ad

ad

AZIZA WA FACEBOOK....SEHEMU YA 2



ILIPOISHIA
MIMI: Kipi?

EDUADO: Otea.

MIMI: Hebu niambie kipi?

EDUADO: Ugonjwa wako.

MIMI:Unamaanisha nini?

EDUADO: Mtoto Mpemba.

MIMI: Hahahaha! Kaka acha utani, utanifanya nimfuate sasa hivi.

EDUADO: Ndio hivyo. Mtoto ni pini sana, pini ile iliyosimama.

MIMI: Hahaha! Pini kama ya Blackberry vile.

EDUADO: Acha kaka. Mtoto ni pini zaidi ya zile za Blackberry. Kwanza ukimuona tu, mtoto utampenda. Mavazi yake sasa…weeeeeee.

 Songa nayo....
MIMI: Hebu nipe sifa zake kwa ujumla.
EDUADO: Nisikilize. Mtoto ni wa kipemba. Ana nywele ndefu zinazomfikia chini ya mabega yake, mtoto ana hipsi zilizopangika, hapa mashavuni mwake ana vijishimo viwili, lipsi lainiiiii kila wakati zinang’aaaaa.
MIMI: Kingine?
EDUADO: Mtoto ana sura nyembamba, masikio hayaonekani sana, kifuani hapa kumesimama vizuri sana, mavazi yake huwa ni suruali za jinsi kwa sana.
MIMI: Umesema anaishi wapi?
EDUADO: Anaishi Masaki.
MIMI: Halafu mimi naishi uswahilini Tandale. Umesema anamiliki simu gani?
EDUADO: Anamiliki iPhone 5.
MIMI: Halafu mimi namiliki Nokia ya Tochi. Umesema baba yake ana gari?
EDUADO: Yeah! Yeye mwenyewe analo.
MIMI: Mimi sina gari na baba yangu hana hata gari.
EDUADO: Acha kujizarau Ibra. Mtoto unang’oa huyu.
MIMI: Usijali. Ushawahi kufika kwao?
EDUADO: Yeah kaka. Kwanza hiyo nyumba yao….duh! Kuna watu wanakufuru. Kwanza bonge la nyumba. Limezungushiwa ukuta, jumba lina fensi kwa juu, ndani kuna kamera, nyumba vigae, ukiingia ndani unakutana na bwawa la kuogelea. Kuna ungo wa Dstv, kuna bustani kali ya maua mbalimbali, kuna walinzi wawili ambao wanalinda kwa bunduki kutoka Knight. Yaani wapo full.
MIMI: Ok! Mimi naishi Tandale. Nyumba yetu ndogo, haina ukuta wala fensi, haina mlinzi na kama kuogea, tunaogea bafuni na si kwenye bwawa. Mpaka hapo, nimeshamkosa.
EDUADO: Ibra. Usiniangushe. Yaani mimi lengo langu umchukue huyu mtoto tu.
MIMI: Una namba zake za simu?
EDUADO: Hapana.
MIMI: Basi ngoja nifanye mishe halafu nione itakuwaje. Ila wasiwasi wangu ule ule tu, itakuwa kama Sikitu.
EDUADO:  Usijali kaka. Huyu sio kama Sikitu. Kwanza yule demu mwenyewe alinitaka nikaamua kukurushia wewe. Mimi na mrembo wa mkoa wapi na wapi. Ishi Dar tuwe tunamalizana, mambo ya mikoani haya, tigo pesa zinatumika sanaaaa. Hapa hapa Bongo ndio kuzuri, ukimtaka tu, nauli yako sh 400 kwenda, 400 kurudi. 600 soda yako, 600 soda yake. Mwisho wa siku kwa gharama zote ukitoa buku tano, michenji inarudi mingi mpaka mfuko unaomba poo kwa kuzidiwa uzito.
MIMI: Hahaha! Umeonaeeeee. Hakuna gharama kabisa. Ila poa, usijali. Ngoja nimtumie friend request halafu nianze kumfanyia uninja. Ila niandalie zawadi yangu.
EDUADO: Usijali kaka. Wewe fanya yako, ukimaliza, niache nami nifanye yangu. Au sio?
MIMI: Poa. Mia mia. Ngoja nianze kazi.
EDUADO: Shwari. Ngoja nifanye yangu. Nataka nimfuate mtoto Magreth hapa.
MIMI: Ndio yupi huyo?
EDUADO: Si yule wa facebook wa kipindi kileeeee.
MIMI: Kwani ushang’oa?
EDUADO: Chezea mimi wewe. Mimi noma…kama ni wembe basi Gilette.
MIMI: Sasa mbona hujamkata Aziza kama ni Gilette.
EDUADO: Aziza ana chembechembe za chuma. Ningemkataje? Huyo nakuachia kama wewe mwenye yale maji ya kuyeyushia vyuma ndio utakwenda nae sawa.
MIMI: Basi poa. Acha nikufanyie kazi yako mkurugenzi. Kazi hii niliachana nayo zamani sana ila kwa ajili yako, navaa gwanda nikukamilishie halafu nisepetue.
EDUADO: Mia mia.

