MAJINA YA WACHEZAJI WALIO CHANGULIWA KUBORESHA TIMU YA TAIFA YATAJWA
Kocha
Msaidizi, Salum Mayanga, aliyekuwa na timu hiyo katika Mkutano na
waandishi wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hill View
iliyopo jijini Mbeya.
Waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya.
Na Sophia Mwaipyana,Mbeya
Mkocha aliye kuwa anawaanda wachezaji wa maboresho katika timu
yaTaifa Salum Mayanga ameya taja majina ya wachezaji 16 ambao
wamechaguliwa kujiunga katika timu ya Taifa.
Kikosi hicho ambacho kiliweka kambi ya taifa iliyokuwa Tukuyu
wilayani Rugwe mkoania Mbeya ambao waliingia na wachezaji 34 kambini
mwezi ulio pita tarehe 22 na kumalizika mwezi huu.
Akiongea na wandishi wa habari jana katika ukumbi wa Hill view
aliwataja wachezaji hao kuwa ni mlinda mlango Benedict Mlekwa toka
(Mara),walinzi wakati wawili Emma Simwanda ( Temeke), Joram Mgeveje
(Iringa).
Walinzi wa pembeni Omari Kindamba (Temeke), Edward Mayunga
(Kaskazini Pemba),Shirazy Sozigwa (Illala) na viungo wa ulinzi ambao ni
Yussuf Mlipili (Temeke) na Said Ally (Mjini Magharibi).
Pia aliwataja viungo wa ushambuliaji kuwa ni Abubakar Mohamed
(Kusini Unguja), Hashimu Magona (Shinyanga) na viungo wa pembeni ni
Omari Nyenje (Mtwara), na Chunga Zito (Manyara).
Kwaupande wa safu ya ushambuliaji ni Mohammed Saidi(Kusini
Pemba),Ayubu Lipati (Ilala),Abdurahman Ally (Mjini Magharibi) na Paul
Bundara (Ilala) na wachezaji wa chini ya umri wa miaka 20 (U20), Mbwana
Musa (Tanga) na Bayaga Fabian (Mbeya).
Alisema kuwawachezaji walio chaguliwa wataondoka leo kuelekea Dar
es salaam kwajili ya kuungana na wachezaji wengi kwajili ya kunda kikosi
cha Taifa.
Naambao hawaja changuliwa katika kikosi hicho watabaki katika uwangalizi wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF).
Post a Comment