AZIZA WA FACEBOOK SEHEMU YA O5
MIMI: Ila
mimi sijawahi kuchati namna hiyo Aziza.
AZIZA: Najua.
Ila ninakumegea siri juu ya vitu ambavyo msichana anavipenda na vile
asivyovipenda.
MIMI: Dah!
Umeifungua akili yangu.
AZIZA: Ila
wewe..dah! Wewe mtu noma.
MIMI: Kwa
nini?
AZIZA:
Kama kuna msichana ulichati nae halafu akaonekana kuchoka na chatting zako,
basi hakika hatoweza kuridhika na chatting za mtu yeyote yule duniani.
MIMI:
Hahaha! Kwa nini?
AZIZA:
Unaandika maneno kwa ujumla, hauandiki vifupi, cha kushangaza sasa
MIMI:
Kipi?
AZIZA:
Unafuatilia mpaka alama za maandishi. Penye kiulizo, unaweka, penye nukta,
unaweka, penye mkato, unaweka, penye alama ya mshangao, unaweka. Nimekuvulia
kofia.
MIMI:
Hahaha! Ni kawaida sana Aziza. Napenda kuchati na mtu katika staili ya kuandika
hadithi.
AZIZA:
Hongera yako. Naomba nikuulize swali.
MIMI:
Uliza tu.
AZIZA:
Ulinimis?
MIMI: Sana
tu.
AZIZA:
Ulimiss nini kutoka kwangu?
MIMI:
Chatting na mambo mengine.
AZIZA:
Kama yapi?
MIMI:
Uzuri...koh koh koh
AZIZA:
Hahaha! Hebu acha kunitania, umewahi kuniona mpaka useme mimi mzuri?
MIMI:
Unajua unapoongea na msichana usiyemfahamu simuni halafu ukasikia sauti yake,
unajua tu kwamba huyu mzuri na huyu mbaya.
AZIZA:
Sasa kwani mimi umeisikia sauti yangu?
MIMI: Hata
unapochati na mtu, mwandiko wake unajionyesha kwamba huyu mzuri na huyu mbaya.
Ila kuna kingine pia.
AZIZA:
Kipi?
MIMI:
Nilichogundua ni kitu kimoja. Wasichana wengi wanaoweka profile picha zao picha
za wanawake maarufu wazuri, huwa wabaya. Ila walioweka picha za profile zao
kama maua au midoli, huwa ni wanawake wazuri.
AZIZA:
Hahaha!
MIMI:
Yeah! Hii ni kwa sababu yule msichana mbaya kamuweka Rihanna kwa sababu anataka
kutuonyesha kwamba yeye ni mzuri ila yule aliyoweka picha ya ua anataka
kutuonyesha kwamba yeye ni mtu wa thamani, mzuri na ananukia kama ua au mdoli.
Nililifuatilia hilo kwa marafiki zangu wengi na nikaligundua.
AZIZA:
Kweli wewe mfuatiliaji. Kwa hiyo ukagundua mimi kuwa ni mzuri?
MIMI:
Yeah! Nimegundua hilo kiasi ambacho kama nitaambiwa niombe kitu kimoja duniani
nacho kitafanikiwa, basi ningeomba kuwa na wewe, basi.
AZIZA:
Hahah! Acha utani Ibra.
MIMI: Kwani
naonekana kutania?
AZIZA:
Yeah!
MIMI: Huwa
sifurahii pale ninapokuwa serious halafu mtu ananiona natania. Nipo serius
Aziza.
AZIZA:
Sasa umenipendea nini? Hujawahi kuniona wala nini.
MIMI:
Ngoja nikwambie kitu Aziza. Mapenzi ni hisia, mapenzi hayajalishi uwe umemuona
mtu au haujamuona, vyote hutokea moyoni. Unapotumia kipindi kirefu kuchati na
msichana fulani, automatical moyoni unafall inlove, hicho ni kitu ambacho
hutokea kwa binadamu wengi wenye moyo wa nyama kama wa Ibra.
AZIZA:
Duuh! Hivi naomba nikuulize kitu.
MIMI:
Uliza.
