AZIZA WA FACEBOOK SEHEMU YA 08
AZIZA:
Mungu wangu! Baba!
MIMI:
Unasemaje?
AZIZA:
Baba. Baba amerudi.
MIMI:
Amerudi (Nikainuka na kwenda kuchungulia dirishani, gari aina ya Range la baba
yake lilikuwa linaingia)
AZIZA:
Mungu wangu! Sijui nifanye nini.
MIMI: Wewe
si ulisema baba yako anarudi saa mbili usiku?
AZIZA:
Ndio. Sijui leo imekuwaje.
MIMI:
Mmmh! Hiki kifo (Nilijisemea moyoni huku nikitetemeka na haja ndogo ikitaka
kunitoka)
Aziza
alionekana kama kupigwa ganzi, hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya
kwa wakati huo, nilimuona akianza kutetemeka huku kwa mbali kijasho chembamba
kikianza kumtoka. Hakuonekana kuamini kile ambacho alikuwa akikiona mahali
pale.
MIMI: Kwa
hiyo?
AZIZA:
Sijui nifanye nini.
MIMI:
Chumba chako kipo wapi?
AZIZA:
Njoo.
Nikaanza
kumfuata kule aliponiambia nimfuate, chumbani. Nilijua fika kwamba katika
kipindi hicho akili yake haikuwa sawa, mimi kama ninja nikatakiwa kufanya
manuva. Tukaenda mpaka chumbani kwake, alikuwa akiendelea kutetemeka tu. Baada
ya kufika chumbani, mtu mzima nikabaki nikikiangalia chumba kile, kilionekana kuwa
na mvuto sana.
AZIZA: Kwa
hiyo.
MIMI:
Daah! Ngoja nizame chini ya kitanda (Sikutaka kuchelewa hata sekunde kumi, mtu
mzima nikazama chini ya kitanda)
Huko chini
kulionekana kusafi ajabu, kitanda kile kikubwa cha chuma kilikuwa na nafasi ya
kutosha kabisa. Kitu cha kwanza nilichokifanya ni kuichukua simu yangu na kisha
kuiweka katika silent. Nilibaki nikijiuliza sana kwamba kwa nini jambo kama
lile lilikuwa likinitokea? Kwa nini Aziza alikuwa ameniaminisha sana mimi
kwenda kwao mpaka kutaka kuniletea msala? Kila nilichojiuliza nikakosa jibu.
Kule chini ya kitanda nikaanza kuchati na Eduado kupitia sms za kawaida.
EDUADO: Ibra
umefikia wapi?
MIMI: Kaka
acha. Nipo kwao.
EDUADO:
Du! Upo kwao? Wewe noma. Ilikuwaje kuwaje hadi umefika kwao?
MIMI:
Alikuja kunichukua home.
EDUADO:
Sikupatii picha mtu mzima. Leo malovee hapo hapo chumbani kwake.
MIMI:
Haha! Kaka acha, huku msala. Nipo uvunguni.
EDUADO:
Uvunguni! Kivipi tena?
MIMI: Baba
yake amefika na wakati dogo alisema kwamba anarudi saa mbili usiku. Karudi kwa
kushtukiza, yaani hapa nimeingia chumbani kwake na kujificha uvunguni.
EDUADO:
Hahaha! Kaka hiyo kweli noma, sikupatii picha aisee ulivyojipinda huko mtu
mzima, kama dawa ya mbu.
MIMI: Kaka
wewe acha tu, huku ni noma. Ukisikia nimepigwa risasi, usishangae.
EDUADO:
Dah! Ngoja nikuombee Mungu akuokoe.
MIMI: Wewe
unafikiri Mungu atanisaidia hapa?
EDUADO:
Atakusaidia tu.
MIMI:
Kunisaidia anaweza ila dah! Kaka mimi ni mwenye dhambi. Nafikiri atataka
nikamatwe ili nisirudie mchezo wangu wa kusalandia watoto wa watu.
EDUADO:
Kaka pole sana. Sasa mtoto anasemaje?
MIMI:
Yaani hapa ni kujiokoa mwenyewe. Aziza anazingua, anaonekana kuogopa sana.
