BARCELONA, PSG ZATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA
BARCELONA
imemalizia vizuri biashara baada ya kuichapa Manchester
City mabao 2-1 na kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa
ushindi wa jumla wa mabao 4-1.
Katika
mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Camp Nou, mabao ya Barca yalifingwa na
Lionel Messi dakika ya 67 na dani Alves dakika ya 90, wakati bao City
lilifungwa na nahodha wake, Vincent Kompany dakika ya 89.
Man
City iliyofungwa 2-0 Uwanja wa Etihad katika mechi ya kwanza ya hatua
ya 16 Bora, ilipata pigo jana dakika ya 78 baada ya mchezaji wake, Pablo
Zabaleta kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Katika
mchezo mwingine, PSG nayo ilimalizia vizuri biashara baada ya kuifunga
Bayer Leverkusen mabao 2-1 Uwanja wa Pac de Princes hivyo kufuzu kwa
ushindi wa jumla wa 6-1, baada ya awali kushinda 4-0 ugenini.
Biashara imeisha: Lionel Messi akisherehekea na wachezaji wenzake baada ya kuifungia Barcelona bao la kwanza.
Messi akimtungua kipa Joe Hart.
Asanteni: Messi akiwapungia mkono mashabiki wa Barca Uwanja wa Nou Camp.
Post a Comment