AZIZA:
Unaongea mambo mengi sana mazuri Ibra. Unaonekana kuwa una kitu cha ziada
kichwani mwako.
MIMI:
Hapana, sina kitu cha ziada. Akili nilizonazo mimi ndizo ambazo hata mtu
mwingine anazo, tofauti kwenye kuzitumia hizo akili tu.
AZIZA:
Unaonaaa. Kila unachoongea point. Ibra una kitu cha ziada akilini mwako.
Matumizi ya akili yako nayaona kuwa tofauti sana. Wewe genius.
MIMI:
Genius! Acha utani. Niwe vipi Genius na wakati shuleni sijawahi kuingia hata kumi
bora?
AZIZA:
Sikiliza Ibra. Kuna wale genious wa darasani. Haimaanishi ukiwa genious
darasani basi hata kwenye kuongea na kuandika utakuwa genious, haiko hivyo. Kwa
magenious wamegawanyika. Kuna wale wa darasani na wale wa sehemu nyingine
kwenye maisha. Unaweza ukawa genius darasani lakini katika maisha ukawa
mbumbumbu. Unakubaliana nami?
MIMI: Kiasi.
AZIZA:
Hahaha! Usijali. Utanielewa tu. Turudi kwenye mada yetu.
MIMI: Kwa
hiyo hivyo ndivyo mapenzi yalivyo Aziza.
AZIZA:
Nimekuelewa Ibra.
MIMI: Naomba nikuulize swali moja tu.
AZIZA:
Uliza.
MIMI:
Ushawahi kujisikia kitu chochote romantic moyoni mwako juu yangu?
AZIZA:
Swali gumu kujibika Ibra.
MIMI: Najua.
Hata mwalimu anapoamua kutoa mtihani mgumu, kuna wengine wanafaulu japokuwa ni
mgumu. Najua swali langu gumu lakini naona linaweza kujibika kirahisi sana.
AZIZAl
Swali gumu Ibra.
MIMI: OK!
Ngoja nibadilishe swali. Unanipenda?
AZIZA:
Ninakupenda sana Ibra. Nahisi katika marafiki zangu wote facebook. U are the
best.
MIMI: Dah!
Ushatoka nje ya mada.
AZIZA: Kivipi?
MIMI: Hebu
turudi ndani ya mada. Unanipenda?
Swali lile
likaonekana kuwa gumu kwa upande wake, nikaona ukimya ukiwa umetawala mahali
hapo, nikawa naisubiria meseji yake huku nikionekana kuwa na kiu kubwa ya
kutaka kusikia kitu chochote kutoka kwake, hasa jibu la swali ambalo nilikuwa
nimemuuliza.
AZIZA:
Mhh!
MIMI: Nini
tena?
AZIZA: Una
haraka sana Ibra. Maswali yako mengine yanakufanya nikuone mtu wa haraka mno.
MIMI: Tatizo
muda Aziza. Nahofia kwamba nikichelewa, nitakuta ushachukuliwa kitu ambacho
sitaki kitokee.
AZIZA:
Hahaha! What if nikisema sikupendi?
MIMI:
Nafikiria litakuwa neno baya ambalo sijawahi kulisikia katika maisha yangu.
AZIZA: Hahaha!
Ibra una maneno sana. Hivi unayatoa wapi hayo yote?
MIMI:
Kutoka moyoni mwangu Aziza. Nimetokea kukupenda sana.
AZIZA:
Lakini bado mapema sana.
MIMI: Najua.
Najua kwamba mapema ila kumbuka kwamba vitu vingine ni lazima vifanyike mapema.
Nadhani sina makosa juu ya hilo.
AZIZA:
Nikuulize swali?
MIMI: Niulize.
MIMI: Niulize.
AZIZA: Una
mpenzi?
MIMI:
Nadhani ningekuwa na mpenzi nisingeweza kukwambia kwamba nakupenda na
kukuhitaji.
AZIZA: Kwa
nini usiweze?
MIMI:
Uaminifu. Napenda sana kuwa mwaminifu hasa kwa mtu nimpendae.....thats all.
AZIZA:
Sawa. Ila mbona haujaniuliza kama nina mpenzi au la?