EDUADO: Kwa
hiyo utatokaje humo uvunguni?
MIMI:
Ngoja kwanza giza liingie manake huku mtu unaweza kufa.
Mtu mzima
nilikuwa nazidi kutetemeka chini ya uvungu wa kitanda, Aziza hakuwa akitulia,
mara aingie, mara atokea hali ambayo ikanionyeshea angetoa boko muda wowote
ule. Nilichokifanya nikachukua simu yangu na kisha kuanza kumtumia meseji.
MIMI: Nini
kinaendelea hapo?
AZIZA:
Baba amekaa sebuleni, amekuja na wageni. Tena wageni ambao watalala hapa hapa
nyumbani.
MIMI: Hilo
sio tatizo sana. Wa kike au wa kiume?
AZIZA: Wa
kike.
MIMI:
Duuh! Ila si watalala chumba cha wageni?
AZIZA: Yeah!
Ila wengine watalala katika chumba changu. Mbaya zaidi baba ameniambia nije
kusogeza kitanda ili kiingizwe kitanda cha pili.
MIMI:
Duuuh! Leo kazi ipo.
AZIZA:
Mbaya kuliko zote amemwambia mdogo wangu aje kufagia chumbani.
MIMI: Wewe
si ulisema wadogo zako wapo shule bording?
AZIZA:
Nilikuwa nimekudanganya.
MIMI:
Mungu wangu! Nimekwisha.
AZIZA:
Naomba uniambie nifanye nini Ibra.
MIMI:
Kwanza kabla ya yote punguza presha.
AZIZA:
Sawa.
MIMI:
Najua kwamba leo nakwenda kukamatwa, kabla sijakamatwa naomba uniambie kitu
kimoja.
AZIZA:
Kitu gani?
MIMI:
Unanipenda?
AZIZA: Nakupenda
Ibra.
MIMI: Upo
tayari tuingie katika mahusiano kwa muda mchache uliobakia kabla sijauawa na
baba yako?
AZIZA: Ibra
usiseme hivyo.
MIMI: Wewe
unafikiri nitasemaje? Naomba unijibu. Upo tayari?
AZIZA:
Nipo tayari lakini jua hautokwenda kuuawa.
MIMI:
Nimefanya kila kitu kwa ajili yako, nilihisi mambo haya yatatokea tu toka
tulipokuwa tukija. Ila usijali. Ngoja nikuonyeshe jinsi mchezo unavyofanyika
Aziza. Nataka nikuonyeshe kwamba huwa sikamatwi kijinga jinga.
AZIZA:
Utafanya nini sasa?
MIMI: Cha
kwanza hakikisha mdogo wako haji kusafisha chumba, akifika chumbani mpokonye
fagio, ng’ang’ania kusafisha chumba chako.
AZIZA:
Sawa. Cha pili?
MIMI:
Hakikisha kila unapotoka chumbani, unafunga mlango kwa ufunguo, cha tatu, uache
mlango wa jikoni wazi, cha nne mpe taarifa baba yako kwamba kuna mtu alikuja
kumuulizia.
AZIZA:
Mmmh! Huyo mtu nani?
MIMI: Ibra...ila
leo niite jina la Ahmed.
AZIZA:
Akisema yupo vipi?
MIMI: Mwambie
kama jinsi nilivyo. Usitie shaka.
AZIZA:
Kingine nisemeje?
MIMI: Mwambie
kwamba ningekuja baadae kumuulizia tena.
AZIZA:
Mhh!
MIMI:
Usijali. Kila kitu kipo under control.
AZIZA:
Sawa.
Baada ya
dakika kadhaa, nikasikia mlango ukifunguliwa, nikasikia vishindo vikija kwa
kasi, alikuwa mdogo wake ambaye alitaka kusafisha chumba kwa kukifagia, Aziza
akafika na kisha kumpokonya ufagio kwa kutaka kufagia yeye mwenyewe. Mdogo wake
alipoondoka, akakiinamisha kichwa na kisha kukutana nami.
MIMI: Vipi
huko?
AZIZA: Bado
hali ni ngumu.
