi ana bastola,ila bado sijaamini hilo”.
“Ha ha haaa,awe na bastola atolee wapi mchungaji huyu?”.Niliongea kwa dharau.
“Ha ha haaa,mimi mwenyewe nilicheka sana. Ila nitafatilia nijue kama kweli. Ila haka kakati,kenyewe kametulia sana,hakana tatizo. Ningekuwa mimi,ningepiga wote”.Alikuwa bado Gasper.
Nilitabasamu kimoyomoyo na kujisemea kwa kejeri.
“Ungejua malengo yangu. Ungesipotoa siri zao”.Niliwaza hivyo.
“Ndiyo hivyo kaka. Watoto wa Kimasai hawa,wanajua mambo hatari. Piga mizigo. Halafu usiofu kuhusu magonjwa,ndomu zipo. Tumia ujilinde”.Gasper alizidi kumfundisha mwalimu jinsi ya kujibu mtihani.
“Haya kaka.  Ngoja nimsubiri anitege tena sasa. Napiga bila kukwepesha. Kumbe cheche bwana”.Nilidhamiria kweli kupiga Farida.
“Kazi ni kwako kaka”.Gasper alinijibu na tukaanza kupiga soga nyingine hadi mida ya jioni ambapo aliondoka na kuniacha mimi nikijipumzisha kitandani kwangu.

Siku hiyo nakumbuka ilikuwa ni Jumatatu. Kaka kama kawaida alikuwa kaenda mzigoni kwake ambapo alikuwa anarudi siku za wiki endi. Baba wa Farida alikuwa naye kaelekea kanisani afanyapo kazi.
Nikiwa bize na kuacheza play station ambalo nilimuomba kaka anunue,mara akaingia Farida akiwa kavaa koti langu lile nililompa wiki tatu zilizopita.
“Ayaaa,na wewe umekuwa mtoto?”.Alianza Farida baada ya kuniona nacheza game.
“Aaah,kawaida bwana”.Nilimjibu na kuacha kucheza ili nimkaribishe.
Alikuwa kapendeza sana,kila siku alikuwa anajaribu kujiweka mpya. Hicho ndicho kitu nilichokuwa namsifu. Siku hiyo alikuwa kavalia sketi kama ya kutereza,ni kama mpira hivi,au leiza. Halafu ilikuwa si ndefu sana bali imeishia juu ya magoti,basi na ule urefu wake,haki ya MUNGU sikuweza kujizua kumsifia.
“Mmmh!Leo mama yangu umetoka. Kama Jojo vile”.Nilimsifu.
“Embu toka hapa. We kazi yako kunifananisha na huyo msanii tu”.Alijibu huku tabasamu halimuishi midomoni mwake.
“Ndo umeniletea koti langu nini,maana nimelimiss”.Niliachana na mada za utani na kwenda kwenye kitu changu.
“Wewee,hapa hupati kitu. Hili umenipa mwenyewe”.Alinijibu huku bado kasimama karibu na mimi. Wakati huo nilikuwa bado sijaamka pale chini nilipokuwa nacheza game.
“Embu acha masihara hayo. Koti elfu arobaini hilo”.Nilimjibu huku bado nikiwa palepale.
“Ndo nshakudhurumu hivyo”.Alinijibu na kisha kugeuka kama anaondoka. Hapo nilinyanyuka haraka na kuanza kumfata.
Kitendo kile cha kunyanyuka haraka vile,kilimfanya kama ashituke na kutaka kukimbia,ila tayari kamanda nilikuwa karibu yake nikivuta koti langu.
Ikawa vuta nikuvute,mimi huku,yeye kule. Lakini wasichana wana nguvu za kipekee. Niliona kama litachanika tukiendelea kulivuta. Hivyo nikaamua kumwachia.

Kitendo cha kumuachia,alianza kujigamba na kujiona kashinda. Basi kwa hasira nikamfata hadi pale alipokuwa amesimama kisha nikalianzisha tena.Yaani nilianza kulitaka tena koti langu.
Basi ilikuwa nikifata mkono huu,analeta mkono ule.Nikiufata mkono ule,analipeleka kwa nyuma. Dah!Ilikuwa mshikemshike hatari lakini hatimaye nililibamba kwa mikono yangu miwili. Lakini mikono hiyo ilikuwa imepita kiunoni kwake,na kulikamatia koti kwa nyuma kwa sababu ndipo lilipokuwepo.
Hekaheka nyingine zikaanzia hapo.Koti lipo kwa nyuma,na mimi nimelikamatia hukohuko.Hapo ikawa balaa,kwani alijipapatua na mwisho wake tukajikuta tunadondokea kwenye kochi,yeye kwa chini mimi kwa juu.

Kile kifua chake kilikuwa sawa kabisa kwenye kifua changu. Hapo sasa nikapata mihemko minginee.
Tuliangaliana kwa muda,na tukajikuta wote tunacheka,na tulipoacha kucheka,tuliacha sawia.Hapo kamanda nikaanza kusogeza midomo

yangu taratibu kwenye midomo yake. Ile mishe ya koti,nikawa nimeisahau.

“Aaah, shit!. Nataka kufanya nini hapa?”.Nilijikuta nalalama peke yangu na kujitoa kwenye kifua cha Farida kwa kukaa pembeni.
Farida naye kwa aibu akainuka bila kusema neno na kukaa pembeni ya kochi lile kama mimi. Wakati huo nilikuwa nimejiinamia huku nimejishika kichwa kuonesha kama kujilaumu kwa kitu nilichokuwa nataka kufanya,na kumbe ilikuwa chezo tu!. Kamanda nilikuwa nataka kubembelezwa ili mtoto ajilengeshe mwenyewe.
Baada kama ya dakika moja na nusu,nilisikia kama kuna msukumo kwenye kochi kuja kwangu. Msukumo ule ulikuwa ni wa Farida akijivuta kuja kwangu.
“Sasa mbona umepoa hivyo P?”.Aliniuliza kwa sauti ya puani.
**Chombezo hili litakuwa likitoka kila siku  ya Jumapili na Jumatano tu.
Chombezo: MPANGAJI
Sehemu: 14
Mtunzi: Frank Masai
Simu: 0717 738973

No comments

Powered by Blogger.