MIMI:
Nadhani sitakiwi kujua kwani kwa upande mwingine nikitokea kujua, nitaumia kitu
ambacho sitaki kitokee moyoni mwangu.
AZIZA: Nakuonea
huruma Ibra.
MIMI: Kwa
nini?
AZIZA:
Unampenda mtu usiyewahi kumuona.
MIMI:
Hahaha! Hilo si tatizo Aziza. Kukuona haijalishi. Kitu kinachojalisha ni wewe
na mimi kuwa pamoja tu.
AZIZA:
Sasa kama nina mpenzi itakuwaje?
MIMI:
Sijajua itakuwaje lakini kitu ninachokihitaji ni kimoja tu, kupata nafasi
moyoni mwako, kuthaminiwa na kupewa kipaumbele.
AZIZA: Kwa
hiyo mpenzi wangu nimuache kwa sababu yako?
MIMI:
Simaanishi hivyo Aziza.
AZIZA:
Hiyo ndio maana yake. Yaani nimuache mpenzi wangu.
MIMI:
Wakati mwingine inawezekana. Ngoja nikupe kijistori cha kizushi.
AZIZA: Aya
nipe.
MIMI: Kuna
mwanamke mmoja alikwenda kuchota maji siku moja, alikuwa amechoka na kuchafuka
sana. Sehemu alipokuwa amechota maji kulikuwa mbali sana, kichwani alikuwa na
ndoo na mkononi alikuwa na kidumu. Bahati mbaya, akajikwaa, ndoo ikadondoka na
kupasuka, maji yakamwagika na kushindwa kuzoleka.
AZIZA:
Dah! Alifanya nini sasa?
MIMI:
Kurudi bombani kulikuwa mbali sana na alikuwa amechoka kupita kawaida. Kile
kidumu ambacho alikuwa nacho mkononi ndicho kilichomsaidia kuoga.
AZIZA:
Stori nzuri.
MIMI:
Yeah! Ni nzuri na iliyojaa mafunzo. Umejifunza nini?
AZIZA:
Nimejifunza kwamba yatupasa kuwa na kidumu pia katika kipindi tunachokwenda
kuchota maji.
MIMI:
Umekuwa mwerevu sana. Nadhani ushajua nimemaanisha nini.
AZIZA:
Hahaha! Kumbe ndio umemaanisha hivyo? Yaani nina ndoo na unataka niwe na
kidumu?
MIMI: Yeah!
Ila naomba ufahamu kitu kimoja. Wakati ndoo inapopasuka, kidumu kitaweza
kufanya kazi kama ndoo. Kwa hiyo ni muhimu kuwa na kidumu pia japokuwa
haulazimishwa kufanya hivyo.
AZIZA: Ibra
unanifundisha tabia mbaya.
MIMI:
Hapana. Sikufundishi tabia mbaya ila nakupa tekniki nyingine ya maisha. Njia
ambazo unaweza kufanya plan B mara plan A inapoonekana kuharibika.
AZIZA: Ok!
Nimekuelewa.
MIMI: Sasa
umechukua hatua gani baada ya kunielewa?
AZIZA:
Inabidi unipe muda wa kufikiria kwanza manake duh! Kuwa na kidumu inahitaji
moyo.
MIMI:
Nisikilize Aziza. Unataka kwenda kuomba ushauri wapi? Kwa mama?
AZIZA:
Hapana Ibra, ila nahitaji kujifikiria juu ya hilo.
MIMI:
Kwani moyo wako unakwambia nini sasa hivi juu yangu?
AZIZA: Hauniambii
kitu chochote.
MIMI:
Unanidanganya Aziza. Hautakiwi kulifikiria jambo hili, unapoamua kufanya
maamuzi ya maisha yako yakutakiwa kuwa peke yako Aziza.
AZIZA: Najua.
Sasa wewe unafikiri natakiwa kumuomba ushauri nani zaidi ya mama?
MIMI:
Niombe ushauri mimi.
AZIZA:
Hahaha! Aya basi nishauri juu ya hili. Unaonaje, niwe na Ibra au?