MIMI:
Daah! Sikamatwi kijinga hapa. Fanya kama nilivyokwambia, umesikia?
AZIZA:
Sawa.
MIMI:
Nakupenda mpenzi.
AZIZA: Nakupenda
pia (Tukafanya kile tulichotaka kukifanya pale sebuleni....lol)
Aziza
akaondoka, nikaona sio ishu, niliendelea kukaa uvunguni mule. Nazo dakika
zilikuwa zikisogea tu, zilisogea zaidi na zaidi, mpaka saa moja usiku inaingia,
mtu mzima nilikuwa mule mule ndani, chini ya uvungu. Saa mbili kasoro nikaona
ungekuwa ujinga, nikamtumia Aziza meseji.
MIMI: Njoo
uvunguni kwanza.
AZIZA:
Sawa.
MIMI: Ila
kabla ya kuja, cheki kuna nani jikoni.
AZIZA:
Yupo mama.
MIMI:
Vizuri sana
AZIZA:
Vizuri?
MIMI: Yeah!
Njoo kwanza huku uvunguni.
Baada ya
muda, Aziza akafika, hakuonekana kuwa na amani.
AZIZA:
Unasemaje baby?
MIMI: Hapa
naondoka na kuelekea jikoni, cha msingi kamtoe mama yako jikoni.
AZIZA: Mmmh!
Nitamtoa vipi?
MIMI: Kamwambie
kwamba baba yako anamuita.
AZIZA:
Eeeh!
MIMI:
Fanya hivyo. Una dakika moja ya kufanya hivyo. Nakwenda na muda.
AZIZA: Halafu?
MIMI: Wewe
kamwambie hivyo. Akija sebuleni mimi utanikuta nje ambapo huko sebuleni utamwambia
baba yako kwamba kulikuwa na mtu alikuja kumuulizia. Umesikia
AZIZA: Na
mama akifika sebuleni na kusema kwamba kaitwa kumbe hajaitwa?
MIMI:
Mwambie uliskia vibaya.
AZIZA:
Sawa. Umeifungua
MIMI: Kwenye
ile dakika moja, umebakisha sekunde arobaini. Nenda, ukitoka zima taa ya humu
chumbani na uuache mlango wazi kidogo
AZIZA:
Sawa.
Aziza
akaondoka mahali hapo, na kweli akaelekea jikoni na kumwambia mama yake kwamba
alikuwa akiitwa na baba yake, nilipomuona mama yake akipita ukumbini kueleka
sebuleni, nikaufungua mlango na kupita kuelekea jikoni kwa kasi huku
nikihakikisha sisikiki, nikaufungua mlango na kutoka nje kwa nyuma, nikaanza
kuambaa ambaa mpaka pembeni ya gari lao.
MAMA
AZIZA: Nimekuja mume wangu.
BABA
AZIZA: Kuna nini?
MAMA
AZIZA: Aziza amekuja na kuniambia unaniita.
BABA
AZIZA: Mimi! Hapana, labda kasikia vibaya.
AZIZA: Si
nimesikia unamuita mama.
BABA
AZIZA: Hapana.
AZIZA:
Basi samahani nilisikia vibaya
MAMA
AZIZA: Usijali. Nipo jikoni naandaa chakula kwa sababu dada wa kazi anaumwa,
amelala na huyu Aziza asije akatoa chakula kibichi
BABA
AZIZA: Sawa. Aziza, wapeleke chumbani wageni hawa.
AZIZA:
Sawa. Ila leo kuna mtu alikuja kukuulizia.
BABA
AZIZA: Nani?
AZIZA:
Sijui, ila alisema atarudi usiku.
BABA
AZIZA: Yupo vipi?
AZIZA:
Mrefu kidogo, maji ya kunde halafu ana.........!