Hapo nikatulia kwanza. Nikaanza kujifikiria ni kwa jinsi gani nilitakiwa kuanza kumfuata msichana Aziza. Kitu ambacho kilikuwa kikiniumiza kichwa changu kwa wakati huo ni kwamba hata Aziza mwenyewe sikuwahi kumuona kwa hiyo niliogopa kuuziwa mbuzi kwenye kiroba kama ilivyokuwa kwa Sikitu. Ngoja nikupe kijistori changu na huyu Sikitu.
Eduado alinifuata inbox na kuniambia kuhusu Sikitu, alimsifia na kumpamba sana, alinifanya nivutiwe nae sana na yeye alitaka nimchukue, nikasema poa. Mzee nikaanza mishemishe zangu kama Michael Scotfield wa Prison Break na kweli ndani ya wiki mbili, mtoto akawa mikononi mwangu. Unajua jinsi mtu anavyokwambia kwamba msichana mzuri hata kama wewe mwenyewe haujamuona unaanza kumtengeneza msichana wako kichwani, hivyo ndivyo nilivyofanya kwa Sikitu. Nikamtengeneza Sikitu wangu kichwani, kumbe nilikuwa namuumba Sikitu wa tofauti bila kujua. Siku aliponitumia picha yake inbox niione mara baada ya kumlazimisha sanaaa, akanitumia. Alikuwa mrembo lakini hakuwa na urembo kama ambao Eduado aliniambia. Nikaachana nae.
Sikitu hakukoma, chating zangu nzuri za inbox za maneno ya hapa na pale alikuwa akizipenda sana, hivyo alitaka tuendelee kuchati. Haikuwezekana tena, nilimkatia maguu mara baada ya kuniambia kwamba anaishi Musoma, mbaya zaidi huku Dar hakuwa hata na ndugu kwa hiyo hakuwa na ndoto za kuja Dar, sasa mimi ningeonania nae wapi? Yaani nisafiri mpaka Musoma kwa ajili yake? Niliona kuwa suala gumu sana kufanyika. Basi ndio hivyo, tukapotezana potezana na hatimae mapenzi kutoweka, siku hizi simuoni, bila shaka, kaniblock.
Baada ya miezi miwili, leo Eduado kaja na mpya, kaja na mrembo mpya ambaye wala sijawahi kumuona, huyu anaitwa Aziza. Sikutaka kufanya vitu kwa presha sana, nilichokifanya ni kumuomba urafiki na kisha kuanza kusubiria majibu. Kila siku nilipokuwa naingia facebook, hakuwa amenikubalia, sikuwa na shaka, niliendelea kusubiria zaidi na zaidi na baada ya siku mbili, akakubali kuwa rafiki yangu, furaha iliyoje? Hapo ndipo nilipoamua kuuanza mchezo wangu, mchezo ule ule ambao ulimfanya Sikitu kuchanganyikiwa kwangu, ila kwa hapa, kutokana na sifa ambazo niliambiwa na Eduado, ilinipasa nitumie mbinu kubwa zaidi, mbinu ambazo zingeendana na uzuri wake, mtoto wa kipemba bwana, hakutakiwa kufuatwa kikawaida, nami nikaanza kumfuata kipemba kipemba na mapenzi ya Kihindi….mtu mzima nikawa najiona kama Shahruk Khan vile.
****
   Mtu mzima nikaingia kazini kwa ajili ya kuanza kazi yangu ambayo nilikuwa nimepewa ya kuhakikisha kwamba mtoto wa Kipemba, Aziza anakuwa wangu. Ni kweli kwa mambo ambayo alikuwa amenieleza Eduado yalikuwa yamekwishanitenga kwa kiasi kikubwa sana kutoka kwa Aziza lakini ilitakiwa pia nifanye yangu katika kipindi hicho.
Kitendo cha Aziza kuukubali urafiki pamoja nami kilionekana kuwa kitu kizuri sana, kwa hiyo nilichokifanya nikajifanya bonge la bwege, nikamfuata kwa wall yake na kuandika ‘Asante A’ na kisha kusikilizia.
Kweli, kama alivyosema Eduado ilikuwa vile vile, mrembo hakuiLIKE asante yangu wala kuitolea comment, nikaona poa, vyote hivi ni mwanzo wa kumbukumbu zangu nitakazompa hapo baadae. Kwa upande wa Eduado, hakutaka kujishika, kila siku alikuwa akinisumbua tu kwa inbox.
EDUADO: Kaka vipi?
MIMI: Kuhusu nini?
EDUADO: Mtoto. Hujaniambia chochote kile. Umefanikiwa au?
MIMI: Wewe umeniambia mambo mengi kuhusiana na huyu mrembo, unadhani ningeweza kumamilisha ndani ya siku tatu?
EDUADO: Hapana. Nilikuwa nauliza manake nimeona hapa sasa hivi u rafiki yake.
MIMI: Yeah! Ni rafiki yangu ila kila kitu kinatakiwa kufanywa kimahesabu.
EDUADO: Usiniangushe basi Sharukh Khan.
MIMI: Hilo usijali.

Katika kipindi hicho nilikuwa nafikiria mambo mengi sana, huyu mtoto kwangu alionekana kuwa na pozi ajabu, yaani nilikuwa nikizipitia post za kizushi alizokuwa akiziweka, watu walikuwa wakicomment halafu yeye hatokei. Hata kama kaweka picha ya mdoli, watu walikuwa wakicomment halafu yeye hatokei na mbaya zaidi kulikuwa na watu wengi wanaolike na kucomment jambo lililonifanya kugundua kwamba kuna siku huyu msichana alikwishawahi kuweka picha na hivyo wanaume kujua ni mzuri na kisha kuzitoa.
Bado kiu yangu ilikuwa ni kuwasiliana na Aziza tu ambaye alionekana kuwa mtu wa mapozi sana. Sikujua ningeanzia wapi ila nilichokifanya ni kuanza kumtumia meseji nione kama angeijibu au kuipotezea.


Unataka niwe nakutumia stori kama hizi na kila nyingine inayonifikia? jiunge na familia ya 2jiachie.com kwenye  facebook hapa LIKE PAGE YETU HAPA ==> 2JIACHIE

ITAENDELEA SIKU YA KESHO JUMANNE

No comments

Powered by Blogger.