MIMI:
Hahah! Ninachokushauri ni kwamba inakupasa kuwa nae kwani kwa muonekano wake tu
anaonekana kukupenda na kukuhitaji sana tofauti ya unavyofikiria Aziza.
Usimuumize, mpende, kama ameamua kukupenda, kuutoa moyo wake kwa ajili yako,
mfanyie the same.
AZIZA:
Hahaha! U mshauri mbaya sana.
MIMI: Kwa
nini?
AZIZA:
Unanishauri vitu vibaya. Ila ok! Naomba nikufikirie kwani sitaki kukuumiza.
Nikisema nitoe jibu langu sasa hivi, utaumia na mimi sitaki uumie.
MIMI:
Sawa. Kama unaona ukitoa jibu la papo kwa papo utaniumiza, basi usifanye hivyo.
Kwa hiyo lini utanijibu.
AZIZA:
Wewe unataka lini?
MIMI: Sasa
hivi....lol!!
AZIZA: Utaumia.
Naomba unipe muda. Bado tuna nafasi kubwa ya kuzidi kuwasiliana Ibra.
MIMI: Poa.
Kama ndio hivyo hakuna noma, acha tuzidi kuwa na nafasi zaidi.
AZIZA:
Umekasirika?
MIMI:
Hapana. Sijakasirika. Kwani umeongea neno lolote la kunikasirisha?
AZIZA:
Hapana ila wanaume wengine huwa ukiwakataa wanakasirika sana na kesho
wanakuwekea post.
MIMI: Acha
nao. Hawajui mapenzi, mapenzi yanahitaji subira, mapenzi yanahitaji kujitoa kwa
kila kitu, hautakiwi kukata tamaa ila mapenzi pia yanahitajiiiii........
AZIZA:
Yanahitaji nini?
MIMI:
Kuyafuatilia sana kama unafuatilia kazi.
AZIZA:
Hahaha! Una maneno wewe mtoto.
MIMI:
Kawaida tu. Ila kiukweli...dah! hongera.
AZIZA:
Hongera ya nini?
MIMI: U
mzuri sana. Yaani dah! Sijui niseme nini. Kuna mengine nikisema naona kama
nitaonekana muongo.
AZIZA: Hahaha!
Kivipi? Niambie tu.
MIMI: Jana
nilipokuwa nikinywa maji, nilikuona kwenye glasi, nilipokuwa najitazama kwenye
kioo, nilikuona wewe. Usiku silali, nakuota wewe tu.
AZIZA:
Hahaha!
MIMI:
Maneno ya zamani hayo. Wanawake wa zamani ulikuwa ukiwaambia hivyo....fasta
unamchukua. Ila nyie wa siku hizi mmejanjaruka sana.
AZIZA:
Hahaha! Kwa sasa hivi tunajua ukweli kwamba huwezi kuniona kwenye maji.
MIMI: Ok!
Tuachane na hayo. Hivi tunaweza kuonana?
AZIZA:
Kuonana. Mbona mapema sana!
MIMI: Poa,
usijali. Tutaonana tukizeeka kwa sababu ndio utakuwa muda muafaka.
AZIZA:
Hahaha!
MIMI: Hiyo
ndio maana yake. Yaani kuonana tu unataka tupeane kalenda. Kweli makubwa.
AZIZA:
Usijali. Tutaonana soon. Ngoja nikamilishe vitu fulani hivi vya kifamilia.
MIMI: Ok!
Hakuna tatizo. Unaweza kuchukua muda gani?
AZIZA: Si
muda mrefu, kama siku mbili tatu hivi. Unatamani kuonana na mimi?
MIMI: Yeah!
Ninatamani sana Aziza.
AZIZA: Ok!
Hakuna tatizo. Utaonana na mimi kwa masharti.
MIMI:
Masharti gani?
AZIZA: Uje
nyumbani.
MIMI: Mh!
AZIZA: Nini
tena?
MIMI: Kwa
nini usije nyumbani. Au unaogopa matope, unaogopa kuchafuka kutokana na matope
ya uswahilini?
AZIZA:
Hapana. Nitakuhitaji uje nyumbani.
MIMI:
Unataka nife nini?