MLANGO:
Ngo ngo ngo ngo (Nilikuwa nikipiga hodi huku mlinzi akionekana kunishangaa
kwani aliniona ninavyoingia na Aziza, alikuwa hajui sababu kwa nini nilikuwa
nimetokea nyuma ya nyumba na kuanza kugonga mlango. Mlango ukafunguliwa,
alikuwa Aziza, kama vile sterring, nikaingia ndani, Baba yake Aziza akabaki
akiniangalia, sikufichi, nilijiamini kama Van Damme)
Baba yake
Aziza alikuwa amenitolea macho pamoja na wageni wote ambao walikuwa sebuleni,
mtu mzima sikutaka kuteteleka hata kidogo, nilionyesha uso wa kujiamini kupita
kawaida. Kwa Aziza, kwa mbali alionekana kuwa na hofu kwani alidhani kwamba
nisingekuwa na ujasiri wa kusimama na kuzungumza.
MIMI:
Samahani mzee. Shikamoo.
BABA
AZIZA: Marahaba.
MIMI:
Nilikuja katika kipindi kilichopita lakini sikukuta.
BABA YAKE
AZIZA: Sikuwepo. Sawa, umeshanikuta. Kuna nini?
MIMI:
Niliagizwa na mzee Badour wa kule Msasani, ameniambia kwamba leo utatakiwa
kufika katika kikao kile cha harusi kinachoendelea (Baba Aziza akaonekana
kushtuka)
BABA
AZIZA: Kikao gani?
MIMI: Kile
cha mtoto wake, Farhia.
BABA
AZIZA: Huyo mzee ndiye nani?
MIMI:
Mfanyabiashara mwenzako.
BABA
AZIZA: (Huku akionekana kushangaa zaidi) Alikutuma uje kwangu?
MIMI: Ndio
(Nilijibu huku nikiwa serious)
BABA
AZIZA: Una uhakika ni mimi?
MIMI:
Ndio.
BABA
AZIZA: Yeye alikwambia uende kwa nani?
MIMI: Kwako.
BABA
AZIZA: Nani?
MIMI: Mzee
Mahmoud.
BABA
AZIZA: Hapana. Mimi sio mzee Mahmoud. Mimi ni mzee Mansour.
MIMI:
Mmmh! Mbona unanichanganya? Hii si nyumba namba 315?
BABA
AZIZA: Hapana. Hii ni nyumba namba 511. Nyumba kuanzia namba 300 zipo kule
mbele.
MIMI: Ok!
Basi samahani kwa usumbufu mzee wangu. Nikosea namba, ila nilipomuuliza mlinzi
alijibu hapa ni kwa mzee Mansour ila jina likanichanganya, si unajua sisi
wengine majina ya kiarabu hatuyajui vizuri.
BABA
AZIZA: Usijali kijana. Najua vijana wa sasa hivi mnakuwa na mambo mengi
vichwani. Sawa. Nenda.
MIMI:
Usijali (Nikageuka na kisha kuufungua mlango huku Aziza akibaki kutetemeka tu)
MLINZI:
Ebwanaa vipi tena, mbona sikuelewielewi?
MIMI:
Hakuna tatizo. Nilikuwa nataka kuonana na mzee Mansour tu, kuna uninja nilikuwa
nakamilisha mara moja.
MLINZI:
Uninja gani?
MIMI: Wa
kucheza na akili za watu
MLINZI:
Kivipi?
MIMI:
Usijali, hili liko nje ya uwezo wako, ukitaka kulifahamu, utachanganyikiwa.
MLINZI:
Mmmh! Sawa! Karibu.
MIMI:
Asante.
:: Endelea ku LIKE PAGE YETU na ku COMMENT chombezo hili kali na lakusisimua.
:: Kwa wale watakaokuwa waki SHARE 100 wa kwanza nitawapa kipaumbele kwa kuwa TAG chombezo hili kila litakapokuwa likitoka litakuwa katika wall yao. LIKE PAGE YETU HAPA ==>www.facebook.com/2jiachie
:: Kwa wale watakaokuwa waki SHARE 100 wa kwanza nitawapa kipaumbele kwa kuwa TAG chombezo hili kila litakapokuwa likitoka litakuwa katika wall yao. LIKE PAGE YETU HAPA ==>www.facebook.com/2jiachie
HII NDO YA SIKU YA KESHO ITAENDELEA SIKU YA JUMANNE

Post a Comment