AZIZA: Kwa
nini?
MIMI: Baba
yako. Nadhani ataniua.
AZIZA: Usijali.
Ninapokwambia uje nyumbani, namaanisha kwamba siku hiyo itakuwa poa na
hakutokuwa na tatizo.
MIMI:
Sawa. Ukiwa na nafasi naomba uniambie. Shida yangu nikuone tu.
AZIZA:
Sawa. Usijali. Tutaonana tu.
Siku hiyo
tulichati sana mpaka saa saba usiku muda ambao alitaka kulala, niliridhika na
hivyo kumruhusu kwa moyo mmoja kulala. Siku zikakatika mpaka kufikia siku ambayo
Aziza akataka kuonana na mimi. Nakumbuka siku hiyo ilikuwa kama ndoto kwangu,
baada ya miezi miwili ya mawasiliano bila kuonana leo hii Aziza akaniambia
kwamba alikuwa akitaka kuniona, nilitamani kurukaruka kwa furaha.
Siku ya
tukio ilipofika, nikaoga na kujiweka makini, nikachukua jinzi yangu na kuivaa,
nikachukua raba zangu za kawaida na kuzivaa huku kofia yangu ikiwa kichwani
mwangu. Kutoka nyumbani mpaka kwao Masaki wala hakukuwa mbali, nilitegemea
kuchukua daladala na hatimae kwenda nyumbani kwao. Mara baada ya kumaliza
kujiandaa, nikaingia facebook na kisha kuanza kuwasiliana nae.
AZIZA: Ok!
Chukua namba yangu. Hii hapa. 0718 069 269.
MIMI: Ok!
Ndio najiandaa kwenda kituoni sasa hivi.
AZIZA:
Kwani umeshatoka nyumbani?
MIMI: Bado.
AZIZA:
Basi usijali. Nielekeze nije kukuchukua.
MIMI: Uje
kunichukua?
AZIZA: Yeah!
Kuna ubaya?
MIMI: Yeah!
Sijawahi kufuatwa na gari toka nizaliwe.
AZIZA: Usijali.
Leo nitakuwa wa kwanza kukufuata. Umesema Tandale, napafahamu kidogo, nitakuja
mpaka kwa Mtogole then unielekeze.
MIMI: Hakuna
tatizo. Nakusubiria.
Sijui
niseme nini aisee, huyu mtoto alikuwa akijiandaa kuja kunichukua nyumbani kwa
ajili ya kuelekea nyumbani kwao, nilikuwa na presha sana, sikuwa nikijiamini
kwamba nilikuwa mimi Ibra. Moyo wangu ukawa na dukuduku kupita kawaida, mavazi
niliyoyavaa niliyaona kutokuwa fresh hali iliyonifanya kubadilisha mara kwa
mara. Sikujua Aziza alikuwa akifanana vipi, uzuri ambao aliusema Eduado, leo
nilikuwa nakwenda kuuona kwa macho yangu.
Kwa sababu
aliniambia kwamba angekuja mpaka kwa Tandale Kwa Mtogole wala sikuwa na
wasiwasi, nilichokifanya ni kuelekea katika sehemu ya Mafyoso Camp ambapo
vijana wengi tulikuwa tukitumia kukaa na kutulia. Siku hiyo, mawazo yangu yote
yalikuwa juu ya msichana Aziza ambaye alitarajiwa kufika muda si mrefu,
sikutaka kumwambia mtu, nilichotaka kukifanya nilitaka kiwe sapraizi kwa kila
mtu mahali pale. Ilipofika saa tisa na robo alasili, simu yangu ikaanza kuita,
nikaipokea na kisha kuipeleka sikioni.
AZIZA:
Nimekwishafika hapa kwa Mtogole.
MIMI: Ok!
Unaiona hiyo njia ya vumbi kushoto kwako?
ITAENDELEA SIKU YA KESHO
Unataka niwe nakutumia CHOMEZO watu 200 wa
kwanza kulike PAGE YA 2JIACHIE Mtatumiwa imbox chomezo LIKE PAGE YETU
HAPA ==>www.facebook.com/2jiachie
Post a Comment